SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,336
- 4,694
Ndugu yangu Otorong'ong'o elewa kuwa tunaoabudu siku ya JUMAMOSI ama siku ya SABATO tupo kwenye madhehebu mengi sana yanakadiria kufikia madhehebu tofauti kama 500 na zaidi. Mimi na dhehebu langu hatutumii kabisa aina yoyote ile ya "sanamu" au picha au msalaba. Isitoshe sisi katika kanisa la KWELI la MUNGU tunafahamu kuwa MESSIAH hakufa "msalabani", bali alikufa "mtini", yaani alitundikwa kwenye "nguzo" na siyo "msalaba".
Ukisoma Biblia yako vizuri(nafahamu wewe huijui wala huisomi Biblia), utaona kuwa YESU alitundikwa kwenye "NGUZO" na siyo kwenye MSALABA. Kuna tofauti kubwa sana ya NGUZO na MSALABA..... Ukiona kwenye Biblia pameandikwa neno "msalaba" fahamu kwamba ni makosa ya "utafsiri wa lugha" yaliyofanywa kwa makusudi na watafsiri wa mwanzo.
Tunafahamu kwamba vitabu vyote vya Agano Jipya viliandikwa kwa Lugha ya KOINE GREEK. Ni kitabu kimoja tu cha WAEBRANIA ndicho kilikuwa kimeandikwa kwa KIEBRANIA. Neno la Kigiriki linalomaanisha NGUZO ni "stauros", neno hili ndilo linalopatikana kwenye maandiko ya kale na maana yake ni nguzo na siyo "msalaba". Neno la Kigiriki linalomaanisha "msalaba" ni "diaschizo", neno hili diaschizo halikuwepo kabisa katika vitabu vyote vya kale vya Injili.
Msalaba mnaoutumia ninyi Wakatoliki asili yake ni UPAGANI ulioanzishwa na Tamuzi huko Babiloni ya kale. Herufi "T" ilitumika ili kumuenzi Tamuzi ambaye baada ya kufa aliabudiwa kama mungu. Kutokea hapo Upagani ukaenea dunia nzima na alama yao kuu ni "+" msalaba ambao asili yake ni neno Tamuzi.
Hivyo basi sisi tulioa katika CCOG kamwe hatutumii alama ya "msalaba" sababu tunaujua UKWELI, na ukweli ni huu; MUNGU hafungamani na Upagani hata siku moja. Huwezi kuchanganya mambo ya MUNGU na mambo ya Beliari, huwezi kuchanganya IBADA ya MUNGU na ibada ya mashetani kama wafanyavyo Wakatoliki na Maprotestant.
Hivyo basi kutokana na swali lako nafikiri hao SDA ndiyo wanatakiwa kukujibu na siyo mimi. Nafikiri umeelewa sasa kuwa mimi siyo Msabato wa SDA, mimi ni MSABATO wa CCOG, ili kujifunza zaidi ingia hapa; www.ccog.org
1. Siku zote sikuwahi kufahamu kama wewe ni muumini Wa MASHAHIDI WA YEHOVA.
2. Kuhusu kwamba Neno "Msalaba" ni istilahi ambayo imepatikana kimakosa kutokana na tafsiri sijakuelewa. Ninaona kama kuna kujichanganya. Nani hasa alifanya tafsiri ya hiyo Biblia? Ni huyo mpagani TAMUZI au nani hasa? Maana Mara unasema neno "Strauros" lilitafsiriwa vibaya Mara unasema ni neno ambalo lilitumika kumuenzi TAMUZI!
3. Nitaleta Uzi hapa siku moja kueleza jinsi msalaba wenye + ndio uliotumika kumsukubisha YESU.
4. Ama Yesu alisulubiwa msalabani au kwenye mti lililo la muhimu ni damu yake iliyomwagika.