Wizara ya Afya: Mchakato wa chanjo umekamilika, itatolewa bure

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
SERIKALI imetangaza kuwa tayari mchakato wa kuingiza na kutoa chanjo ya ugonjwa COVID-19 (Corona) umekamilika huku ikisisitiza tahadhari zaidi ziendelee kuchukuliwa na wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 4,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi kwenye mkutano wake na wandishi wa habari ambapo amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni hiari.

Prof. Makubi amesema Serikali itatoa chanjo hiyo bure bila kuwatoza wananchi huku akionya kuwa hawataruhusu uingizwaji holela wa chanjo hiyo au kutoza fedha kwa ajili ya kuchoma chanjo hiyo.

Amesisitiza ofisi zote za serikalini nchini wananchi wanaoenda wakiwemo watumishi na kuzingatia taratibu zote za kitabibu za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuvaa barakoa kabla ya kuingia kwenye Ofisi hizo pamoja na kuwepo kwa maji tiririka kwa ajili ya kunawa mikono.

" Tunatoa ushauri kwa Ofisi zote za Umma nchini kuzingatia taratibu za kujikinga na Corona kwa kuweka vifaa vya maji tiririka ili kila mwananchi anaeingia aweze kunawa mikono lakini pia tunasisitiza uvaaji wa Barakoa," Amesema Prof Makubi.

Aidha Prof. Makubi amesema miongozo na utaratibu huo ufuatwe pia mashuleni kwa kuhakikisha kunakua na Maji tiririka na uvaaji wa barakoa
 
Safi kabisa. Tunavunjika moyo sehemu moja tu. Kwamba Prof. Makubi alikuwa mmoja wa wahimiza maombi, nyungu, michai chai na malimao.

Kwamba alikuwa sehemu ya kudai kuwa huu ugonjwa ni vita vya kiuchumi, kwa kweli alitukwaza sana!

Nitakuwa wa mwanzo kabisa kwenye kuipata hiyo chanjo.
 
Yeye amechoma huyo aliyejikuta kawa mkuu wa nchi amechoma wanzane kwanza wao
mashuleni watoto wavae barakoa upumbavu mtupu
 
UHURU JR ndiyo hivyo tena. Kama wewe na familia yako hamtaki siyo wote
Sijui kwanini huwa mnanichanganya na wanaopinga zisiletwe chanjo, mimi suala la kuletwa au kutokuletwa chanjo hata silitilii maanani walete au wasilete sio issue kwangu.

Muhimu ni kwamba mnaoona hakuna usalama pasina hizo chanjo basi mjitahidi kujitokeza kudungwa hizo chanjo hasa watu wa humu mitandaoni, basi ni hivyo tu sie wengine maisha ni yaleyale tu.
 
Mimi nataka ile ya Madagascar , ile timu ya Prof. Kabudi iliishia wapi kwenye mchakato ?
 
Back
Top Bottom