Hakuna watu wajinga na wenye roho mbaya duniani kama Watanzania?

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Jan 3, 2018
1,816
5,151
Mtanzania ni mtu ambaye ukisema umshitue kwenye dili fulani tambua umeumia.

Ukimsaidia Mtanzania elewa kabisa utajuta katika maisha yako. Ndiyo maana Watanzania kibao wanafursa nje ya nchi lakini hawataki kuwashitua Watanzania wenzao kwasababu tabia zetu zinafahamika. Mtu anaona ni heri hiyo fursa ipotee kuliko kumshirikisha Mtanzania!

Nimekuwa nikiwafuatilia jamaa wawili YouTube waishio Marekani, mmoja ni Mtanzania anajiita Jack wa USA na mwingine ni Mkenya anajiita Ibrahim Onami.

Huyu Mkenya kwenye YouTube Channel yake anajaribu kuonyesha fursa zilizoko Marekani na kutoa Ushauri kwa watakaobahatika kwenda, pia amekuwa akieleza namna kazi mbalimbali zinavyopatikana na namna zitakavyokuingizia kipato.

Huyu Mtanzania mwenzetu Jack wa USA yeye kazi yake ni kuonyesha starehe, nyumba, magari, mademu wa kizungu na viwanja vya starehe. Huyu jamaa hajawahi kutoa ushauri kwa Watanzania wenzie na kuwatia moyo kama ukihitaji kufika Marekani ufanyeje na fursa zilizopo. Mimi simlaumu kwasababu ndiyo tabia zetu Watanzania zilivyo.

Kuna Watanzania kibao Marekani na nchi za nje ikiwemo Canada lakini ndugu zao wakijitahidi wapewe ushirikiano namna ya kwenda ili wawapokee wao wamekuwa wakitoa sababu za kijinga tu eti huku kuna maisha magumu kuliko huko nyumbani.

Hivi aliyewaambia sasa hivi duniani kote kuna maisha marahisi nani? Watu wanataka fursa angalau za kikazi tu ili wakabiliane na ugumu wa maisha, hii roho mbaya haijengi.

Wakenya, Nigerians, Ghananians, Ugandans wao wamefanikiwa kwa kushikana mikono kama watu wamoja wanaotoka nchi moja.

Mimi sishangai kwasababu Mtanzania atakuchekea tu usoni ila rohoni huwa ni chuki mbaya sana, pia tuna tatizo kubwa la kutokuwa waaminifu. Jitu utalisaidia mwisho wa siku litakudhurumu au kukuibia kabisa.

Kuna tukio moja nilisoma hapa, kuna jamaa Mtanzania anaishi Afrika Kusini aliamua kumsaidia Mtanzania na kufika kule dogo akaiba kwa mwajiri wake na msala ukabaki kwa aliye msaidia. Jamaa tangu hapo akaapa kutokuwasaidia Watanzania. Sijui ni kitu gani kinatusibu!

Aisee!
 
Mtanzania ni mtu ambaye ukisema umshitue kwenye dili fulani tambua umeumia.

Ukimsaidia mtanzania elewa kabisa utajuta katika maisha yako,Ndiyo maana watanzania kibao wanafursa nje ya nchi lakini hawataki kuwashitua watanzania wenzao kwasababu tabia zetu zinafahamika,mtu anaona ni heri hiyo fursa ipotee kuliko kumshirikisha mtanzania.

Nimekuwa nikiwafuatilia jamii wawili YouTube waishio Marekani,mmoja ni mtanzania anajiita JACK WA USA na mwingine ni Mkenya anajiita IBRAHIM ONAMI.

Huyu Mkenya kwenye YouTube Channel yake anajaribu kuonyesha fursa zilizoko Marekani na kutoa Ushauri kwa watakaobahatika kwenda,pia amekuwa akieleza namna kazi mbalimbali zinavyopatikana na namna zitakavyokuingizia kipato.

Huyu mtanzania mwenzetu JACK WA USA yeye kazi yake ni kuonyesha Starehe,Nyumba,magari,mademu wa kizungu na viwanja vya starehe,Huyu jamaa hajawahi kutoa ushauri kwa watanzania wenzie na kuwatia moyo kama ukihitaji kufika Marekani ufanyeje na fursa zilizopo.Mimi simlaumu kwasababu ndiyo tabia zetu watanzania zilivyo.

Kuna watanzania kibao Marekani na nchi za nje ikiwemo Canada lakini ndugu zao wakijitahidi wapewe ushirikiano namna ya kwenda ili wawapokee wao wamekuwa wakitoa sababu za kijinga tu eti huku kuna maisha magumu kuliko huko nyumbani.Hivi aliyewaambia sasa kuna maisha marahisi nani?,watu wanataka fursa angalau za kikazi tu ili wakabiliane na ugumu wa maisha,hii roho mbaya haijengi.

Wakenya,Nigerians,Gahanians,Ugandans wao wamefanikiwa kwa kushikana mikono kama watu wamoja wanaotoka nchi moja.

Mimi sishangai kwasababu mtanzania atakuchekea tu usoni ila rohoni huwa ni chuki mbaya sana,pia tuna tatizo kubwa la kutokuwa waaminifu,jitu utalisaidia mwisho wa siku litakudhurumu au kukuibia kabisa.

Kuna Tukio moja nilisoma hapa,kuna jamaa mtanzania anaishi Afrika Kusini aliamua kumsaidia mtanzania na kufika kule dogo akaiba kwa mwajiri wake na msala ukabaki kwa aliye msaidia,jamaa tangu hapo akaapa kuto kuwasaidia watanzania.Sijui ni kitu gani kinatusibu.

Aiseeeeee!.
Ungesema hivi hamna mtu mbaya kama mtazania kwa mtazania mwenzie wa kiongonzwa na kabila la wahaya, lakini mkenya kwa mtu asio mkenya mwenzie ni mkatili mwenye roho mbaya ya kuua, mbongo amfikii, nime ishi nao hao wakenya asikwambie mtu, wana ubaguzi wa hali ya juu hususani ukiwazudi pesa au utendaji.
 
Mkuu,Jack wa USA ameelezea vizuri sana jinsi ya kufika US na fursa,kuna clip yake You tube special ameelezea hilo tu,nenda ukasearch Youtube utaona,


Kingine sio kila clip yake awe anaelezea fursa tu,hua anaelezea maisha ya US pia na changamoto zake,namfuatilia sana ila lawama ya kusema hajawahi kutoa ushauri kwa watz jinsi ya kufika US hilo sio kweli.
 
Ungesema hivi hamna mtu mbaya kama mtazania k kwa mtazania mwenzie wa kiongonzwa na kabila la wahaya, lakini mkenya kwa mtu asio mkenya mwenzie ni mkatili mwenye roho mbaya ya kuua, mbongo amfikii, nime ishi nao hao wakenya asikwambie mtu, wana ubaguzi wa hali ya juu hususani ukiwazudi pesa au utendaji.
Usihamishe Magoli Mkuu!
Mbona mada ipo wazi, jamaa kaeleza vizuri tu namna watu wa mataifa mengine wanavyosaidiana wao kwa wao!

Lakini kwa Watanzania ni tofauti, sasa hapo hujaelewa nini!?

Kwa sisi tunaozurura nje ya nchi tunayaona, Wivu, roho Mbaya, vimejaa miongoni mwa Watanzania.
 
Huo mfano wako hauna uhusiano na kichwa cha habari. Hata magazeti yapo ya Hard News na Udaku. Hawezi tengeneza maudhui ambayo hayatamlipa, Watanzania hawana muda wa kufuatilia fursa za nje ya mipaka yao.
 
Back
Top Bottom