Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Hofu ya ghasia na mauaji ya chuki dhidi ya wageni imerejea Johannesburg ambapo Jumamosi iliyoisha nyakati za asubuhi takriban wageni saba walichomwa moto wakiwa hai katika kitongoji cha Diepsloot nje ya mji wa Johannesburg.
Hii ilifuatia msako mkubwa wa wanajamii kutafuta waharifu Ijumaa usiku na Jumamosi asubuhi.
Marehemu, wote wakiwa wanaume, walishukiwa kufanya uhalifu mbalimbali katika mitaa ya extension 12 na 13 katika kitongoji cha Diepsloot.
Wakiwa na silaha kali na mawe mikononi mwao, wanajamii waliwawinda waharifu.
Siku ya Ijumaa usiku, wawili kati ya wanaume hao wanaosadikika kuwa ni waharifu walikamatwa na jamii.
Waliwavamia na silaha kali na kuanza kuwapiga kwa fimbo na hata mawe.
Kisha wakawaweka kwenye mafuta ya petroli kabla ya kuwasha.
Kwa mujibu wa Diwani wa eneo hilo bwana Abraham Mabhuke, watu hao wanashukiwa kufanya uhalifu wa kikatili katika kitongoji hicho.
Diwani Mabhuke alidai wanaume wote ni raia wa Zimbabwe.
Alisema "Wazimbabwe wawili ambao wanadaiwa kuhusika na uhalifu unaofanyika katika Diepsloot Ext 12 & 13 walikamatwa na wanajamii."
Alisema wanajamii wa gatvol walikuwa wamevamia siku ya Jumamosi asubuhi, wakiwasaka wale wanaosadikika kuwa ni wahalifu wengine waliotoroka katika msako wa Ijumaa usiku.
"Katika hali ya kushangaza, watu watano zaidi wanaodaiwa kuwa Wazimbabwe waliuawa kwa kupigwa mawe asubuhi ya leo na wanajamii wenye hasira."
Alisema siku ya Ijumaa, watu wanne ambao ni raia walipigwa risasi na wanaodaiwa kuwa wahalifu. Mmoja alifariki, na wengine watatu walikuwa hospitalini wakitibiwa majeraha ya risasi.
Mauaji ya Jumamosi ya washukiwa hao yamefikisha watu saba, idadi ya watu walioteketezwa kwa moto wakiwa hai.
Wakaazi wanasema kila jioni kunakuwa na milio ya risasi katika mji wa Johannesburg wenye msongamano na idadi kubwa ya watu.
Lizzy Maluleke kutoka mtaa wa ext 12 aliiambia chombo cha Habari cha Scrolla Africa kwamba si salama kukaa katika kitongoji hicho. "Tunajiweka ndani na kufunga milango mapema sana kama mida ya saa 1 usiku, nyakati hizo kila mtu anakuwa ndani ya nyumba. Inasikitisha" alisema.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, wakazi wa Diepsloot wamekuwa wakiandamana kupinga uhalifu.
Viongozi wake watatu walikamatwa kwa kuchochea ghasia za umma.
Mnamo Juni, walidai kukutana na Rais Ramaphosa. Hata walisafiri hadi kwenye Majengo ya Muungano huko Pretoria kwa nia ya kukutana na rais wa jimbo.
Wakaazi wanasema wataendelea kuwawinda wahalifu wenyewe kwa mikono yao na kuwatokomeza, wakidai kuwa polisi wamewafeli.