Mheshimiwa Mwenyekiti, katibu mkuu wa chama, viongozi wa chama ngazi ya Taifa, mikoa na wajumbe wa mabaraza yote ya chama ngazi zote.. leo nachuua nafasi hii kuwapa summary ya mjumuiko wa utafiti wangu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 kuzungumzia hali halisi. Yamkini waraka huu umelenga jambo moja tu muhimu sana ktk mapitio yangu ya siasa za Tanzania na hasa mapenzi yangu ya dhati kwa chama cha Chadema na uongozi wake kutika maendelezo ya kukijenga chama hasa ktk wakati huu kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Ni baada ya kusoma mada kadhaa humu JF ambazo binafsi yangu nimezisoma kwa umakini mkubwa ktk kutazama fikra za wananchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoja, maoni na mitazamo wa wanajanvi nimekuja na waraka huu makusudi kukinusuru chama hiki kuepukana na umaarufu wa muda. Waheshimiwa, tujihadhari sana na umaarufu wa muda ama kutukuza wingu hili la umaarufu wa muda kwa sababu lengo kuu la ujenzi wa chama hiki ni kupigania dhamana ya wananchi kuwapa mamlaka ya kuongoza nchi yetu na watu wake. Tukumbuke tu ya kwamba ngoma ikivuma sana mwisho wake hupasuka.
Hivyo basi mada nilizozitazama na kuzipa uzito mkubwa ni kama zifuatavyo:-
1. Mchambuzi Bofya
2. Profesa Bofya na
3. Ibambasi Bofya
Waheshimiwa,
Mada hizi nimezipa uzito kutokana na nafasi ya chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015. Zote hizi zimebeba uzito mkubwa sana wa tafiti zangu ktk jukwaa hili la Siasa pamoja na mkusanyiko wa hoja na mawazo ya wadau ambao kwa kuelewa ama kutoelewa wameweza kuonyesha wazi tofauti zao za kisiasa, kiimani na hata kujenga matumaini hasi japokuwa chama hiki hakitakiwi kabisa kupoteza dira yake kwa manufaa ya mtu ama baadhi ya watu.
Ikumbukwe tu kwamba wananchi wa nchii hii pamoja na tofauti zao bado ni Watanzania wenye kuthamini mila na desturi zao, wanaothamini imani zao za dini, UTU wao na wanaotukuza Ujamaa kama msingi bora na wajibu wa kila mmoja wao kulingana na hali na mali hivyo kufikia kuwapeni dhamana kubwa ya kusimamia UHURU, HAKI na USAWA kwa wawananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapodharau vitu hivi kama chimbuko la WATU wenyewe kwa kuaminishwa kwamba tunaweza kuwazuia WATU kutoamini (exclusive) badala ya kuwawezesha wao kutumikia imani zao kama sehemu ya jamii yetu (inclusive) basi tuondoe tumaini la ushindi ifikapo 2015.
Waheshimiwa,
Toka kujiunga kwangu JF nimejifunza mengi sana na nimepanua kiwango changu cha ufahamu wa Mtanzania hasa ktk hali ya Umaskini, Ujinga na maradhi. Nimeweza kuzifukua nyoyo za watu katika maabara ya fikra, hisia na kutazama tatizo hasa linatokana na ukweli upi. Hivyo kama saini yangu (signature) miaka yote hapa JF isemavyo (signature) ni wajibu wangu kuendeleza kile nachokiamini ktk ku explore reality, na nimegundua rasilimali kubwa ambayo chama kinachotaka kuongoza kitakumbana na vikwazo gani na kwa gharama gani. Hivyo kughairi haya ni sawa na kutafuta dhahabu, mafuta au gasi ktk nyanda za mbuga tupu au jangwani..
Hata wachimba Dhahabu, mafuta au gasi nchini huanza na exploration wakajua maliasili hizi zinapatikana wapi precisely, kisha ndio shirika la uchimbaji huchukua report hiyo na kuifanyia kazi.. Hii ndio kazi yangu kwa leo. Kazi yangu ni kuwapa ushauri viongozi wa Chadema tokana na utafiti wa mijadala mbalimbali na hapa JF na nje ya ukumbi huu ktk mkusanyo wa fikra mbalimbali zinatujenga jamii hii ya Kitanzania.
Waheshimiwa,
Kama tulivyowahi kuzungumza awali kuhusu nafasi ya Chadema ktk utawala na maandalizi ya chama kugombea mwaka 2015, bado nina imani kubwa na chama lakini bado kabisa chama chetu kimeshindwa kupasua ngome ya CCM ipaswavyo na kujenga imani za wananchi kwa chama hiki. Kinachotokea ni kujaribu kwa chama chetu kuwavuta wanachama wa CCM zaidi ya kuwavuta wananchi kuichagua Chadema. Kauli mbiu kama VUA GAMBA vaa GWANDA ni moja ya kauli nyingi zilizoonyesha wazi vita ya chama hiki ni kupambana na uongozi wa CCM badala ya kupambana na sera za CCM zilizotufikisha hapa tulipo.
Ebu tutazame Mchambuzi ktk mada yake utagundua kwamba Chadema inajaribu sana kufanya wajibu wake ‘Do the right thing' kukemea Ufisadi, utawala wa mabavu, mapungufu ya JK na kadhalika lakini tumeshindwa kuyafanya ipaswavyo ‘Do things right' hivyo tunashindwa kujenga uaminifu kwamba Chama hiki kitaweza kurekebisha kero za wananchi. Na hivyo wale walioko vyama vingine mbali na CCM wamekosa tujmaini, wale wasiokuwa na mapenzi ya siasa hawana imani na vuyama mvyote na hata wale wanaokichuka chama CCM hatuwapi matumaini isipokuwa kujiunga chama uanachama..
Waheshimiwa, sio mwanachama atakaye tupa ushindi mwaka 2015, bali mwananchi mlalahoi anayetakiwa kwenda ktk sanduku la kupiga kura siku ya Uchaguzi na kutupa imani yake kwenye kipande cha karatasi kama tumaini lake kwa miaka mitano ya uongozi wa nchi hii..
Ndugu Mchambuzi kaorodhesha mambo tisa na haya yana umuhimu wake ktk kumtambua adui yako ngao zake.. Japokuwa ngao hizi haziwezi kuwapa ushindi pasipo mashambulizi ya nguvu ambayo yanategemea na silaha walizonazo..Hivyo katika mada nzima ya Mchambuzi tumeona ngao kubwa za chama CCM ambazo zinaweza tu kutupa matumaini ya ushindi ikiwa tutaweza kuwa na silaha za kuzibomoa.
Hapo hapo tukumbuke tu kwamba nasi tuna ngao gani ambazo zinaweza kuvumilia makombora ya CCM maana ushindi wa vita hii hautokani na kushambulia tu.. Ukweli ni kwamba Chadema hatuna defence zaidi ya kushambulia na kwa bahati mbaya mara kwa mara hushindwa hata kujitetea isipokuwa wa tu kukimbia kimbia maporini kama wakimbizi wa vita au insurgents.
Na kwa nini basi tumeshindwa kuwa na ngao ktk mashambuliz makali yanayoelekezwa kwetu?. Jibu nalipata kwa Mchambuzi tena akisema hivi:- Leo hii masuala ya Uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya UKANDA, UKABILA na UDINI. Mheshimiwa hili tupende tusipende ndivyo watanzania watawahukumu viongozi wetu kwa sababu ndivyo siasa za nchi hii zimejikita iwe kutokana kupoteza dira ya Kitaifa, kuwepo kwa vyama vingi ama hisia na wajibu wa viongozi wenyewe kuwajibika ktk makundi ya watu wanaowawakilisha.
Waheshimiwa,
Hii ni tahadhari kubwa sana kwa chama na hasa vyama vya Upinzani ambavyo vimetokana ama kuasisiwa na watu waliopingana ndani ya utawala wa CCM hivyo kuanzisha fikra mpya kinzani ili mradi kujaza ubao wakati nyuma ya pazia hilo kuna KUJUANA..Ni rahisi kusema CCM imeshindwa kutuongoza kwa miaka 50 na watu wakakuelewa lakini ni vigumu sana kuwavuta wananchi ikiwa wataona chama kimeshindwa kupambana na siasa za KUJUANA ndani yake hivyo nje wataweza vipi?.. maana tunawalaumu CCM kwa kujuana lakini pia vyama vyote nchini vinafanya mambo yake kwa KUJUANA.. na pale ngome hii inaposhambuliwa vyama hivi hushindwa kujitetea.
Naye Profesa anawekamaswali yanayowakabiri wananchi wengi sana naomba ninukuu.. anasema kuhusu vyama vyetu vikuu vitatu kati ya CCM, Chadema na CUF ya kuwa –
"Nani kati ya hawa watatu ambao bila ubishi wanashikilia hatamu ya siasa za Tanzania, atatupeleka kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini au kiasili? unahitaji nini kati yao, moja wapo ya chama hiki au Kiongozi kati yao atakaebadilisha upepo na kutuepusha na mgao unaofanywa na vyama vyote hivi (kwa manufaa ya hao wanaoongoza vyama hivi kwa kuwa wanataka kuendelea kuwepo madarakani?) Huko madarakani kuna nini?
Nani atatuambia tutatokaje na siku moja itakayolengwa kwa sisi kuwa sehemu ya taifa Afrika, au Duniani imara kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimaendelo kwa ujumla (sayansi, usalama wa chakula, nafasi sawa ya elimu kwa wote, huduma za afya wote, maji safi kwa wote, ziada ya fedha, dhahabu na mafuta ambavyo tunavyo na kila mtu akimvumilia mwenzake na kumheshimu)."
Waheshimiwa,
Mawazo haya sii ya kutafanyia mzaha hata kidogo. Ni mawazo yanayofikiriwa na Watanzania wengi nchini, Watanzania ambao wanajaribu sana kutazama chama mbadala ambacho kinajaribu kwa kila hila kuwajumuisha watu wote ktk Utanzania wao pasipo kujali tofauti zao. Na hatuwezi kuwezesha jambo hili pasipo kuwaunganisha (Inclusive) kama jamii moja badala ya kuwatenga (exclusive) baadhi kwa fikra za kwamba ni wao, wale, hawa ni tofauti na sisi hivyo kama wanataka wayapendayo wafanye wenyewe hili sii jukumu la serikali au uongozi kuwavuta hawa ndnai ya jamii yetu..
Waheshimiwa,
Ndugu Ibambasi katika makala yake naye pia amehoji ushiriki wa serikali hii ktk shughuli za dini, amehoji mambo mengi japokuwa kajiweka ktk kundi la wale wasiokuwa na imani za kigeni isipokuwa za jadi zetu na kudai haki yao kikatiba ili kulindwa na kupewa fursa sawa ktk kushiriki ibada zao. Binafsi yangu pamoja na kutokubaliana juu ya tafsiri fasaha ya ibara inayozungumzia kuwa NCHI yetu haina dini isipokuwa WANANCHI wake ndio wenye dini hushindwa kuelewa nini maana ya NCHI na nini maana ya WATU ikiwa serikali haitawawezesha watu wake wenye dini zao kushiriki ktk ibada zao. Lakini ni muhimu kuyasikia maombi, mawazo kama haya na kuyapatia majibu wala sii kuyapuuza ama kuyazuia kunaweza kutupatia ufafanuzi kamili..
Nchi yetu haina dini kwa maana kwamba mihimili ya utawala wa nchi yetu haitakiwi kuundwa ama kujenga policies zinazotokana na imani ya dini moja isipokuwa serikali inawawezesha wananchi wenye ibada zao. Kuwakwaza wananchi kuabudu kama walivyofanya China na Urusi ni kuondoa ama kupokonya sehemu isemayo watu wake wana dini. Kupingana na mawazo ya kiimani kwa kutunga sheria moja kwa wote itatafsirika tu kama exclusive ama sheria ya kuwatenga wao hivyo kuzaa underground movement kupingana na sheria hiyo. Imetokea sana nchi zilizowakwaza waumini wa dini au kuwayenga makabila kama Wayahudi nchi za Ulaya.
Na Mataifa makubwa yote tokea Roman Empire hadi utawala wa Marekani leo wameanguka ama kupata mtihani mkubwa pale wanapojaribu kuwatenga watu kwa kutumia dini, kabila au tamaduni zao hivyo ni muhimu sana kwa chama hiki kuzingatia pamoja na kwamba serikali haina dini lazima tukumbuke wananchi wetu wana dini zao na makabila yao, wana maumbile yao hivo ni lazima vienziwe na sio kupigwa vita. Tunapiga vita wale wanaojaribu kukwaza wengine, wale wanaojaribu kuleta Ukabila na Udini (kudharau wengine) lakini sio wale wanaoitaka haki ya kuabudu kama alivyosema Ibambasi kwa utetezi wa waumini wa jadi..
Waheshimiwa, Inabidi nikomee hapa ktk waraka huu ambao unasisitiza zaidi kujitazama upya. Kutazama makundi ya jamii zetu kama sehemu ya Utaifa wetu badala ya kujaribu kuwabadilisha ama kuwakwaza. Chadema ktk hali hii inahitaji sana nguvu ya Watanzania wapiga kura ambao kwa nafasi zao hawawezi kushawishika na Utaifa ulojaa KUJUANA na sii rahisi wanaongoa watu wasikuwa na Imani.
Hivyo, Tuache UNAFIKI, tuache kujidanganya kwa unafiki wa wapambe wa vyama wanaotumia siasa kaa uwanja wa kujuana. Sisi sote ktk nafasi tulizopo na kutambua kwamba Utanzania wetu unajumuisha tofauti zetu za maumbile, makabila na imani za dini na yeyote atakaye jaribu kumdharau hata mmoja wetu ni kielelezo cha Ubaguzi ambao hautakiwi kupewa nafasi bali kuupiga vita. Hizi ndio ngao zetu, ndizo zinazo tu identify kama jamii ya Kitanzania na lazima tuzilinde dhidi ya siasa za chuki na uutengano. Bila utayari wa kuwajumuisha watu wote kwa tofauti zao kama sehemu ya Utanzania wetu itakuwa vigumu sana kupata ushindi mwaka 2015 maana CCM wanaifanya kazi yao ipaswavyo – Kushambulia nasi ktk kujilinda lazima tuwe na kinga zetu kwa kufanya vitu sawa – Doing things right !
Nawakilisha..

Last edited by a moderator: