Tunaambiwa kuwa wengi wao wamesoma kwenye Ivy League Universities na wengine walifanya kazi World bank na of course wengine wanastahili kuchukua nafasi ya Ugavana.....tangu JK achukue nchi kwa nini idadi ya wanaopitisha mizigo Bandari ya Mombasa imeongezeka kuliko wanaotumia Bandari ya Dar...
Unajua kuna kitu ambacho waafrika wengi huwa wanachanganya au tunachanganya ni Usomi wa vyeti, akili za darasani, utendaji wa kazi, kufikiria na uongozi kwa ujumla. Shule au elimu ya mtu huwa haiongezi akili au uelewo wa mtu, kitu kinachotakiwa kiongezeke ni kufikiria (ku reason) katika angle tofauti tofauti na bila kuwa na upendeleo wowote katika hizo fikra mpaka upate jibu au majibu.
Hao wachumi inawezekana wemeenda Oxford au Havard, na wakafanya World Bank, je akili zao za darasani ziliwaongezea busara ya kufikiria, kutafakari na kuweza ku manage kwenye crisis??, Wengi labda walikuwa World Bank je walikuwa viongozi au walikuwa decision makers?....Inawezekana kabisa kule WB walikuwa wanachangia kwenye utafiki uliolekea ki elimu zaidi na siyo kutatua matatizo ya kila siku, na hili ndilo tatizo ambalo linasabisha watanzania hadi leo tuwe tunateseka, hatutofautishi ufanisi wa kazi (real world)na ufanisi ki elimu ki-falsafa)
Nakumbuka Profesa Mbilinyi alipopewa wizara ya Fedha ilikuwa mbinde, kwani hata kule TRA rushwa ndipo ilipojengaka hadi leo hii. Mtu huyuhuyu alikuwa mzuri kwenye elimu (academiics), ila kwenye real work (kazini) hakuweza kuoanisha theory anazofundisha wanafunzi, research zake, kazini na mahusiano yake na mtanzania wa kawaida mtaani. Matokeo yake ndiyo haya.
Hivyo basi hao wachumi wa JK inawezekana kabisa wao ni academicians tu. Kutafakari ili nchi iende mbele kwao inakuwa shida hususan kwenye practice.
Ukingalia Ma katibu wakuu wa wizara na mawaziri wengi wengi wana PhD na Masters, Ma MBA ndo usiseme, vitu wanavyovifanya haviendani na hizo shahada zao, je ni kwanini?- Mimi husema wengi ni wazito wa kufikiri au kupambanua vitu kati ya elimu na maisha ya watu wawatumikiao- nahisi wengi shuleni walikuwa wana nukuu tu bila kujua maana halisi.
Tatizo jengine ni kuwa wasomi karibu wote lengo lao la mwisho siyo kuwa magwiji wa elimu walizosomea bali kuwa wanasiasa- yaani wanalimbikiza shahada nyingi ili waweze ingia kwenye siasa, kwa sababu hizo hizo wanakuwa hawawezi fikiria tofauti na kiongozi wao ( mfano JK) aliyewachagua kwani watamwaga unga. We nambie nani anaweza mwambia JK apunguze safari katika hao washauri wake?, wao wenyewe wanataka wakafanye shopping huko na kupalilia unga wao.