CCM na watawala wa sasa....
Oneni waraka wa maaskofu kama ni mrejesho wa dhati na wazi japo kuwa ni mchungu! ( Honest Feedback).
Honest feedback is like a mirror, whether you like it or not that is what you are from the perspective of whomever gives you the feedback.
Kama kusingekuwa na shida inayosumbua watu sio tu wenye akili timamu, wenye exposure ya kutosha na uwezo mkubwa wa kung'amua mambo mazuri na mabaya kwa wakati mwafaka kwa kuwasaidia wale wanaowaongoza, watu hawa (Maaskofu)ambao sio tu wanautashi wa kufuata imani zao wa ustawi wa himaya ya Mungu bali wanawajibu mkubwa wa kukemea mabaya ( whether yanafanywa na waumini wao au bin adam mwingine yeyote) hata kama kitendo cha kukemea mabaya hayo kitahatarisha maisha yao ama uhuru wao.
Siamini shida iliyowapelekea maaskofu hao kuandika waraka huo kwa "waumini wao" ni uchu wa madaraka, au upendeleo wa kuwafanya watu wa sect fulani kushinda katika uchaguzi ujao, au ni chuki dhidi ya watawala wa sasa bali ni sustainability ya ustawi wa wafuasi wao amabayo inaonekana kuzingirwa na choyo, nia mbaya, tamaa, ulevi wa na matumizi mabaya ya madaraka, kukosa mwelekeo, vision vinyu na zaidi kukosa hata aibu pale wanapogundua kuwa walio wengi wanawaona ni wachafu, badala ya kujirudi wanatumia muda na rasilimali zetu kujisafisha.
Naamini pia kuwa hata kama hawa maaskofu wangetumia nguvu ya ziada kuueneza na kuuelezea waraka wao, kama hauna relevance ya kile kilichopo, kama hauna touch ya ukweli, na kama hauna nafasi ya kurekebisha hali iliyopo, waumini wao wangeupuuza, usingekuwa hot cake kama ilivyo sasa. Kwa maana nyingine ni ukweli mchungu kwa wale unaowagusa.
Kwa wakati huu, CCM na watawala waliopo kila wanavyozidi kuukemea na kulalama juu ya waraka kuu wanaufanya uwe popular zaidi, na kujenga hamu ya kutaka kujua kilichomo. Walio wengi mara baada ya kujua hauna ubaya, wanakuwa mabalozi wazuri wa kuueneza na kuuelezea. Labda ni mpango wa Mungu. Kuwa wale walevi wa madaraka waendelee kuupinga ili uzidi kuenea ili awareness iongezeke, maana hili ni darasa lililokuja by default ( ngumbaru) kwa kila mtu bila gharama kubwa. Na kwa akili za binadamu wanadhani wakiongea na wale walioutoa mambo yatakwisha...
Nionavyo mimi swali sio tu waraka wenyewe peke yake, hapana, kinacho watisha CCM ni kwamba hii RATIBA YA UFUATILIAJI iliyowekwa na maaskofu kwamba kila kilichopangwa kinatekelezwa scientifically na kwa ukamilifu ikitekelezwa italeta balaa..maana lazima perfection ya waraka itaendelea kutokana na mrejesho wa wasomaji na reaction ya walengwa, ili siku za mwisho kabla ya uchaguzi hukumu itakuwa wazi kwa wale waraka huu unaowalenga....kila mtu atapata haki yake Mpiga kura na mpigiwa!
Wito wangu, waraka uendelee kusambazwa, na uendelee kuboresha kila wakati kadiri siku zinavyozidi kwenda. Watu na mashirika yanayosimamia utawala bora watoe sponsorships ya kuhakikisha kuwa kila mtu anapata ujumbe uliomo, na waamue wenyewe kama yaliyomo yanawafaa au la, maana waraka huo haulazimishi watu, bali unatoa changamoto, kwanini watawala na CCM wanataka kuwaamulia watu mambo yakujua au kusikia? Wakati ule wa chombo cha habari kimoja(redio na magazeti) waliotulazimisha kusikia yale waliyotaka tusikie umepitwa na wakati.
Sasa hivi kila mtu anataka kusikia kila kitu then afanye maamuzi. Kingunge na wenzio acheni kuwahadaa watanzania, you are not so special to decide for everyone, you must respect other people's opinion and their way of thinking. You are not God fathers of Tanzanian, you have become irrelevant and obsolete...you should thus step back and let the will of people prevail.
Waraka wa maaskofu was a consulted effort, make no mistake kwamba wamekurupuka. It was thought thru well and thoroughly. Kwa sie waamini Mungu amewapa maneno ya kuongea kwa wakati wake ili watu wake ambao ni matajiri mno wenye kila kitu ndani na nje ya ardhi yao, wame tekwa na wajinga na walafi wachache, ambao wako tayari kufanya chochote waendeleze ulafi na dhurumati kwa walio wengi.
Your days are counted enyi iwatawala wabovu na wezi wa mali za walio wengi!