MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,649
- 48,411
Enzi za katiba ya zamani hapa kwetu ilikua hivi hivi kama tunavyoshuhudia kwa Watanzania, kwamba maskini wanyonge wanalaghaiwa na kunyanyaswa bila msaada wowote, hata wakifika kwa wakuu wa mikoa taswira inabaki ile ile, mpaka siku msafara wa rais utapita, kisha umpigie rais makelele hadi akuskie halafu unapewa mic uongee tatizo lako, hapo sasa ndio unakua umefika mwisho wa mateso yako maana ataamrisha suluhu.
Huwa natazama video za rais Magufuli, kweli ana nia ya dhati ya kutatua matatizo ya watu wake, lakini naona mzee wa watu ameanza kuchoka, siku za mwanzo mwanzo kwwenye hii misafara alikua anaskliza kesi za namna hii, lakini sasa hivi naona ameanza kuzichunia na inabidi mtu apige makelele sana ya kichizi kwenye hii mikutano ya kampeni ndio usklizwe.
Kwa hali ya hivi, maelfu na maelfu ya kero haziwezi kutatuliwa, lazima mtegemee katiba na sio kukaa mkisubiri misafara ya rais, mtamchosha sana.