Ok nimekupata,sasa kwahiyo musikilize malalamiko ya waislam ama muweke viongozi waislam,maana hizo ni strategies mbili tofauti.Naomba ushauri wako hapo.Mana siamini kama nyie chadema mtaweka viongozi waislam ili wawakilishe mambo ya waislam peke yao,kwasababu tukisema hivyo,je ina maana wakristo wanawakilishwa chadema na viongozi wakristo?can you see where I'm coming from?
Kama umewahi kunisoma ktk mada tofauti siku zote hupingana na hili neno UUWIANO. Silipendi silipendi lakini nakumbuka kwa mara ya mwisho nilipokutana na Kitila alinambia "hili swala huwezi kuliepuka ktk siasa za Tanzania". Litakuwinda maisha yako yote na huwezi kuwafahamisha wananchi wakakuelewa. Siku zote Watanzania hupima quantity na sio quality ni mila na desturi za maskini. na tumeyaona ktk mfumo wa Utawala wa Jamhuri yetu, bungeni na hata lawama ktk wizara, mashirika ya Umma na kadhalika. sasa nataka tujiulize kwa nini Bima ililalamikiwa kuwa na Wanyakyusa wengi wakati ulee ikiwa bonge la scandal?. Hivi kweli TZ watu hawa ajiriwi kutokana na KUJUANA? kama ndivyo kwa nini tusitazame kwanza makosa haya isipokuwa tutazame makosa ya wale wanaolalamika na kudai kuwa wanataka wapendelewe wao wakati tayari wameisha pendelewa wengine..
Mkuu wangu pamoja na kuwepo ukweli mkubwa kwamba waraka wangu ulilenga tu CDM kuwafikia Waislaam na kujali matatizo yao bado sintosema CDM ifanye nini bora zaidi ya kingine isipokuwa HAKI na USAWA ambao utaweza kuonekana kwa watu maskini ambao wanataka kutoka. Changes haziwezi kutokana na kuiondoa CCM madarakani bali promise ilingane na kutoa majibu ya kuutawanya mfumo mbovu uliopo na tukigusia sehemu ambazo wananchi wanazilalamikia.
Binafsi yangu siwezi kutumia uuwiano hata siku moja lakini lazima nitajaribu kuepuka lawama... Unaweza kuweka viongozi wengi wa kiislaam kama CUF lakini hawana mchango wowote kwa wiaslaam zaidi ya kulitumia jukwaa lao. Muulize Muislaam yeyote CUF imekuwafanyia nini ktk maisha yao zaidi ya kuwajaza chuki kwa Wakristu na Chadema. hawana la kusema na wala viongozi wa CUF hawana mpango wowote wa kuboresha maisha ya waislaam zaidi ya wakristu isipokuwa maskini wajinga wameuvaa mkenge. Ukitazam CCM yale yale lakini hii haina maana Waislaam hawana matatizo. Kubuka tunazungumzia waislaam kwa sababu umeelekeza swali lako kwao wao na sii Wapagan au Wasukuma na Bulyanhulu, Wamasai na Loliondo..
Huu ni mfumo wa maisha ya mtu maskini kutaka kutoka tu, sana sana viongozi wa CUF husali misikiti ile ile wanayosali Waislaam wengine na wakiombwa hela za lunch, lift na kutuliza njaa ya siku wakilishwa samaki..Ni mfumo wa kujuana tuloujenga toka Ikulu kuomba rais ajaye awe mtu wako ili akutoe, mawaziri wetu, makatibu, na hata wabunge wetu kazi yao kubwa ni kuondolea watu matatizo ya siku, ukienda asubuhi utakuta msuluu wa wananchi wakisubiri sadaka yao ya siku na ndio maana wanadai mishahara haitoshi. Nchi nzima tunagawiwa sadaka toka Ikulu hadi Mkandara akienda kijiweni ni kuombana hela tu kwa wale TUNAOJUANA.. Na hapa ndipo nadhani matatizo yalipotokana.
Kwa hiyo pamoja na mimi kutokubaliana na uuwiano lakini hatuwezi kuepuka hali hii kutokana na kwamba vyeo, ajira, nafasi, sadaka yaani income kwa ujumla wake nchini inapatikana kwa KUJUANA japokuwa siamini CDM wamepeana ila wapo watu wanaamini hivyo. Hivyo badala ya kuridhisha watu ktk mfumo huu, CDM inatakiwa kuonyesha utofauti (changes) na utofaiuti huo utatokana na CDM kupeleka maendeleo kwa wahitaji wenyewe. Itawafanyia nini wanawake badala ya kuahidi viti maalum kwa sababu chama kinatambua juhudi za wanawake na vikwazo vinavyowakuta ktk maisha yao ya kila siku iwe hata Urithi au ndoa zao. CDM inatakiwa kuonyesha uwezo wa kukabiri matatizo ya Waislaam, wakristu na Wapagan kwa kuwafikia, kuwasikiliza na kuwaahidi kuyatatua maana sio lazima awe Sheikh Ponda ndio mwakilishi wa waiislaam ispokuwa sera inayolenga kuleta haki na usawa..
Hivyo kinachoonekana sasa hivi ni kwamba wananchi hao hawajui hizo change zitakuwa vipi zaidi ya kumwonda CCM madarakani. Wananchi wanalijua hili na wameisha ichoka CCM isipokuwa wanataka kujua wewe CDM utafanya nini tofauti na CCM. Unatuahidi nini kama waislaam walionewa wakati wa CCM na mifano watakupa. hata kama Chadema itashidwa kuwaahidi chochote lakini lazima iwaonyeshe msimamo wake juu ya maswala muhimu ktk ibada zao, malalamishi yao na watu wengine wote walionyang'anywa ardhi zao, nyumba zao, mashamba yao, kazi zao, kodi zao na kadhalika..