Watanzania acheni roho mbaya kuhusu Zuchu na mziki wake, embu mwambieni ukweli

Jan 31, 2024
42
119
Acheni roho mbaya bali semeni ukweli. Kwa Sasa Tanzania na East Africa hatuna msanii wa Maana kama Zuchu, bidada anajua kwa kweli sijui hawa wakina Nandy, Nadia Mukami na wasanii wengine wa kike ambao mnawapa maua ya uongo na ukweli wamepigwa gap sana na Zuchu tena kubwa kuanzia uandishi, sauti na hata ubunifu kawaacha palefu sana wenzie.

Kuna kipindi niliwaza sana nikasema ni msanii gani anaweza akachukua mikoba ya Vanessa Mdee na Shaa(kusema ukweli hawa wadada wawili walijitahidi sana enzi zao) hasa Vee Money na walipokuja kuachana na muziki nikahisi labda Maua Sama anaweza kutufuta machozi kwa sababu na huyu bidada enzi zake alikuwa wa moto sana sijui aliteleza wapi kama hujawai ambiwa wewe ndo ulikuwa msanii wa kutubeba sisi WATANZANIA baada ya wakina Shaa na Vee Money kuachana na mziki ila ulijiangusha mwenyewe sijui ni issue ya management au vp ila ulikuwa na kila kitu rafiki yangu.

Najua Nandy mnashangaa kwanini sijamtaja, binafsi Nandy naonaga ni msanii ambaye anaweza kutamba ndani labda na nchi za jirani tu kama Kenya, Congo na Majirani zetu wengine ila hatuwezi kumtegemea Nandy atupeperushie bendera yetu Afrika na duniani kiujumla.

Why Zuchu ukiachana na issue za management yake kwanza bidada ana kipaji kikubwa sana uwezo wake wa kubadilika badilika kama kinyonga ndio unaomtofautisha na wasanii hao wengine akiamua aimbe nyimbo za kuamsha vibes, zenye melody kali, zenye ujumbe mkali imagine ngoma za Napambana na Naringa mnaziona za kawaida ila ni ngoma za hatari zile nyie.

Zishindanishe watu hapa ila nasema Zuchu ndiye msanii bora Tanzania na East Africa.

WATANZANIA mnasubiri Zuchu afe ndo mseme ukweli! Mpeni maua yake sasa hivi.
 
watanzania gani hao wamesema Nandy ni mkubwa kuliko Zuchu? Tuanzie hapo kwanza
 
Oyaa ushawahi kumsikia Zuchu akiimba live, ni kweli studio wanachuja sana sauti ila kwa Zuchu nahisi maproducer huwa wana kazi ya ziada maana siyo kwa sauti ile, uwezo wa msanii hautakiwi kuonekana studio tu bali hata jukwaani kwenye show
 
Mkuu ingekua kuchuja sauti ni rahisi na inatoka vizuri kama ya zuchu basi wasanii wengi wangekua wazuri.

Gigy money anaimba, kwa nn hatoki na melodies nzuri kama zuchu?
Live performance inategemea umemuona ngapi. Ni ngumu kufanya vizuri show zote. Hata Messi sio kila mechi anacheza vizuri
Pamoja na kusema zuchu umeona hana sauti nzuri live lakini bado ana uwezo mkubwa wa ku-engage na crowd na moja ya kitu muhimu kwenye live performance

Ruby wanasema ana sauti nzuri sijui ana sauti natural, lakini akiwa live hana uwezo wa ku-engage na crowd mwisho anakua anajiimbia mwenyewe na show yote inaonekana mbaya
 
Wewe nakujua shabiki wa zuchu 😂😂😂
Hebu niimbie kale kawimbo kake unakokapenda ka kitoto 🤣
 
Mkuu ingekua kuchuja sauti ni rahisi na inatoka vizuri kama ya zuchu basi wasanii wengi wangekua wazuri.

Gigy money anaimba, kwa nn hatoki na melodies nzuri kama zuchu?
Live performance inategemea umemuona ngapi. Ni ngumu kufanya vizuri show zote. Hata Messi sio kila mechi anacheza vizuri
Pamoja na kusema zuchu umeona hana sauti nzuri live lakini bado ana uwezo mkubwa wa ku-engage na crowd na moja ya kitu muhimu kwenye live performance

Ruby wanasema ana sauti nzuri sijui ana sauti natural, lakini akiwa live hana uwezo wa ku-engage na crowd mwisho anakua anajiimbia mwenyewe na show yote inaonekana mbaya
Dooh kwahiyo unabisha kwamba wasanii hawachujiwi sauti, wakati baadhi ya wasanii wenyewe pamoja na maproducer wanakiri hilo, msanii kuwa na sauti ni jambo moja na kuwa na mafanikio ni jambo lingine mkuu

Hadi nimesema hivyo basi ujue nishaangalia shows nyingi za Zuchu hadi ile ya US ambayo alikuta watu wachache, akaanza kuimba huku analia ndio kabisa akazidi kuharibu, kwa kifupi yule hamfikii Nandy wala Ruby

Mkuu we zunguruka tu umsifie kwenye mambo mengine ila kwenye sauti uongo, wasanii wengi ni wabana pua tu mpaka wanakera ila ni vile wanatumia ujanja ujanja, wanaimba content ambazo wabongo wengi na akili zetu fupi ndio tunazipenda hivyo hatuzingatii vocals
 
Kuna kitu nadhani hatujaelewana.
Sijasema sauti haichujwi. Nilichomaanisha kuchuja sauti haiondoi sana uhalisia ule ulionao, ndio nikakutolea mfano ungekua ni hivyo kila muimbaji angekua na sauti nzuri unapomsiliza iwe redioni, au kwenye platforms zingine.

Kuhusu kufatilia show za zuchu na kugundua ameunderperform hapa hukutakiwa kutoka hitimisho la jumla jumla ndio maana nikasema ulipaswa usema katika show ngapi za live amefanya vibaya kati ya ngapi. Umetolea mfano wa US kwa zuchu, inawezekana alifanya vibaya kutokana na mazingira na ugeni alionao. Hawa unaowasifia show za ndani tu hapa mbona ndio kila mara wanalia wakifanya vibaya wanasingizia kuhujumiwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom