Miili ya Watanzania waliofariki kwa Moto Afrika Kusini kurejeshwa nchini

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Ubalozi wa Tanzania, nchini Afrika Kusini umesema miili ya Watanzania 3 waliofariki dunia kwa ajili moto Agosti 31, 2023 huko Jijini Johannseburg itarejeshwa Nchini kuanzia leo Jumatano, Januari 24, 2024 baada ya kutambuliwa

Taarifa ya Ubalozi imeeleza mwili wa Said Kisarazo na Mohamed Kisarazo itaondoka Afrika Kusini leo Januari 24, 2024 Usiku huku mwili wa Mohamed Amir utaondoka Afrika Kusini Januari 25 saa 2:30 asubuhi na kuwasili Tanzania saa saba mchana

Mnamo Agosti 31, 2023, moto mkubwa ulizuka katika ghorofa la Usindiso, uliogharimu maisha ya watu 77 huku ukiwaacha wengi na Majeraha, ambapo hadi sasa Mwanaume mmoja (29) anashikiliwa kwa kukiri kuwasha moto huo huku Polisi ikisema anatarajiwa kufikishwa Mahakamani anapokabiliwa na Mashtaka 120 ya Jaribio la Mauaji
 
kwa hio toka mwezi wa 8 mpaka sasa hivi miili ipo mumetunza tu ?

ili mgundue nini ?
 
Back
Top Bottom