Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA

Kwa ujumla nimesoma waraka wako na nami naona ni vema sana. Umetanguliza tahadhari kwamba chadema kitafakari vizuri kisahihishe makosa yake kisha kichukue hatua kujisafishia njia kueleke 2015.

Bila kuangalia neno moja moja au sentensi kwa sentesi ujumbe utasaidia Chadema kujipima. Chadema ina advantages kubwa nzo ni kwanza, wanachi wengi kuichoka CCM na hivi wanaweza ku-opt chadema.

Pili sasa cdm ina popularity kubwa kupitia viongozi wake wa kitaifa na wabuge walio wengi kwa hoja zao bungeni. tatu ni harakati zake na sapoti kubwa wanayoipata katika kampeni yake ya M4C.

Kwangu mimi haya ni sawa tu. sasa hatua muhimu inayofuata iende mbele zaidi ambapo mtu wa kawaida akiulizwa kwa nini chadema na si ccm aweze kueleza mambo ya msingi kabisa tofauti na haya ya siku zote. Chadema ikae sawa zaidi kwa kuonyesha matumaini ya wazi kabisa tena yanayoelezeka tena kwa watu wote wa makabila yote, dini zote na hata matabaka yote, hata na vyama vote wakiwepo wana CCM.

Mimi naona mantiki ya Mkandara inagusa haya. ikumbukwe kuwa harakati hizi zinawalenga wote maadui na marafiki, wenye uelewa mkubwa na uelewa wa kawaida, masikini na matajiri; wasomoi na wasio wasomi n.k
 
Nayale magari yalokua yakipita Arusha kutangaza mikutano yenu yanapiga nyimbo za mapambio nailo nalo nilakawaida?!
Mkuu Siera, kwa Arusha na Moshi mapambio ndio zao!. Anzia mabasi ya Moshi-Arusha mpaka bar ni mapambio!.
Kwa vile sijawahi kushiriki mkutano wowote wa M4C, kama ni kweli, kwenye mikutano yao yote, mikoa yote, maeneo yote, huanza kwa sala ya dini fulani na kuhamasishwa kwa mapambio, then hiki ndicho anachokizungumza Mkandara
Chadema inahitaji kuwa na religious divesity, religious considerations and religious tolarance!.
 
Ufaransa ilipiga marufuku uvaaji wa hijabu mashuleni, uko wapi uhuru huo unaojidai kuu-site. Narudia kukwambia tena, nimekuelewa vizuri sana, ona mapovu ya kidini yanavyokutoka

Unaweza fanya jambo moja jema sana ikiwa utazingatia kwenye red, mshaurini Mufti, kuruani iandikwe/itafsiriwe kwa kiswahili, umeonyesha uwezo mkubwa wa kufanya hivyo.
Ahahaha hahaa chuki zako kwa waislaam wala hazinisumbui isipokuwa wewe mwenyewe. Huelewi na hutaelewa hata kikiandikwa kiswahili maana niloandika hapa ni kiswahili na bado huelewi maana. Kujua kusoma sio kuelimika - nambie kabia yako nitaandika kikwenu.
 
Mkuu wangu nimekuacha muda bado wanitafuta tuuu..haya kuna sehemu moja nimeisoma hii signature ya mtu ikisema hivi:- Tanzania lead economist Jacques Morisset said, The GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

Sijui kama unaweza kunipa tafsiri ya maneno haya ktk mtazamo huo hapo juu kama anavyoainisha Jmushi1 ya who did what and what was done by who.
Mkuuunadhani ata nina personal problem na wewe?hata mimi nashangaa kwanini unanisepa,tatizo ni kuwa tupo katik public domain na issue yoyote inayoleta maswali huwa inajadiliwa kwa hoja.

Sitaki kujibu hili kwani hata kama ningekuwa sijui kiingereza ningetumia google ningepata tafsri,ila ningepungukiwa katika sentence na ulichopungukiwa hapa.

Soma hapa chini ulipotokea,halafu uniambie kama nilikuwa sahihi kufata tafsiri.
quote_icon.png
By jmushi1

Kuna tofauti kubwa tu kati ya "Doing the things right" vs "Doing the right things",the latter has to do with leadership...
Jmushi1 aliweka kama hapo juu.Na wewe ukaquote kama hapa chini.

quote_icon.png
By jmushi1

Kuna tofauti kubwa tu kati ya "Doing the things right" vs "Doing the right things",the latter has to do with leadership...

Aaaah Jmushi1 mku wangu mbona unatoka nje sasa. Unajua fika kwamba sisi wote tunatakiwa kufanya the right thing na unapovifanya lazima uvifanye sawa. Unaweza kuamua kufanya kitu kizuri lakini ukakifanya vibaya na kisilete mafanikio. Mkulima akipanda mbegu vibaya sizipoota unafikiri wazo zima la kulima ni baya..

Nadhani alichokisema Mchambuzi kwamba Chadema maadam inataka kuingia IKULU ni lazima safari hii wahahakishe are doing thing right kwani hapa ndipo tunapopwaya..
jmushi1 akakujibu kama hivi
Re: Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA
quote_icon.png
By jmushi1
Mkuu unaifahamu tofauti kati ya hizo statement mbili yaani "doing the right things" vs "Doing the things right"?Things right is more of a managerial focus where as right things is about leadership.
​
Kama unataka chadema wa lead,then they should do right things...
​
Na wewe ukaquote hivi na jibu lako ndilo kama hili.
Re: Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA
quote_icon.png
By jmushi1
Mkuu unaifahamu tofauti kati ya hizo statement mbili yaani "doing the right things" vs "Doing the things right"?Things right is more of a managerial focus where as right things is about leadership.
​
Kama unataka chadema wa lead,then they should do right things...
​
nakubaliana nawe hata wanapojitangaza. Swala ni NIA njema na ufanye ipasavyo..
Hembu pitia hizo red Vizuri halafu uone wapi nimeona shida.Najua upo very delicate and sensitive mtu anapokata stim zako wakati unaona kuwa umeshapata flow.Usisahau mimi nina shija sana na uongo.

au kukusaidia check nilichoandika
jmushi umesoma vizuri?Check ktk red
Re: Waraka wangu kwa viongozi wa CHADEMA
quote_icon.png
By jmushi1
Mkuu unaifahamu tofauti kati ya hizo statement mbili yaani "doing the right things" vs "Doing the things right"?Things right is more of a managerial focus where as right things is about leadership.​
Kama unataka chadema wa lead,then they should do right things...​

nakubaliana nawe hata wanapojitangaza. Swala ni NIA njema na ufanye ipasavyo..

Huyo ni mkandara bwana.You will never be in the same logical calibration.Yeye yupo katika mission
Mukandara ujue hata kuchagua jina la kutumia hapa hata kama ni "ID" ya kujificha bado aina ya jina ulichagualo lina maana kubwa sana kuelezea ama nia yako au jinsi ulivyo.Pia ujue mti wenye matunda ndio upigwao mawe..So usinikimbie sana kwani unaweza kuwa mti wenye matunda mheshimiwa.usiogope kwa vile you are a very interesting and most controversial figure.
 
.... Kwani kuna tatizo gani chadema ikishindwa kuchukua madaraka 2015? Mi naona ni sawa tu, cha msingi ni kwamba tuna chama imara cha upinzani. Tukijikita tu kwenye kuiondoa CCM madarakan kwa"gharama" yeyote tutagundua kwamba tumebadilisha chupa ila mvinyo ni ule ule. I love CDM, but am not hell-bent to see them takeover from CCM by hooks and crooks.
 
Mukandara nakubaliana sana uwezo wako wa kuandika kwa mpangilio na kuchagua maneno yenye urembo.Ila kwa upande mwingine napata shida elewa kwanini upo so much obsessed with chadema?its not the first time nimekukuta ukiwa na hayo mafiga matatu ya CCM "ukanda,ukabila na udini".Umejitahidi sana kujipa role ya mshauri na mchambuzi,but its pathetic that huna nia njema sana.

Kwa kukosa hiyo "Nia Njema" kumenifanya nichukue kama personal responsibility.Na hii ni kwa vile watu wanaamua chuku malengo ya kipuuzi sana.No matter how much ccm is trembling.Wana CCM hawana haki ya kuinyima hii nchi chama mbadala.Tena lilipaswa kuwa jukumu la CCM kuruhusu vyama makini kuwepo ili wanaposhindwa endesha nchi kama sasa hivi basi wapumzishwe wapata muda wa kujipanga na kuja na mikakati mipya itakayowachukua miaka mingine kama 50 kama wataweza maintain.Na mengine mengi sana ambayo yanasikitisha zaidi ya chochote.Haiwezekani miaka yote nchi ilitumia kujenga nidhamu, kujenga uzalendo na baadaye kujenga misingi ya amani ije haribiwa kirahisi na CCM kiasi hiki.I can`t believe mambo yanayotokea katk hii nchi yakichochewa na hisia za udini mioyoyoni mwa watanzani.Hizi ndizo sababu zilizonifanya nikakomaa sana na CUF.watu wamesahau kuna michezo mingi sana ila hizi chuki si mchezo.

Nikirudi kwa mukandara.Kwa muda wote nimepitia posts zako kuna traces za mamabo ya kutisha sana.Na wala usiogope kwanini nimekuwa na interest ya kukuchagua wewe.Sababua kubwa ni uwezo wako wa kupangilia maneno na unaandika mengi sana ,maneno yanayoweza "Distract" attention ya msomaji .Katik ahizo post nimeona angalau haya:

-Umejaribu jiestablish kama undisputed free and great thinker.(ingawa ukibanwa unafunguka sana).

-Umejaribu kujiweka kama mshauri wa kudumu wa chadema in public.Sijui kwanini usifanye privately?

- Umejaribu kubrain wash sana watu.Umchukua sura tofauti ila the skeleton ni ileile upo na mafiga matatu according to ccm "ukanda,ukabila na udini".Na hili upo very determined kutokubali kuwa cdm wameshakabiliana nalo ,kuna thread nilikukuta inayomhusu Zitto.Kule tulibishana sana.

-Hujamaintain consistency logically.kama jinsi unavyo refer CDM( tuta, kita, mta,....nyie , kwenu , chetu, etc).Huku ukijificha katika kivuli cha uanachama.na hapo umetumia nguvu nyingi sana kuchamazisha watu.Ila unahama sana ndani na nje ya CDM.

-Unabadilika sana kutokana na mzingira.Nime kunote sehemu kadhaa .Ukianza kwa confidence,ukibanwa kidhaifu unakuwa mkali, ukibanwa zaidi una unatishia kuwa wengine hawakuelewi n akuwadharau kuwa ndipo akili zao zimeishia, ukibanwa zaidi tena unageuza kuwa ulichokuwa ukisena mawazo mazuri na wasiposikiliza wasije juta ikila kwao, ukibanwa tena zaidi unahamia ktk mtazao kuwa ni individual issue tuu kama mawazo yao , ukibanwa zaidi unawaambia waliokubana wachane na wewe.katika kila stage umekuwa ukihamisha sana topic unaposhindwa jibu kitu,halfu unachokiahamia hakina uinganifu sana na unachotaka kifikisha.Then unaonyesha kitu cha kushangaza unahamia sehemu nyingine kuendelea na kazi kama kawa.Upo determined.

My friend, naomba uamue moja tuu kuwa muwazi sema,nia yako wajue wazi kuwa unaamini mafiga matatu km CCM na upo determined kuya publish kwa nguvu zote.CDM watakujibu na raia wengine watajua jinsi ya ku approach ulichoandika.Hakuna sababu ya kujifanya huelewi kwa kiasi gani CDM wameshaonyesha kuwa yote ni uongo na tayari viongozi kibao wa CDM na vyama vingine wamekuwa wakiaibika kwa kujikuta wakiongea ujinga, na upotoshaji katika jamii.Mukandara nilikukuta ktk thread iliyokuwa ikiongelea kuhsu mh Zitto na nilikuwa kinyume chako ulijikongoja sana msemea Zitto, ukaongea mambo mabaya sana na kiasi fulani ukajiweka kama Zitto.Nilihukia sana,kwani hata kama ungekuwa ndiye Zitto kwa nini uchukue that low path?Mbona katik upinzani maisha unayala tuu.Na jamabo linalotokea ni suala la kitaifa na amani na ustawi wa taifa.

Labda tuu kukutaarifu, kwa mitizamo unayoiweka humu,unafiki unaouonyesha, na kutojua unapopeleka taifa sidhani kama nitaacha kukubana sana ili utoe majibu na si porojo.Humu ndani kuna watu wanajikuta wakishindwa elewa kwanini njia si moja,ingawa unaongea lugha ya upande wao.Its not healthy hata kwa JF.Ungeingia katika special side ili ukadanganye na wajanja wote.
 
.... Kwani kuna tatizo gani chadema ikishindwa kuchukua madaraka 2015? Mi naona ni sawa tu, cha msingi ni kwamba tuna chama imara cha upinzani. Tukijikita tu kwenye kuiondoa CCM madarakan kwa"gharama" yeyote tutagundua kwamba tumebadilisha chupa ila mvinyo ni ule ule. I love CDM, but am not hell-bent to see them takeover from CCM by hooks and crooks.

the issue ni kwamba tunahitaji chama mbadala very urgently.hatuna hakika ya uhai wa ccm hata kama itashinda .
 
Nicholas,hapo kwenye point ya consistency hata miye nimeiona kwa ndugu yetu Mkandara.Ni kweli anasema "nyie chadema",(kwenye posti moja aliyonijibu alifanya hivyo),lakini bado wakati mwingine akisema yeye ni chadema.Sikutaka kuli pinpoint kwasababu mjadala huu ni mkubwa na mpana.So sikutaka kutoka nje ya mada.Lakini hilo nililiona hata miye,yani akitoa reference kama siyo mwanachadema na sometimes kama vile ni mwanachadema.
 
Last edited by a moderator:
Nicholas,hapo kwenye point ya consistency hata miye nimeiona kwa ndugu yetu Mkandara.Ni kweli anasema "nyie chadema",(kwenye posti moja aliyonijibu alifanya hivyo),lakini bado wakati mwingine akisema yeye ni chadema.Sikutaka kuli pinpoint kwasababu mjadala huu ni mkubwa na mpana.So sikutaka kutoka nje ya mada.Lakini hilo nililiona hata miye,yani akitoa reference kama siyo mwanachadema na sometimes kama vile ni mwanachadema.

Ana vitu vingi sana vipo flawed kwa vile nia yake ipo palepale:
Wakati anakubalina na mlichokuwa mkieleweshana yeye alimalizia na ufanye ipasavyo.
Haya ni maneno mawili tofauti .. ufanye ipasavyo na ufanye ipasayo km
"Doing the things right"na "doing the right things" sijui alikubali nini?Nilipo highlight akauliza swali jingine tofauti,then akatokomea nilipomsaidia kuona.Kaweka Distractions kama kawaida yake.Kuwepo kwa distractions kunamsaidia kukimbia kuhitimisha mazunguzo au hata kujibu swali gumu kwake.
 
Mkandara

Kwa sehemu ndogo niliyokupata umemaanisha watu wanaojipambanua kwa dini zao wapewe nafasi ya kubembelezwa!!!!

Mimi nawaambia viongozi wangu wa chadema; ni heri kutokuingia ikulu kuliko kuingia kwa upendeleo wa wanaojitambua kwa imani zao.

Waelimisheni wajitambue kwa utanzania wao ndipo wawape ridhaa ya kuwaongoza.
Haihitajiki mistari miiiiiiiiiingi unazunguka zunguka kisa unataka waislamu wapewe aproach ya kiislamu.

kwenye ukombozi huu wanatakiwa watanzania-waislamu pamoja watanzania wa imani zingine na wala si waislamu-watanzania . . . .
wewe umenena.
 
Mkuuunadhani ata nina personal problem na wewe?hata mimi nashangaa kwanini unanisepa,tatizo ni kuwa tupo katik public domain na issue yoyote inayoleta maswali huwa inajadiliwa kwa hoja.

Mukandara ujue hata kuchagua jina la kutumia hapa hata kama ni "ID" ya kujificha bado aina ya jina ulichagualo lina maana kubwa sana kuelezea ama nia yako au jinsi ulivyo.Pia ujue mti wenye matunda ndio upigwao mawe..So usinikimbie sana kwani unaweza kuwa mti wenye matunda mheshimiwa.usiogope kwa vile you are a very interesting and most controversial figure.
Mkuu Nicholas, sio siri hii level ya hoja zako na kibano unachoshusha kinahitaji level ya ma great thinkes wa ukweli tuu ndio wakuelewe, naomba pia uzingatie na sisi watu wa kawaida ambao sio ma great thinkes tupo na mnatufungua macho na kupanua uelewa wetu kwa post zenu na majibishano yenu, Asante kwa hili!.

Naomba unifafanulie hapo kwenye bold, unamaanisha hata verfied user huyu nae hujificha uvunguni na kupaza tokea shimoni?..
 
Hujanisoma . hunielewi na wala hutanielewa waislaam wanasema - Summun bukmun umyun fahum layarji..

Nani kazungumzia Pinda au kkiti cha Ikulu au nazumgumzia Utawala unaowapa uhuru haki na usawa waumini wake. Mbna Uingereza na Marekani ni nchi ya wazungu na Kikristu, lakini wanatoa Uhuru, haki na usawa kwa wananchi wake waumini wa dini zote wafanye ibada zao pasipo kupingwa?..

Kaka Mkandara,
Kwa Tradition za Mtanzania au let say Africans, hatuna kitu kinaitwa Dini, hizi dini zote zimeletwa. Wewe unataka sasa tuanze kugawanyika kama Wakristu au Waislam tuongeze wapagani na kadhalika. Je kwa nini unaona ni rahisi sana ati Watanzania tujiingize kwenye dini zaidi kuliko kujiingiza kwenye ukabila. You are very comfortable to be called a Christian or Moslem than being called Mkerewe au Mhehe!!
If you accept religious lines to divide us also please accept our tradition ethenic tribal lines to take root also.

WE cannot be learning all these foreign cultures all our generations, we have to reach a stage whn we say to hell such brain washing!! WE are Tanzanians. Education, hardwork, innovation, discipline, in line with our culture have to determine our way up and intergration!!
 
Ana vitu vingi sana vipo flawed kwa vile nia yake ipo palepale:
Wakati anakubalina na mlichokuwa mkieleweshana yeye alimalizia na ufanye ipasavyo.
Haya ni maneno mawili tofauti ..ufanye ipasavyona ufanye ipasayo km
"Doing the things right"na "doing the right things" sijui alikubali nini?Nilipo highlight akauliza swali jingine tofauti,then akatokomea nilipomsaidia kuona.Kaweka Distractions kama kawaida yake.Kuwepo kwa distractions kunamsaidia kukimbia kuhitimisha mazunguzo au hata kujibu swali gumu kwake.
JF ni shule tosha
Nimejifunza kumbe doing the right things peke yake hakutoshi, you got to do that right thing in a a things right! na kiswahili chake ndio hiki sio tuu yakupasa ufanye ipasayo, bali yakupasa ufanye ipasayo kwa kuifanya ipasavyo!.
 
Mkuu Mkandara heshima juu.Huwaga naheshimugi sana michango yako objective humu jamvini mkuu, but hili bandiko lako la sasa limekaa kiutata utata kidogo nadhani (at least kwa mtizamo wangu).Ninachokisoma kati kati ya mistari ya uzi wako ni kama theme ya kuwahanikiza Chadema wajipange kushika dola 2015 by hooks and crooks, clean or dirt, etc....the end justifies the means, right?. It's like "hey Chadema, put on that fake smile and win it all". Alright, come 2015 Chadema wanaingia Magogoni kwa style hiyo, then what's next? And how long will they sustain that "fake smile"?
Mkuu, umenena vyema!Ninachokiona mimi mabadiliko ni LAZIMA! Hata akiingia mbwa ikulu. Yaani litakalo kuwa na liwe! Kutesa kwa zamu na kuteseka kwa zamu, nao waje wafaidi rakaa ya pande la muhogo bichi lililo wekwa chumvi na pilipili!
 
Ndugu yangu mkandara mtu yeyote anayetumia udini kufanikisha mambo yake lazima siku moja udini huo huo utamuaribia mambo yake. Unasema CCM wamefanikiwa kwa hilo lakini ukweli ni kwamba mbinu hii sasa inawatafuna si unaona yanayoendelea.

Nikuulize swali moja tusengetawaliwa na wakoloni wa kizungu na kiarabu leo kauli yako ungesemaje? je dini za makabila zaidi ya 120 ungetumiaje? Je uwezo wako wa kusoma kwa umakini na kuelewa mijadala hapa JF kama ulivyosema ulipata toka dini ipi?

Note: you may chain the tongues of men but you will never touch their minds.
 
the issue ni kwamba tunahitaji chama mbadala very urgently.hatuna hakika ya uhai wa ccm hata kama itashinda .

Ni kweli tunahitaji chama mbadala as soon as yesterday. Tatizo ni kwamba baadhi ya watanzania hawapo tayari kwa mabadiliko (mfano mzuri ni propaganda za "udini" wa CDM zimewashika barabara baadhi ya waislam-wasomi na wasio soma). Ktk mazingira kama haya, CDM can settle for less than they deserve. Yaani, kama CDM itapata nusu ya wabunge wote 2015-things will never be the same again.

Kwa kifupi, Ndugu Nicholas, mabadiliko ni hatua-wasioelewa dhamira na tumaini jema kutoka CDM leo, wataelewa kesho. Ingawa kuendelea kuwa na CCM kwa siku moja zaid ni maumivu zaid, kuiweka CDM madarakani leo kunahitaji kafara kubwa sana ambayo nina wasiwasi baadhi ya watanzania bado hawapo tayari kuifanya. Bado msimamo wangu ni kwamba CDM haina haja ya kujipaka mkorogo ili ivutie mposaji, naamin CDM itaposwa bila kutumia mkorogo.
 
Pasco,
Ushauri wako ni wa ujenzi ni hiari yao Chadema waufuate au wauache.

Kimsingi Chadema haina tofouti na CCM wana virusi vya ung'ang'anizi vya kurithishana nafasi za uongozi, kwa kuwa wasisi wa Chadema wanatoka ukanda huo wa Kaskazini nao pia wamerithisha familia zao nafasi nyeti za uongozi.
Mkuu Ritz naona unatokwa povu kwa uhakika CHADEMA wamekushika pabaya!! Wakienda kufungua matawi Iringa tulia basi acha kupiga watu mabomu!!!! Lakini hata mfanyeje M4C kuzima moto wake ni ndoto, kila kitu kina mwanzo sasa CDM inasambaa nchi nzima kuanzia pwani hadi Kigoma, kaskazini Arusha na Moshi hadi Lindi na Mtwara, kama unabisha ngoja uone!!! Acha siasa za vitisho kupiga watu risasi na mabomu wasio na hatia, wailobeba matawi ya miti na mabango upate joto lake!!!!

 
WanaJF, nimeisoma uzi wa Mkandara na wachangiaji waliotangulia, kwa uelewa wangu Mkandara anasema hivi, tuhuma tunazowatuhumu CCM hata wa CHADEMA wana tuhuma zao. (Tuhuma si lazima ziandikwe na mara nyingi ni uvumi ambao watu wanauandaa na kupigana kwa nguvu kuhakikisha watu wanaamini kuwa ni kweli) Tuhuma za Chadema ni ukanda i.e. kanda ya kaskazini, pili udini yaani Chadema inaviongozi wakristu wengi kuliko waislam na tuhuma ya tatu ni kuwa Chadema inaendeshwa kwa kujujuana.

Na anaomba hivi, sisi wafuasi na wapenzi wa Chadema lazima tuandae majibu ya kulidhisha sio kupuuzia shutumu hizi. Anatolea mfano wa CUF ambayo imesambartishwa kwa tuhuma za udini. Na nakumbuka juzi kati hapa watu walidai kuwa hata Julius Mtatiro naibu katibu mkuu wa CUF ni muislam ila kajibandika jina la kikristu kwaajili ya kupata unga. Sasa anataka Chadema katika mikakati yake ya kuchukua nchi 2015 ije na mikakati ya kufuta tuhuma hizo.

Sijamuelwa vizuri pale aliposema kupuuza imani zingine maana nimewaona viongozi wa chadema wakishiriki shughuli zote za kikristu na kiislam. Ndoo nilivyomsoma Mkandara. Na ningeomba kama alivyosema yeye mwenyewe tusikimbilie kukurupuka tutafakari na kuja na hoja sio lawama na kupuuza
 
Ni kweli tunahitaji chama mbadala as soon as yesterday. Tatizo ni kwamba baadhi ya watanzania hawapo tayari kwa mabadiliko (mfano mzuri ni propaganda za "udini" wa CDM zimewashika barabara baadhi ya waislam-wasomi na wasio soma). Ktk mazingira kama haya, CDM can settle for less than they deserve. Yaani, kama CDM itapata nusu ya wabunge wote 2015-things will never be the same again.

Kwa kifupi, Ndugu Nicholas, mabadiliko ni hatua-wasioelewa dhamira na tumaini jema kutoka CDM leo, wataelewa kesho. Ingawa kuendelea kuwa na CCM kwa siku moja zaid ni maumivu zaid, kuiweka CDM madarakani leo kunahitaji kafara kubwa sana ambayo nina wasiwasi baadhi ya watanzania bado hawapo tayari kuifanya. Bado msimamo wangu ni kwamba CDM haina haja ya kujipaka mkorogo ili ivutie mposaji, naamin CDM itaposwa bila kutumia mkorogo.

Well Said...kama umeona vile wachangiaji wengi humu ndani wanajenga hoja ndeefu ili wawaaminishe CDM kuwa wapo in a wrong track,na wanahitaji chukua njia ya kujipaka mkorogo ili waanze kuwa dhaifu.

Wasomi wengi watz wana reflect sana fikra zao tofauti na wanavyodhani kuzificha.Wachangiaji wanasisitiza udini, ukanda na ukabila, na hata wakipewa ushuhuda wa jinsi CDM wameshinda hilo,baada ya mwendo si mrefu wanakuja tena same msg kwa mgongo wa USHAURI.

Hawa jamaa wamejaribu sana jenga mazingira kwa wana CDM kuwa CCM ilishinda kirahisi na kihalali sana.Ili kuhalalisha mambo yao mengi waliyopenda CDM wajipake.


Wapo wengi kama wacheza "karata 3" wanajitambulisha kama CDM halafu wanawahi support ushauri, kuwa ni somo zuri sana na si la kupuuzwa.Yeah si la kupuuzwa kwa vile limetoka CDM,ila linapakwa na adui.Na hapa CDm hawahitaji acts na kuanza dilute watu kwa matabaka.Hapa mtu akiwa na sifa na kuwavutia wajumbe basi apitishwe(dini,ukabila, ukanda) vinakuwa masked.

Watu wengi humu hawana tofauti na CUF(mchungaji fake) kuweka vitu fake na dhaifu wakidhani wanajenga nortion ya kudhalilisha upande mmoja na kuupa umaarufu upande wa pili.

Mfano:Wote wanaotoa ushauri wamekuwa wakiaminisha watu kuwa CCM inapendwa sana ila ni mgombea sahihi tuu hajawekwa.Ni sahihi zaidi kusema kuna baadhi ya maeneo CCM ilijiongezea "kuaminika" kwa propaganda za "Umwagaji damu na vitisho vingine" zilizojenga hofu,ila si kuwa wanapendwa hata kidogo.Na imani hii si kuaminika katika Rasilimali. Kila mtu nawajua ni wezi.

Hoja nyingi ni basis ya kujenga mashambulizi zaidi ya ushauri.Na hasa kwa mleta mada.Wamekuwa wakijenga udhaifu wa CDM wa kufikirika halafu wakijitahidi sana ficha au hata kudhoofisha uchafu wa CCM na vyama vingine.
 
Back
Top Bottom