Wasomi na kiingereza

Wasomi na kiingereza

Swali fikirishi. Ningependa kujua kwanini umeuliza swali hili na Unalenga nini kwa kuuliza swali hili.

#Interesting#jia kuu ya kujua lugha ya watu ishi na hao watu.
Zifuatazo ni sababu za kujua lugha ya watu husika.
1. Kuishi na watu wa lugha husika

Nimemuonyesha ya kuwa hata yeye ameweza kuandika Kiswahili au anakitumia Kiswahili, sababu anaishi au amekuzwa katika lugha hiyo.

2. Sababu hii inarudi katika sababu ya kwanza, ya kuonyesha ya kuwa ni upungufu wa akili kuona ajabu au kumdhihaki mtu msomi ambaye lugha yake ya kwanza ni Kiswahili ila masomo yake amesomeshwa kwa Kiingereza. Anaye tushangaa sisi anafikiria kitoto sababu sisi hatukusomeshwa Kiingereza kama fani ila kwa muda mchache sana ila tumesomeshwa masomo ya fani tofauti kwa lugha ya Kiingereza, hapa kuna tofauti. Ili uwe mzuri wa lugha lazima uitumie kama njia yako ya mawasiliano.

Kadhalika kuna suala la ufasaha au kuwa fasaha wa lugha fulani hili ni jambo kando pia.

Ahsante.
 
Safi sana.

Kwenye hoja nambari moja , Tunajifunza zaidi nje ya darasa kuliko ndani ya darasa.. Mazingira.. Uko sahihi sana..

Japo kwenye hoja nambari mbili.. Sote tunajifunza "Basic Communication Skills" kama tunaamua kujifunza basi tujifunze kweli.. maana iko kwenye Mtaala.. na mimi nachukia mtu kufanya vitu nusu nusu.. ukiamua kufanya kitu fanya kwa utimilifu wake.

Kwa msomi kwenda shule na ashindwe kutengeneza sentensi tatu kwa usahihi ni udhaifu mkubwa sana.. na kukosa nidhamu. (Kwa mtazamo wangu)

Otherwise, Nakubaliana na wewe... interesting observation...
 
Hahahaha! ... Akikuita Asubuhi.. unalaani 😀 unajua zoezi la Ung'eng'e linaanza 😀
Ha haaa hapana, Ni mkubwa kamaliza form four so hanisumbui sana nowdays,akileta ung'eng'e wake namjibu kiswahili.
Tangu ana miaka 4 anaongea kiingereza vzr kabisa
 
Labda tatizo ni viwango vya kuelewa...ama uzingatiaji wa wanachofundishwa
Unakuta shule hiyohiyo moja anatoka mmoja yuko fluent mwingine hajui

Labda tatizo ni viwango vya kuelewa...ama uzingatiaji wa wanachofundishwa
Unakuta shule hiyohiyo moja anatoka mmoja yuko fluent mwingine hajui
Halafu kiingereza hata usome kayumba misingi yake inaanzia huko
Mfano chekechea wanafundisha numbers,matumizi ya this,that,kufahamu vitu KWA kiingereza mfano sabuni-soap
Embe-mango etc

Sasa kadri unavyopanda ndo mafunzo yanapanda mfano wakifika la saba utakuta wanafundishwa tenses,past tense,future tenses.sasa wakizingatia hapa tayari wamejua,wanavuka wanapenda secondary huko ndo kiingereza tupu kwenye kitabu..
Chuo miaka kibao

Mtu anamaliza masters kuandika paragraph ya kujieleza wanapata ugumu?
I think kusoma kiingereza kama somo ndio tatizo.
Hapa naongelea kwa shule za msingi hivyo tunaaungukia kwenye mfumo wa elimu.

Mtoto akiwa na umri mdogo ni rahisi zaidi kumfundisha lugha kuliko akifikia umri mkubwa.
So utakuta mtoto mwenye 6 years anafundishwa masomo yote kwa Kiswahili then anarudi nyumbani anapiga tena Kiswahili vilevile.

Hapo unategema huyo mtoto aje kujua kusoma, kuongea na kuandika kiingereza hapo ni kujiongopea.
Then after 7 years huyohuyo mtoto ghafla anaswap kutoka Kiswahili na kiingereza kama somo la kujitegema mpaka kuwa kiingereza na Kiswahili kama somo linalojitegemea.

Nilisema ni rahisi kwa mtoto kuelewa lugha au vitu vingine vingi kuliko anapofikia umri mkubwa.
Hapa naongelea msingi wa huyo mtoto.

So hapo lazima umchanganye zaidi.
That's why wanafunzi wengi wa secondary wanaishia kukariri instead ya kuelewa walichofundishwa.
And that's why wanafeli sababu wanasahau walichofundishwa na sababu kubwa ya kusahau ni kwa asilimia kubwa sababu walikariri.

Ukikariri always lazima usahau lakini kama ukielewa hata ukisahau.
kile kitendo cha wewe kupata kichocheo cha kitu ulichofundishwa kabla lazima ukumbuke.
That's why utakuta kuna watu ukiwahoji juu ya taaluma zao wenyewe wanagwaya.

Mtu huyohuyo aliyekariri anaendelea kukariri mpaka anamaliza chuo.
Sasa ukitegemea mtu huyo awe na uwezo mzuri wa kuongea, kuandika na kusoma kiingereza utakuwa unamuonea.
Sababu msingi wake ulishajengwa vibaya.

So haitakiwi kuwalaumu bali solution ni kubadilisha mfumo wa lugha uliopo na tuchague moja.
Tutumie Kiswahili or tutumie English kuanzia primary level mpaka secondary level.
I suggest English sababu ni lugha ya kimataifa so ni essential kuijua.
Unless umeplan kujifungia Tanzania milele mpaka kifo chako.

Tatizo ni mfumo wa lugha tunaotumia sasa kwenye mfumo wa elimu.

Mother language haiwezi kupotea kamwe sababu mtoto ataendelea kuitumia mara nyingi akiwa nyumbani.
Au Kiswahili kingepotea miaka mingi nyuma sababu Tanzania kuna lugha zaidi ya 1000 ila Kiswahili bado kipo.
So English ni kitu kidogo sana.

Kama tukiweza kufanya hivyo basi hilo tatizo litapungua kwa asilimia 50.
Labda tatizo ni viwango vya kuelewa...ama uzingatiaji wa wanachofundishwa
Unakuta shule hiyohiyo moja anatoka mmoja yuko fluent mwingine hajui
Naamini kila mtu mwenye ubongo uliokamilika na asiye na tatizo lolote la akili basi huyo mtu ana uwezo sawa na wengine.

Tatizo ni msingi wa huyo mtu upoje.
Msingi ndio unadetermine kila kitu kuhusu mtu huyo.
 
chezea lugha ya malkia wewee, unawza jikojolea hadharan ukiambiwa tuu salimia umati huu kwa ng'eng'e…….
 
I think kusoma kiingereza kama somo ndio tatizo.
Hapa naongelea kwa shule za msingi hivyo tunaaungukia kwenye mfumo wa elimu.

Mtoto akiwa na umri mdogo ni rahisi zaidi kumfundisha lugha kuliko akifikia umri mkubwa.
So utakuta mtoto mwenye 6 years anafundishwa masomo yote kwa Kiswahili then anarudi nyumbani anapiga tena Kiswahili vilevile.

Hapo unategema huyo mtoto aje kujua kusoma, kuongea na kuandika kiingereza hapo ni kujiongopea.
Then after 7 years huyohuyo mtoto ghafla anaswap kutoka Kiswahili na kiingereza kama somo la kujitegema mpaka kuwa kiingereza na Kiswahili kama somo linalojitegemea.

Nilisema ni rahisi kwa mtoto kuelewa lugha au vitu vingine vingi kuliko anapofikia umri mkubwa.
Hapa naongelea msingi wa huyo mtoto.

So hapo lazima umchanganye zaidi.
That's why wanafunzi wengi wa secondary wanaishia kukariri instead ya kuelewa walichofundishwa.
And that's why wanafeli sababu wanasahau walichofundishwa na sababu kubwa ya kusahau ni kwa asilimia kubwa sababu walikariri.

Ukikariri always lazima usahau lakini kama ukielewa hata ukisahau.
kile kitendo cha wewe kupata kichocheo cha kitu ulichofundishwa kabla lazima ukumbuke.
That's why utakuta kuna watu ukiwahoji juu ya taaluma zao wenyewe wanagwaya.

Mtu huyohuyo aliyekariri anaendelea kukariri mpaka anamaliza chuo.
Sasa ukitegemea mtu huyo awe na uwezo mzuri wa kuongea, kuandika na kusoma kiingereza utakuwa unamuonea.
Sababu msingi wake ulishajengwa vibaya.

So haitakiwi kuwalaumu bali solution ni kubadilisha mfumo wa lugha uliopo na tuchague moja.
Tutumie Kiswahili or tutumie English kuanzia primary level mpaka secondary level.
I suggest English sababu ni lugha ya kimataifa so ni essential kuijua.
Unless umeplan kujifungia Tanzania milele mpaka kifo chako.

Tatizo ni mfumo wa lugha tunaotumia sasa kwenye mfumo wa elimu.

Mother language haiwezi kupotea kamwe sababu mtot ataendelea kuitumia mara nyingi akiwa nyumbani.
Au Kiswahili kingepotea miaka mingi nyuma sababu Tanzania kuna lugha zaidi ya 1000 ila Kiswahili bado kipo.
So English ni kitu kidogo sana.

Kama tukiweza kufanya hivyo basi hilo tatizo litapungua kwa asilimia 50.

Naamini kila mtu mwenye ubongo uliokamilika na asiye na tatizo lolote la akili basi huyo mtu ana uwezo sawa na wengine.

Tatizo ni msingi wa huyo mtu upoje.
Kwani Kuna shida akifunzwa kwa kiswahili tuu!?

Wako Watu waliojifunza kichina ukubwani na wamekielewa tunawaweka kundi gani!?

Hebu tujiulize wahindi wanasoma kihindi na wanavumbua na kuunda vitu, Wachina na wajapani vile vile... Tukisoma kiswahili pekee kuna shida gani !?
 
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree, masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa? Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
Unashangaa wakati jiwe ana Phd ila lugha ya malkia inampiga chenga ya mwili
 
Imagine waandishi wa vitabu wangefikiria kama hivi! Kwamba there is not need to follow language rules we can just do whatever we see fit as long as I/we understand.. 🙂

Unadhani ingechukua muda gani kuleta mkanganyiko kwenye urithishaji wa maarifa!?
Pia mtu anaye tunga kitabu ujue yuko na target moja ya kuuza sana (kibiashara),hivyo ni lazima afate utaratibu zote ikiwemo lugha nyepesi, ili kuwafikia watu wengi zaidi,kwa kifupi tulio soma science mtuache jamani .
 
At 95% level of significant,we see that p- value is greater than alpha then we reject null hypothesis.(haya unae jua engine tafsiri hapo)
Kwahiyo wewe hapo umeona hiyo ni "technical English?" Halafu ingekuwa "fluency English" ingeandikwaje?(japo mpaka sasa bado sijui ni kitu gani hiki kiitwacho "techical au fluency English".
 
Kwahiyo wewe hapo umeona hiyo ni "technical English?" Halafu ingekuwa "fluency English" ingeandikwaje?(japo mpaka sasa bado sijui ni kitu gani hiki kiitwacho "techical au fluency English".
yaan ni hivi kuna lugha ya wote ,na kuna lugha wanaelewa watu wa fani husika, ambozo ndizo zina fundishwa kwenye fani nyi ngi za science. Mfano nikisema "R commender" umelewa nini hapo?
 
Kwani Kuna shida akifunzwa kwa kiswahili tuu!
Shida ipo.

Hutoweza kucommunicate na taifa lolote duniani or should I say nje ya africa
Wako Watu waliojifunza kichina ukubwani na wamekielewa tunawaweka kundi gani!?
Well kama ni hivyo basi leo kungekuwa hakuna tatizo la watu wazima ambao ni graduates kushindwa kumudu English sababu hata wao wamejifunza ukubwani for 6 years ukiondoa miaka ya chuo kikuu.

Na hao watu waliojifunza kichina ukubwani ni wangapi au ni asilimia ngapi ya graduates wote?
Hebu tujiulize wahindi wanasoma kihindi na wanavumbua na kuunda vitu, Wachina na wajapani vile vile... Tukisoma kiswahili pekee kuna shida gani !?
Hautoweza kusoma vitu vilivyoandikwa nje ya lugha yako kwa kutumia lugha yako kama hata kutumia hiyo lugha yako ni tatizo na hauwezi.

Tanzania kuna lugha zaidi ya 100 na asilimia 10 tu ya watanzania ndio wanatumia Kiswahili kama main language na 90% wanatumia kama second language.

Sasa hapo hata ukikitumia Kiswahili shuleni effect itakuwa ndogo vilevile na kutakuwa hakuna tofauti na kutumia English at all.

Considering mpaka leo hii tumeshindwa kubadirisha kutoka kiingereza kwenda Kiswahili.
Unadhani tutaweza kutumia Kiswahili wakati hata kubadirisha kwenda Kiswahili tumeshindwa?
Even kutumia lugha yenyewe ya hayo masomo tumeshindwa.

China na India wana lugha nyingi lakini lakini wanaoutimia main languages ni zaid ya asilimia 10.
Hivyo hata wakitumia lugha zao effect itakuwepo.
So kujifananisha nao ni kama kumpa tembo maji anayokunywa mbuzi.

Na kama kufundisha kwa lugha mama kutaleta wavumbuzi.
Kwanini primary Level wanafundisha Kiswahili masomo yote ukiondoa English na hakuna wabunifu au wavumbuzi wadogo?
Usiniambie hakuna wabunifu au wavumbuzi wadogo duniani.

Na mkuu unataka kusema kwamba hizi shule za kata zinafundisha masomo ya English kama inavyotakiwa?
Hapana bali wanatumia English na Kiswahili kwa asilimia kubwa na wanafunzi bado hawaelewi na still hakuna wavumbuzi wala wabunifu labda wapo lakini wapo wapi?.

Kingine ni kwamba wahindi na wachina sio kwamba hawajui kiingereza kabisa hapana wanajua.
Sababu wanajua umuhimu wa kiingereza kwenye kasi ya maendeleo duniani na kushirikiana na mataifa mengine so kiingereza ndio main key kwa kuwasiliana.

Sababu kiingereza kina umuhimu wake duniani au huo umbuzi na ubunifu wetu hautofika popote considering taifa bado masikini na wala hakuna watu wanaojua umuhimu wa ubunifu na uvumbuzi.
Kwani sasa hivi hakuna wabunifu au wavumbuzi watu wazima wa kiafrika?
Hapana wapo lakini huwezi kuwaona wala kuwasikia sababu hata waijitangaza hakuna mwafrika atawaikiliza maybe angetumia English kujitangaza angesaidiwa na watu wanaojua umuhimu wa ubunifu na uvumbuzi.

Na ndio sababu nikasema tatizo lipo.
Sababu hata ukiwa na uvumbuzi kama huwezi kucommunicate na watu wanaojua umuhimu wa uvumbuzi na ubunifu basi utakufa na uvumbuzi wako hapahapa.

Mkuu kiingereza ni essential kwenye ulimwengu wa leo.
 
Back
Top Bottom