Bifu 30 nzito zilizoutikisa muziki wa kizazi kipya Tanzania

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,224
Kupitia hapa leo naomba tuangazie bifu 30 Kali zaidi kuwahi kuwakumba wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya nchini, kiasi cha kugonganisha vichwa vya wadau wa muziki na pengine kwa kiasi fulani kuukuza muziki wao au hata wengine kuchangia kuwapoteza kabisa kisanii.

1. Sugu na Ruge.
2. Clouds Media na Vinega.
3. TMK Wanaume na East Coast Team.
4. Juma Nature na Inspector Haroun.
5. Zay B na Sister P.
6. TMK Wanaume na Wanaume Halisi.
7. Dudubaya na Mr Nice.
8. Afande Sele na O Ten.

10. Kikosi cha Mizinga na Nako 2 Nako.
11. Roma na Joh Makini.
12. Afande Sele na Professa J.
13. Rado na Fid Q.
14. Inspector Haroun na Luteni Karama.
15. Kalapina na Chid Benz.
16. Dogo Mfaume na Omari Omari.
17. Sugu na Mwana FA.
18. Mwana FA na Lady Jaydee.
19. Diamond na Ali Kiba.
20. Sholo Mwamba na Man Fongo.

21. Afande Sele na Madee.
22. Madee na Ney wa Mitego.
23. Langa na Jay Moe.
24. Kikosi cha Mizinga na baadhi ya Wasanii wa Hip Hop nchini.
25. TID na Q Chilla.
26. Bob Junior na Diamond Platinumz.
27. P Funk na Professa J.
29. P Funk na Clouds Media.
30. Kalapina na Clouds Media.

Unaweza kuongeza pia orodha ya wasanii waliokuwa na bifu kupitia muziki wa kizazi kipya ambao nimesahau kuweka majina yao.
 
Sugu na FA kivipi, eleza kwa kina kidogo
Sugu alikuwa amepanga uzinduzi wa album yake Sugu, akamwalika Mwanafalsafa, naye akakubali.

Zikiwa zimebaki siku kama saba hivi, Clouds wakaanza kupròmote show ya uzinduzi wa album ya Mwanafalsafa. Siku na muda uleule, unaambiwa show ya Mwana FA ilikuwa na watu hawafiki 20 wote wafanyakazi wa Clouds. Kwa Sugu nyomi kama lote.

Ikabidi Clouds waanze kutangaza nendeni kwenye show ya FA kiingilio ni bure, watu bado hawakufika 50. Yaani ilikuwa kama jamaa anatumbuiza sherehe ya mtoto wa kike kuvunja ungo.
 
No 10 N2N walahi ndio bifu hatari zaidi usikatize mitaa ya N2N wakakujua ni wa kikosi vha mizinga utapigwa UFE.

na shida ni kwamba enzi hyo polisi walikua wanaogopa hayo makundi.

asee ni bifu hatari
 
No 10 N2N walahi ndio bifu hatari zaidi usikatize mitaa ya N2N wakakujua ni wa kikosi vha mizinga utapigwa UFE.

na shida ni kwamba enzi hyo polisi walikua wanaogopa hayo makundi.

asee ni bifu hatari
Ukweli
 
Back
Top Bottom