Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

*Laanzisha mafunzo ya kuchagua viongozi bora
*Lasema wananchi wanaburuzwa kwa kukosa upeo
*Latamka siasa na dini haziwezi kutenganishwa

Na Peter Masangwa na Salum Pazi

KANISA Katoliki nchini limeanzisha programu maalumu yenye lengo la kuwafundisha waumini wake namna ya kupata viongozi bora katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.

Mbali na hilo, kanisa hilo limeonya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakipinga viongozi wa dini kuingilia masuala ya siasa na kueleza kuwa kamwe vitu hivyo haviwezi kutenganishwa.

Kanisa hilo limesema Serikali imepoteza imani yake kwa wananchi kutokana na kuendelea kukumbatia mafisadi kwa kushindwa kufikia maamuzi ya haraka ya kesi za tuhuma za ufisadi, jambo ambalo kanisa hio limesema litazidi kukemea bila woga.

Akizungumza katika maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu ya Kutoa Komuniyo ya Kwanza kwa vijana wa Parokia ya Manzese, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Baptiste Mapunda wa Shirika la Wamisionari wa Africa, alisema wakati umefika chama tawala CCM kukubali kubalika kwani Watanzania sasa wameelimika na hawako tayari kuendelea kuburutwa.

"Maovu ni mengi sana katika nchi hii na yanasababisha kuporomoka kwa maadili, ambapo vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa kuyagundua na kuhabarisha umma na sasa wananchi wameshaamka na wanataka demokrasia ya kweli hivyo utawala lazima ubadilike," alisema Padri Mapunda.

Akifafanua kuhusu uchaguzi mkuu ujao mwakani, Padri Mapunda alisema viongozi wa kanisa hilo wamekubaliana umuhimu wa kufundisha waumini wao na tayari wameanza kutoa mafunzo na semina mbalimbali kuwaelimisha namna ya kupata viongozi bora na kwamba viongozi hao watapatikana kutokana na uwezo wao si kwa kutoa rushwa.

"Viongozi wasio na uwezo ndio wanaotumia nguvu kubwa (rushwa) kupata nafasi za kuingia madarakani ambapo badala ya kulitumikia Taifa wanafikiria kujilimbikizia mali ili kufidia gharama walizotumia wakati wa uchaguzi, hivyo tuwe makini nao,"alisisitiza Padri Mapunda.

Alisema wakati wa mabadiliko ukifika hauepukiki hivyo kama viongozi hawako tayari kubadilika mabadiliko yatawabadilisha kwa lazima kwani huo ndiyo mfumo wa maisha ya binadamu.

Alisema suala la ufisadi limekuwa wimbo usio na mwitikio kwa wananchi kutokana na Serikali kuchukua muda mrefu kumaliza kesi za ufisadi jambo ambalo linaweza kupatiwa ufumbuzi mapema.

Alisema maovu yanayoendelea kutokea hapa nchini kama yale ya ufisadi na mengine yanatokana na ubinafsi, mmomonyoko wa maadili na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa watu wachache wenye nafasi za juu Serikalini.

"Tatizo ni ubinafsi wa watu wachache wenye tamaa ya kujilimbikizia mali ndio unaoumiza Watanzania wengi," alisema na kuongeza kuwa ni "Nguvu za Mungu pekee ndizo zitakazosaidia kupiga vita ufisadi huu unaoshamiri kwa kasi"

Alisema neno, 'ufisadi' na 'rushwa' sasa yamekithiri katika vinywa vya Watanzania na kuonya kuwa hali hiyo inaonesha kuwa sasa wamechoka na wakiamua kupambana na uovu huo wataweza.

Alisema ipo haja ya kufanyika mabadiliko Katiba kwa ya sasa imejaa viraka na haitoshelezi mahitaji ya demokrasia ya kweli.Alieleza kuwa hali hiyo inayotoa nafasi kwa watu kufanya maovu wanavyotaka bila ya kuchukuliwa hatua stahiki.

Alisema kuwa Katiba hiyo ni ya muda mrefu na ina maelekezo yaliyopitwa na wakati hivyo haikidhi mahitaji ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia na inachangia kukwamisha maendeleo ya Taifa.

''Tunahitaji mapinduzi ya kikatiba wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu kwani hata mtu asiye msomi anaweza kugundua udhaifu wa Katiba yetu na kama viongozi hawatakuwa tayari nguvu ya watu italeta mabadiliko,"alisema.

Padri Mapunda aliongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeshindwa kuonesha demokrasia ya kweli kwa kushindwa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi jambo ambalo linasababisha vyama vya siasa kulalamika kila uchaguzi unapofanyika kwa kutotendewa haki.

Alisema NEC inateuliwa na viongozi wa chama tawala na wakati huo huo inasimamia uchaguzi wa viongozi wa vyama vyote ambapo mwanya wa kupendelea CCM unakuwa mkubwa.

"Hakutakuwa na amani hadi mabadiliko haya yafanyike kama jipu litaendelea kupakwa mafuta ipo siku litapasuka tu, hivyo ni bora marekebisho yakafanyika mapema kuliko kusubiri misukumo kutoka kwa wananchi waliochoshwa na Katiba hiyo," alisema.

Amevitaka vyama vya siasa kuacha ubinafsi kwani ni vigumu kwa chama kimoja kuchukua nchi kwa sasa ikiwa havina ushirikiano na badala yake vinapaswa kuweka malengo ya muda mrefu kwa kuzingatia maeneo ambayo vinaweza kuunganisha nguvu na kuweka mgombea anayekubalika na wengi.

Alisema kuwa malumbano baina ya vyama vya upinzani yamezidi kushamiri kutokana na mamluki walio ndani ya vyama hivyo kukwamisha mikakati endelevu na kushindwa kufikia malengo na kupoteza imani kwa wananchi hata pale wanapokuwa na malengo mazuri.

"Malumbano hayo yameikumba hadi CCM kufikia kiasi cha kupigana wakigombe madaraka hali ambayo inadhihirisha kuwa utawala sasa unahitaji mabadiliko kwani baadhi ya viongozi wamekosa uadilifu,'' alisema Padri Mapunda.

Chanzo:
Majira

Animated%2Bline7.gif


animated%2Bupdated.gif


Kupata nakala ya waraka huu, fuata link hii (follow this link): Attachments (waraka wa kanisa)
 
One may criticize catholic church for other things, but in this one the cleric is simply RIGHT!!!!!
If that is the case, wananchi have a credible platform in which to align their wishes and try to reform the constitution, bring real democracy and responsible leadership for the benefit of all Tanzanians.
 
Hadithi ziishe kivipi Junius? Unataka wananchi waelimishwe na nani maana mafisadi wanataka wasubiri siku zifike waje 'wawaelimishe' wananchi kwa kofia, khanga, fulana na kila aina ya takrima. Kanisa endeleeni na moyo huo mzuri!
 
Kama wangesema wanateua watu wa kuwapenyeza kwenye uongozi ningeona ni vibaya. Kwa kuwaelimisha wananchi kuna ubaya gani? Lakini hayo yote ni matunda ya ufisadi. Niliwahi kusoma gazeti moja la Al-Nuur siku za nyuma kwamba mfumo wa kiutawala wa kiraia umeshindwa kwa hiyo walipendekeza mfumo wa Sharia. Anyway kila watu wana muono wao tofauti na wengine katika kui-shape jamii ili maendeleo yapatikane.
 
nilvyoona askofu nilizania pengo nikataka kushangaa tangu lini yeye akapinga ufisadi...
 
Niliwahi kusoma gazeti moja la Al-Nuur siku za nyuma kwamba mfumo wa kiutawala wa kiraia umeshindwa kwa hiyo walipendekeza mfumo wa Sharia.

Buchanan,
Si nilikwambia?
Umeona kilichokuwa kinatafutwa hapo?
 
Mbona haya yalifanyika pia chaguzi zilizopita. Waliwafundisha waumini wao jinsi ya kupiga kula na nani wa kumpigia kula.

Matoke yalipotoka wakatuambia kuwa ni chaguo la Mungu...!

Jakaya Mrisho alipoteuliwa kugombea urais, viongozi mbalimbali wa Kikristo walimsifu sana na kusema eti Roho Mtakatifu amewajia na kuwaeleza kuwa huyo ni chaguo la Mungu...
...Hata hivyo, Askofu Kilaini alipoulizwa kwamba alishawahi kutamka kuwa Rais Jakaya Kikwete ni chaguo la Mungu na hivi sasa ana maoni gani, alisema kuwa kiongozi yeyote anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi ni chaguo la Mungu.

"Ni vema nikaeleweka kuwa maandiko ya Mungu yanasema uongozi na mamlaka yote hutoka kwa Mungu, hivyo basi rais aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe ndilo chaguo la Mungu na sisi tutaendelea kuwa na msimamo huo," alisema Askofu Kilaini
Wamekosa walicho ahidiwa waamua kutamka hadharani.

Kamati hiyo imesema iwapo Bunge halitachukua hatua hiyo, basi kanisa nalo litaomba viti saba vya uwakilishi, wakivigawa vitatu kwenda kwa makanisa ya kiprotestanti yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), viwili Kanisa Katoliki chini ya TEC, na makanisa ya kipentekoste yapate kimoja na kimoja kingine kiende kwa makanisa yanayojitegemea.

Tamko la kamati hiyo, lililosainiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu Mwela na Katibu wake, Godfred Lema, linasema hatua yao hiyo imelenga kuboresha uwiano wa uwakilishi bungeni, tofauti na hali ilivyo sasa.

source: Waraka mzito wa maaskofu kwa JK
 
Halisi,

Kuwa muangalifu na hao "ndugu" zako watakuita mdini ilhali wewe huna mambo hayo na umekuwa ukifanya nao kazi bega kwa bega na always kwako Tanzania kwanza halafu ndio mambo mengine.

Hayo hayo ya "elimu kwa wapiga kura" yangesemwa msikitini au kwenye kongamano la waislam ungeona michango ya "ndugu" zako hapa na hoja za 'kusilimisha" nchi zingemwagwa hapa.

Lakini kwa kuwa wamesema wao wenye haki ya kusema chochote bila kuonekana wadini hakuna taabu hapo.

Tahadhari yangu kwako ni kuwa wewe hawa huwajui, nasisitiza huwajui lakini muombe mola wako uhai mrefu utakuja kukumbuka haya ninayo kuambia. Kwa ufupii tu kwa sura ya nje utawaona "wenzio" lakini wakiwa wao kwa wao wewe sio mwenzao lakini kwa sasa kwa kuwa unacheza ngoma yao watajitahidi kwa kadiri ya uwezo wao wote usilione hilo.

Hii vita ya ufisadi imeficha mambo mengi ndani yake unahitaji miwani mikali kuliona hilo.

Na ndio maaana hakuna atakae kemea hilo la "kuandaa waumini uchaguzi 2010" kwa sasa ni la kwao na tazama choice ya maneno hapo wameitwa "waumini" sio wakristo sasa sijui Kanisa Katoliki litawapata wapi waumini wasio wakristo kuwapa hiyo elimu je hao waumini "wanaoandaliwa" ni waumini wa aina gani hapo? huhitaji kuwa rocket scientist kujua hilo. Na katika hilo zile rhetoric za tusichanganye dini na siasa, nyumba za dini kwa ajiri ya dini tu nk. haina nafasi kwa sasa.

Huu ni wangu wasia nasisitiza ila endelea "kukaa vizuri" na ndugu zako hao ukijua utamu wa mua ukiisha ganda hutupwa!

Masalaam
 
Kama wakatoliki walianza kuelimisha waumini wao siku nyingi na hakukuwa na malalamiko. Sasa hivi malalamiko ya nini? Mbona baadhi ya misikiti ilikuwa inaendesha mazoezi ya kareti kwa ajili ya 'kulinda kura' wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Pia kadi za uanachama za CUF ziligawiwa sana misikitini. So things seems to be more complicated than our simple imagination against only one side and forgetting others!
 
Kama wakatoliki walianza kuelimisha waumini wao siku nyingi na hakukuwa na malalamiko. Sasa hivi malalamiko ya nini? Mbona baadhi ya misikiti ilikuwa inaendesha mazoezi ya kareti kwa ajili ya 'kulinda kura' wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Pia kadi za uanachama za CUF ziligawiwa sana misikitini. So things seems to be more complicated than our simple imagination against only one side and forgetting others!
Taarifa yako yaweza kuwa kweli au si kweli. Ila ukweli sasa umedhihirika.

Rais aliyekuwepo madarakani ndiye chaguo la Mungu. Ukimpinga unapinga chaguo la Mungu na Kanisa.

Hao waliokosa kula (Kura) hawakuwa chaguo la Mungu!

Tuendelee kumuunga mkono kwa kila analofanya... La sivyo tutapata laana toka kwa yule aliye mchaguwa.
 
eti chaguo la mungu.. why wud Mungu give a toss about who gets elected?lol This is just stupidity. Watu wamejaa makamasi kwenye akili let them continue to be controlled by these so called elects-of-god. They are just imposters, their history tells it all.
 
eti chaguo la mungu.. why wud Mungu give a toss about who gets elected?lol This is just stupidity. Watu wamejaa makamasi kwenye akili let them continue to be controlled by these so called elects-of-god. They are just imposters, their history tells it all.

Be careful bro... wasije wenyewe wakakusikia... Oh!
 
eti chaguo la mungu.. why wud Mungu give a toss about who gets elected?lol This is just stupidity. Watu wamejaa makamasi kwenye akili let them continue to be controlled by these so called elects-of-god. They are just imposters, their history tells it all.


For sure they ar elects of gods not our almighty God. Kwani siamini kwamba mungu wetu hatupendi kiasi hiki..
 
For sure they ar elects of gods not our almighty God. Kwani siamini kwamba mungu wetu hatupendi kiasi hiki..
Sasa wewe unapingana na wale walio toa tamko rasmi kuwa Presidenti tuliye naye ni Chaguo la Mungu?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom