Mpaka September 2012, record inaonesha kuna alumni 85 kutoka nchi ya Tanzania
🙁 (
http://www.worldwide.harvard.edu/iws/pdf/International_Alumni_Breakdown_by_Country_2011.pdf)
Kenya wapo 183 na Uganda 47!
Inaweza kuwa kazi ngumu kupata majina yao.
Shukrani sana mkuu, nilikuwa sijaiona hii, imenisaidia kujibu maswali mengi niliyokuwa nayo kichwani - uchambuzi wangu mfupi huu hapo chini:
Watanzania:
Harvard Law School (HLS) = 22
Harvard School of Public Health (HSPH) = 21
Harvard Business School (HBS) = 17
Harvard College (COL) = 10
Harvard Graduate School of Education (HGSE) = 3
Graduate School of Arts and Sciences (GSAS) = 2
Graduate School of Design (GSD) = 0
Harvard Medical School (HMS) = 0
Tumesomesha wanasheria wengi zaidi na kwa kiasi kikubwa uwakili uko vizuri Tanzania, tatizo ni mifumo ya kisheria na wale majaji waliotajwa na mheshimiwa fulani.
Pengine kutokana na kuwepo kwa miradi ya afya ya Harvard nchini Tanzania ndio maana wamepokea wanafunzi wetu wengi (rejea posti yangu inayofuatia), na kwa sasa kuna miradi mingi ya afya ya jamii Tanzania, natumai inatusaidia.
Kundi la tatu lenye watu wengi ni waliosomea shule ya biashara ambapo kwa kawaida watu wanaenda hapo kusoma MBA, pengine ndio maana siku hizi uwekezaji, ujasiriamali na sekta ya mabenki inakua japo sina uhakika kama hawa wanatusaidia sana kama taifa.
Hiyo COL ndiyo inayotoa shahada ya kwanza, kwa kweli hapo vijana wetu ni wachache sana ukilinganisha na wa Nigeria, Kenya n.k.
Da, hapo kwenye elimu panajieleza penyewe ila kama HakiElimu imesaidia sekta hiyo nchini basi tukumbuke mwanzilishi wake ni mhitimu wa Harvard pia (nasikia na Mungai naye ni zao la chuo hiki).
Nashangaa hatuna hata msanifu majengo wale mtaalamu wa mipango miji aliyepitia GSD, ila hapo wana profesa huyu aliyetafiti Dar es Salaam katika tasnifu yake ya uzamivu:
Harvard Graduate School of Design - Homepage
Pia nashangaa hatuna watu HMS japo tunao wengi HSPH, pamoja na hayo madaktari wetu kina Ulimboka wako vizuri tatizo ni vitendea kazi na mishahara/marupurupu.