Omukazi Murungi Music Festival: Tamasha litakalotoa fursa kwa wasanii wa kike kuionesha dunia vipaji vyao

ndo vile

Member
Mar 11, 2023
25
12
OMUKAZI MURUNGI MUSICFESTIVAL

Sekta ya sanaa na burudani ni moja ya sekta inayokuwa kwa kasi hapa nchini kwetu Tanzania, sekta hii imekuwa chachu katika kuchangia mapinduzi ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, na kiteknolojia hapa nchini Tanzania na wanufaika wakubwa wa mapinduzi haya ni kundi la vijana, maelfu ya vijana wameweza kupata ajira na wengineo kutokana na vipato wanavyovipata wameweza kufungua biashara namakampuni yaliyoweza kuajiri vijana wengine, pia wapo baadhi ya vijana kupitia sekta ya sanaa na burudani wameweza kuonekana na kuaminiwa na jamii na sasa ni wanasiasa wakubwa.

Wapo baadhi ya vijana kupitia sanaa na burudani wameweza kulitangaza vema taifa la Tanzania kwa kushiriki aukushinda tuzo mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika, makampuni makubwa ya kibiashara sasawanawatumia vijana kutoka sekta hii katika kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali, serikali inajipatiamabilioni ya mapato yatokanayo na kodi inayotokana na sekta hii.

Pia imekuwa ikiitumia vijana kutokakatika sekta ya sanaa na burudani katika kuelimisha na kuhamasisha kampeni mbalimbali za kijamii vilevile vijana kutoka katika sanaa na burudani wamekuwa wakitumika sana katika mambo ya kisiasahaswakatikawakati wachaguzi nchini Tanzaniapianachaguzizanchi jirani.

Ukubwa wa sekta hii ya sanaa na burudani unaoonekana sasa haujaja kwa bahati mbaya, wapo vijanawa kipindi iko,kama wakina Joseph kusaga, hayati Ruge Mtahaba, Dr.cheni, Joseph haule, Richiemtambalike, Judith wambura,na wengineo waliopigana kuakikisha mitazamo hasi katika jamii zakitanzania kuhusu sekta hii inaondoka, katika miaka iliyopita sekta hii ilikuwa siyo rasmi na washiriki wa sekta hii walikuwa wanachukuliwa ni wahuni nawasio na maadili katika jamii zetu, ni kutokukata tamaa kwa hao watu tajwa wakishirikiana na wengineo ndo kumepelekea maendeleo ya sekta hii mpaka ilipofikia sasa.

Sekta ya sanaa na burudani ni pana sana inayojumusha mambo mengi sana kamauigizaji, uchoraji, sarakasi, uchezaji, ushereheshaji, muziki wa aina mbalimbali n.k ila pamoja na upana wasekta hii swala la muziki haswa muziki wa kizazi kipya umekuwa kinara katikakupendwa, kufuatiliwa, kushabikiwa na hata kuitangaza nchi yetu vyema ndani na nje ya mipaka yaAfrika, kwa kupitia muziki huu vijana wadogo wamekuwa maarufu duniani kote, wamekuwamatajiri, wamekuwa na heshima kubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, siku hizi si ajabu kumuona msanii wa kizazi kipya akiteta jambo na muheshimiwa Rais Ikulu, hii inachangiwa na heshima na ukubwa ulionao mziki wa kizazi kipya kwasasa.

Pamoja na maendeleo yaliyopo katika kiwanda cha mziki wa kizazi kipya kwa sasa bado hakuna uwiano wa kijinsia kati ya vijana wa kiume na vijana wa kike, idadi vijana wa kike walioko kwenye kiwanda chamziki ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya vijana wakiume ukianzia wanamuziki wa kuimba, wanamuziki wa kufoka, ma djs,watangazaji wa vipindi vya muziki wa kizazi kipya na pamoja na uchachewao kwenye kiwanda bado uwepo wao kwenye muziki umekuwa ni wakipindi kichache.

Yani vijana wa kike wamekuwa wakiingia kwenye muziki na kusikika kwa kipindi kifupi na kupotea kabisa,Pamoja nauchache uwo wa vijana wa kike upo ushahidi kwamba vijana hawa wamejaliwa vipaji kubwa sanaambavyo kama vikitiliwa mkazo wanaweza kusaidia katika kukua kwa muziki huu wa kileo na kuitangazanchi yetu maradafu,mfano wasanii kama Jolie, Nandy, Ruby, Zuchu, Mwasiti, DJ kama Senorita, mtangazaji kama Fetty ni mifano ya vipaji vikubwa ambavyo kama vikitumika vizuri vinaweza kusaidia katika kukuza mziki wetu vizuri na ukaweza kupaa kimataifa zaidi,katika malengo endelevu17 ya 2030 ambayo duniakupitia umoja wa mataifa imejiwekea lengo namba tano linasema ifikapo 2030 kuwe kuna usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na mabinti.

Lengo hili limewekwa kwa kuzingatia umuhimu wawanawake katika maendeleo ya jamii zetu na dunia kwa ujumla,upo msemo wa kiswahili unaosema "ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima" na ukweli wa msemo huu katika kiwanda cha mzikiwa kizazi kipya umedhihirishwa na msanii shilole ambapo kufanikiwa kwake kwenye muziki kumekujakutengeneza ajira nyingi za vijana wengine kupitia uwekezaji alioufanya katika migahawa yake ya shishifood aliyoifungua katika mikoa mbalimbali, kwa hiyo kama mziki huu ukiweza kuwa na vijana wengi wakike na wakafanikiwa upo uwezekano mkubwa wa mziki wetu kupaa kimataifa zaidi, pia kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu.

OMUKAZI MURUNGI MUSIC FESTIVAL

OmukaziMurungi nineno linalotumiwa na moja ya makibila yanayopatikana hapa nchini kwetu tanzania, kabila la wahaya likiwa na maana ya " mwanamke mzuri, mrembo, anayevutia, kwa kuzingatia umuhimu wa kutunza tamaduni zetu, hili tamasha litaitwa Omukazi Murungi Festival, likiwa na maana ya kuielezea dunia ni kwa namna gani wanawake kutoka Tanzania ni wazuri kuanzia muonekano, tabia na vipaji, tamasha hili ni la tofauti na la kipekee na halijawahi kutokea hapa Tanzania wala Afrika, katika"Omukazi murungi festival" watoa burudani wote kuanzia wanamuziki wanaoimba au wakufokafoka, madjs, madancers, washehereshaji, wapiga ala na vyombo vya muziki, photographers, hypers, watakuwani vijana wenye jinsia ya kike, hakutokuwa na mtoa burudani hata mmoja ambaye siyo jinsia ya kike.

Hii itatoa fursa pana kwa wasanii wetu wa kike kuionyesha dunia ni kwa kiasi gani wamejaliwa vipaji vyakuimba, kufoka, kucheza, DJ's skills, kuhyper, kupiga picha kali n.k kwa maana kwenye matamasha mengiyanayofanyika hapa nchini Tanzania uwezo wa wasanii wetu wa kike hufichwa kwenye vivuli vya wasaniiwa kiume, vilevile kwa kupitia tamasha hili wasanii wetu wa kike watapata fursa ya kubadilishana mawazo, ushirikianokatika kazi, pia kutoa fursa kwa wasanii chipukizi wakike kuonesha talanta zao.

Faida ya tamasha
  • Ujio wa wasanii wapya wa kike
  • Muziki wa kizazi kipya kuchangamka zaidi
  • Kufungua fursa za vipaji vingine nje ya kuimba mfano djs, dancers, photoshoters n.k
Idadi ya wasanii wakike kuongezeka kiwandani.

Vipato kutokana malipo watakayoyapata kwenye show.

N.B Kwa maana hii ya mwanamke mzuri tamasha hili linaweza kubadilika jina kulingana na mkoa husika wanavyomwita mwanamke mzuri!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom