Wasomi na kiingereza

Wasomi na kiingereza

Kwa bahati mbaya sana, vijana wa sasa hapa Tz sio tu wanashindwa kuzungumza au kuandika Kiingereza:- Hata Kiswahili wanachoandika au kukiongea mara nyingi sana kina makosa. Ukitaka kujua tatizo ni lugha (iwe Kiswahili au Kiingereza), pitia tu mambo watu wanayoandika wanapochangia mada kwenye mitandao.

a) WENGI SANA hawawezi kutofautisha kati ya herufi L na R. Unamsikia mtu anasema "nilipokuwa nachumbia mahari ambapo mahali ilipelekwa ni kwa mjomba"

b) Ni Watanzania wengi (hata baadhi ya viongozi wanasiasa) wanasema:- "Tangia sasa...." wakimaanisha kuanzia sasa. Hawajui wangepaswa kusema "Tangu sasa", au "kuanzia sasa"

c) Wapo pia watu wengi ambao hawajui the difference between a subject and a predicate (samahani kwa kuchanganya kimombo ndani maana hata mimi yapo maneno ya Kiswahili siyajui - kwa mfano subject and predicate). Nilitaka kusema kwamba watu wengi "wanachanganya mambo" wakati wanazumgumzia mambo mawili tofuati.

Kwa mfano mtangazaji wa habari anasema:- 'Lile gari lilimgonga mtu na kufa" Maana ya mstari huu ni kwamba gari ndio lilikufa. Angetaka kusema mtu ndie kafa angesema "lori lilimgonga mtu akafa"

d) Makosa yapo mengi tu kwenye Kiswahili kinachozungumwa na baadhi ya wasomi wa Tanzania. Kosa lingine ni pale mtoa habari anaposema:- "Alipigwa risasi akaweza kufa" badala ya kusema alipigwa risasi akafa. Unaposema mtu ameweza kitu fulani una maana hicho ni kitu ambacho alikuwa anataka akipate na akajitahidi mpaka akakipata. Hivyo sio sawa kusema mtu aliyepigwa risasi aliweza kufa maana hakuwa anajitahidi kufa.

So, my question to your dear readers is this:- If we can make SO MANYA MISTAKES in Kiswahili which is our mother tongue, do you expect us to be proficient, and efficient in making utterences in a foreign language? No way ! CIAO !

hata mimi yapo maneno ya Kiswahili siyajui - kwa mfano subject and predicate)

Subject ni kiima na predicate ni kiarifu.

Kwa mfano mtangazaji wa habari anasema:- 'Lile gari lilimgonga mtu na kufa"

Hiyo sentensi ipo sahihi na inaeleweka, hiyo inaitwa "sentensi tata" na hata katika lugha zingine sentensi za aina hiyo zipo (Ambiguous sentences).
 
Or just get rid of it.. get better at our Swahili then go ahead and learn something new!?

Kiswahili ndio Uswahili wenyewe(Ustaarabu wa kiswahili).. Utastaajabu wajerumani wangapi hawajui Kiingereza...and it's okay.. but they speak their language very well.. na ni sifa njema na kubwa mtu kuzungumza lugha yao vema.. mpaka wanatoa misaada kuifundisha duniani.

Shida kama tulivyo Watu wa temporary... Grass is always greener on the other side.. tumejikuta kizungu kimekuwa deal kubwaaa.. na kiswahili we can just go ahead and abuse it as much as we want..

Its not right!
The problem is its too late now to turn back with all these changes around the globe for example imagine to change the whole advanced physics in kiswahili how you going to do that it will take very very long time and it may be impossible. Look all the technological advance and note in mind we do not invent them we re just users.
 
Translation can't be word to word... First people need to learn and understand contextually ...then retell the same thing in an understandable way and language.

Ukiwa umesoma physics or chemistry theories na ukawa huwezi kuzieleza kwa kwa ufupi na kwa lugha yako kwa urahisi na usahihi basi hukuelewa kitu.. ila ulifahamishwa na ukakariri.

Translation inawezekana... Japanese, French, Germans, Chinese and Indians did it.. so ugumu siuoni.. ila nitakubaliana na wewe kuwa tunahitaji commitment.
 
Imagine umesoma kayumba hlf unafika chuo unakutana na walimu vilaza anaingia anachomeka flash anasoma slides hana analijua, utafanya nini zaidi ya kukariri?
Tatizo ni elimu yetu kuna sehemu haipo sawa
 
Kujua "WHAT" tumeweza..
Sasa Kimbembe ni "WHY" then "WHERE" and "WHEN"

Usishangae ukakutana na Dr... Amekwama pia.
 
Ha haa ni shida. Kiukweli simcheki asiyejua kiingereza maana na mimi ni zao la kayumba. Nikisoma naelewa vzr hainipi shida, mtu akiongea hata Kama ni mzungu namuelewa vibaya mno, hata mtu akikosea najua kabisa hapa kakosea...ila uniambie niongee fluently..maweeeee
 
At 95% level of significant,we see that p- value is greater than alpha then we reject null hypothesis.(haya unae jua engine tafsiri hapo)
Kuna technical language na english Language for everyday communication purpose.

Kama hukusoma fizikia huwezi kujua misamiati ya Kifizikia. Vivyo hivyo kwa daktari hawezi kuielewa Lugha ya Wasanifu majengo...

That has nothing to do with English language comprehension skills ..ila ni tatizo la uelewa wa kitaaluma na lugha yake.
 
Jambo la msingi majuku yanaenda, kingereza siyo issue sana.
 
Ha haa ni shida. Kiukweli simcheki asiyejua kiingereza maana na mimi ni zao la kayumba. Nikisoma naelewa vzr hainipi shida, mtu akiongea hata Kama ni mzungu namuelewa vibaya mno, hata mtu akikosea najua kabisa hapa kakosea...ila uniambie niongee fluently..maweeeee
Hahaha! Kuwa Fluent kwenye lugha yoyote ni zao la mazoezi..bila mazoezi ufanisi unapungua...

Sasa sisi tunashinda Masasi mjini, kazi inanikutanisha na Na waswahili wenzangu tuu miaka 20 unataka niwe Fluent kwenye kizungu cha kusema naanzia wapi.

Cha kusikia utasema at least nitaangalia sinema.. cha kuongea labda useme mwenyewe kama mwehu.. 🙂

Kama unasikia inatosha.. na kama unaweza kuweka sentensi moja moja kuhakikisha ujumbe wako unafika.. ubarikiwe.. kikubwa lugha yako moja.. jitahidi uwe Fluent.. na ufahamu kuiandika kwa ufasaha.. basi.
 
Kujitahidi kuwa fluent ni kazi ya ziada, kwasasa sifanyi shughuli inayonitaka niongee kiingereza yaani hata sikutani na anaeongea kiingereza kwa mazingira niliyopo. Ila mwanangu anatema ung'eng'e kama Barack Obama vile
 
The problem is its too late now to turn back with all these changes around the globe for example imagine to change the whole advanced physics in kiswahili how you going to do that it will take very very long time and it may be impossible. Look all the technological advance and note in mind we do not invent them we re just users.

It is not too late at all rather it is too early.

With all the technologies around us it is a ripe time to start translating the scientific books from English etc, into kiswahili, only what we have to do, so as to make the job easy, is to leave all technical jargons intact and concentrate on the normal auxiliary words.

During the 15 century in England, the medium of instruction in higher learning institutions Latin was used the same as we use English in our Schools and colleges, when they managed to switch to English as medium of instruction, they left intact many latin technical words (jargons). We have to imitate the same way in order to make Kiswahili as medium of instruction in our schools and colleges.

The words like computer and names of diseases and medicines, the nanes like Velocity, momentum, acceleration, mass etc, have to be left intact.

Eg, My car having 2000kg mass travelled a distance of 500 metre at a velocity of 4 metres per second.

In kiswahili: Gari langu lenye mass (masi) ya kilo 2000 ilisafiri umbali wa mita 500 kwa velocity (velosite) ya mita 4 kwa sekunde.

As you can see, the words remained intact are mass, Velocity, sekunde.

That is an example of what should be done in the course of translation.

It is said by pychologists that a man understands things better in his "mother tongue" than in a learned language.

It is high time to use Kiswahili in our schools as medium of instruction, kiswahili is a number 2 in highly spoken languages in Africa. Why not now???
 
Kujitahidi kuwa fluent ni kazi ya ziada, kwasasa sifanyi shughuli inayonitaka niongee kiingereza yaani hata sikutani na anaeongea kiingereza kwa mazingira niliyopo. Ila mwanangu anatema ung'eng'e kama Barack Obama vile
Hahahaha! ... Akikuita Asubuhi.. unalaani 😀 unajua zoezi la Ung'eng'e linaanza 😀
 
It is not too late at all rather it is too early.

With all the technologies around us it is a ripe time to start translating the scientific books from English etc, into kiswahili, only what we have to do, so as to make the job easy, is to leave all technical jargons intact and concentrate on the normal auxiliary words.

During the 15 century in England, the medium of instruction in higher learning institutions Latin was used the same as we use English in our Schools and colleges, when they managed to switch to English as medium of instruction, they left intact many latin technical words (jargons). We have to imitate the same way in order to make Kiswahili as medium of instruction in our schools and colleges.

The words like computer and names of diseases and medicines, the nanes like Velocity, momentum, acceleration, mass etc, have to be left intact.

Eg, My car having 2000kg mass travelled a distance of 500 metre at a velocity of 4 metres per second.

In kiswahili: Gari langu lenye mass (masi) ya kilo 2000 ilisafiri umbali wa mita 500 kwa velocity (velosite) ya mita 4 kwa sekunde.

As you can see, the words remained intact are mass, Velocity, sekunde.

That is an example of what should be done in the course of translation.

It is said by pychologists that a man understands things better in his "mother tongue" than in a learned language.

It is high time to use Kiswahili in our schools as medium of instruction, kiswahili is a number 2 in highly spoken languages in Africa. Why not now???
We can Do it..

Lakini lazima tuanze kwa dhamira ya kutokushindwa.
 
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree, masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa? Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
Wewe umewezaje kuandika au kuongea Kiswahili ?
 
Back
Top Bottom