#COVID19 Watakaochanja chanjo ya Corona kesho kuingia bure uwanja wa taifa, hii sio siasa?

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Wizara ya Afya kesho watatoa tiketi za bure za mechi ya Simba na Yanga kwa wale watakaokubali kuchanja siku ya kesho.

Kwanza kabisa naipongeza Wizara ya Afya kwa ubunifu huu, ila kuna jambo litaonekana haliko sawa.
Chanjo ya corona ikiendelea kuwekewa zawadi hizi ni kutengeneza zaidi mashaka badala ya kupunguza mashaka.
Wapo wataojiuliza kwa nini iwe hivi?
Wizara ilipaswa iendelee kutoa elimu juu ya watu kupata chanjo. Ila kuweka hizi zawadi kunazidisha maswali.

Wizara haioni kwamba wale waliochanja na ni wapenzi wa soka, hawana uwezo wa kununua tiketi watakuwa wanajilaumu sana?

Yote kwa yote kila la kheri!
Screenshot_20210924-192429_1.jpg
 
Uchanje uingie Bure uwanjani kwani ikichanjwa hakuna mabadiliko ya mwili? Usijekuwa unaingia uwanjani kusinzia mwanzo mwisho!!!!
 
Watahangaika sana lakini wajue kitu kimoja Mungu wa Mbinguni hadhihakiwi na hulipiza kisasi hadi kizazi cha nne.
 
Uchanje uingie Bure uwanjani kwani ikichanjwa hakuna mabadiliko ya mwili? Usijekuwa unaingia uwanjani kusinzia mwanzo mwisho!!!!
Labda waseme chanjo itakupa nguvu za ziada kupigana vikumbo kuingia uwanjani. Hapo wanaweza pata 'wateja'.
 
Chanjo mbona n nzur tu nguvu Kubwa Sana ya nn ndomana watu wanakuwa waoga kuchanja
 
Wanatengeneza mazingira ya chanjo hii kuogopwa na jamii. Why promo
 
Ni Tanzania tu kila jambo ni kumfurahisha mwanasiasa. Haingii akilini chanjo inasababisha matatizo kwa wengine mpaka kufa then TFF inasisitiza watu waende kuchanjwa kitu ambacho ni hatari.
Kuna Mtanzania yeyote aliyekufa kwa sababu ya Chanjo?
 
Back
Top Bottom