Wasanii wamuziki wa kizazi kipya wanagawiwa viwanja Dar

Hiyo issue ni kweli mie nimeisikia ila dau ulilotaja Nguli naona limepanda kunawatu wamelipa elfu kama 50 tu. Lakini mimi najiuliza kwanini sasa hivi na hizo hela zisije zikaingia kwenye kampeni tukaingizwa mkenge buree.

Inatehgemea na eneo elfu 50 unaishia kupewa CHANIKA

Tutaburn CD mpaka kina Nguli wafulie :confused2:

Ha ha ha ha ha
 
Kwani mnategemea nini kuhusu thithiem, kazi wanayo ijua ni RUSHWA KWA KWENDA MBELE. Kufuta ujinga, umasikini na malazi vimewashinda, lakini hongo za kila aina, wanaongoza.

Nadhani Serikali ingefikilia wapewe kwanza wanao jitolea kusaidia watoto wa mitaani
Kama Vile clouse?
 
Kawapa Viwanja ili watunge nyimbo za kumsifia JK na Mafisadi wake...Mr Sugu, Joe makini (Mwamba wa kazikazini) nae yupo naimani wana hip hop maana kidogo huonyesha kutetea wanyonge....
 
Serikali imetukumbuka tumepewa viwanja ndio tuko kwenye foleni hapa ofisi za SHIWATA ilala Bungoni. Kama kuna mwandishi wa HABARI aje anihoji sijawahi kuhojiwa na mwandishi hasa wa TV naomba mjee na raha sana hapa tunatoa laki 1 tu kama ada.

Kama kuna msanii ambaye hajasikia hii habari naomba mumfahamishe.

Si ndo nyie mnao kipigia chama tawala kampeni, hicho cha bure kila walakini.
 
Watu wamekuwa wakali hata thanks hawatoi anyway wk end njema wakuu
 
Jibu hilo hapo juu tena ndio wanaotulinda hao takukuru wako

ukisikia rushwa ndio hizi....jk kwa kuwa yeye ndio anayemiliki ardhi..basi anahonga wasanii ili apate kupigiwa debe....kwa wasanii mmepata rushwa nzuri kuliko ya pilau....lakini still ni rushwa!!
 
Kura za vijana, maana za wafanyakazi tulizikataa.

Mbayuwayu bana!!!!
 
Takukuru wako wapi? Ahaaaaaaaaaaaaaaaaa ccm bwana ,kizazi kipya wengi wanampigia kampeni mkwere .duh noma
 
Ulishanionaga jukwaa la SIASA mimi? na je ninaweza kufanya joke kwenye hili jukwaa hata siku 1? nimetoa mpaka eneo la tukio na nimeomba nihojiwe sasa naona kimyaaaa
Nilikuona kule na Maxshimba.,... hivi ile album ya hip-gospel tayari?
 
hongera shemeji, nasikia mnataka kujenga Tollywood yenu huko chanika,
 
nilikuwa najiuliza kulikoni washika nyeti kushabikia wao m,kumbe mkono umerefushwa tayari !hii kali kama c ya kulevya kabisa
 
Serikali imetukumbuka tumepewa viwanja ndio tuko kwenye foleni hapa ofisi za SHIWATA ilala Bungoni. Kama kuna mwandishi wa HABARI aje anihoji sijawahi kuhojiwa na mwandishi hasa wa TV naomba mjee na raha sana hapa tunatoa laki 1 tu kama ada.

Kama kuna msanii ambaye hajasikia hii habari naomba mumfahamishe.
Hongeraa.
Hapo kwenye bold naomba nikusahihishe kwamba mnatoa elfu 53 cash na siyo laki moja. kama umepewa na receipt basi ada itakuwa imepanda.
sisi wa mwanzo tulilipa alfu 35, waliokuja awamu ya pili wanalipa hizo alfu 53.
Kama kuna msanii, mwanamichezo na Mwanahabari achangamkie hiyo ishu maana kuna wajanja wameshakula sana vichwa kwa kuwalipisha malaki kibao ilihali bei ni chee. Ukilipa zaidi ya elfu 53 nitumie PM nitakuelekeza cha kufanya ili urudishiwe chenji yako.

Viwanja hivi ni juhudi za viongozi wa SHIWATA na siyo maono ya serikali, tuliifuata serikali baada ya kuanza kutekeleza habari hii. Ingawa baadhi ya viongozi serikalini wanaipiga vita hii programu lakini tunajitahidi kukubalika na kufuata taratibu muktadha ili kupata viwanja zaidi.
(nadeclare interest------ mimi nimo ktk mradi huu)
 
Takukuru wako wapi? Ahaaaaaaaaaaaaaaaaa ccm bwana ,kizazi kipya wengi wanampigia kampeni mkwere .duh noma
Hii ishu ya viwanja haiusiani na kampeni za Kikwete.
Nenda pale SHIWATA ukasome katiba na malengo ya shirikisho ndipo utafunguka kwamba hakuna smaslahi ya kisiasa kwenye mradi wa viwanja.
 
Wanataka kuwa deceive kipindi hiki cha uchaguzi. Watu wanavunjiwa nyumba au kupata majanga hawapewi hata hivyo viwanja iweje watu wanaofanya kazi na kupata hela tena wengine wanavutia unga na kulewea tu bila kufanya kitu cha maana wapewe? Kisa nini kama siyo agenda za siri? Wale wa mikoani wamewakumbukaje au Kampeni mwisho ni Dar?

Bahati nzuri wasanii wengi wanaimba weee halafu hawapigi kura
 
Hii ishu ya viwanja haiusiani na kampeni za Kikwete.
Nenda pale SHIWATA ukasome katiba na malengo ya shirikisho ndipo utafunguka kwamba hakuna smaslahi ya kisiasa kwenye mradi wa viwanja.

So why bongo flava ,?
mimi nachangia maada kutokana na hoja ilivyowekwa hapa.Kwa kuwa wanamziki wengi wa bongo flava wanampigia kampeni mkwere na sasa tunasikia wanapewa viwanja.
Kama uleta maada kasahau kitu au kapindisha na wewe unajua Please weka ndio maana ya forums..ili mjarada uwe sahihi na sisi tutachangia accordingly.
Kumbuka si wote tunaweza fika hapo SHIWATA,ivi ndivyo ilivyo .Still Swali why bongo flava n why now?
 
Hongeraa.
Hapo kwenye bold naomba nikusahihishe kwamba mnatoa elfu 53 cash na siyo laki moja. kama umepewa na receipt basi ada itakuwa imepanda.
sisi wa mwanzo tulilipa alfu 35, waliokuja awamu ya pili wanalipa hizo alfu 53.
Kama kuna msanii, mwanamichezo na Mwanahabari achangamkie hiyo ishu maana kuna wajanja wameshakula sana vichwa kwa kuwalipisha malaki kibao ilihali bei ni chee. Ukilipa zaidi ya elfu 53 nitumie PM nitakuelekeza cha kufanya ili urudishiwe chenji yako.

Viwanja hivi ni juhudi za viongozi wa SHIWATA na siyo maono ya serikali, tuliifuata serikali baada ya kuanza kutekeleza habari hii. Ingawa baadhi ya viongozi serikalini wanaipiga vita hii programu lakini tunajitahidi kukubalika na kufuata taratibu muktadha ili kupata viwanja zaidi.
(nadeclare interest------ mimi nimo ktk mradi huu)

Mimi ni msanii wa ngoma za kibogobogo kule kijijini kwetu, je ninaweza pia kufaidika na zawadi hiyo ya rais Kikwete?
 
Back
Top Bottom