Washauri wa JK wa UCHUMI

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
832
Tunaambiwa kuwa wengi wao wamesoma kwenye Ivy League Universities na wengine walifanya kazi World bank na of course wengine wanastahili kuchukua nafasi ya Ugavana

Hivi tangu JK achukue nchi kwa nini idadi ya wanaopitisha mizigo Bandari ya Mombasa imeongezeka kuliko wanaotumia Bandari ya Dar

Strange enough mtu yuko radhi atoe mpaka laki tatu zaidi kule Mombasa na kuipa revenue jamaa wa KRA kuliko TRA na wakaguzi wao

Hivi kama hao washauri wa Uchumi wanashindwa kushauri kuhusu urasimu pale bandari Dar au Airport what makes you think hawa jamaa ni washauri wazuri?

Hawa jamaa kila kukicha wanamshauri rais aende kwenye mikutano isiyo na kichwa wala miguu ulaya na America lakini matunda mbona hatuyaoni?

Hamuoni kuwa media Tanzania wanaconspire ili kuendeleza political elite na nadhani tuanze na hawa jamaa wanaomshauri JK kwenye uchumi. In short jamaa sioni cha maana walichomshauri na zaidi mpaka leo sielewei kulikuwa na umuhimu gani wa kupewa msaada wa kujengewa uwanja wa mpira wa mamilioni wakati tungeomba msaada yw akujengewa kilimita kadhaa za bara bara kule Bukoba ambako mpaka leo bado wana makovu ya vita and of course walisufffer zaidi.

sasa sijui tatizo liko wapi? inawezekana ikawa JK ni mbishi kufuata ushauri au washauri wake wa uchumi wote ni BOMU

wenzangu mna maoni gani kuhusu hili
 
GM

Refer kwenye thread ya bodi ya wachumi Tanzania. In short ninaweza kusema either people are not doing their work properly ama politics inaingilia na kuweka kando taaluma ya wachumi.
 
Tunaambiwa kuwa wengi wao wamesoma kwenye Ivy League Universities na wengine walifanya kazi World bank na of course wengine wanastahili kuchukua nafasi ya Ugavana.....tangu JK achukue nchi kwa nini idadi ya wanaopitisha mizigo Bandari ya Mombasa imeongezeka kuliko wanaotumia Bandari ya Dar...

Unajua kuna kitu ambacho waafrika wengi huwa wanachanganya au tunachanganya ni Usomi wa vyeti, akili za darasani, utendaji wa kazi, kufikiria na uongozi kwa ujumla. Shule au elimu ya mtu huwa haiongezi akili au uelewo wa mtu, kitu kinachotakiwa kiongezeke ni kufikiria (ku reason) katika angle tofauti tofauti na bila kuwa na upendeleo wowote katika hizo fikra mpaka upate jibu au majibu.

Hao wachumi inawezekana wemeenda Oxford au Havard, na wakafanya World Bank, je akili zao za darasani ziliwaongezea busara ya kufikiria, kutafakari na kuweza ku manage kwenye crisis??, Wengi labda walikuwa World Bank je walikuwa viongozi au walikuwa decision makers?....Inawezekana kabisa kule WB walikuwa wanachangia kwenye utafiki uliolekea ki elimu zaidi na siyo kutatua matatizo ya kila siku, na hili ndilo tatizo ambalo linasabisha watanzania hadi leo tuwe tunateseka, hatutofautishi ufanisi wa kazi (real world)na ufanisi ki elimu ki-falsafa)

Nakumbuka Profesa Mbilinyi alipopewa wizara ya Fedha ilikuwa mbinde, kwani hata kule TRA rushwa ndipo ilipojengaka hadi leo hii. Mtu huyuhuyu alikuwa mzuri kwenye elimu (academiics), ila kwenye real work (kazini) hakuweza kuoanisha theory anazofundisha wanafunzi, research zake, kazini na mahusiano yake na mtanzania wa kawaida mtaani. Matokeo yake ndiyo haya.

Hivyo basi hao wachumi wa JK inawezekana kabisa wao ni academicians tu. Kutafakari ili nchi iende mbele kwao inakuwa shida hususan kwenye practice.

Ukingalia Ma katibu wakuu wa wizara na mawaziri wengi wengi wana PhD na Masters, Ma MBA ndo usiseme, vitu wanavyovifanya haviendani na hizo shahada zao, je ni kwanini?- Mimi husema wengi ni wazito wa kufikiri au kupambanua vitu kati ya elimu na maisha ya watu wawatumikiao- nahisi wengi shuleni walikuwa wana nukuu tu bila kujua maana halisi.

Tatizo jengine ni kuwa wasomi karibu wote lengo lao la mwisho siyo kuwa magwiji wa elimu walizosomea bali kuwa wanasiasa- yaani wanalimbikiza shahada nyingi ili waweze ingia kwenye siasa, kwa sababu hizo hizo wanakuwa hawawezi fikiria tofauti na kiongozi wao ( mfano JK) aliyewachagua kwani watamwaga unga. We nambie nani anaweza mwambia JK apunguze safari katika hao washauri wake?, wao wenyewe wanataka wakafanye shopping huko na kupalilia unga wao.
 
sasa sijui tatizo liko wapi? inawezekana ikawa JK ni mbishi kufuata ushauri au washauri wake wa uchumi wote ni BOMU

wenzangu mna maoni gani kuhusu hili

Inawezekana yote, lakini nafikiri la ubishi ni zaidi. Viongozi wetu wanapenda kushauriwa vile wanavyofikiri tayari. Hii imewafanya washauri wetu wawe vilaza maana badala ya kuhangaika kutafuta data za maana wao wanahangaika kutafuta majungu ya kikada ya kumfikishia Rais. Mbaya zaidi washauri wetu ni mahodari sana wa kusifia badala ya kushauri, kwa hiyo akina JK wana mengi ya kujifunza kutoka hapa JF kuliko kwa washauri wao.
 
Kuna conflict kubwa sana kati ya uchumi na siasa!

Ushauri wa kiuchumi huwa uko very unpopular kwa wanasiasa. Zama hizi za JK ni zama za wana siasa wanaopenda umaarufu na hawako tayari kuona huo umaarufu wao unayeyuka.

Mfano, mabilioni ya JK, viongozi walitaka yatolewe bila masharti as if ni sadaka na kumbe ilikuwa ni mikopo yenye masharti nafuu. Baadhi ya benki ziligoma uwakala mpaka pale serikali ilipotoa tamko jingine kwamba kuna masharti ya kujaza fomu za maombi na bla bla za hapa na pale.

Kuwa mshauri wa wana siasa ambao wanapenda umaarufu ni kazi ngumu sana. Najua kuna mengi ambayo wanashauriwa lakini huwa hawayatekelezi (ubishi), kwa kuwa wanajua kwamba wakiyatekeleza yatashusha umaarufu wao. Wachumi walio makini ili ku-avoid kuharibu credibility yao huwa wanaamua kujiuzulu, kama alivyofanya marehemu J. Rweyemamu zama za Mwalimu Nyerere (RIP).

Serikali nyingi za Afrika zilisita sana kukubali muarobaini wa IMF/WB wakati wa economic reforms na hasa kipengele cha kupunguza civil servants. That was very unpopular na hasa kwa nchi iliyokuwa inaelekea kwenye uchaguzi, unaweza kupoteza urais ivi ivi, japo ulichoshauriwa ni cha kweli na muhimu.

Ili kupunguza hizo conflict washauri wazuri wanatakiwa kuwa wamesoma political economy ambayo huwasaidia kufanya analysis katika pande zote mbili, yaani anaangalia impact ya ushauri wake kisiasa na kiuchumi. Then baada ya hapo anachukua position ambayo itamuacha mshauriwa (Rais) kwenye nafasi nzuri bila kuharibu sana uchumi na kutojiharibia kisiasa. Pamoja na hayo ni ngumu kiasi, maamuzi mengi ya kiuchumi yana madhara makubwa kisiasa!
 
Unajua kuna watu mpaka leo nikiwauliza kwa nini wanaprefer kutumia Bandari ya MOmbasa kutoa mizigo yao wanipa straiht answers:

1) Hakuna Urasimu kama Dar

2) Unaweza kutoa Lori au kontena lako on the same day

3) wako radhi kuingia Gharama mpaka laki tano zaidi kuliko milioni 2 au 3 ambazo wangezitoa Dar

sasa sidhani kama mtu unatakiwa uwe economist toka UNIVERSITY OF CHICAGO ukaelewa kuwa BANDARI zetu zime jaa urasimu usio na kichwa wala miguu

Kwa nini TRA na wale COTECNA (kama bado wapo) wasiwe na ofisi kule Bandarini na kama wanahitaji info basi computer zipo kufanya hilo)

Suala lingine mimi sielewi kwa nini Mtu akishusha mizigo ZANZIBAR anaambiwa lazima alipe tena ushuru Dar? na kwa nini ukiwa na gari uliloligomboa ZNZ unaambiwa eti namba plates za ZNZ huwezi kuzitumia Dar zaidi ya miezi sita (if i am not mistaken)

Na sielewi kwa nini tenda ya kutengeneza namba plates alipewa mke wa kigogo exclusively (sina hakika kama upuuzi huu bado unaendelea)

hivi mnajua kama airport DAR wanasema kuwa hii monitor ya APPLE COMPUTER ni kifaa cha sinema hivyo lazima ulipie kodi ya SINEMA!
specs_top20071026.jpg

mambo madogo madogo kama haya ndiyo kero zenyewe na hata MEMBE analijua hili
 
...

Hivi tangu JK achukue nchi kwa nini idadi ya wanaopitisha mizigo Bandari ya Mombasa imeongezeka kuliko wanaotumia Bandari ya Dar

...

Hivi kama hao washauri wa Uchumi wanashindwa kushauri kuhusu urasimu pale bandari Dar au Airport what makes you think hawa jamaa ni washauri wazuri?

...
sasa sijui tatizo liko wapi? inawezekana ikawa JK ni mbishi kufuata ushauri au washauri wake wa uchumi wote ni BOMU

wenzangu mna maoni gani kuhusu hili

Yaani hii inasikitisha sana, kisa cha tanzania kukosa biashara yote hii ni kuhakikisha mtu mmoja anaweka ndani faida yote ndogo inayopatikana bandarini.

Hivi mifano hai tu kama enzi za urasimu wa usafiri Dar, ambapo UDA peke yake ndio ilikuwa ikisafirisha watu bongo, matokeo yake ilifika wakati huduma za usafiri zikakuwa mbaya sana, hawa hawawezi ku-relate na kuona kwamba urasimu unaua huduma? hapo haitajiki hata mshauri mmoja ni huyo decision maker kuona kwamba hii ya urasimu itaharibu huduma, he probably knew it, lakini kwa sababu anazozijua na kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kumsuta katika hili au wote walikuwa ni washirika basi liwalo na liwe tenda anapewa mtu mmoja tu bila kuzingatia matokeo.

Imagine huduma ya simu za mikononi ingekuwa inatolewa na shirika moja tu, je communication ingefika hapa tulipo?na bei zingekuwa affordable kama sasa? Mifano kama hii kuweza kuiona na ku-relate kwenye biashara nyingine wala haihitaji digirii ya oxford wala mama yake oksfod.

Kama kusingekuwa na urasimu pale Dar, basi ujue ajira kibao zingepatikana kwa ajili ya bandari na huduma ingekuwa safi, hapo JK wala hana haja ya kukuna kichwa kuhusu utengenezaji wa ajira ni kuweka mifumo tu ya kinamna fulani halafu ana-relax na ajira zinajitengeneza zenyewe na watu wanachakarika na kupunguza umasikini.
 
Old-fashion communism is intact in the system of administration in most public (even private) organizations.
 
HII NI HOJA NZITO,IJADILIWE KWA UMAKINI WAKE,HII BANDARI IMEKUWA KERO KWA MDA MREFU SASA.IN GENERAL THE WHOLE SYSTEM IS CORRUPT,WATZ IN MOST CASES HAWAJUI KUTOA HUDUMA SAFI,THEY ARE NOT ACTIVE HATA UMLIPE MAMILION SIJUI KWA NIN?WANALIZIKA NA DHARAU KWA WANAOWAUDUMIA,this is a bad culture in deed.nakumbuka Bwana Mkapa alikuwa amerudisha heshima ya kazi,mda wa kuingia kazin na kuondoka and effectiveness of time at work,hii ideology ya kasi mpya imekuwa vice versa INAKATISHA TAMAA KWAKWERI
 
Yote yatawezekana kama Siasa itabakia kwa wana Siasa na watendaji maofisini waache kuingiliwa na siasa na wao kuchukuliwa msukule na kuimba kasi mpya huku wakijua wanalitumikia Taifa na si watu wa kasi mpya pekee. Unaona wameharibu kila kitu hata Maximo kaamua kuingia siasa badala ya kufundisha mpira kazi kubwa TZ.
Wasomi na wachumi ni wa majina na kutanguliza Dr.,Prof nk lakini reasoning na kuchapa kazi ney
 
Nashukuru kwa aliyeanzisha hii mada. Mimi ni mwathirika wa haya yanayosemwa hapa. Nina kagari kangu nimeagiza huko Japani. Meli imekuja imekosa mahali pa kupakulia imekaa nje ya Badari kwa karibia siku kumi imeamua kuondoka kwenda kupakulia Afrika kusini. Wapo watu ambao wameagiza vitu kwa ajili ya x-mas hadi sasa hizo kontena hazijatoka kuna mtu mmoja kaniambia alikuwa ameagiza Christmas Tree kontena lilifika hapa mwezi wa 12 mwanzoni hadi sasa hajaweza kutoa sijui atauza lini Christmas Tree.
Jamani msifanye mzaha mzaha ni swala kubwa kuliko watu wanavyoongea. Wapo watu wa Zambia wamekaa hapa zaidi ya wiki 3 wanasubiri meli zipakue bidhaa zao lakini bado haiwezekani.
Kwa sasa navyoandika nimetokea huko Bandarini kuna Meli 7 zipo zinasubiri mahali pa kuegesha ili zipakuliwe. Nimejaribu kuwadadisi watu pale wamesema labda hizo meli zitapakuliwa baada ya wiki 3 kwani kwa kawaida Meli moja inapakuliwa kwa siku 3.
Tatizo ni Lipi?
1. Tatizo lililo kubwa kuliko yote ni Vifaa vya kupakulia kuna Kampuni inaitwa TICS ya Mheshimiwa Sana Karamagi. Tangu Mwaka mwezi wa nne imekuwa ni stori ndefu kuwa watakuwa wameleta vifaa vya kisasa ifikapo mwezi wa nane, hadi sasa ni stori tuu.
2. Tatizo lingine ni sehemu ya kuyaweka hayo makontena. Wadau mbalimbali wameshakaa kwenye vikao zaidi ya 30 kujadili hilo ikakubalika kuwa zitafutwe Bonded warehouse nje ya bandari na maeneo kadhaa yameshapatikana ila sasa utekelezaji wake imakuwa ni hadidhi, kwa hiyo wanataka kontena ziendelee kukaa pale ili ulipe storage kubwa kwa hiyo hapa kuna kamchezo fulani kanachezeka kuongeza mapato kisirisiri.
3.COTECNA nao wamekuwa kero yaani wanaona kila kitu ni cha wizi kama wao walivyozoea. hawawezi kukubali kuwa mtu anaweza kununua kitu kwa bei iliyopo kwenye invoice watakusumbua weee hadi utoe rushwa kwa kweli ni tabu tupu.

Naomba tuijadili hii mada kwa umakini zaidi. Uchumi wa Nchi unashuka kwa upuuzi wa watu wachache tuu. Kwa nini wazaire, wazambia wapitishe mizigo Mombasa? ni shilingi ngapi tunapoteza hapo?
Wewekezaji unaenda kuwatafuta wa kufanya nini? watapitisha wapi hiyo mizigo yao?
Washauri wa Muungwana mwambieni huyo mtu aweke kwanza mambo ya ndani sawa kisha ndio atoke nje.
 
Kama bado wanaendelea kukwamishwa basi nicheki kwenye PM nikupe contacts za Mombasa na mambo yako yatakuwa safi maana bora zikutoke pesa kwa wale wakenya lakini mizigo yako inatoka same day bila upuuzi wa kuzungushana na COTECNA na TRA. Na usiwe na wasi wasi na Horo horo huko nako nitakusort out

Tanzania ni ubabaishaji tu siku zote- JK na Lowasa sijui wako wapi na wanatamba nini -eti ndege sasa inapaa!

Aibu tupu!!!!!

Iko siku haya mambo yatabadilika! Tumechoka sasa!
 
Kwanini wasiweke ushindani kwa kampuni ya Karamagi?

I dont think kama tatizo ni KARAMAGI bali ni MENEJIMENTI NZIMA YA BANDARUI YA DAR...ninamaana kuanzia BODI YA BANDARI, MENEJA MKUU na of course MARKETING MANAGER WAO WA SASA
 
Hivi jamani ni lini tulikuwa na washauri wazuri wa kiuchumi na huduma zipi za kiuchumi zilikuwa nzuri kama mnakumbuka..Mimi sioni ndani kabisa!
Hilo la UDA kusema kweli mimi sikubaliani nalo kuwepo hapa kama mfano kwa sababu ninaamini kabisa kuwa usafiri wa mijini ni huduma inayotakiwa kuwa chini ya halmashauri na shirika moja tu kwa kila Halmashauri ama mkoa kama ni mdogo. Daladala ni ugonjwa mbaya sana na unaleta umaskini zaidi yaani ndio kurudi nyuma huko at the same fare or more ni bora nipande bus la UDA mara kumi kuliko adha za daladala.
UDA haikufanikiwa kutokana na mengi sana na pengine swala la huduma mbaya ktk Bandari yetu linatokana na kuwepo mashirika mengi yenye mkono ndani yaani huwezi kutoa kitu bila kupitia kwao kiasi kwamba hujui nani wa kumlaumu. Ukiritimba kila sehemu na sasa hivi imekuwa kila sehemu unapokwenda huwezi kupata kitu hadi upitie kwa mjumbe, mara Ofisi fulani ni muwakala na kadhalika. Nafikiri sina uhakika bandari ya Mombasa kila kitu kipo wazi na mambo yote yanakwenda pale pale bandarini bila wewe kwenda huku na kule mikono kibao...
Ni mawazo yangu tu, tukirudi ktk swala la washauri wa rais ktk Uchumi wazee yote mliyoyasema yanachangia sana...nadhani ipo haja ya vijana wetu kwenda nje ktk nchi walikofanikiwa kutazama wanafanya nini. Mombasa sio mbali ni swala la kujifunza na kukubali kuwa tunavurunda.
 
Whaaat Bandari ya Dar!!!!!!!!!???.....................hivi hamjui kuwa walishaziba masikio yao kwa gunzi!!

Kuhusu washauri wa uchumi................mimi namshauri JK kuwa aangalie sana hapa JF kuna vichwa hapa....wapo akina Kamundu, GT, FD et al ......ajaribu kuwatumia
 
Nafikiri sina uhakika bandari ya Mombasa kila kitu kipo wazi na mambo yote yanakwenda pale pale bandarini bila wewe kwenda huku na kule mikono kibao...
Ni mawazo yangu tu, tukirudi ktk swala la washauri wa rais ktk Uchumi wazee yote mliyoyasema yanachangia sana...nadhani ipo haja ya vijana wetu kwenda nje ktk nchi walikofanikiwa kutazama wanafanya nini. Mombasa sio mbali ni swala la kujifunza na kukubali kuwa tunavurunda.

Mzee Bandari ya Mombasa ni kama vile uko Rotterdam

Contena likishafika kila kitu kiko elctronic, Jamaa wa KRA huwa wanakuwa tayari wanado details za mizigo yako toka huko ulikoituma na wale jamaa wa inspection ni watu walioenda shule wakaelimika na ofisi zao ziko PUA na MDOMO siyo kule kwetu Uende MAKTABA ukabishane na COTECNA kisha urudi LONGROOM ubishane na wale wendawazimu wa TRA ambao watakuambia suala lako litashughulikiwa baada ya siku mbili kwani Computer zimefeli

Mombasa mzeeupuuzi huo hakuna kila kitu kiko straight forward na Contena lako unalitoa same day

sasa bado unatak kutumia bandari ya Dar tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom