Watanzania 5 waripotiwa kufariki kwenye ajali ya Moto Afrika Kusini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120

Watu wasiopungua 70 wamepoteza maisha na wengine 52 wamejeruhiwa kufuatia moto uliozuka katika jengo la ghorofa tano katikati ya mji wa Johannesberg nchini Afrika Kusini.

Moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la jiji hilo kubwa la Johannesburg.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha jiji la Johannesburg, Robert Mulaudzi, moto huo umesababishapia watu wengine takriban 52 kujeruhiwa.

Hata hivyo Mulaudzi amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi kwa kuwa jitihada ya kutafuta miili ya watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine inaendelea.

Katika taarifa yake ya ziada aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, kampuni ya awali iliyokuwa ikijulikana kama Twitter, msemaji huyo amesema watu kadhaa wameokolewa.

Jengo lililozuka moto ni makazi holela ya watu.

Pamoja na hiyo, akinukuliwa na vyombo tofauti vya habari nchini Afrika Kusini msemaji huyo amesikika akisema jengo hilo lililowaka moto lilikuwa linafanywa makazi kwa wasio na majumba.

Lakini pia mbali ya vifo vilivyotokana na moto, vipo vya baadhi ya watu ambao wanatajwa kufanya jaribio la kuruka kutoka katika jengo hilo refu,katika nyakati za usiku, kipindi ambacho moto huo unaendelea kwa lengo la kutaka kunusuru uhai wao.
1693555899918.png
 
Hao watanzania walikuwa masikini kiasi gani mpaka wakapange kwenye gofu hilo. Wanasema hilo jengo lilitelekezwa na wenyewe wahuni wakajitwalia wakawa wanapangisha walalahoi wanaotafuta maisha huko afrika kusini
 
Baada ya kuiona habari hii nimeongea na Mtanzania kwa njia ya simu, yupo Johannesburg. Anasema hao wengi wao ni majambazi, vibaka na wanajihusisha na uhalifu ikiwemo madawa ya kulevya.

Wa Afrika kusini wamewachoma makusudi, walishapewa "warning" mara nyingi wao wakawa wanachukulia powa tu.
 
Baada ya kuiona habari hii nimeongea na Mtanzania kwa njia ya simu, yupo Johannesburg. Anasema hao wengi wao ni majambazi, vibaka na wanajihusisha na uhalifu ikiwemo madawa ya kulevya.

Wa Afrika kusini wamewachomamakusudi, walishapewa "warning" mara nyingi wao wakawa wanachukulia powa tu.
ni watanzania wenzetu au??
 
Atakua kakudanganya SA wanajali sana watu hayo majengo yalikuwepo mengi sana JHB na yaliachwa na wazungu waliokimbilia Nchi zingine ipo Kampuni ikishayanunua inatumia Polisi kuwafukuza na kujenga makazi majengo yalikuwepo mengi Bree Street,End street huko lakini hakujawahi kuchomwa moto ili wachukue majengo yao vitu vingine mkiambiwa jaribu na wewe kujiongeza kidogo basi...
 
Baada ya kuiona habari hii nimeongea na Mtanzania kwa njia ya simu, yupo Johannesburg. Anasema hao wengi wao ni majambazi, vibaka na wanajihusisha na uhalifu ikiwemo madawa ya kulevya.

Wa Afrika kusini wamewachomamakusudi, walishapewa "warning" mara nyingi wao wakawa wanachukulia powa tu.
Acha upumbavu huu, kwako maisha yamekua bora kwa kudhulumu poor of the poorest, kesho unajifanya ni muumini mkubwa mwenye imani wakati umejaa roho ya kikatili, sijui hizi nyumba za ibada mnafanya nini mle,mchawi mkubwa, wewe unajua Mapigano na mahangaiko ya maisha? Endelea kuishi kwenye hiyo AC,but one day upepo utageuka tu, rambi rambi kwa waliofiwa na ndugu zao waliokwenda ku fight for better life, salute kwao wamekufa in the battleground, Amina
 
FaizaFoxy nataka uwe rafiki yangu/ niku follow maana una data za uhakika
 
Nimewahi kufika Jos na niliyaona majengo mfano wa hilo lililoungua. Ni maskani za kihuni haswa na siku nilipoenda umeme ulikuwa changomoto kwenye jengo so kulikuwa na giza .

nachoweza kusema MUNGU awabariki wapiganaji wote katika maisha. Wanapitia mengi sana
 
Baada ya kuiona habari hii nimeongea na Mtanzania kwa njia ya simu, yupo Johannesburg. Anasema hao wengi wao ni majambazi, vibaka na wanajihusisha na uhalifu ikiwemo madawa ya kulevya.

Wa Afrika kusini wamewachomamakusudi, walishapewa "warning" mara nyingi wao wakawa wanachukulia powa tu.
Siwezi kusema kama wamewachoma kwa makusudi ila mengi uliyoyasema yana ukweli.

Binafsi nimewahi kufika hayo maeneo Mungu atunusuru katika utafutaji niliyoyaona kule niliogopa sana halafu sasa nilienda kishua kwenye training SA nikapewa barua niifikishe kwa mwana Raras aka Buti Kubwa kutoka kwa mama yake so nilipofika Johanesburg nikamtafuta na kuna mbongo mmoja akanipeleka anapoishi kwenye hiyo mijengo halafu muda wa jioni giza lishaingia. Raras mwenyewe nilimkuta kazimika na mipombe sijui unga.

Kesho yake niliwasimulia watu nilipoenda wakaniambia mshukuru MUNGU umetoka salama. Nilikuwa nimevaa koti na tai na wakati tunapanda ngazi watu walikuwa wananishangaa sema nadhani giza ndio lilinisaida
 
Nimewahi kufika Jos na niliyaona majengo mfano wa hilo lililoungua. Ni maskani za kihuni haswa na siku nilipoenda umeme ulikuwa changomoto kwenye jengo so kulikuwa na giza .

nachoweza kusema MUNGU awabariki wapiganaji wote katika maisha. Wanapitia

Acha upumbavu huu, kwako maisha yamekua bora kwa kudhulumu poor of the poorest, kesho unajifanya ni muumini mkubwa mwenye imani wakati umejaa roho ya kikatili, sijui hizi nyumba za ibada mnafanya nini mle,mchawi mkubwa, wewe unajua Mapigano na mahangaiko ya maisha? Endelea kuishi kwenye hiyo AC,but one day upepo utageuka tu, rambi rambi kwa waliofiwa na ndugu zao waliokwenda ku fight for better life, salute kwao wamekufa in the battleground, Amina
Upumbavu wake nini ndugu yangu, hoja hupingwa kwa hoja, wala siyo kwa kumshambulia mtoa hoja, mimi nimesikia toka BBC asbuhi, wengi wanaishi humo ni wahuni wasio kuwa na makazi, serikali imeenda mahamani mara kadhaa kwa ajili ya kuwaondoa ila ikawa inashindwa kesi.
 
Baada ya kuiona habari hii nimeongea na Mtanzania kwa njia ya simu, yupo Johannesburg. Anasema hao wengi wao ni majambazi, vibaka na wanajihusisha na uhalifu ikiwemo madawa ya kulevya.

Wa Afrika kusini wamewachomamakusudi, walishapewa "warning" mara nyingi wao wakawa wanachukulia powa tu.
Kwani kwenu hakuna wezi majambazi

Waache watu watafute huko wajuavyo

Wao

Ova
 
Ni majonzi na masikitiko makubwa Kwa baadhi ya familia hapa nyumbani TANZANIA 🇹🇿🇹🇿🇹🇿 kupotezaa vijana wake kwenye ajali ya moto Jana Johannesburg south Africa.

Najua hapa Jamii forum ni Familia kubwa na tumetapakaa sehemu mbali mbali ULIMWENGUNI mwenye access na south Africa tunaweza kupeana update hapa jukwaani...

ina lilah waina allah rajiun

Mwanga wa amani uangazie milele..

Acha upumbavu huu, kwako maisha yamekua bora kwa kudhulumu poor of the poorest, kesho unajifanya ni muumini mkubwa mwenye imani wakati umejaa roho ya kikatili, sijui hizi nyumba za ibada mnafanya nini mle,mchawi mkubwa, wewe unajua Mapigano na mahangaiko ya maisha? Endelea kuishi kwenye hiyo AC,but one day upepo utageuka tu, rambi rambi kwa waliofiwa na ndugu zao waliokwenda ku fight for better life, salute kwao wamekufa in the battleground, Amina
FaizaFoxy ni Muislamu
 
Back
Top Bottom