Makampuni ya China yasaidia Afrika kuendeleza uchumi wa kidijitali

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
111
VCG111437121553.jpg
Katika msimu uliopita wa ununuzi wa Krismasi na mwaka mpya, Kilimall imekuwa jukwaa la biashara la mtandaoni linalopendedwa zaidi na wateja wengi nchini Kenya, kutokana na bidhaa zake bora na zenye bei nafuu, pamoja na huduma nzuri ya kupeleka vifurushi.

Kilimall iliyoanzishwa na mfanyabiashara wa China mwaka 2014, ni jukwaa la kienyeji la biashara la mtandaoni nchini Kenya. Hadi sasa, idadi ya watumiaji waliojiandikisha kwenye jukwaa hilo imezidi milioni 10. Mbali na Kenya, Kilimall imeanzisha shughuli nchini Uganda na Nigeria.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kudidimika kwa uchumi wa dunia, nchi nyingi za Afrika zimechukulia uchumi wa kidijitali kama injini mpya ya kukuza maendeleo.

Ripoti ya uchumi wa kidijitali barani Afrika iliyotolewa mwaka 2020 na Benki ya Dunia inakadiria kuwa uchumi wa mtandaoni wa Afrika unatarajiwa kufikia dola bilioni 180 za Kimarekani ifikapo mwaka 2025, ikiwa ni asilimia 5.2 ya pato la bara hilo (GDP).

Hata hivyo, wakati huo huo, Afrika bado inakabiliwa na pengo la maendeleo ya uchumi wa kidijitali ikilinganishwa na mabara mengine duniani. Moja ya sababu kuu ni kwamba Afrika haina makampuni makubwa yanayoweza kuongoza maendeleo ya uchumi wa kidijitali.

China na Afrika zimedumisha uhusiano na ushirikiano wa kirafiki, na China ni mshirika mzuri wa Afrika katika kuendeleza uchumi wa kidijitali. Licha ya hayo, China ina uzoefu mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa kidijitali, na ina makampuni mengi ya kidijitali yenye nguvu kubwa na teknolojia za juu, ambayo inaweza kuzisaidia nchi za Afrika kupata maendeleo katika uchumi wa kidijitali.

Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa kidijitali umekuwa mwelekeo mpya kwa China kuunga mkono maendeleo ya Afrika, ambapo makampuni ya China yametoa mchango zaidi.

Wakati wa janga la COVID-19, idadi kubwa ya makampuni ya kidijitali ya China, ikiwa ni pamoja na Alibaba, yameongeza shughuli katika soko la Afrika, na kutoa msaada wa teknolojia na uzoefu kwa nchi za Afrika ili kufufua uchumi.

Ushirikiano husika kati ya China na Afrika umeingia katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya uchumi wa kidijitali barani Afrika.

Mwezi Juni mwaka jana, Kampuni la Cainiao Network, ambalo liko chini ya Shirika la Alibaba la China, lilifungua njia ya kwanza ya kusafirisha vifurushi ya kuvuka mpaka kati ya China na Afrika, ambayo ilirahisisha kwa kiasi kikubwa biashara kati ya pande hizo mbili.

Meneja mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Nje cha Cainiao, Xiong Wei, amesema biashara ya mtandaoni kati ya China na Afrika inakua kwa kasi, na ina mustakabali mzuri. Kuhusu suala la kuongeza mauzo ya bidhaa za Afrika kwa China ambalo linafuatiliwa sana na nchi za Afrika, makampuni ya China barani Afrika pia yana mkakati wa muda mrefu.

Meneja wa masoko wa Kilimall Lu Xiaoyong amesema nchi nyingi za Afrika zinazalisha mazao ya kilimo ya hali ya juu, na zinataka kuyauza katika soko la China. Katika siku zijazo, Kilimall itasaidia nchi za Afrika kufanya hivyo kupitia tovuti yake.

Ushiriki wa makampuni ya China katika maendeleo ya uchumi wa kidijitali barani Afrika umekaribishwa na kupongezwa. Kamishna wa Miundombinu na Nishati wa Umoja wa Afrika Abu-Zeed Amani amesema Afrika inatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi wa kidijitali na China ili kukuza mafungamano wa uchumi wa Afrika.

Mtaalamu mwingine wa kifedha wa Afrika anaamini kwamba katika sekta nyingi za uchumi wa kidijitali, hasa katika teknolojia za malipo mtandaoni, makampuni ya China yanaongoza duniani. Nchi za Afrika zinaweza kujifunza mengi kutoka kwa makampuni ya China, hii ni muhimu sana kwa Afrika, na uchumi wa kidijitali ni fursa nyingine nzuri kwa kukuza ushirikiano kati ya China na Afrika.
 
View attachment 2869203Katika msimu uliopita wa ununuzi wa Krismasi na mwaka mpya, Kilimall imekuwa jukwaa la biashara la mtandaoni linalopendedwa zaidi na wateja wengi nchini Kenya, kutokana na bidhaa zake bora na zenye bei nafuu, pamoja na huduma nzuri ya kupeleka vifurushi.

Waafrika tunapenda habari za umbeya izi wachangiaji ni wachache sana. Wengi maswala ya kiuchumi wapo zero Akili
 
Back
Top Bottom