Mkandara, bado watu wengi hawajauelewa huo waraka na nadhani hata wewe pia. Kusema hujauelewa siyo sawa na kusema huwezi kuuelewa. Swali la kujiuluza ni hili: kwanini kuna 'Mpango wa Kichungaji na Ilani'? na vyote vinaelezea vipaumbele vilevile?
Vipaumbele vilivyopendekezwa viko 7 na vimo katika vijitabu viwili. Kimoja kinaitwa "Pastoral Programme..." (Mpango wa Kiuchungaji..." na Kingine "ILANI" (Manifesto). Kijitabu kinachoitwa "Pastoral..." addressees wake ni waamini na ukisoma humo ndani ya kijitabu hiki, utakuta kuwa hao waamani wanaaswa siyo tu wawachague viongozi waadilifu na wenye sifa kwenye siasa tu bali pia ndani ya Kanisa lenyewe.
Kwa hiyo, Kanisa lenyewe wakati linatoa elimu ya uraia kwa waamini wake linataka pia elimu hiyo isaidie kuwapata viongozi waadilifu ndani ya Kanisa lenyewe. Ndani ya Kanisa kuna jumuia ndogondogo, vigango, parokia, mabaraza ya walei hadi kufikia ngazi ya taifa katika uongozi wa Kanisa na ngazi zote hizi zinapewa elimu hiyo ya uraia na wahusika ni waamini, wana CPT, maparoko, viongozi wengine wa Kanisa na Maaskofu.
Kuna programme nzima lini, wapi na tukio gani mwisho kabisa wa kijitabu hiki cha 'Pastoral Programme' - ni kijitabu cha kijani.
Kijitabu kinachoitwa "Ilani" (Manifesto) kimeelezea vipaumbele vyenyewe. Hiki hakina neno "pastoral" na hivyo hiki ni kwa ajili ya mtu yeyote yule - kwa maana kwamba kila individual, dhehebu, NGO au dini (kama na wao wanaona hivi vipaumbele vinawagusa) wanaweza kutoa hiyo elimu ya uraia kulingana na 'structures' za NGO, dhehebu au dini waliyomo.
Kitu ambacho Watanzania tunapaswa kujua ni kuona nani yuko au anaguswa wapi kuliko kusema mbona neno 'parokia' limetumiwa au 'jumuiya ndogondogo' au 'paroko' au 'askofu' au 'mafundisho ya Kanisa na Injili'. Kitu cha kujiuliza ni hiki, je lengo la CPT au TEC ni kuhamasisha hiyo 'quotation' uliyo'underline' au ni wewe umechagua kitu unachotaka utumie kukosoa huo waraka?
Waraka umeandikwa ili kuhamasisha vipaumbele 7. Wakatoliki wameanza kwa kuanza na "Pastoral Programme..." Sasa badala ya watu kukosoa vipaumbele, wanakosoa jinsi wao (Wakatoliki) walivyojipanga kutoa hiyo elimu. Mimi ungeniambia kuwa ulipohudhuria hiyo elimu ya uraia wanayotoa, ulikuta wanahubiri kuwa watu wao wanapaswa wawachague Wakatoliki tu.
Kwa hiyo, "Tumetumwa katika jumuiya zetu, Parokia na jumuiya ndogo ndogo, kuwahamasisha watu wafanye tafakari juu ya hali halisi ya maisha na kujua ni kwa namna gani mafundisho ya Kanisa na Injili yanatupatia mwanga wa namna ya kuboresha maisha yetu na katika Taasisi za jamii yetu. Tunachukua hatua katika kurekebisha mambo yanayokwenda vibaya na kuimarisha mambo mazuri. Ni mwaliko wa kuwasaidia watu katika kutekeleza maamuzi yaliyothibitishwa katika ahadi yao waliyoweka wakati wa ubatizo" addressees wake ni wanakanisa wenyewe - waamini wanaoamini sturctures na ujumbe wa injili na mafundisho ya Kanisa, ambayo kwa ujumla unahusu haki, upendo na amani.
Hivyo, kama waamini wanaaswa kufuata elimu ya uraia kwa kuzingatia mafundisho ya Injilii ya Yesu na mafundisho ya Kanisa (Social Teaching of the Church), utakuta kuwa vlaues ambavyo zinazingatiwa ni kuhusu haki za binadamu, amani na upendo.
Unless kama utaweza utaweza ku'prove' au una ushahidi kuwa umekuta (witness) Wakatoliki wanahamasishwa kinyume na hayo niliyotaja. Bado nasema, wakosoaji wanakosoa kwa kufuata hisia tu na siyo 'substance' ya waraka wenyewe!