#COVID19 Watakaochanja chanjo ya Corona kesho kuingia bure uwanja wa taifa, hii sio siasa?

Wizara ya Afya kesho watatoa tiketi za bure za mechi ya Simba na Yanga kwa wale watakaokubali kuchanja siku ya kesho.

Kwanza kabisa naipongeza Wizara ya Afya kwa ubunifu huu, ila kuna jambo litaonekana haliko sawa.
Chanjo ya corona ikiendelea kuwekewa zawadi hizi ni kutengeneza zaidi mashaka badala ya kupunguza mashaka.
Wapo wataojiuliza kwa nini iwe hivi?
Wizara ilipaswa iendelee kutoa elimu juu ya watu kupata chanjo. Ila kuweka hizi zawadi kunazidisha maswali.

Wizara haioni kwamba wale waliochanja na ni wapenzi wa soka, hawana uwezo wa kununua tiketi watakuwa wanajilaumu sana?

Yote kwa yote kila la kheri!
View attachment 1951083
Hatudanganyiki ng'o!
 
Labda chanjo ya ukimwi ndo itagombaniwa

EAC38EB5-CD64-409F-888E-1F956F433527.jpeg
 
Back
Top Bottom