Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

Udhaifu wa waraka huo upo kwenye utoaji wa taarifa hiyo. Jukwaa kuu litumikalo kutoa taarifa hizo mpaka sasa hivi ni katika kanisa. Waumini wa katoliki ni yapata asilimia 23 ya watanzania wote. Na wahudhuriao kanisani yahesabiwa kama asilimia 15 ya watanzania wote.

Sasa hebu fikirieni, waraka muhimu kama huo uliochukua sura ya kitaifa kuwafikia wananchi wapatao asilimia 15, kweli huku si kutenda haki kwa watanzania. Nchi ambayo imeamua kuendeshwa bila dini, yaani wananchi wqake wana dini lakini serikali haina dini. Maelezo haya ni lazima yafanyike kwa vitendo.

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?

Ndugu Zawadi kwenye kiingereza kuna kitu kinaitwa "consituency". Sina tafsiri nzuri ya kiswahili ila niseme ni kitu kama "himaya?". Kanisa Katoliki "constuency" yake ni waumini wa dini ya kikatoliki. Kanisa haliwezi kuandika waraka na kuusambaza nje ya waumini wake. Likifanya hivyo litakuwa limekwenda mbali na siyo sahihi. Kanisa lina wajibu wa kutoa elimu ya uraia kwa mambo mbali mbali. Kwa mfano kanisa linapo pinga utoaji mimba na kuzuia matumizi ya condom lengo lake hasa ni kwa waumini wake. Watu wengine wakiamua kufuata wakiona ni vizuri sawa lakini hawawajibiki kufanya hivyo.

Kanisa limeona mapungufu katika katika elimu ya upigaji kura na likaona litowe mwongozo kwa waumini(constituency) wake jinsi ya kuchagua viongozi waadilifu. Mwongozo huu hauwezi kuwa kwa watu wote maana Tanzania ni ya watu wengi zaidi ya wakatoliki. Hata chama kama CCM hakiwezi kutoa mwongozo kwa watu wote ila wa wana CCM maana ndio constituency yake. CCM ikitaka kufanya hivyo itabidi itumie mlago wa nyuma kwa kuigiza serikali ifanye hivyo kama chama tawala si vinginevyo. Hivyo kanisa halijakosea kuwapa waumini wake mwongozo juu ya kuchagua viongozi waadilifu. Watu wengine wakiona mwongozo unafaa wanaweza wakaufuata au wakautupilia mbali.

Binafsi sioni jinsi waraka huu unavyoweza kuondolewa maana wengi wetu tumeusoma na yaliyomo sasa yapo kichwani mwetu. Sasa hao waaskofu watafanyaje ili kuuondoa waraka vichwani mwetu? Waingereza usema " The ginie is alredy out of the bottle!"
 
Last edited:
Tayari CCM wamechelewa. Waraka huu uko kila kona ya Nchi yetu. Kizuri wanachoweza kukifanya ni kuchambua mazuri yaliyomo na kuyaweka kwenye ILANI yao ya mwakani. Itawasaidia sana hata kama watanyambulisha lugha.
Kuna usemi unaosema aliyelala usimuamshe ...kanisa halikuwashitua mapema CCM. Wamejikuta wamekamatwa kwa suprise.Kilichopo si kupinga bali kujenga mazingira ya kupambana na hali halisi iliyopo
 
Magobe T:

Waraka huo ni nzuri. Lakini matatizo yaliopo Tanzania yanajulikana kabisa. Na mafisadi wanakaa katika safu za mbele za misikiti na makanisa. Kama viongozi wa dini wanashindwa kuwataja mafisadi huo waraka utakuwa another piece of crap.

'Coversion' is a gradual process. Inachukua muda mtu kujitambua na kuamini anachohubiriwa. Ndiyo maana pamoja na kuhubiriwa Kanisani, maaskofu wakaona wauhamasishe umma usichague tena viongozi wanaoweka maslahi yao mbele bali wale wanaoonekana kuwajibika.

Kwa bahati mbaya, badala ya kuunga mkono tumewapinga na kuufanya huo waraka usiwe na maana tena bali watu wauogope na waone tu ndani yake kuna udini na nia ya kuligawa taifa. Kama dhamiri zetu hazitusuti kwa hili basi tumeshakuwa 'relativists' kabisa maana kitu kibaya na kizuri tunaona ni kitu kilekile 'depending on how you look at it'.

Tumekwisha! Haya tuliyoyafanya kwa maaskofu tutaendelea kuyafanya kwa watu wengine pia. Kila atakaye simama na kusema kitu Tutaangalia: kama ni wa chama fulani tutasema anatetea maslahi ya chama chake; kama ni wa dini au dhehebu fulani tutasema anatetea maslahi ya dhehebu au dini yake; kama anatoka kabila fulani tutasema anasema analeta ukabila; kama ni tajiri anataka kutunyonya na kama ni maskini tutasema huyu ana nia ya kutuibia tu, hajajitoshereza kifedha! Sasa nani atatushauri kitu? Nani ataweza kukemea maovu kwenye jamii yetu? We've finished ourselves!
 
naunga mkono hoja ya kuwa zitolewe kasoro za huo waraka na sio kusema tu utolewe. nauliza wakatoliki wakianzisha shule/chuo huwa wanatoaga matangazo sehmu ingine zaidi ya makanisani? iweje watu wasio wakatoliki wanpata habari na kujiunga?au kuhudhuria hospitals zao? hii ni wazi kuwa unawagusa mafisadi,hakuna haja ya kuwa na PHD kuelewa hili, waraka unapingwa sababu unawagusa!! ajitokeze mtu aseme waraka huu umecontain 1,2,3...5 ambavyo si sahihi na wananchi msivifuate, More napenda sana wanavyoupinga kwani ndo wanau 'market' zaidi, watu wanautafuta je una nini?u see thats good. mimi bibi kijijini amenidai nimtafutie huo ni kitu gani nikampelekea kausoma aah kafurahi sana.so its a war but ni marketing ya waraka!!kwani hakuna anaebishana na contents
 
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

Udhaifu wa waraka huo upo kwenye utoaji wa taarifa hiyo. Jukwaa kuu litumikalo kutoa taarifa hizo mpaka sasa hivi ni katika kanisa. Waumini wa katoliki ni yapata asilimia 23 ya watanzania wote. Na wahudhuriao kanisani yahesabiwa kama asilimia 15 ya watanzania wote.

Sasa hebu fikirieni, waraka muhimu kama huo uliochukua sura ya kitaifa kuwafikia wananchi wapatao asilimia 15, kweli huku si kutenda haki kwa watanzania. Nchi ambayo imeamua kuendeshwa bila dini, yaani wananchi wqake wana dini lakini serikali haina dini. Maelezo haya ni lazima yafanyike kwa vitendo.

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?

Mdini mkubwa wewe .
Fisadi wewe in kind. Ama la una shida ya uelewa.Watanzania wanakufa kwa ufisadi wewe unalilia waraka ? Naamini baada ya CCM kuutanbua rasmi si waislam watadanganywa ama Wakatoliki na maneno ya CCM.Moto chini na waambiwa Waislam wenzako waje na waraka wao si waliahidi kuja nao ?

Huu si Pendo wala Kilaini anaweza kuutoa mtaani tena .Unazidi kushika kazi na ndiyo silaha pekee imebakia baada ya CCM kutangaza kwamba wao Ufisadi nin sehemu ya sera zao .
 
'Coversion' is a gradual process. Inachukua muda mtu kujitambua na kuamini anachohubiriwa. Ndiyo maana pamoja na kuhubiriwa Kanisani, maaskofu wakaona wauhamasishe umma usichague tena viongozi wanaoweka maslahi yao mbele bali wale wanaoonekana kuwajibika.

Kwa bahati mbaya, badala ya kuunga mkono tumewapinga na kuufanya huo waraka usiwe na maana tena bali watu wauogope na waone tu ndani yake kuna udini na nia ya kuligawa taifa. Kama dhamiri zetu hazitusuti kwa hili basi tumeshakuwa 'relativists' kabisa maana kitu kibaya na kizuri tunaona ni kitu kilekile 'depending on how you look at it'.

Tumekwisha! Haya tuliyoyafanya kwa maaskofu tutaendelea kuyafanya kwa watu wengine pia. Kila atakaye simama na kusema kitu Tutaangalia: kama ni wa chama fulani tutasema anatetea maslahi ya chama chake; kama ni wa dini au dhehebu fulani tutasema anatetea maslahi ya dhehebu au dini yake; kama anatoka kabila fulani tutasema anasema analeta ukabila; kama ni tajiri anataka kutunyonya na kama ni maskini tutasema huyu ana nia ya kutuibia tu, hajajitoshereza kifedha! Sasa nani atatushauri kitu? Nani ataweza kukemea maovu kwenye jamii yetu? We've finished ourselves!

Magobe mbona tuna ukubali kabisa sisi waraka huo na tuna usambaza kwa kasi kubwa ? Hata Radio Mario inatumia muda wake kuusemea ama bado hujasikia ?Waraka unakubalika ila mafisadi ndiyo waoga tu
 
WARAKA WA WAKATOLIKI: MIAKA YOTE NEC WALIKUWA WAPI?

Kanisa katoliki miaka yote unapokaribia uchaguzi huwa wanatoa waraka kama huo kwa ajili ya kuelimisha waumini wao haki za musingi za uraia kabla ya kushiriki uchaguzi. je NEC huwa iko wapi? mbona haijawai kufikia maamuzi kama ya sasa? kulikoni?

Wanatanzania wanapaswa kujua kuwa kanisa, na siyo wakatoliki tu, linawajibu wa kiutume katika kuelimisha wananchi na hasa waumini wao. Lakini pia kanisa linawajibika siyo kuandaa waumini wao kwenda mbinguni tu bali pia kuwa raia wema wanaopaswa kuishi kama raia wengine na kushiriki matunda ya maendeleo ya nchi yao. Kwa vyovyote kanisa haliwezi kunyamaza kama ufisadi unaitafuna nchi. Na hapa halipaswi kuomba kibali cha NEC kwa kuwa linafanya hivyo kwa kutimiza wajibu wake.
 
Ndugu Zawadi kwenye kiingereza kuna kitu kinaitwa "consituency". Sina tafsiri nzuri ya kiswahili ila niseme ni kitu kama "himaya?". Kanisa Katoliki "constuency" yake ni waumini wa dini ya kikatoliki. Kanisa haliwezi kuandika waraka na kuusambaza nje ya waumini wake. Likifanya hivyo litakuwa limekwenda mbali na siyo sahihi. Kanisa lina wajibu wa kutoa elimu ya uraia kwa mambo mbali mbali. Kwa mfano kanisa linapo pinga utoaji mimba na kuzuia matumizi ya condom lengo lake hasa ni kwa waumini wake. Watu wengine wakiamua kufuata wakiona ni vizuri sawa lakini hawawajibiki kufanya hivyo.

Kanisa limeona mapungufu katika katika elimu ya upigaji kura na likaona litowe mwongozo kwa waumini(constituency) wake jinsi ya kuchagua viongozi waadilifu. Mwongozo huu hauwezi kuwa kwa watu wote maana Tanzania ni ya watu wengi zaidi ya wakatoliki. Hata chama kama CCM hakiwezi kutoa mwongozo kwa watu wote ila wa wana CCM maana ndio constituency yake. CCM ikitaka kufanya hivyo itabidi itumie mlago wa nyuma kwa kuigiza serikali ifanye hivyo kama chama tawala si vinginevyo. Hivyo kanisa halijakosea kuwapa waumini wake mwongozo juu ya kuchagua viongozi waadilifu. Watu wengine wakiona mwongozo unafaa wanaweza wakaufuata au wakautupilia mbali.

Binafsi sioni jinsi waraka huu unavyoweza kuondolewa maana wengi wetu tumeusoma na yaliyomo sasa yapo kichwani mwetu. Sasa hao waaskofu watafanyaje ili kuuondoa waraka vichwani mwetu? Waingereza usema " The ginie is alredy out of the bottle!"

Naungana na wewe. Niongezee tu kitu kimoja: 'subject' ya siasa - Serikali - ni 'governance' na ya Kanisa/religious institution ni 'salvation' (righteousness). Mwakanisa au 'believer' ni pia mwanasiasa (kwa maana ya kuwa taxpayer na mdau wa siasa ya nchi yake). Kwa jinsi hiyo, ana embrace Serikali (sheria za nchi) na spiritual values.

Mwisho wa siku, inatakiwa fadhila anazojifunza kwenye nyumba ya ibada zimfanye aishi 'as humanely as possible'. Bila kufanya hivyo, imani imekufa! Ndiyo maana Kanisa, mfano, linaamini 'faith has to be inscribed in responsible social action' na waraka wa Kanisa Katoliki ni namna mojawapo tu ya hiyo 'responsible social action'.

After all, nani anataka aishi kwenye nchi ambayo raslimali zake zinaendelea kutafunwa na wachache na wengi hawana sauti hata za kuhoji? Baadhi ya watu wanafikiri ukiwa kiongozi wa dini huwi tena mwananchi na huna tena haki ya kutoa maoni namna ya kuboresha siasa ya nchi yako. Hii siyo kweli!

Kwani, kukitokea machafuko nani hataathirika? Kwa nini basi viongozi wa dini waambiwe kukaa kimya pindi wanapotoa changamoto kwa uongozi wa nchi? Jesus alihubiri kuleta uhuru kwa maskini na nafuu kwa wanaoonewa... Leo hii, askofu akikemea maovu tunaanza kumnyooshea kidole wakati anatimiza wajibu wake! I bet you; kama CCM ikiendelea kupuuza vilio vya wengi na kuwakumbatia mafisadi, itaanguka tu!

Nani alijua kuwa ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi utapungua/kwisha Afrika Kusini? Nani alijua kuwa chama tawala nchini Malawi kingeshindwa mwaka 1994 maana hakuna chama kilikuwa powerful kama Malawi Congress Party na kilishindwa kwa sababu ya kujisahau na kuanza kuwakandamiza watu wake, huku wakiwa maskini wa kutupwa Dr Banda alitaka kila mwananchi wa Malawi aseme anaishi maisha bora na Rais wao ni wa maisha.

Hatimaye mwaka 1992 Kanisa katoliki likaandika waraka kuitaka Serikali irekebishe baadhi ya mambo katika nchi. Wakati huo ilikuwa marufuku kwa mtu yeyote ile kukosowa Serikali ya Malawi isipokuwa kutaja mema yanayofanyika na Serikali hiyo ma pia kuwa maisha ya watu yalikuwa bora.

Kanisa lilibidi lichague kukubali hali hiyo au kuikosowa with a price! Hivyo, Kanisa liliitaka Serikali kuwapa wananchi uhuru wa kutoa wa kutoa mawazo yao bila kuogopa vitisho vya vyambo vya dola na pia Serikali iboreshe hudama za jamii.

Reaction ya Serikali ilikuwa hivi: waraka ulipigwa marufuku (polisi ilibidi waukusanye ule uliopatikana na kuuchoma moto) na ikatangazwa mtu yeyote atakayekutwa nao atakabiliwa na kosa la sedition; maaskofu waliwekwa chini ya ulinzi na wakaitwa wajieleze kwa Dr Kamuzu Banda kwa nini "wametukana" (maana kimkosoa ilikuwa kumtukana Dr Banda); Malawi Congress Party (MCP) wakaitisha kikao cha chama na kujadili waraka huo na baadhi ya wanachama walipendekeza maaskofu wauliwe, Kanisa katoliki lifungwe kabisa nchini Malawi, walitukanwa hata matusi ya nguoni hadharani na kudharilishwa...

Lakini ya Mungu ni mengi, June 14, 1993 kulifanyika referundum na kukaingizwa sera ya vyama vingi na May 1994 MCP ikaangushwa kwenye Uchaguzi Mkuu! Yako wapi ya kupinga waraka na kutaka kuwanyamazisha maaskofu?
 
Waraka wa kanisa naona CCM umewatishaa sanaa na kingungee alitumwaa tuu na wenzie kuupinga hadharani ila ndo hivyoo tena wananchi wameamka na kuulewaa kadri unavyopingwa..Natoa rai kwa media kuendeleaa na kasi ya kuhabarisha jamii umuhimu wa waraka huu ili wauelewe vema na ifikapo uchaguzi kuanzia SM na ule wa 2010 wachague viongozi na sio BORA VIONGOZI.
 
Hata Kanisa likikubali kuuchomoa, it is too late kwa sababu Speed ya kuusoma imeongezeka na wapiga photcopy sasa hivi wanatengeneza pesa nzuri kwa kazi ya kutoa vivuli.

Labda Sisiemu iwachimbe mkwara na wapiga photocopy.
 
Mugo"The Great";557033 said:
Hata Kanisa likikubali kuuchomoa, it is too late kwa sababu Speed ya kuusoma imeongezeka na wapiga photcopy sasa hivi wanatengeneza pesa nzuri kwa kazi ya kutoa vivuli.

Labda Sisiemu iwachimbe mkwara na wapiga photocopy.

Mugo hii imetulia sana na hapa mwendo Mdundo kanyageni mafuta twende tafadhali .
 
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

[COLOR="Red"[/COLOR][/COLOR]
[COLOR="Red"[/COLOR]
Udhaifu wa waraka huo upo kwenye utoaji wa taarifa hiyo. Jukwaa kuu litumikalo kutoa taarifa hizo mpaka sasa hivi ni katika kanisa. Waumini wa katoliki ni yapata asilimia 23 ya watanzania wote. Na wahudhuriao kanisani yahesabiwa kama asilimia 15 ya watanzania wote.

Sasa hebu fikirieni, waraka muhimu kama huo uliochukua sura ya kitaifa kuwafikia wananchi wapatao asilimia 15, kweli huku si kutenda haki kwa watanzania. Nchi ambayo imeamua kuendeshwa bila dini, yaani wananchi wqake wana dini lakini serikali haina dini. Maelezo haya ni lazima yafanyike kwa vitendo.

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?[/QUOTE

hapa ndugu umebandika kitu gani??? au umelewa??? Hebu angalia upya bandiko lako.
 
Haya malumbano hayana sababu, hayatujengi. Waraka ulilenga kuleta maendeleo kwa kutafuta viongozi waadilifu. Lakini unapoona mwana JF anakaa chini anawaza kidini, anatoa takwimu zisizo sahihi kujenga hoja(eti RC ni 23%! na wanaokwenda kanisani ni 15%), unaanza kuwaza kama kweli kuna tija katika hoja hizi. Tukubali wakati ni huu wa kubadili mifumo yetu ya siasa na kukubali kukosolewa pale tunapokosa. Kwamba tumewachagua mafisadi kutuwakilisha katika chaguzi zilizopita hakuna ubishi, orodha tunayo ni refu. Tuwaache hao RC waelimishane, wenye kupenda kujifunza kwao na wafanye hivyo
 
Waraka ni mzuri sidhani kama Cardinal Pengo atauondoa kwani umeshafanyiwa kazi kwa kiasi fulani. Hao wanaodhani kuwa ni mbaya watujuze ili tuone huo ubaya kwa kuchambua hoja moja baada ya nyingine siyo kulea siasa.
 
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

Udhaifu wa waraka huo upo kwenye utoaji wa taarifa hiyo. Jukwaa kuu litumikalo kutoa taarifa hizo mpaka sasa hivi ni katika kanisa. Waumini wa katoliki ni yapata asilimia 23 ya watanzania wote. Na wahudhuriao kanisani yahesabiwa kama asilimia 15 ya watanzania wote.

Sasa hebu fikirieni, waraka muhimu kama huo uliochukua sura ya kitaifa kuwafikia wananchi wapatao asilimia 15, kweli huku si kutenda haki kwa watanzania. Nchi ambayo imeamua kuendeshwa bila dini, yaani wananchi wqake wana dini lakini serikali haina dini. Maelezo haya ni lazima yafanyike kwa vitendo.

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?

Wewe nadhani ni kingunge na kama siye basi ni mpagani kama kingunge. Huwa unasali kanisa gani? Ni wapi ulikuwa ukichukua attendance ya wahudhuriaji kanisani? Au umetumwa kuropoka??

Hiyo serikali unayojidai kuitetea eti imenyang'anywa kazi yake ilikuwa wapi miaka yote?? Kwa kuwa wamelikoroga basi ndo wanona wanashindwa, taabu inaanza?

Najua wewe ni wale boko haram, tayari mmeambiwa anzisheni wenyewe gulio la kukatana viganja na vikanyagio, sasa tusikie tena mnataka sijui nini??

Kazi kupeleka watoto madrasa tu alafu wanaishia kusigina!!!
 
Naungana na wewe. Niongezee tu kitu kimoja: 'subject' ya siasa - Serikali - ni 'governance' na ya Kanisa/religious institution ni 'salvation' (righteousness). Mwakanisa au 'believer' ni pia mwanasiasa (kwa maana ya kuwa taxpayer na mdau wa siasa ya nchi yake). Kwa jinsi hiyo, ana embrace Serikali (sheria za nchi) na spiritual values.

Mwisho wa siku, inatakiwa fadhila anazojifunza kwenye nyumba ya ibada zimfanye aishi 'as humanely as possible'. Bila kufanya hivyo, imani imekufa! Ndiyo maana Kanisa, mfano, linaamini 'faith has to be inscribed in responsible social action' na waraka wa Kanisa Katoliki ni namna mojawapo tu ya hiyo 'responsible social action'.

After all, nani anataka aishi kwenye nchi ambayo raslimali zake zinaendelea kutafunwa na wachache na wengi hawana sauti hata za kuhoji? Baadhi ya watu wanafikiri ukiwa kiongozi wa dini huwi tena mwananchi na huna tena haki ya kutoa maoni namna ya kuboresha siasa ya nchi yako. Hii siyo kweli!

Kwani, kukitokea machafuko nani hataathirika? Kwa nini basi viongozi wa dini waambiwe kukaa kimya pindi wanapotoa changamoto kwa uongozi wa nchi? Jesus alihubiri kuleta uhuru kwa maskini na nafuu kwa wanaoonewa... Leo hii, askofu akikemea maovu tunaanza kumnyooshea kidole wakati anatimiza wajibu wake! I bet you; kama CCM ikiendelea kupuuza vilio vya wengi na kuwakumbatia mafisadi, itaanguka tu!

Nani alijua kuwa ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi utapungua/kwisha Afrika Kusini? Nani alijua kuwa chama tawala nchini Malawi kingeshindwa mwaka 1994 maana hakuna chama kilikuwa powerful kama Malawi Congress Party na kilishindwa kwa sababu ya kujisahau na kuanza kuwakandamiza watu wake, huku wakiwa maskini wa kutupwa Dr Banda alitaka kila mwananchi wa Malawi aseme anaishi maisha bora na Rais wao ni wa maisha.

Hatimaye mwaka 1992 Kanisa katoliki likaandika waraka kuitaka Serikali irekebishe baadhi ya mambo katika nchi. Wakati huo ilikuwa marufuku kwa mtu yeyote ile kukosowa Serikali ya Malawi isipokuwa kutaja mema yanayofanyika na Serikali hiyo ma pia kuwa maisha ya watu yalikuwa bora.

Kanisa lilibidi lichague kukubali hali hiyo au kuikosowa with a price! Hivyo, Kanisa liliitaka Serikali kuwapa wananchi uhuru wa kutoa wa kutoa mawazo yao bila kuogopa vitisho vya vyambo vya dola na pia Serikali iboreshe hudama za jamii.

Reaction ya Serikali ilikuwa hivi: waraka ulipigwa marufuku (polisi ilibidi waukusanye ule uliopatikana na kuuchoma moto) na ikatangazwa mtu yeyote atakayekutwa nao atakabiliwa na kosa la sedition; maaskofu waliwekwa chini ya ulinzi na wakaitwa wajieleze kwa Dr Kamuzu Banda kwa nini "wametukana" (maana kimkosoa ilikuwa kumtukana Dr Banda); Malawi Congress Party (MCP) wakaitisha kikao cha chama na kujadili waraka huo na baadhi ya wanachama walipendekeza maaskofu wauliwe, Kanisa katoliki lifungwe kabisa nchini Malawi, walitukanwa hata matusi ya nguoni hadharani na kudharilishwa...

Lakini ya Mungu ni mengi, June 14, 1993 kulifanyika referundum na kukaingizwa sera ya vyama vingi na May 1994 MCP ikaangushwa kwenye Uchaguzi Mkuu! Yako wapi ya kupinga waraka na kutaka kuwanyamazisha maaskofu?

asante kwa hii post,

CCM kama mnaiga ya Kamuzu banda sasa mmekwisha, na tunaomba Mungu awasaidie Kanisa katoliki wawe na nguvu na wendelee kutusambazia waraka huu hlio bora sana.

"Ee Mungu mkuu uliye Mbinguni na mahali popote na usiyeonekana, mpe nguvu kaldinali Pengo ili asishindwe na mafisadi wa CCM, amina"
 
Hebu mwenye nao autundike hapa JF tuone. Woga ni wanini kama mtu unaona huko safi kimaadili? Hata uwe mkristu au muislamu utachaguliwa kulingana na matendo yako. Waraka unasema na kuhimiza wananchi wawe waangalifu na wagombea, wawtazame matendo yao. Haujasema mtu wa dini ipi ndo achaguliwe, kama ni mkristu na maadili ni mabovu hatapita.
Woga ni yale madudu yalikwisha fanywa na viongozi/wabunge walioko madarakani wakichekecha wanaona hakuna pa kutokea 2010.

Naunga mkono waraka huo.
 
BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA

(TEC)​

MPANGO WA KUHAMASISHA

HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010​

Idara ya Kichungaji

TUME YA HAKI NA AMANI - TEC​

MPANGO WA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI

KATIKA JAMII KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010​

DIRA

Mungu anakuita, anakuhitaji.
Dunia imeumbwa na Mungu ili iendelee kuwa mahala panapodhihirisha Ufalme wa wake. Ukuu wa uumbaji huu ni mwanadamu ambaye ndiye kiumbe aliyekirimiwa utashi na uelewa ili awe mshiriki na mdhamini wa kazi ya Mungu. Mungu ametuchagua tuchukue wajibu huu, na pamoja naye tupunguze uovu na taabu, na kujenga dunia ambamo upendo na maelewano vinamhakikishia kila mmoja kufurahia utu wake.

Kama wakristo, tunapokea mwaliko wa Kristu uwe mwaliko wetu. “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Lk 4: 18 – 19).
Kwa kutilia mkazo mwaliko huu, tunaelezwa kuwa Mwana wa Mtu atakaporudi atayahukumu mataifa kwa kigezo cha huduma tuliyotoa kwa wenye njaa, kiu; walio wageni, uchi, wagonjwa na wale walio kifungoni (rej. Mt. 25: 31 – 46).

Mungu alipomuumba Mwanadamu alimpa wajibu wa pekee, sio tu kuwa mlinzi na mdhamini wa dunia/uumbaji, bali pia kuwa mshiriki katika kuumba, na kutunza. Ni wito wa kushirikiana na Mungu katika kupambana ili kuuondoa uovu katika jamii yetu na kujenga ulimwengu ambamo kila mmoja ana wajibu wa kutekeleza na wakati huo huo ana haki ya kufurahia matunda ya dunia yetu.

Programu yetu ya kulihamasisha Kanisa kutekeleza wito wa kichungaji katika mambo ya kijamii ni kuwatia moyo waamini wote kutambua na kukubali wito wao wa Kikristo, wito wa kuwapelekea watu habari njema ya Yesu katika mambo ya kijamii na ya kitaifa. Kutakatifuza malimwengu, kuifanya nchi yetu na watu wetu kuishi pamoja huku manufaa ya kila mmoja yakiwa yanatimizwa: kupata huduma msingi za maisha na kuheshimiwa utu wa kila mmoja. Hapa maslahi na manufaa ya wote na ya kila mmoja katika jamii yanapaswa kuzingatiwa. Huu ni wajibu wa kila mmoja.

Mungu anakuhitaji, haya si maneno tu, bali ni uamuzi wa makusudi wa Mungu anayetukabidhi wajibu huu. Kutopokea mwaliko huu unaotoka kwa Mungu ni kushindwa kutimiza wajibu wetu, ni dhambi ya kutotimiza wajibu wa wito wetu wa Kikristo. Wito wa kutimiza wajibu wa kijamii, ambao ni kutia chachu ya tunu za injili na Mafundisho ya Kristo katika masuala na shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa ya taifa letu.
Wito huu haujaeleweka vema na jumuiya zetu. Watu wengi wanadhani kwamba mambo ya umma sio sehemu ya majukumu yetu ya kidini na kiimani, na hivyo Kanisa halipaswi kujishughulisha na mambo hayo. Kinyume chake Kristo anatualika kuleta mafundisho ya Mungu, maadili ya asili yetu ya kibinadamu kama tulivyoumbwa na Mungu. Tunaalikwa kuyafanya hayo yawe ndio msingi na mwanga unaoongoza maamuzi na sera zetu.

Tunaona kwamba ikiwa maadili hayo yatakuwa sio msingi wa maisha yetu ya pamoja na kuyashuhudia katika utendaji wetu na mienendo yetu, hapo tutaingia haraka katika uovu na ubinafsi na uchoyo, mambo ambayo yanaangamiza jamii yetu.

Katika miaka ya hivi karibuni sote tumeshuhudia haya yakitokea na tumepata madhara yake katika amani na utulivu katika taifa letu. Kumekuwa na mgawanyiko miongoni mwetu, kumejengeka matabaka ya wenye mali nyingi na watu wengi ambao wana mali kidogo sana, maskini na fukara hasa . Mwelekeo huu unatishia na kuhatarisha amani na moyo wa ujamaa tuliokuwa nao na kushamiri kwa utengano na chuki kati yetu.

Sote tunawajibika kwa nchi yetu na taifa letu. Ndio maana Mungu ametujalia sote kuenzi hadhi ya utu wetu sawa. Kwa hiyo tusiruhusu nchi yetu Tanzania ikawa na watu ambao thamani ya utu wao ni zaidi ya wengine. Tusisahau kila mmoja wetu ameumbwa katika sura na mfano wa Mungu (Taz. Mwa 1: 2.

Ni kwa sababu hiyo tunazindua programu hii ya kuhamasisha jumuiya zetu kuelewa wito wao wa kijamii, kuinjilisha na kuifanya jamii yetu iwe ya kiutu kulingana na mpango wa Mungu wa uumbaji na haswa kwa jamii ya wanadamu. Msingi wa utu wa mwanadamu ni asili yetu ya kwamba tumeumbwa na Mungu. Huu ndio msingi ambao dini zote zinausadiki na kuuheshimu. Kwa hiyo tunaweza kushirikiana na waislamu, wahindu, na watu wenye kufuata dini za jadi. Sote kwa pamoja tujenge dunia yetu kulingana na mpango wa Mungu.

WITO

Tumetumwa katika jumuiya zetu, Parokia na jumuiya ndogo ndogo, kuwahamasisha watu wafanye tafakari juu ya hali halisi ya maisha na kujua ni kwa namna gani mafundisho ya Kanisa na Injili yanatupatia mwanga wa namna ya kuboresha maisha yetu na katika Taasisi za jamii yetu. Tunachukua hatua katika kurekebisha mambo yanayokwenda vibaya na kuimarisha mambo mazuri. Ni mwaliko wa kuwasaidia watu katika kutekeleza maamuzi yaliyothibitishwa katika ahadi yao waliyoweka wakati wa ubatizo.

Hatua zifuatazo zinapendekezwa kutumika katika utekelezaji:
- Kuchunguza hali, kutambua na kubaini tatizo.
- Kutumia Mwanga wa mafundisho ya Kristo na kutoka katika Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
- Kuamua hatua ya kuchukua na namna ya kufuatilia utekelezaji.

UTARATIBU WA KUZINGATIA (METHODOLOJIA)

Programu hii ya kichungaji inahitaji uongozi mzuri na hatua madhubuti za ufuatiliaji. Hapo tutaweza kufanikiwa na kuleta matokeo katika maisha ya Jumuiya ya Kanisa na ya taifa letu.

Katika hatua ya utekelezaji wa programu hii tunapendekeza:

1) Kufanyika mikutano ya makleri na viongozi wa halmashuri walei. Ni lazima katika mkutano huu ijadiliwe programu hii katika ngazi ya Jimbo na kupewa umuhimu unaostahili.
2) Wajumbe wa Mkutano huu: Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani watakuwa wakufunzi – kueleza na kufafanua mada za programu yetu.
3) Katika kazi ya kuongoza mkutano (no. 1), wajumbe wa CPT na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi.
4) Inapendekezwa paundwe timu ya Jimbo kwa ajili ya ufuatiliaji wa programu hii.
5) Katika ngazi ya Parokia programu ilenge kufundisha wanavijiji/watu mitaani na katika Jumuiya Ndogo Ndogo ili waweze kujadili masuala yaliyomo katika programu.
6) Ripoti za majadiliano hayo zitumwe Parokiani (Paroko na Halmashauri) kila baada ya miezi mitatu. Ripoti hizo zionyeshe mambo yaliyojadiliwa na maamuzi yaliyofikiwa.

Kwa kupata uelewa zaidi mada zilizojadiliwa katika mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani (TEC) ni:
1) Vipaumbele kwa mujibu wa Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
2) Umuhimu wa uongozi wenye maadili katika kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini katika Tanzania.
3) Mfumo wa Sheria Tanzania: Nguvu na Changamoto.
4) Haki za Binadamu katika sera za biashara na fedha.
5) Mtazamo wa kimaadili katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi.
6) Hifadhi ya jamii.

Mada hizi zinapatikana kwa kiswahili na kiingereza, kama unazihitaji wasiliana na:
- Ofisi ya CPT - St. Josephs Cathedral Dar es Salaam
Tel: 022-2127675/0713-329984
E.mail: cptprofessionals@yahoo.co.uk

Tunaweza pia kukusaidia kupata Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa utatujulisha mahitaji yako.

MADA KUU ZA TAFAKARI​

Agenda hizi ndizo zilizoazimiwa katika Mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani TEC uliofanyika tarehe 20 – 22 Januari, 2009.

1. UTU
Utu aliokirimiwa kila mwanadamu bado haujawa ndio kiini na msingi wa mienendo yetu kama watu binafsi, katika vikundi na kama jamii. Kasoro hii tunaiona katika jumuiya za kidini, katika mila, desturi na tamaduni zetu, katika shughuli zetu za kiuchumi na katika uwanja wa kisiasa.

Kila mwanadamu ana utu sawa na utu wa mwingine na kwa hiyo lazima utu wa kila mmoja uheshimiwe na wengine: watu binafsi, taasisi na utawala. Ikiwa mwanadamu anapewa hadhi kutokana na utu wake, na haki zake atajengeka na kuwa na utu kamili, na yeye mwenyewe atajenga uwezo wake kikamilifu.

Vile vile bila kufanya hivyo jamii yetu haiwezi kamwe kukua na kuwa jamii yenye watu wenye kuenzi ukweli, utu na usawa. Kuigawa jamii katika matabaka ni kosa na ni dhambi, licha ya kuwa huko ni kuzuia jamii kufikia uwezo wake kamili na kuwa jamii yenye furaha. Katiba ya Jamuhuri imeweka bayana kwamba haki, wajibu na uhuru wa binadamu lazima vilindwe, viheshimiwe na kutolewa sawa kwa wote.

Kwa hiyo tunapaswa kufundisha watu dira hii katika:

- Ngazi ya familia, katika ujirani na Jumuiya ndogo ndogo. Ni hapa ndipo msingi wa jamii na kanisa unapojengwa.
- Katika mashule, tuangalie upya sera zetu za elimu na malezi na upande wa kimaadili tuchunguze yaliyo katika mitaala na ratiba katika mashule. Kwa sasa hakuna msisitizo wa kutosha katika malezi ya ubora/sifa za kiutu.
- Katika mambo ya kisiasa na kiuchumi: heshima na utu wa mtu sio suala la kubaki katika maneno na hotuba nzuri na matamko. Taasisi na sheria zetu lazima zikumbuke kuwa kanuni za kimaadili yapasa ziongoze kazi yao.
- Katika ngazi za Kanisa: mkazo zaidi uwekwe katika kuwajenga watu katika mambo ya kiroho ambayo ni ya lazima katika kuongoza tabia ya kijamii. Hapa ni zaidi ya kuweka kanuni na taratibu. Kinachohitajika hasa ni roho ya kiinjili na wito wa kinabii.

Mambo yanayopendekezwa kufanywa katika kufundisha na kuhamasisha utu ni:
- Mafungo katika ngazi ya Parokia na taasisi za Kanisa.
- Mikutano na wazazi ili kuwahamasisha na kutafakari namna ya kufundisha maadili katika ngazi ya familia.
- Semina na Waalimu.
- Kujadili na mamlaka ya elimu ngazi ya wilaya na mkoa.
- Tathmini ya kiroho ili kupima mambo ya kiroho na kupendekeza dhamira za kichungaji ambazo zinaweza kutumika katika mahubiri na miongozo ya katekesi.
- Kufanya utafiti katika ngazi ya Parokia ili kujua nini vijana wanapendelea na kutafuta njia ya kuwajengea hadhi ya utu wao kwa kutumia mambo yanayowavutia vijana.
- Kuchunguza vitabu vinavyotumika mashuleni kama vinahimiza au vinachochea maadili mema.

2. UONGOZI
Dira
Suala la uongozi ni pana. Kuna aina nyingi za uongozi (kiroho, kiutamaduni, kielimu, kiutawala, kisiasa, kiuchumi). Vile vile zipo ngazi mbalimbali za uongozi (familia, ujirani, vijiji, taasisi, kidini, kitaifa). Uongozi unahitaji watu wenye sifa ya huduma, wanaojali, walio wazi, wanaowajibika, wanyenyekevu, wenye hekima na upendo. Uongozi kila mara unashawishika kutenda kinyume na hayo na kuwa na uchoyo na kutumia madaraka vibaya. Kwa hiyo ni muhimu kuandaa viongozi, kushirikiana nao na kushikamana nao na kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuwa jasiri walio waaminifu katika kazi zao.

Hali yetu inadhihirisha kuwa:
- Katika miaka ya hivi karibuni tumeona matatizo mengi ya uongozi. Kwanza kabisa yapasa tujadili kiini chake na kisha tutafute tiba yake.
- Katika uwanja wa kisiasa tunapaswa kuangalia namna wagombea wa na vyoteuliwa na vyama vyao. Tunahitaji kutafuta taarifa ya njia na vyanzo vya upatikanaji wa fedha za vyama vya siasa na namna wanavyozitumia. Watu wajadili kama mfumo wa uwakilishi kiuwiano (proportional representation system) haungeweza kuwa bora kuliko ule wa sasa. Kuna haja kubwa pia ya kusaidia watu kuijua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Ni lazima katika mambo ya kijamii tuwahimize watu kueleza matatizo wanayokumbana nayo katika maisha yao na kuyatolea taarifa katika ngazi ya Parokia hadi Jimbo/Wilaya. Tuwasaidie kushiriki katika utawala tangu ngazi ya Serikali za kijiji/mitaa hadi ngazi ya halmashauri ya wilaya na kutafuta taarifa kisha kufuatilia nini watumishi wa umma wanafanya katika kuhudumia watu. Njia nzuri ni kuanza na kundi mahalia kushughulikia matatizo ya hapo walipo.
- Katika Kanisa tuhimize watu kutoa maoni yao katika Jumuiya ndogo ndogo na kusaidiana kuwa waaminifu katika wito wa Kikristo. Jumuiya ya Kanisa ni mahala ambapo mtu anakuwa na nafasi ya kutimiza wajibu wake wa kushiriki vilivyo katika shughuli za jumuiya. Hiarakia ya Kanisa haimaanishi kuwa ni kutoa amri tu kwa watu wa ngazi ya chini, bali kazi ya Hiarakia ni kuongoza namna ya kutimiza ahadi tuliyoweka wakati wa ubatizo.

Kwa agenda hii tunapendekeza:

Katika ngazi ya kisiasa: kuunda timu ya CPT na wajumbe wa halmashauri kutengeneza maswali maalum, kuendana na hali mahalia, watu wajadili na ili kutoa mawazo na maoni mazuri, wapatiwe habari zinazohitajika kwa ajili ya tafakari. Hapa tusiwape nafasi wale ambao ni wagombea wa kisiasa kutawala mjadala.

Kijamii: Watu watafute ni mashirika gani yapo hapo na huduma zipi hutolewa, na wangeweza kupata msaada gani katika kutatua matatizo yao. Ni taarifa gani tunapaswa kuwapatia watu ili waweze kufanya tafakari katika Jumuiya ndogo ndogo.

Kanisa: Tunawezaje kuimarisha tafakari katika jumuiya juu ya namna Parokia inavyoendeshwa. Halmashauri inafaa iwe chombo ambamo tathmini hiyo inaweza kufanyika. Ikumbukwe Parokia sio chombo cha utawala, bali lazima iwe ni jumuiya hai ya kusaidiana katika kuleta ubora wa maisha ya kiimani, matumaini na mapendo. Kwa pendekezo hili tufanye tathmini ya kiroho katika dhamiri na kuweka ahadi ya uwajibikaji katika kuwa zaidi mashahidi wa ujumbe wa Kristo katika hali halisi ya Tanzania leo.

3. HAKI

Dira
Lazima mfumo wa sheria uwe ni kwa ajili ya jumuiya ya watu katika kulinda na kudumisha amani, ukweli, haki, uhuru, mshikamano na usalama. Mfumo huu unapoleta ukosefu wa haki, watu wanapoteza imani nao.

Tutafute:
- Kwa njia gani tutawasaidia watu kujua haki zao na kuelewa sheria zinazoathiri maisha yao.
- Kuona kama shule zetu zinafundisha Katiba ya nchi na umuhimu wake.
- Tuone kama Wabunge wanawasiliana na majimbo yao na kuwa kweli wawakilishi wao. Kujadili kama wanadhibiti ya kutosha utendaji wa serikali. Ni kwa vipi watu wanapeleka masuala yao katika vyombo vya serikali na kusikilizwa?
- Mahakama za mwanzo zinahudumia watu wengi lakini ziko katika hali mbaya. Je, tunaweza kuziboresha vipi?
- Watu wanaona adhabu zinatolewa kwa makosa madogo, lakini wenye makosa makubwa, wanaachwa tu. Kwa nini watu wanafikiri hivi?
- Lazima tufikiri njia mbadala ya kutoa adhabu na kuona wafungwa kama watu wenye haki pia. Vile vile kutambua kuwa lengo la magereza ni kujenga amani na kurekebisha watu waliofanya makosa.
- Kila mara mfumo wa sheria unafanya kazi taratibu na hivyo watu husubiri mno haki kutendeka. Kukosa ufanisi na utaratibu wa utekelezaji vinasababisha ukosefu mwingi wa haki. Tunawezaje kuboresha hali hii?
Katika mjadala tulenge kuona kwamba “Mamlaka za siasa zichaguliwe na uamuzi wa hiari wa raia, nazo lazima zijali kanuni ya “utawala wa sheria,” ambamo ukuu ni wa sheria na si wa matashi ya watu wasio na sheria.”1

4. BIASHARA NA FEDHA

Dira
Hizi ni taasisi za biashara na fedha na shughuli nyingine zinazotoa huduma katika jumuiya. Biashara zinazotoa mahitaji ya vitu/bidhaa na kubadilishana na bidhaa hizi. Taasisi za fedha zinatunza thamani ya fedha, kwa kuweka kiwango cha kubadilisha fedha.

- Katika biashara, motisha haipaswi kuwa katika faida tu. Biashara inawafikishia watu bidhaa, hivyo isiendeshwe kiunyonyaji.
- Ni vipi tunaweza kuwasaidia watu kutetea maslahi yao na kuzuia wasinyonywe.
- Moyo wa ushirika umepungua mno na matokeo yake watu wameathiriwa na biashara zilizokosa uwaminifu. Tunawezaje kusaidiana.
- Mfumo wetu wa benki unafikisha huduma kwa watu wachache tu, na hasa kwa watu wa mijini na kwa wale wenye kiwango kizuri cha kipato. Lazima tusaidiane, hasa wale ambao hawana kipato cha kutosha, kuunda SACCOS na vikundi vya kusaidiana. Kanisa lazima lifanye bidii kuhamasisha hayo.
- Wachache walio katika mamlaka au katika nafasi za juu za utawala wana marupurupu mengi mno. Tusukume kupunguziwa hayo ili wawe na maisha ya kawaida.
- Tuwe makini na uporaji wa ardhi unaofanywa na makapuni makubwa na watu binafsi, matajiri. Tukumbuke ardhi ni ya thamani na ni hitaji la lazima kwa kila mmoja.
- Rushwa katika biashara, huduma duni, bidhaa duni vinaleta sifa mbaya, na hii ni tabia iliyo dhambi. Miongoni mwa watu hali hii inawajengea hasira na kukosa uaminifu na vile vile watu hujitetea kwa nguvu na kujengea watu fikra ya kulipiza kisasi.
- Udanganyifu katika biashara ni kushusha sifa mmiliki kwa wateja.
- Serikali iwe makini katika kuweka mikataba na wawekezaji wa umma na watu binafsi. Imekwishabainika kuwa katika mikataba hiyo maslahi ya wananchi hayalindwi kikamilifu badala yake wawekezaji hupewa unafuu mkubwa kwa kisingizio kuwa ni kivutio kwao.
- Makapuni ya ndani ni lazima yatiwe moyo na kuungwa mkono ili yaweze kuboresha utendaji wao uwe wenye tija.

5. UCHUMI.

Dira
Uchumi ni kwa ajili ya kuhudumia watu ili wawe na maisha mazuri: wapate mahitaji msingi na walindwe dhidi ya hali zinazowakuta na kutishia usalama wao na majanga mengine yanayoadhiri ubora wa maisha. Maadili katika shughuli ya kiuchumi na kuhakikisha mahitaji haya muhimu katika kumpatia mtu maisha mazuri yanapatikana. Sera za kiuchumi ni lazima ziweke kipaumbele kwa kuzingatia maadili na hivyo kufikia manufaa kwa wote na kulinda utu wa kila mmoja. Kwa hiyo tujadili pamoja na kama jumuiya za kanisa ni lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Maoni yetu yasikilizwe na kufanyiwa kazi, tunu za kikristo tunazosimamia zionekane katika sera na katika mgawanyo wa bajeti ya serikali.

- Tunaweza kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa katika nchi yetu ikiwa watu wataelewa wajibu wao na kushiriki katika kutatua matatizo yetu: kwa mfano: kushiriki katika namna ya kupata huduma ya maji vijijini, namna ya kudhibiti matumizi ya fedha zinazotumwa katika serikali za mitaa.
- Ni kwa njia gani madiwani watafikisha maombi ya watu wao katika mgawanyo wa bajeti ngazi ya wilaya.
- Je, matumizi katika serikali ngazi ya chini yanawekwa wazi kwa wananchi kujua?
- Wabunge na viongozi katika ngazi ya Mkoa wanatoa fursa ya watu kuwauliza na kuwaeleza mahitaji yao? Tunawezaje kuboresha hali hiyo?
- Je, wakristo wetu wanazielewa fursa zilizopo; huduma zinazotolewa na serikali, mipango ya kusaidiana kama SACCOS, MVIWATA, vyama vya ushirika, jitihada za TASAF. Kwa nini wakristo wetu hawafanyi bidii kuanzisha vikundi/mipango ya kusaidiana? Pia parokia zetu ziwajibike vema katika kujenga ushirikiano na kujenga uwajibikaji wa kijumuiya ili kuboresha maisha.
- Kwa nini watu wetu hawaaminiani? Na tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu miongoni mwetu?
- Kwa nini wakristo wetu wanaogopa kuzungumza na wenye mamlaka na walio katika huduma za utawala ili kupeleka malalamiko na kufuatilia utekelezaji wa maamuzi yaliyofanyika. Pia tutafakari namna ya kupambana na tabia ya uvivu.
- Tuna mali nyingi, lakini kila mara tunasubiri “wengine “ au “Serikali” kufanya kitu au kutuletea fedha. Lazima tujifunze kutumia vipaji vyetu na uwezo wetu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu. Kusaidiana kwa kuunganisha nguvu zetu na uwezo wetu ni wajibu wa kikristo. Mungu ametupa vipawa, lazima tuvitumie.
- Umaskini wa fikra, umaskini wa utashi duni na uwajibikaji ndio hasa husababisha umaskini. Ni kwa vipi jumuiya ya wakristo wanaweza kuwa mahala pa uwajibikaji ili kuweza kuboresha hali yetu.

6. HIFADHI YA JAMII

Dira
Mungu ametujalia uhai na anatupa mwaliko wa kutunza maisha na kuongeza ubora wa maisha. Mungu pia anatutaka kujali kwa namna ya pekee watu wasio na uwezo katika jamii yetu: yatima, wajane, walemavu, wagonjwa, watoto wa mitaani na wazee.

Hifadhi ya jamii maana yake ni kuweka mipango ya kuwahakikishia watu mahitaji na huduma ili wasiishi katika hali ya kukosa hifadhi/ usalama. Tunapozungumzia hifadhi ya jamii haswa tunamaanisha mifuko ya pensheni, elimu, bima ya afya na misaada ya kijamii.

Watu wengi miongoni mwetu hawafikiwi na huduma hii na familia zao zinakwama wanapoingia katika kuhitaji huduma hizo. Tunapaswa kuwa na mtazamo fikiriki ili kuweza kupata njia za kusaidiana. Mipango rasmi iliyoanzishwa na serikali au mashirika ya umma ama makampuni binafsi zinawafikia watu wachache tu ambao ni kama asilimia sita (6%) ya kundi la wafanyakazi.
- Jumuiya ndogondogo wangeweza kuwa chombo cha kusaidiana katika mahitaji ya kila siku ya wanajumuiya wao. Tunawezaje kuzifanya jumuiya zetu zitimize wajibu huu?
- Kutoaminiana ni kikwazo kikubwa katika kuwa na mipango na mifuko endelevu ya jumuiya. Tunawezaje kujenga moyo wa uaminifu? Viongozi wazuri walio tayari kuhudumia wanawezaje kupatikana na tutawawajibishaje viongozi wabovu?
- Lazima tutafute taarifa juu ya huduma na fursa zilizopo. Katika ngazi ya Parokia iundwe timu kwa ajili ya kutafuta taarifa na kuzifikisha katika Jumuiya ndogo ndogo. Taarifa hizo ni pamoja na zihusuzo mfuko wa afya ya jamii, sera ya serikali juu ya karo ya shule, sheria zinazohusu huduma ya tiba kwa mama na mtoto, wazee.
- Katika jamii yetu kuna watu walemavu wengi: Takwimu zinaonyesha kuwa walemavu ni 10% ya watu wote. Hawa ni wenye ulemavu wa namna moja ama nyingine. Kwa kawaida wahitaji hawa wanabaki kutegemea wanafamilia wao wachache, hasa mama au bibi. Kundi hili ndio maskini kupindukia kwa sababu jitihada za kuwainua ni ndogo sana.

Tatizo hili sio rahisi kulitatua. Lakini kwa kutegemea mifumo rasmi ya hifadhi ya jamii tu haitoshi na huduma hii kwao haitakuwa endelevu. Kwa hiyo tunapaswa kutafuta njia ambazo misingi yake ni katika njia za kizamani za kusaidiana, tuzitumie katika mazingira yetu ya leo kwa namna ya kisasa. Wazo hili linaweza kutekelezekaje?

PROGRAMU YA KUHAMASISHA HUDUMA YA KICHUNGAJI KATIKA JAMII KUELEKEA

UCHAGUZI MKUU 2010​

(2009 - 2011)​

TUKIO​

WALENGWA

WAPI/NGAZI

LINI

MHUSIKA/MWEZESHAJI​

Mkutano wa Taifa wa kutengeneza Programu
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume ya H & A (Majimbo)

TEC​

20 – 22 Januari, 2009
- Katibu wa Idara ya Kichungaji TEC
- Katibu Tume ya Haki ya Amani – TEC
+ CPT (T)
Kukamilisha programu (booklet form)

TEC​

Februari 2009

,,​

Kutuma Programu Majimboni
- Maaskofu
- Wakurugenzi wa Uchungaji – Majimbo
- Viongozi wa Tume Majimbo

TEC​

Machi 2009

,,​

Mkutano wa Jimbo kuzindua Programu
- Mapadre, Watawa
- Halmashauri na vyama vya Kitume
- Taasisi

Jimbo​

Aprili 2009
I. Kuanza Mapadre na Watawa, wa
II. Walei
- Askofu
- Mkurugenzi
- Tume (Jimbo)
Mkutano wa Makatekista
Makatekista

Jimbo​

Aprili 2009
- Mkurugenzi Uchungaji
- Tume/Mkurugenzi Katekesi
Semina/Mikutano ya Walei/Vyama
Halmashauri (Viongozi wa JNN & Vyama, Kamati)

Parokia​

Mei - Juni 2009
- Paroko/mjumbe kutoka Jimboni
- Kamati Tendaji, Viongozi wa vyama
Kufikisha Programu JNN
Waumini/Wakazi

JNN​

Julai – Sept. 2009
- Paroko
- Halmashauri ya Parokia
Mijadala na utekelezaji
,,
- JNN
- Vyama vya Kitume
Okt – Des. 2009
- Paroko, Kamati tendaji
- Viongozi wa Jumuiya
Mkutano wa Taifa
(Tathmini ya I)
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume

TEC​

Januari 2010
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume – TEC
+ CPT (T)

Mwendelezo wa Mijadala na utekelezaji
Waumini na Wakazi
- Jimbo
- Parokia
- JNN
Febr. – Sept. 2010
- Askofu
- Paroko
- Walei

Kushiriki Uchaguzi kwa tathmini
Waumini na Wakazi
- Taifa
- Jimbo
- Parokia, JNN
Okt – Des. 2010

,,​

Mkutano wa Taifa (Tathmini ya II) + kubainisha agenda
- post election
- post synodial
- Wakurugenzi wa Kichungaji
- Wajumbe wa Tume

TEC​

Januari 2011
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume
+ CPT (T)
Mwendelezo wa Programu
- Post Election
- Post Synodial
Waumini na Wakazi
- Jimbo
- Parokia
- JNN
Febr. - Sept. 2011

- Askofu
- Paroko
- Walei

Kuandaa Ripoti ya Majimbo na kutuma Taifa

Jimbo​

Oktoba 2011
- Mkurugenzi wa Uchungaji
- Viongozi wa Tume
Kuandaa Ripoti ya Kitaifa ya utekelezaji wa Programu.

TEC​

Novemba 2011
- Katibu Mtendaji Idara ya Kichungaji
- Katibu Tume ya H & A – TEC

Sahamahani wakuu kompyuta yangu imesumbua ku-attach word document, nikaona nimsaidie huyu kwa kuibandika hivi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom