Washauri wa JK wa UCHUMI

Mimi nadhani mheshimiwa rais hawasikilizi washauri wake wa masuala ya kiuchumi(naamini wapo na wana qualifications nzuri tu).

Tukumbuke kuwa huyu rais anapenda umaarufu usiokuwa na maana, "mwenzetu", "mcheshi na wote", "mtu wa watu"...hayuko serious hata kidogo, well at least he is serious when it comes to his hobby, globe-trotting!
 
Sidhani kama kuna rais wa Tz ambaye alikuwa anasikiliza washauri wake wa uchumi, hapa kwa kiasi namtetea JK, si kwamba anafanya vizuri, bali tu kwa sababu anaendeleza utamaduni wa marais wetu- tangia awamu ya kwanza!- Kisa cha G Mtei mnakikumbuka? nadhani karibu wote yaani awamu zote wanaishia kupewa jila la Haambiliki!
 
Thanx GAME coz umekuja na very interesting topic ambayo binafsi yangu ilikuwa inausumbua mtima wangu kwa mda mrefu.Nakubaliana kimsingi na wale wachangiaji ambao wamesema kuwa academic qulifications per se cant me potential ya mtu katika actual ground,thats true lakini je kwa washauri wa JK wana potential kiasi gani on the actual ground?, what so far this fellas have achieved kiasi kwamba tukawaamini kuwa washauri wa part nyeti kama hii?
For the poor nchi like tz you appoint a 3yrs woman who specialize in financial markets to advise you on the the way forward for the crippling economy like ours, ivi are serious wewe?, au ndo dhana ya "ushkaji" inaendelea hadi kwenye foundation of development kama tunavyoshudia?,can she interacts "wakaelewana vizuri" na Dr Gregory Mankiw[chief ec. advisor wa Bush] au Pro. Wiseman Nkhulu[EC ADVISOR WA MBEKI]?......kwa hali hii jamani ivi hii "ndege" itapaa kweli? au itapaa na wachache?,nahisi kama kwanza wameshaizima kabisa hawa jamaa.
 
To serve the master!...Kumtumikia bwana.

wanabodi ningependa sana kuelewa ethics za kazi kwa mtumwa wa bwana...hasa kwa wale mnaojua taratibu za washauri wa Masultan, malkia na wakoloni ktk kumtumikia bwana ulikuwa ukienda vipi na nini nafasi ya mshauri wa kiongozi ktk kuleta mabadiliko ya aina yeyote hasa pale mtawala anapokuwa na dream yake mwenyewe. Je, utajenga mikakati inayouwiana na malengo ya mtawala ama unafanya kile unachofikiria kuwa nibora hata kama kinapingana na fikra za mtawala. Tukumbuke lile neno zidumu fikra za mwenyekiti!...
Nakumbuka pia sinema ya King of Scotland yule mzungu alokuwa mshauri mkuu wa Idd Amin ambaye katoa sinema akijaribu kujikosha kuwa yeye alikuwa daktari tu, hali Waganda wote wanafahamu mchango wake ktk Utawala wa Idd Amin. waganda wanamsifia sana lakini ukienda ktk maswala ya kimataifa Idd Amin alikipaka kishenzi na huyu mzungu tunamtazama kwa mchango wake nje ya mtazamo wa Waganda wenyewe.
Je, alitakiwa kutofautiana na Idd Amin kimawazo hata kama inge cost kazi ama maisha yake? ama kumtumikia bwana siku zote fuata unalo ambiwa.
Hapo hapo nimetazama hali iliyoko Zimbabwe, hivi ukichaguliwa kufanya kazi chini ya Utawala wa Mugabe, utafanya nini hasa ili uweze kuonekana tofauti na Mtawala dhalimu kama Mugabe..mfano huu unaendelea kunitatiza pale napofikiria Coup ambayo huwachanganya watumwa wa bwana kuwa ni kundi moja na mtawala.. Je, ni wakati gani mtumishi unaweza kumwambia master wake sitaki kazi ama jukumu fulani kwa sababu sikubaliani na utawala wako. Where do U draw the line ktk utumishi wako kwani kushiriki/kutoshiriki kwako ni sehemu ya kuiangamiza nchi vile vile..hapa hata ukiweka sura mbili zote bado mchango wako kivitendo ni muhimu zaidi. Wazimbabwe wengi wamesimama kupinga Utawala leo wanakufa njaa kwani hakuna uzalishaji kabisa.
Kwa wale ambao wameisha wahi fanya kazi chini ya tawala wasizokubaliana na malengo ya kiongozi wao ni njia zipi bora ambazo unaweza zifanya ili kuhakikisha kwamba malengo yale mabaya yanakoma bila kuathiri Umma kwa ujumla.
Ukiacha kazi na kuwa against kama kina Kambona ndio kwanza unawapa nafasi ya kuendeleza mabaya yao na Umma ndio wakaokuwa victims, na pengine utaitwa wewe msaliti pande zote mbili yaani ktk Utawala na wananchi wenyewe ulowaacha ktk mataa.
What is the best way (weapon) to fight the POWER!
 
Back
Top Bottom