Wasomi na kiingereza

Nipe mfano wa technical English na fluency english
Hizi ni porojo ''mfu'' za kuhalalisha huu upungufuy. Mtu ukisoma degree unatumia kiingereza cha kawaida kwa asilimia kubwa. Kuna dada mmoja ana masters ya Chuo Kikuu hata ukiongea naye mambo ya kawaida kichwani ni ''mweupee pe''
 
Yale yale john pombe magufuli[emoji3582],
John Pombe Magufuli [emoji3581]
 
Nini hiyo wapo wahitimu wengine wa vyuo hata matumizi ya R na L kwenye lugha mama ya kiswahili ni shida
wengi wameathiriwa na lugha zao za kibantu. Kuna baadhi ya lugha za kibantu ni nadra sana kukuta herufi "r" ikitumika.
 
Kiingereza za kujibia mitihani hakijawahi kua kigumu, hivyo mtu kumaliza had PHD na kutoongea kiingereza fasaha sioni shida.
Pia kiingereza sio akili, Wakandarasi wanaojenga barabara zetu kutoka china hata salamu za kiingereza hawajui. Wakandarasi wa SGR kutoka Turkey kiingereza hawajui, kajamba nani kutoka buza anapiga ngeli nzuri ila hata elfu hamsini kwenye bank account hana achilia mbali ujuzi wowote.
Rais wa China, Russia na korea kaskazini sijawah kusikia wanaongea kiingereza lakini nchi zao zina maendeleo makubwa sana... Ndugu zangu mkataa kwao mtumwa
 
Niujinga mkubwa sana kuamini mtu asiyejua kiingereza hana akili. Stop embraising western culture wazungu hawana muda na wewe hata ukijua Kiingereza chao
 
Kiungereza sio kachumbari Tanzania, ni lugha ya kufundishia ambayo kwa mtu aliyefika angalau kiwango cha digree atakuwa ameitumia kwa miaka 10. Kama kilikushinda miaka hiyo yote ulikuwa unasomaje na utawezeje kazini? Hembu tumia akili zako.
ni fikra zangu lkn... I mean mtazamo wangu...
 
inawezekana wewe hesabu rahisi tuu za calculas zina kupiga chenga, mbona sisi atukusemi?? wakati mtu kama mimi calculas naona kama hesabu za darasa pili vile.(Ni dhambi kutusema watu tulio soma science)
Mimi hesabu hainipigi chenga.. na unlike many ninaamini mtu anatakiwa afunzwe "namna ya kujifunza na kutafuta maarifa" hilo ndio somo kubwa kuliko somo lolote.

Kama unaweza kuelewa Calculus unashindwaje kuelewa matumizi sahihi ya maneno kwenye sentensi!? Au unashindwaje kutafuta maarifa ya swala hilo ujifunze!?

Katika hesabu na kuna Argument and Logic ni muhimu sana kuelewa hili.. maana hesabu na maisha in general yame-base on this...

Ukisema Ungwini haukupeleki sehemu yoyote... So is Calculus. Kama hujui how to sell your mathematical knowledge with great words to non mathematicians it will be as good as nothing...

Kwa kifupi hakuna kitu muhimu sana na kisichokuwa muhimu sana.. everything does its part.. ofcoz inabidi uondoe Bitcoin na sports betting πŸ™‚ ..hivyo sio muhimu.
 
Na hapa ndipo elimu yetu ilipofeli...


Mitaala yetu ni bora kabisa.....sasa tatizo lipo kwenye lugha ya kufundishia.
 
Uko sahihi Mkuu... Nimesoma Engineering... Kwa kweli kiingereza chetu ni cha Kihandisi... Technical English....

Nimekupata vilivyo....
 
Hahahahah [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umesema vitu vingi. Lakini nadhani unachokosa ni picha pana tu ya umuhimu wa kujifunza kwa lugha yako.

Utamaduni ukipanuka uhitaji wa bidhaa za kiswahili unakuwa... Mfano kupanuka kwa kiingereza kumefanya watanzania na dunia kufurahia Filamu za kiingereza ..maana wanaelewa.

Sasa Ukisema hatuwezi nakushangaa maana kiswahili chenyewe its hardly 150 years.. ukisema ni safari ndefu nitakubali ila kusema haiwezekani nitashangaa...

Wanaojifunza lugha ukubwani ni wengi.. hakuna mtu aliyesoma kichina toka akiwa mdogo nchi hii ni leo tuna wakalimani lukuki wa lugha ya kichina.. simply kwa sababu ya uhitaji.. wapo Watu wanazungumza kiarabu na mie nimejifunza kihehe na kisukuma ukubwani. Hiyo sio kazi ni interests .

Tutawezaje:
Kwa kufasiri.. lazima kufasiri maarifa sio vitabu. Elimu often hakusaidii kama haiwezi kufasiriwa katika mtazamo wa mazingira yako.

Baada ya kujua Taifa liko wapi, na linapaswa liende wapi, Kwanza tunajiwekea nini kifundishwe, kisha Kwa nini, Lini kifundishwe ,halafu kwa namna gani kifundishwe

Mfano unanifunza geografia ya Central Amerika for what!? Au Kakao (Ghana) Hii inanisaidia nini!? Lazima ujue kwanini unataka Watu wajifunze kile Unachotaka wajifunze.

Swala la communication ni swala la kuhitajika. Kama huna unachoweza kunivutia niwasiliane na wewe, then tusiwasiliane... Ila ukiwa na chochote kitakachofanya tuhitajiane naamini tutawasiliana.. bila kuwa na sababu ya kuwasiliana kujua lugha hiyo ya kizungu ni umbea tu. Maana hakufanikishi lolote.

Fundisha.kiswahili Watu waweze kuyajua maeneo yao vizuri ili waweze kuyatawala... Hiyo ndio Intelligence... Unapenda kijijini unaambiwa wakati wa upepo usipite njia ya chini maana utawashwa.. wamejifunza upepo huvumisha upupu..wameyatawala Mazingira yao.. kiakili.

Uvumbuzi sio kujenga meli pekee... Hata aliyegundua uyoga huu unaliwa na huu hauliwi... Aliyegundua Michembe ni njia bora.ya kutunza viazi.. na maparage ni equivalent ya conflackes wote walivumbua... Ni Mainjinia wetu waliokariri ndio wanaowatisha wananchi wavumbuzi namna bora ya kuboresha teknolojia zao.

Tukiwa tunasoma kulikuwa na vijana toka vijijini kabisa kwenye Umitashumta walikuwa wanafanya vumbuzi kubwa mno.na za maana zenye tija kama zitaendelezwa... shinda ni management of talents...

Kuongea kiingereza hakukufanyi miraculously smart.. na wala hakukufanyi uwe mvumbuzi... Wavumbuzi wako wengi na kwa taifa letu ukiondoa dharau wavumbuzi wengi wako vijijini na mashambani... True innovation.
 


Hahahaa kalitaja sana hilo neno kwenye NONDO zake humo.
 
Basi mseme tuu kuwa tuongeze bidii kwenye kujifunza English ,na si kusema tunatia aibu wakati tuna lugha zetu huku vyuoni ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…