Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Akili ya Kingunge kwa sasa ni sawa na betri iliyo ishiwa charge, na siyo rechargeable ni ya kutupwa tu.
 
NINI tamko la NEC kuhusa warka huu?

Bila shaka kikao cha wiki iliyopita walitoa tamko kama walivyotoa kuhusu mahakama ya kadhi
 
..Sheikh Ponda anatarajia kutoa Waraka wake hivi karibuni. anadai huo utakuwa na madukuduku ya Waislamu.

..sasa nasubiri kuona kama Mheshimiwa Mzee Ngombale Mwiru atauchana-chana waraka wa Sheikh Ponda kama alivyofanya kwa waraka wa Wakatoliki.
 
Jamani hakuna hata mmoja wetu aliyejibu swali la msingi. Kwamba Je Mzee Kingunge kweli aliuchanacnana waraka wa Kanisa Katolik kwenye mkutano wa NEC?. Taarifa hiyo tutaipata wapi? Mwenye kujua anifahamishe!!!
 
mimi bado sijausoma huo waraka manake muda mrefu sijaingia JF.Kama kuna mtu anao tafadhali nitumie
 
Sitta na Waraka wa Wakatoliki inahusiana nini, Kama huyo babu ana hasira na huo waraka angeuchana bungeni wakati anautolea maoni ili aonekane kwa watu wote, mbona ameamua kujificha ndiyo auchane, ni bora atambue kuwa kwa kufanya hivyo ujumbe aliokusudia utakuwa haujawafikia walengwa.
 
Hii ni tetesi na hakuna aliyejibu swali kama ana uhakika.
Itabaki kama tetesi mpaka tupate hakikisho.
Ni makosa kuanza kumshambulia Kingunge kwa kauli zinazoashilia kuwa ni kweli kafanya hivyo. Hata hivyo tutaendelea kumshambulia kwa mashambulizi aliyokwisha fanya na tuna uhakika nayo.
 
Sina uhakika ila inawezekana kwani yule ameshaishiwa na akili kutokana na umri. Aende kwa mzee wa upako kwani amemwomba akajiunge na kanisa lake huku akimuunga mkono akise RC wanataka kutawala nchi kinamna na tangu zamani wamekuwa wakitawala wanasiasa.
 
Umetoka huko huko kanisani, sema bora ugawiwe kwa wasiofika kanisani, kama vile mzee Caetan Maurice Ngombare Mwiru. 😀

Hii nimeipenda sana.


Nadhani kuna haja ya kuweka ukomo wa kuwa Mbunge ili watu kama kina Kingunge waende kucheza na Wajukuu, Vitukuu, Nyanya, n.k. zao kuliko kutuonyesha ukosefu wa hoja
 
Auchane waraka asiuchane, ujumbe umefika na kama ulimkosesha usingizi kiasi kile basi hautafutika ndani ya kichwa chake!! Lesson taken!! Ameuchana wakati ndani ya mafaili yake ameuweka tena sehemu imara kabisa kwa ajili ya reference!!! Asijipendekeze na kujidai anakipenda chama na watanzania kumbe fisadi mkuu.

Kama anataka kuchana akachane zile contract za kifisadi za Parking systems, kituo cha Ubungo, Uzoaji taka manispaaa ya Temeke, n.k. na zile share lukuki amenunua kwa peasa ya kifisadi.
 
Kauchana hakuuchana mzee huyu kapungukiwa busara,kama hataki aibu bora ang`atuke.Vinginevyo kina kinje wataaibika.
 
..sheikh ponda anatarajia kutoa waraka wake hivi karibuni. Anadai huo utakuwa na madukuduku ya waislamu.

..sasa nasubiri kuona kama mheshimiwa mzee ngombale mwiru atauchana-chana waraka wa sheikh ponda kama alivyofanya kwa waraka wa wakatoliki.


thubutu!

tutamsomea
 
Waraka huu unaweza kuligawa taifa. Bora upelekwe kanisani.

Tangu hapo huu waraka madhumuni yake yalikuwa kuwapa elimu ya uraia waumini wakatoliki na mpaka sasa semina zake zinaendeshwa kwa waumini hao. Ni watu kama Makwaiya wa Kuhenga na Mzee Ngombale Mwiru walipoupigia kelele ndio waraka huu ukawa "hot cake" mpaka watu wengine wakaanza kuununua na kuusoma. Tendo la Kingunge kuhusu kuuchana waraka huu liliripotiwa kwenye gazeti moja wiki jana lakini kanisa kamwe haliwezi kusikiliza achilia mbali kushutushwa na matendo ya kipagani.
 
huyu babu ni sawa na punda anayekata roho anavyopiga mateke hovyo! HE IS A DYING HORSE! Hivi juzi tu mkewe kmpora mtu tenda ya kuzoa taka uhindini! Kwa bahati nzuri huyu aliyeporwa na ambae alianza kazi hii miaka ya nyuma bila malipo kaweka pingamizi mahakamani! JAMANI BABU MBONA ATKUFA KINYWA WAZI!
 
Waraka huu unaweza kuligawa taifa. Bora upelekwe kanisani.
Mimi nafikiri huyu mzee asome alama za nyakati.Wakati wa watu wenye mawazo kama yake sasa umekwisha tunataka mawazo mbadala ya kujenga na kusaidia jamii yenye maadili kama waraka huo wa katoliki unavyo dadavua juu ya viongozi wadilifu. Zile enzi za zidumu fikra za mwenyekiti ndio hizo zimetufikisha hapa tulipo, jamii zima ya kitanzania ikigubikwa na wimbi kubwa la ufisadi na wizi wa mali ya nchi huku likiwaacha watanzania wengi katika umasikini mkubwa.
Yeye achane tu lakini message wa sent and derlivered that`s well and good.,kumbuka waraka huo umepewa baraka zote na MA-ASKOFU wenye daraja takatifu,sawa sawa na mtu kuchana maandiko matakatifu ya BIBLIA au KORAN nini kitamtokea?? Nawaklisha mkuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom