Baadhi ya tungo za wasanii na ukakasi wake

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Kuna baadhi ya mistari au beti za nyimbo za wasanii wetu wa kizazi kipya ambazo ukizisikiliza kwa umakini lazima uondoke na tashwishi.

Lakini kubwa zaidi ni pale unapojaribu kuusikiliza wimbo kisha ujaribu kufikiria nje ya box (kimantiki) kisha jaribu kuwaambia watu ulichokiwaza baada ya kusikiliza wimbo lazima watakuona chizi japo ndiyo uhalisia wenyewe.

hizi hapa chinini verse chache nilizozinukuu katika nyimbo za baadhi ya wasanii wa kitanzania ambazo nimejaribu kuzielezea kwa mtizamo tofauti wenye kuchekeshajapo mashabiki wamezipokea kwa mtizamo chanya, wamezibariki na kuishi nazo.

Tafadhali changia mada kwa kunukuu mistari michache kutoka katika wimbo wowote wa msanii unayedhani ana tungo yenye utata au katoa maboko na yapo sokoni tunaruka nayo pasipo kujiuliza hiki sasa kina maana gani au mbona kachanganya mafaili/kachapia au mbona kilichoimbwa hapa akieleweki.

"..Kama kupenda, bora nimpende mama yangu..." (Kwahiyo inamaana hapa msanii alishindwa kujiongeza kuwa hata huyo mama yake naye ni mke wa mtu?)

"Fikra zako ziko vibaya kwa kudhani huyu binti nilimpenda..."(huko sawa kabisa uenda jamaa alikosea)
"...Ni kweli nilimpenda lakini ni kama rafiki..." (Sasa hapo jamaa mbona dizaini kama kamba hivi, pili unajifunga mwenyewe)

"Baba na mama walinilea mimi..." (Ni kweli kabisa)"...Sasa ni zamu ya YESU" (hapo sasa unazingua sote twatambua kuwa ni zamu yako)

Inshallah inshallah inshallah inshallah inshallah inshallahΓ—100 (kwani msanii huyu katika lugha ya kiarabu yenye misamiati zaidi ya 100k aliona neno moja tu ndilo alirudie rudie mpaka akinaishe wasikilizaji wake)

"..hawa ni wezi...hawa ni wezi..hawa ni weziii..hawa ni weziii.." (Sasa hapa msanii anahisi mashabiki zake ni polisi ama? Au alipokuwa akiandika mstari huu alitegemea tumjibu nini)

"Ngoja nikusimulie habari za kijana mmoja.." (sawa tafadhali nisimulie) "..kijana mtanashati, mpole tena kipenzi cha wengi.." (mmh!kwa sifa zote hizo kwa huyo kijana handisamu unatafuta nini?) "...mimi aliniona nimechoka, nimechakaa//kijana akanipenda, akanichukua akanitengenezaaa//.." (cha ajabu kuna kidume anayaimba mashahiri haya kwa kuyafatisha kwa sauti kubwa kwenye bufa mpaka anakera majirani ila hawamchukulii kama anachoimba aki-make sense)

"Oyaah pombe siyo sigara, pombe siyo sigara, oyah pombe siyo sigara.." (ukifikiria kwa umakini unaweza tamani hata umwambie msanii we idiot kwani nani hajui kama pombe na sigara ni vitu viwili tofauti mpaka utufokee)

"Tunakupenda roma, tunakumiss baba, rudi nyumbani romaa, ututeteee..." (nani alituma maombi hayo ya wewe kuja kuwa mtetezi na nani alikwambia amekumisiau ni stress za ughaibuni zinakufanya uji-assume kwa verse kisha ujimisi mwenyewe na mwisho ujipe umuhimu papo hapo)

"Nasikia harufu, nasikia harufu..." (Kwani cha ajabu nini hapo au msanii unatumia choo cha shimo? Suala kama hilo ungeweza kumnong'oneza hata jirani yako tu si mpaka uliimbie taifa zima)
 
"..hawa ni wezi...hawa ni wezi..hawa ni weziii..hawa ni weziii.." (Sasa hapa msanii anahisi mashabiki zake ni polisi ama? Au alipokuwa akiandika mstari huu alitegemea tumjibu nini
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Konde boooiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!
 
Nasikia harufu, nasikia harufu..." (Kwani cha ajabu nini hapo au msanii unatumia choo cha shimo? Suala kama hilo ungeweza kumnong'oneza hata jirani yako tu si mpaka uliimbie taifa zima
emoji23.png
emoji125.png
emoji125.png
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom