Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Zakumi,

..Wakatoliki wenyewe wanadai kwamba huu siyo waraka wa kwanza kuutoa. wanadai hata katika chaguzi zilizopita wamewahi kutoa waraka wa namna hii hii na hakuna aliyepiga makelele.

..binafsi nadhani CCM wana matatizo ndani ya chama chao na ktk utawala mzima kwa ujumla hivyo kutolewa kwa waraka wowote ule kuelekea ktk uchaguzi siyo habari njema kwao. hiyo ndiyo sababu kubwa ya Mzee Kingunge kuushutumu waraka huu.

..vilevile naona Mzee Kingunge ameamua kichwa-kichwa kuushambulia waraka huu kwasababu anawaelewa Wakatoliki wa Tanzania ni wanyenyekevu kitabia. kuna vikundi vingine vya kidini ambavyo vimetoa madai mazito na yenye muelekeo wa kutishia amani lakini Mzee Kingunge amekaa kimya.

..binafsi nadhani huyu Mzee Kingunge ana double standard ktk kukosoa na kuzirekebisha taasisi mbalimbali za kidini nchini.

..mwisho umedai kwamba kama mjadala wa Mahakama ya Kadhi ungekuwa haujapamba moto Wakatoliki wasingetoa waraka wa uchaguzi. lakini ingefaa vilevile ukakumbusha kwamba bila Mzee Kingunge na makada wenzake wa CCM kuweka kipengele cha mahakama hiyo kwenye ilani ya CCM uwezekano mkubwa ni kwamba tusingekuwa hapa sasa hivi.

Jokakuu:

Kama huu sio waraka wa kwanza, basi kopi zitakuwepo za miaka iliyopita. Hivyo hatuwezi kusema waliwahi kutoa bila kuona kopi. Nikiona kopi nitakubali kuwa walisema.

Na mimi nadhani kama wewe unavyodhania kuwa CCM ina matatizo. Na moja ya matatizo hayo ni kushindwa kutekeleza Ilani ya chaguzi zilizopita. Na kushindwa kwao huko kumewafanya wao kutafuta kura kwa udanganyifu. Mahakama ya kadhi ilianzishwa na chama kingine (TLP-Mrema). CCM iliiba hiyo idea hili wapate kura. Walipata kura, na waislamu wanawauliza kwenye ilani yenu mlisema mtaanzisha mahakama ya kadhi na hapo kijasho kinawatoka.

Katika ilani ya CCM kuna mambo mengi waliyosema. Na kama watanzania wangekuwa wanaidai CCM kama vile waislamu wanavyodai yaliyoandikwa kwenye ilani ya 2005, basi nchi ingekuwa mbali na CCM kingekuwa chama chenye majukumu kwa sababu wangejua kuwa wanapotoa ahadi basi watu wanazifuatilia ahadi hizo.

Vilevile ni makosa kulaumu CCM, kwa sababu ilani yao ilikuwa wazi na kila mtu aliisoma. Na kama mtu alikuwa na pingamizi la mahakama ya kadhi, tungetegemea angetoa malalamiko yake mwaka 2005 na sio 2010.

Vilevile kama mtu alishindwa kusoma ilani ya CCM ya 2005, mnategemea asome waraka wa CPT wa mwaka 2010. Unajua watanzania tunapenda sana kufungana kamba. Tunafikiri kuwa kuna imaginary Tanzanian ambaye atasoma ilani za uchaguzi au waraka na siku ya uchaguzi watachagua watu kwa kufuata yale waliyojifunza kwenye vijarida. Kama watu wangekuwa wanachaguliwa kwa namna hii, hakuna ambaye angetoa vitenge, T-shirts au pilau.

Anyway, sehemu kubwa ya waraka inajaribu kuwaagiza watu jinsi gani ya kupiga kura. Quite frankly haisemi lolote kwa wale waliopo madarakani kumrudia Mungu wao, kurudisha mali za umma au kuwatumikia watu. Hawa watu wanajulikana na wengine ni wakatoliki.
 
Za10,
Kweli Tz ina matatizo mengi - lazima tuellewe context ya uandishi wa waraka huu.Nadhani unaelewa kuwa support ya mambo ya Uchaguzi na Kuandaa na ku update daftari la wapiga kura imekuwa miaka yote ikitolewa na wafadhili chini ya mtindo wa Basket funding chini ya Uratibu wa UNDP.Miezi miwili iliyopita UNDP walizindua Project ya Election Support 2010 na kuita wadau mbalimbali zikiwemo taasis za kidini - waislam na wakristo wakimo.Moja ya mambo yaliyomo kwenye support hiyo ni elimu ya wapiga kura na ndipo CSOs/FBOs zinaji commit kuanza kuona ni vipi zitashiriki kwenye kutoa elimu hiyo ambayo hata hivyo toka uchaguzi wa 2005 ilionekana itolewa kwa namna ya kudumu zaidi na siyo event-driven au event-based tu.Hapo Wakatoliki wakafanya kweli kwa kuandika waraka na kuanza kutoa elimu hiyo.Nadhani haya Waislam nao baadae walisema wanaandaa wa kwao japo sina uhakika kama hadi sasa umeshatoka.
Hata Uchaguzi wa 2005 Taasis za kidini zilishiriki kutoa Elimu hii - CSSC na hata BAKWATA walipewa nyenzo chini ya basket fund ya uchaguzi ule na haikuwa tatizo.Nadhani kinachoonekana hapa ni hayo mambo ya Kadhi na OIC ambayo 2005 hayakuwepo.
Huu ni ufafanuzi kutokana na ninachokifahamu.

WoS:

Demokrasi haifundishwi wala hainunuliwi. Hivi viongozi wa dini wanaogopa nini kuwataja mafisadi?
 
Mimi sio member wa CPT na mambo ya imani za dini kwangu ni uzembe wa akili tu.

Kwa mfano: sentensi moja inabeba mzigo mzito. Hapa Marekani kuna mjadala wa health Insurance reform. Sentence moja tu ambayo imeashiria kuwa kutakuwa na death panel imeleta mtafaruku mkubwa.

Tanzania ina matatizo mengi na huu sio uchaguzi wa kwanza. Hivyo CPT ingeweza kuandika waraka katika vipindi vya uchaguzi zilizopita. Hawakufanya hivyo. Kwanini waraka utolewe wakati mijidala ya kadhi na OIC imepamba moto?

Ungekuwa karibu ningekupa kitabu ambacho siyo Tanzania tu bali Maaskofu wa Afrika, ikiwemo Tanzania, wameshasema nini kuhusu haki za binadamu miaka tofautitofauti (nadhani kuanzia miaka ya 1970). Wewe ungesema "hujaona" na ungetaka uone machapisho mengine yakoje kuliko kusema 'mbona CPT hawakutoa hizo nyaraka miaka ya nyuma.'

Nakuomba ufanye hivi: kama utaweza kuje Tz, siku moja nenda pale St Joseph Cathedral kuna ofisi ya CPT na waulize wakupe catalogue ili uone vijitabu vyote ambavyo wameshachapisa kuhusu elimu ya uraia tangu CPT ilipoanzishwa.

Labda hapo utaweza kupata mwanga zaidi. Halafu kitu kingine ni kwamba kwa vile watu sisi ni tofauti hata kama kuna kitu kizuri kiasi gani lazima wawepo wakosoaji tu.

Hata waanzilishi wa falsafa walianza hivyo. Walianza poets (akina Homes), wakaja cosmologists... hivyo hivyo hadi contemporary philosophers. Leo ningekuja sitting room kwako jinsi ulivyopanga na kupamba, mimi ningekosoa tu, yaani ningetaka nipange sittingroom yangu tofauti na yako... Hata wewe ungeona jinsi nilivyovaa, ingawa najiamini nimevaa vizuri, nawe ungeweza kukosoa kitu. Hivyo ndivyo binadamu tulivyo. Mbona hata Mungu tunamkosoa (kwa nini Mungu ameruhusu haya kutendeka?) sembuse binadamu?

Kwa hiyo, hata kama kabla ya kuandika wangem'consult' kila mtu duniani hata hao ambao wangekuwa 'consulted' baadhi yao wangekosoa.

Kwangu kukosoa kitu ni namna tu ya kutaka kuboresha zaidi. Ila tofauti na hiyo, sisi tunasema almost waraka wote ni flawed. Hapo ndipo tunapokosa objectivity na kufuata zaidi hisia zetu kuliko hoja zenyewe. Kitu kibaya ni kwamba, baadhi ya ukosoaji wetu haujengi, unabomoa!
 
Recta:

Nimepitia waraka wote. Katika kipengele cha marekebisho ya katiba kuna sehemu inasema: Kuheshimu kanuni ya kuwa Serikali haina dini na kutoruhusu taasisi za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi (mfano. Mahakama ya Kadhi na uanachama wa OIC).

Ukweli wa mambo ni kuwa bila kuwepo na majadiliano ya mahakama ya Kadhi na uanachama wa IOC, huu waraka usingetoka.
Zakumi, nashukuru kwa kuwa sasa umenifumbua macho na nimeweza kuona sababu ya malumbano yote haya. Nimeelewa sasa kuwa, waraka huu kama ulivyo hauna makosa yoyote na ndio maana wanaoukosoa wala hawasemi makosa yake kwa kuhofia kupata upinzani mkubwa na usio na mipaka. Ila ni dhahiri kuwa waraka ungependwa saaaaaaana kama usingezungumzia Kadhi Mkuu na Taifa kujiunga na OIC. Ina maana pia kuwa, wanaoupinga wanajua hivyo ila wanahofia kutamka wazi kuwa hiyo ndio kasoro yake. Nadhani wangesema ukweli tu.

Mimi nadhani iko wazi kabisa kuwa ili serikali iweze kushiriki katika uundaji wa mahakama ya Kadhi au Kujiunga na/au OIC ni lazima ifanye yafuatayo;
1. Ibadilishe Katiba au
2. Ivunje Katiba
3. Iruhusu taasisi nyingine zote za dini kuwa na Mahakama zake kama inavyoainishwa na dini hizo
4. Iwe tayari kuona mahakama zake zikipokonywa baadhi ya mamlaka na kushughulikiwa na mahakama hizo za kidini.
5. Ifahamu kuwa, ni vigumu kuinyima taasisi moja mamlaka ya kufungua mahakama kamili kulingana na taratibu na kanuni za dini yenyewe.
6. Iwe tayari kukidhi mahitaji sawa kwa kila mahakama ya kidini iliyoanzishwa (kifedha, miundmbinu n.k.)

Nadhani sasa nimeelewa mantiki nzima ya mjadala huu. Na ni vyema kujadili kwa kuzingatia maana mpya zinazojitokeza.
 
WoS:

Demokrasi haifundishwi wala hainunuliwi. Hivi viongozi wa dini wanaogopa nini kuwataja mafisadi?

Anza wewe! Wao ni 'the voice of the voiceless' na lengo lao siyo kuhukumu watu bali kuonyesha njia. Ndiyo maana wanatoa ushauri wa jumla bila kumtaja mtu mmojammoja. Ulishafanya kazi ya counselling? Nia unataka kuongoza watu kufikia uamuzi wa maana na siyo kusema nani aamue vipi. Kanisa linajenga dhamiri njema (informed consciences) za waamini ili waamini wenyewe waweze kuchagua kipi ni chema kwa jinsi walivyoguswa wao wenyewe.
 
Vilevile kama mtu alishindwa kusoma ilani ya CCM ya 2005, mnategemea asome waraka wa CPT wa mwaka 2010. Unajua watanzania tunapenda sana kufungana kamba. Tunafikiri kuwa kuna imaginary Tanzanian ambaye atasoma ilani za uchaguzi au waraka na siku ya uchaguzi watachagua watu kwa kufuata yale waliyojifunza kwenye vijarida. Kama watu wangekuwa wanachaguliwa kwa namna hii, hakuna ambaye angetoa vitenge, T-shirts au pilau.

Anyway, sehemu kubwa ya waraka inajaribu kuwaagiza watu jinsi gani ya kupiga kura. Quite frankly haisemi lolote kwa wale waliopo madarakani kumrudia Mungu wao, kurudisha mali za umma au kuwatumikia watu. Hawa watu wanajulikana na wengine ni wakatoliki.

Mkuu, inaelekea waraka huu utasomwa kuliko ilani au waraka mwingine wowote uliowahi kutolewa. Kampeni ya kuhakikisha hivyo inasaidiwa zaidi na wale wanaoupinga kuliko wanaouunga mkono. Trust me on this one.
 
Zakumi said:

..kumbuka huu ni Waraka ulioandaliwa na Wakatoliki. sasa wakianza kuleta habari ya kumrudia MUNGU watakua wanamuelezea MUNGU huyo kulingana na imani yao ya Kikatoliki. nadhani hapo panaweza kuleta malumbano mengine makubwa zaidi.
 
CCM yatoa tamko kuhusu Waraka wa Wakatoliki, Mahakama ya Kadhi
broken-heart.jpg
Na Habel Chidawali, Dodoma

HALMASHAURI Kuu ya CCM imeiagiza serikali kukutana na viongozi wa dini ili kufanya mazungumzo yatakayosafisha hali ya hewa iliyochafuliwa na waraka wa Kanisa Katoliki (RC), kuhusu uchaguzi, huku ikiridhia kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa dola.

Waraka wa Kanisa Katoliki umekuwa ni gumzo kubwa katika miezi ya karibuni kutokana na kuzungumzia jinsi ya kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, huku wanaoupinga wakidai kuwa, utawagawa wananchi katika misingi ya kidini.

Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, Nec imeagiza viongozi wakuu wa nchi kukutana na viongozi wa dini ili kufanya mazungumzo kwa lengo la kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii.

RC imekuwa ikiwataka wanaoupinga waraka huo kueleza udhaifu wake badala ya kutoa maoni ya kiujumla kuwa haufai, kama ambavyo mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru amekuwa akiupinga.

Kuhusu Mahakama ya Kadhi, CCM imesema inaunga mkono msimamo wa serikali kutaka suala hilo lianzishwe nje ya mfumo wa dola.

Katika ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2005, CCM iliahidi kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi, lakini katika miezi ya karibuni Waislamu wamekuwa wakishinikiza kutaka kuanzishwa kwa chombo hicho wakidai kuwa, CCM iliwahadaa kwa kuahidi kuwaundia chombo hicho.

"Halmashauri Kuu imesisitiza kuwa iwapo Waislamu wanaona haki zao hazikamiliki bila ya kuwa na chombo cha aina hiyo, wasizuiwe, alisema Chiligati.

"Waruhusiwe kuanzisha Mahakama ya Kadhi wao wenyewe na serikali isijihusishe kuiendesha mahakama hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imejiingiza katika shughuli za kidini."

Kwa mujibu wa Chiligati, mahakama hiyo haitajihusisha na kesi za jinai wala madai badala yake itakuwa ikishughulikia masuala ya ndoa, talaka na mirathi.

Katika mkutano huo wa Nec, Jasson Rweikiza alichaguliwa kuziba nafasi ya ujumbe wa chombo hicho kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa.

Rweikiza alipata kura 88 na kumbwaga kwa tofauti ya kura tatu mpinzani wake wa karibu, Ramadhani Maneno ambaye alipata kura 85 huku mwanamke pekee katika kinyang'anyiro hicho, Sifa Swai akiambulia kura 46. Jambo lingine lililojiri ndani ya kikao hicho kikubwa ni pamoja na uteuzi wa makatibu wa mikoa. Katika uteuzi huo, Sauda Mpembalyoto, ambaye alikuwa katibu wa wilaya ya Hai na kapteni mstaafu wa jeshi, Frarten Kiwango ambaye alikuwa katibu wa wilaya ya Kibaha Mjini, waliteuliwa kuwa makatibu lakini vituo watapangiwa baadaye
 
Zakumi, nashukuru kwa kuwa sasa umenifumbua macho na nimeweza kuona sababu ya malumbano yote haya. Nimeelewa sasa kuwa, waraka huu kama ulivyo hauna makosa yoyote na ndio maana wanaoukosoa wala hawasemi makosa yake kwa kuhofia kupata upinzani mkubwa na usio na mipaka. Ila ni dhahiri kuwa waraka ungependwa saaaaaaana kama usingezungumzia Kadhi Mkuu na Taifa kujiunga na OIC. Ina maana pia kuwa, wanaoupinga wanajua hivyo ila wanahofia kutamka wazi kuwa hiyo ndio kasoro yake. Nadhani wangesema ukweli tu.

Mimi nadhani iko wazi kabisa kuwa ili serikali iweze kushiriki katika uundaji wa mahakama ya Kadhi au Kujiunga na/au OIC ni lazima ifanye yafuatayo;
1. Ibadilishe Katiba au
2. Ivunje Katiba
3. Iruhusu taasisi nyingine zote za dini kuwa na Mahakama zake kama inavyoainishwa na dini hizo
4. Iwe tayari kuona mahakama zake zikipokonywa baadhi ya mamlaka na kushughulikiwa na mahakama hizo za kidini.
5. Ifahamu kuwa, ni vigumu kuinyima taasisi moja mamlaka ya kufungua mahakama kamili kulingana na taratibu na kanuni za dini yenyewe.
6. Iwe tayari kukidhi mahitaji sawa kwa kila mahakama ya kidini iliyoanzishwa (kifedha, miundmbinu n.k.)

Nadhani sasa nimeelewa mantiki nzima ya mjadala huu. Na ni vyema kujadili kwa kuzingatia maana mpya zinazojitokeza.

There you go. Lugha ni kitu muhimu sana. Baraka Obama alitumia karibu saa zima kuelezea Health Plan yake. Mwisho wa hotuba yake akaulizwa swali nje ya mada kuhusu kukamatwa kwa profesa mweusi na yeye akaboronga kujibu. Na akatumia zaidi ya wiki ku-repair. Hivyo katika mambo haya waandishi ni lazima wawe makini.

Kuhusu namba 1 na 2, ni vitu vinavoeleweka. Kuhusu mahakama ya kadhi kuna vitu vinaitwa Arbitral Tribunals. Hizi zinaweza kuanzishwa na sio kwa waislamu bali kwa watu wa jamii nyingine. Kwenye masuala ya michezo na vitu vingine. Lakini lazima ziwe na mipaka yale.

Kunaweza kuwepo na arbitral tribunals za michezo. Kama Yanga na Simba wana migogoro sio lazima waende mahakamani.
 
Mkuu, inaelekea waraka huu utasomwa kuliko ilani au waraka mwingine wowote uliowahi kutolewa. Kampeni ya kuhakikisha hivyo inasaidiwa zaidi na wale wanaoupinga kuliko wanaouunga mkono. Trust me on this one.

Mkuu kwenye siasa hotuba na maneno ya mdomoni ni kitu muhimu sana kuliko vitu vilivyoandikwa kwenye makaratasi. Unajua ma-senator wengi wa Marekani hawakusoma mswada wa kuivamia Iraq. Sasa kwanini utegemee watu wasome Waraka.

Nakwambia Mke wa Lowasa na watoto wake watasoma waraka huo na bado Lowasa atapata kura zao.
 
Zakumi,
mkuu nakusikia sana..hivi kweli watu wanashindwa kukuelewa ama wanafanya mzaha tu.

WomenofSubstanc,
Miezi miwili iliyopita UNDP walizindua Project ya Election Support 2010 na kuita wadau mbalimbali zikiwemo taasis za kidini - waislam na wakristo wakimo.
Dada yangu, wala tusitake kuandikia mate, naomba source inayohakikisha vyombo vya dini vilipewa mamlaka hayo.
 
Date::8/18/2009CCM yatoa tamko kuhusu Waraka wa Wakatoliki, Mahakama ya Kadhi
broken-heart.jpg
Na Habel Chidawali, Dodoma

HALMASHAURI Kuu ya CCM imeiagiza serikali kukutana na viongozi wa dini ili kufanya mazungumzo yatakayosafisha hali ya hewa iliyochafuliwa na waraka wa Kanisa Katoliki (RC), kuhusu uchaguzi, huku ikiridhia kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa dola.

Waraka wa Kanisa Katoliki umekuwa ni gumzo kubwa katika miezi ya karibuni kutokana na kuzungumzia jinsi ya kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, huku wanaoupinga wakidai kuwa, utawagawa wananchi katika misingi ya kidini.

Chiligati aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, Nec imeagiza viongozi wakuu wa nchi kukutana na viongozi wa dini ili kufanya mazungumzo kwa lengo la kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii.

RC imekuwa ikiwataka wanaoupinga waraka huo kueleza udhaifu wake badala ya kutoa maoni ya kiujumla kuwa haufai, kama ambavyo mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru amekuwa akiupinga.

Kuhusu Mahakama ya Kadhi, CCM imesema inaunga mkono msimamo wa serikali kutaka suala hilo lianzishwe nje ya mfumo wa dola.

Katika ilani yake ya uchaguzi wa mwaka 2005, CCM iliahidi kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi, lakini katika miezi ya karibuni Waislamu wamekuwa wakishinikiza kutaka kuanzishwa kwa chombo hicho wakidai kuwa, CCM iliwahadaa kwa kuahidi kuwaundia chombo hicho.

“Halmashauri Kuu imesisitiza kuwa iwapo Waislamu wanaona haki zao hazikamiliki bila ya kuwa na chombo cha aina hiyo, wasizuiwe, alisema Chiligati.

“Waruhusiwe kuanzisha Mahakama ya Kadhi wao wenyewe na serikali isijihusishe kuiendesha mahakama hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imejiingiza katika shughuli za kidini.”

Kwa mujibu wa Chiligati, mahakama hiyo haitajihusisha na kesi za jinai wala madai badala yake itakuwa ikishughulikia masuala ya ndoa, talaka na mirathi.

Katika mkutano huo wa Nec, Jasson Rweikiza alichaguliwa kuziba nafasi ya ujumbe wa chombo hicho kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa.

Rweikiza alipata kura 88 na kumbwaga kwa tofauti ya kura tatu mpinzani wake wa karibu, Ramadhani Maneno ambaye alipata kura 85 huku mwanamke pekee katika kinyang'anyiro hicho, Sifa Swai akiambulia kura 46.
Jambo lingine lililojiri ndani ya kikao hicho kikubwa ni pamoja na uteuzi wa makatibu wa mikoa. Katika uteuzi huo, Sauda Mpembalyoto, ambaye alikuwa katibu wa wilaya ya Hai na kapteni mstaafu wa jeshi, Frarten Kiwango ambaye alikuwa katibu wa wilaya ya Kibaha Mjini, waliteuliwa kuwa makatibu lakini vituo watapangiwa baadaye.
Tuma maoni kwa Mhariri
​
 
Wacha tuangalie kama vikao vitakuwa vya siri ama vya wazi na watakuwa na hoja ipi hawa CCM kuomba waraka utoke mtaani .Ina maana CCM hawataki watu wajue ukweli na wajikomboe ?
 
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

Udhaifu wa waraka huo upo kwenye utoaji wa taarifa hiyo. Jukwaa kuu litumikalo kutoa taarifa hizo mpaka sasa hivi ni katika kanisa. Waumini wa katoliki ni yapata asilimia 23 ya watanzania wote. Na wahudhuriao kanisani yahesabiwa kama asilimia 15 ya watanzania wote.

Sasa hebu fikirieni, waraka muhimu kama huo uliochukua sura ya kitaifa kuwafikia wananchi wapatao asilimia 15, kweli huku si kutenda haki kwa watanzania. Nchi ambayo imeamua kuendeshwa bila dini, yaani wananchi wqake wana dini lakini serikali haina dini. Maelezo haya ni lazima yafanyike kwa vitendo.

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?
 
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

[COLOR="Red"[/COLOR]
[I][COLOR="Red"][/COLOR][/I]

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?[/QUOTE
 
Mambo ya dini mahala pake ni kwenye nyumba za ibada na majumbani tu.! Yakishatoka tu hizo sehemu, matokeo ni mauzauza na migogoro.
 
Hujaweka wazi ni maudhi gani yaliyowekwa kwenye waraka.
Unavyosema ni 15% ya watanzania watakaoweza kupata hiyo taarifa huoni kwamba hilo ni jambo zuri coz hiyo 15%i naweza kuambukiza wengine na wengine mwishoni watz wate 2kapata taarifa?
 
pili ucsahau kazi ya kufundisha wananchi kuhusu kuchagua viongozi bora ni ya serikali si ya kanisa wala msikiti, so kuwapa 15% elimu ya uraia ni kuipunguzia serikali gharama.
 
Tayari CCM wamechelewa. Waraka huu uko kila kona ya Nchi yetu. Kizuri wanachoweza kukifanya ni kuchambua mazuri yaliyomo na kuyaweka kwenye ILANI yao ya mwakani. Itawasaidia sana hata kama watanyambulisha lugha.
 
Katoliki ni lazima ifute waraka wake. Hii haitokani na maudhui yaliyokwenye waraka ila jinsi waraka huo utavyowafikia walengwa kwa usawa.

Udhaifu wa waraka huo upo kwenye utoaji wa taarifa hiyo. Jukwaa kuu litumikalo kutoa taarifa hizo mpaka sasa hivi ni katika kanisa. Waumini wa katoliki ni yapata asilimia 23 ya watanzania wote. Na wahudhuriao kanisani yahesabiwa kama asilimia 15 ya watanzania wote.

Sasa hebu fikirieni, waraka muhimu kama huo uliochukua sura ya kitaifa kuwafikia wananchi wapatao asilimia 15, kweli huku si kutenda haki kwa watanzania. Nchi ambayo imeamua kuendeshwa bila dini, yaani wananchi wqake wana dini lakini serikali haina dini. Maelezo haya ni lazima yafanyike kwa vitendo.

Hivyo kanisa katoliki lisitafuite udhaifu wa maandishi ila jinsi inavyochukua shughuli za serikali. Swali ni kwamba ni kwa kiasi gani kanisa lahitaji kuchukua shughuli za serikali?

Hubert Sauper alitutonya kupitia "Darwin's Nightmare Documentary" jinsi raslimali zetu zinavyoibiwa na sisi kubakia kula "mapanki" tukasema anachafua sifa ya nchi yetu; Hakielimu wakaonyesha jinsi mfumo wa elimu yetu usivyokidhi haja na unavyowaacha nyuma watoto wa maskini tukasema kama Hakielimu wanataka wawe chama cha siasa waseme; Kanisa Katoliki likasema jamani tuwe waangalifu na tusidanganywe tena na viongozi wasio waadilifu na wasio na sifa za uongozi na wakati wa kupiga kura tuwe macho, tunasema wanaingilia kazi ya serikali... Hivi ulishawahi kusikia hata siku moja Serikali ikisema wananchi hawana ardhi tuwape, wanafunzi wanateseka tutafute ufumbuzi wa tatizo lao, wanaohamishwa hawafidiwi vizuri na wengine hawana makazi, Mbagala hawana maji ya bomba tangu Kilwa Road ijengwe mwaka jana, mikataba ya madini ni mibovu, raslimali za nchi zinatafunwa na wachahce au wakati wa kupiga kura, baadhi ya kura zinaibiwa?

Waraka wa Kanisa ni wito ili jamii nzima ishiriki kwa namna inavyoweza kulingana na kila mmoja na nafasi yake tumekalia kupinga na kupotosha maudhui yake. Kwa hiyo, Kanisa kusaidia kutoa huduma za jamii, kupunguza umaskini, kutunza watoto wa mitaani na yatima, kutoa elimu na kusaidia waathirika wa ukimwi na hata kutoa huduma za usafiri (maana sehemu nyingine wanategemea gari la mission) wanaingilia kazi ya Serikali (maana hata kufanya hivyo ni siasa)?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom