Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
unajua inanipa shida sana kuelewa hili jambo....???..LIPI HASA TATIZO LA WARAKA WA WANATAALUMA WA KIKATOLIKI....?????...tatizo ni kuwa waraka huo umetolewa na wakatoliki au kuna jingine....?????..maana sijaona watu wakipinga waraka huo kwa kutumia hoja..na wasiwasi na watu wengi...nahisi hawajausoma na hawauelewi...wanaupinga tu sababu umetolewa na wakatoliki...!!!!!!!!
nikirudi kwa Bw. Makwaia na kipindi chake...alikuwa biased katika kipindi chake cha leo..panel yake yote wanaupinga waraka..mi nadhani ingekuwa bora angetafuta na mtu mwingine wasikie na upande wa pili kuliko kuwa na wagen wenye matazamo na mwelekeo mmoja....kwanini asimkaribishe hata mtu mmoja aliyehusika katika kuuandaa huo waraka akasikia walikuwa na malengo gani wakati walipokuwa wanautayarisha...kuliko kutuletea watu ambao wanamawazo ya aina moja..
Haya mkuu ni mawazo yako wewe.. hakuna mtu aliyepinga tu bila hoja.. hoja tumeziweka wazi labda wewe hufuatilii. tazama majibishano ya hoja baina yangu na Mzee Mwanakijiji.

Hata hivyo kwa kukufahamisha tu, hakuna mtu anayepinga wasomi wa Kikatoliki kukaa wakatunga kitu.. hii ni sifa ya elimu yao ktk uchaguzi na miiko ya Uongozi ikiwa ni pamoja na vita dhidi yaUfisadi. Lakini kosa/tatizo linakuja pale mapendekezo yao yanapitia TEC na kisha ati hao TEC wakutane na viongozi wa serikali kuwapa MWONGOZO wao..Halafu basi, tazama vifungu vya malengo ya hao TEC, dini imetumika zaidi ktk kuelezea vifungu vya haki ya wananchi badala ya kutumia elimu zao za darsa..

Mkuu wangu ukipata shahada yako Nyegezi unakubalika ktk nafasi yoyote ya kazi kulingana na elimu uloipata iwe hata kuandika waraka inayohusiana na kazi au elimu yako, lakini unapoitumia dini kuwa juu ya uwezo wako (elimu) ukawakilisha kazi za shirika (waraka) kanisani ikapate baraka hapo ndipo utata unapokuja..Kisha ati madaraka ya kanisa ndilo li deal na shirika.. huoni kama hapa wanachemsha mkuu.. Wahusika wa shirika itawalazimu waondoe hiyo elimu yako na waanze kufikiria uwezo wa Padri ktk maswala ya shirika hilo jambo ambalo haliwezekani.

Kuwa na sifa mbili sii tatizo hata kidogo, tatizo ni pale unapotaka kucheza NBA kwa kutaka watazamaji waitambue degree yako..U wanna play ball paly utasifiwa lakini sio kuingiza degree wakati mchezo huwezi kucheza hata kama rules unazijua..Kila sifa huenda mahala pake huu waraka umepotosha maana na taaluma ya waandalizi..
Kwa madai yenu mnasema ni hulka ya Kanisa Katoliki kutoa mwongozo kila unapokaribia Uchaguzi.. jamani sisi hatutaki, kama mlizoea mchezo huo basi UFE! huko nje fanyeni huko huko iwe Zimbabwe au Italia, kwetu hatutaki - ufe!
 
Last edited:
Tuesday, 21 July 2009 16:39 *Wasema ni haki ya kanisa kuelimisha wananchi wake
*Viongozi wanaopinga wana uelewa finyu wa siasa
*Wanaotimiza wajibu hawaogopi wenzao kuelimishwa
*Lataka dini zote zitoe waraka na kuelimisha waumini
*Mahakama ya Kadhi:Serikali iheshimu Katiba

Na John Danile, Dodoma

KANISA Katoliki nchini limetoa tamko rasmi kwa viongozi wanaopinga waraka wake uliotolewa hivi karibuni unaolenga kutoa elimu ya uraia na kuwaelezea kwamba wana upeo finyu kuhusu siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Holy Cross mjini hapa jana, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini, Askofu Juda Ruwa’ichi, alisema waraka huo una nia nzuri kwani unalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwatoa wananchi pale walipo.

“Kiongozi yeyote anayepinga au kuwa na wasiwasi na waraka huo na kuujadili huenda
ana uelewa finyu kuhusu siasa, Kanisa halishughuliki na viumbe hewa, Kanisa
linajishughulisha na watu wanaohitaji kila kitu kama sehemu ya haki yao ya msingi
ikiwemo elimu ya uraia,”alisema Askofu Ruwa'ichi.

Alisema amesikitishwa na mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yalitolewa na watu
mbalimbali wakiwemo wanasiasa kuhusu waraka huo na kuonya kuwa tafsiri wanazotoa zinajenga chuki miongoni mwa jamii kwa kuwa ni potofu na zinalenga kukwepa uwajibikaji.

“Mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yalitotolewa na wanasiasa unadokeza wazi, wapo wanaojadili ilani hiyo bila kujua kwanza yaliyomo ndani yake, hali hii
inasababisha upotoshaji, kuwakanganya watu na hata kuzusha hisa za chuki katika
Jamii, huu si uwajibikaji, katika hili ninapenda kuwaasa Watanzania kuwa watu wenye kutafuta ukweli na kujenga kauli za hoja juu ya msingi huo wa ukweli na uelewa
sahihi.

“Kanisa Katoliki linatafuta kwa nia njema kabisa kuwasaidia raia wa nchi hii bila
ubaguzi kujizatiti kutambua na kushughulikia maslahi ya wote siyo tu kwa kuzingatia leo, bali pia kwa namna inayoihakikishia nchi hii na raia wake wote amali za amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo mtambuka yaliyo endelevu. Mwelekeo unaokithiri sasa hautuhakikishii hayo,”alisema Askofu Ruwa’ichi.

Alisema anasikitishwa kuona watu wanahusisha waraka huo na uchaguzi wa madiwani na
ule mkuu ujao mwaka kesho wakati si lengo la waraka huo kumwambia mtu achague mtu
fulani bali inalenga kuwatoa watanzania pale walipo kwa kujitambua na kutimiza
wajibu wao.

“Ni Muhimu kuzielewa changamoto na kuzipa kila mmoja uzito unaostahili kwa lengo la
kutafuta kushughulikia maendeleo yetu kwa dhati zaidi, uelewa huo utatuwajibisha
tuamue ni nani mwenye uwezo wa kushirikiana nasi ili tujinasue kutoka hapa tulipo
na kupiga hatua za dhati mbele.

"Viongozi wanaochaguliwa na watu wanapewa dhamana,wanao wajibu wa kutambua na kujadili maslahi ya wote kwa kufanya juhudi za dhati na makusudi ili kuvielewa na kuvishughulikia vipaumbele halali na sahihi bila kujiruhusu kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila udini au ubaguzi wa aina
yoyote," alisema.

Alipoulizwa msimamo wa kanisa hilo kuhusu mchakato wa Mahakama ya Kadhi kwa
kuzingatia kuwa tayari baadhi ya wabunge wameonesha nia ya kuwasilisha hoja binafsi
kupinga Bunge kujadili tena suala lolote la kidini, alisema yeye binafsi anaishauri
sana Serikali kuheshimu Katiba ya nchi.

“Mimi Ningependa tu kuishauri Serikali kuheshimu Katiba, nchi hii inaongozwa kwa
Katiba na sijawahi kusikia sheria za nchi hii zimeshindwa kuwapatia watu wake haki
yao, sasa hakuna sababu ya kuingiza chombo kingine kinachoweza kuvuruga umoja,
mshikamano ulipo, kama kuna upungufu katika sheria basi sheria hiyo ndiyo
ingerekebishwa,”alisema.

Alipotakiwa kueleza ni lini utoaji wa elimu hiyo utakoma, alisema elimu
hiyo ni endelevu na kamwe haitakoma kwa kuwa ni haki ya Kanisa kuelimisha wananchi
wake kila inapoona inafaa kufanya hivyo.

Alisema kiongozi yeyote anayetimiza wajibu wake hawezi kuwa na hofu juu ya mtu
mwingine kutoa elimu inayolenga kuwakomboa watu anaowaongoza na kusisitiza kuwa
Kanisa hilo lina nia njema na halina ugomvi wowote na Serikali wala chama chochote
isipokuwa linatimiza wajibu wake wa kuelimisha wananchi kuhusu elimu ya uraia.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya madhehebu kuweka wazi nia ya kutoa waraka kama huo
alisema “Ni haki yao, tena wamechelewa kufanya hivyo, nawashauri watoe na waelimishe waumini wao,”alisema.

Naye Reuben Kagaruki kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Padre wa Kanisa Katoliki, Shirika la Wamisionari wa Afrika, Baptiste Mapunda, amesema watu wanaopinga waraka huo wanachezea amani ya Tanzania na wanataka kuendelea kubaki madarakani mileleni.

Amewataka watu hao kutambua kuwa viongozi wa dini, hawakuchaguliwa kwa vidole, bali ni wateule wa Mungu.

Akizungumza kwenye ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Padre Mapunda alisisitiza; "Waraka unapotoshwa na kuchezewa na watu wanaojihisi mafisadi, wanafanya hivyo kwa kuogopa mabadiliko.

Alisema wao (Wakatoliki) hawatarudi nyuma kwa kuacha kumtii Mungu na kuanza kufuata matakwa ya watu, kwa kuwa waraka huo haulengi kuvuruga amani.

"Hata kama mtu hana Mungu ndani yake, basi aupitie kwa akili za kibinadamu ataelewa kilichoandikwa," alisema Padre Mapunda na kuongeza;

"Wanaoupinga hawataki Watanzania wajue elimu ya uraia, ili waendelee kubaki madarakani."

Aliendelea kusisitiza kuwa; "Kinachonitisha ni kuona baadhi ya viongozi wanag'ang'ania watu waishi kwenye giza, najiuliza hawa ni viongozi wa aina gani? Hii siyo alama ya demokrasia, bali ndani yake kuna chembechembe za udikteta."

Padre Mapunda alisema wakati umefika sasa wa viongozi, kuongozwa na elimu na siyo uzoefu. "Watu wanafanyakazi kwa mazoea ndiyo maana hatuendelei!" alilalamika Padre Mapunda.

Aliongeza kuwa kama waraka huo, ungekuwa na matatizo watu wa kwanza kuulalamikia wangekuwa wakatoliki, kwa kuwa wengi wamesoma na kuuelewa.

Alisema waraka huo ulipitishwa na maaskofu zaidi ya 30, hivyo kama ungekuwa unahatarisha amani ya nchi wasingeupitisha.

Padre Mapunda, alisema Serikali imekuwa ikiziomba taasisi za dini kusaidia kujenga maadili ndani ya jamii, lakini inashangaza kuona inageuka na kuanza kuona viongozi wa dini kama maadui.

Alisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kitatawala milele. "Kama kuna watu wenye mawazo hayo wanajidanganya kwani anayetawala milele ni Mungu," alisema na kuongeza;

"Ni lazima utafika wakati watu watachoka na huo, ndiyo utakuwa mwisho wa mfumo mzima." Alisema wanaopinga waraka huo hawataki mawazo mapya.

Pia Padre huyo alikemea tabia ambayo imeanza kushamiri ambapo watoto wa vigogo wamekuwa wakijiingiza kwenye siasa kwa kufuata nyayo za wazazi wao.

"Mbegu hii ni chafu, hakuna sababu ya kila mtoto wa kiongozi kuwa mwanasiasa," alisema na kushauri uigwe mfano wa watoto wa Baba wa Taifa Marehemu Julius Nyerere, ambao hawakufuata nyayo za baba yao.
 
Mkuu "Wakatoliki wadhibitiwe" na maneno yako au ya John Danile? Maana tite haiendani na hiyo artice uliyo paste na kucopy.
 
Tuesday, 21 July 2009 16:39 *Wasema ni haki ya kanisa kuelimisha wananchi wake
*Viongozi wanaopinga wana uelewa finyu wa siasa
*Wanaotimiza wajibu hawaogopi wenzao kuelimishwa
*Lataka dini zote zitoe waraka na kuelimisha waumini
*Mahakama ya Kadhi:Serikali iheshimu Katiba

Na John Danile, Dodoma

KANISA Katoliki nchini limetoa tamko rasmi kwa viongozi wanaopinga waraka wake uliotolewa hivi karibuni unaolenga kutoa elimu ya uraia na kuwaelezea kwamba wana upeo finyu kuhusu siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Holy Cross mjini hapa jana, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini, Askofu Juda Ruwa'ichi, alisema waraka huo una nia nzuri kwani unalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwatoa wananchi pale walipo.

"Kiongozi yeyote anayepinga au kuwa na wasiwasi na waraka huo na kuujadili huenda
ana uelewa finyu kuhusu siasa, Kanisa halishughuliki na viumbe hewa, Kanisa
linajishughulisha na watu wanaohitaji kila kitu kama sehemu ya haki yao ya msingi
ikiwemo elimu ya uraia,"alisema Askofu Ruwa'ichi.

Alisema amesikitishwa na mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yalitolewa na watu
mbalimbali wakiwemo wanasiasa kuhusu waraka huo na kuonya kuwa tafsiri wanazotoa zinajenga chuki miongoni mwa jamii kwa kuwa ni potofu na zinalenga kukwepa uwajibikaji.

"Mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yalitotolewa na wanasiasa unadokeza wazi, wapo wanaojadili ilani hiyo bila kujua kwanza yaliyomo ndani yake, hali hii
inasababisha upotoshaji, kuwakanganya watu na hata kuzusha hisa za chuki katika
Jamii, huu si uwajibikaji, katika hili ninapenda kuwaasa Watanzania kuwa watu wenye kutafuta ukweli na kujenga kauli za hoja juu ya msingi huo wa ukweli na uelewa
sahihi.

"Kanisa Katoliki linatafuta kwa nia njema kabisa kuwasaidia raia wa nchi hii bila
ubaguzi kujizatiti kutambua na kushughulikia maslahi ya wote siyo tu kwa kuzingatia leo, bali pia kwa namna inayoihakikishia nchi hii na raia wake wote amali za amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo mtambuka yaliyo endelevu. Mwelekeo unaokithiri sasa hautuhakikishii hayo,"alisema Askofu Ruwa'ichi.

Alisema anasikitishwa kuona watu wanahusisha waraka huo na uchaguzi wa madiwani na
ule mkuu ujao mwaka kesho wakati si lengo la waraka huo kumwambia mtu achague mtu
fulani bali inalenga kuwatoa watanzania pale walipo kwa kujitambua na kutimiza
wajibu wao.

"Ni Muhimu kuzielewa changamoto na kuzipa kila mmoja uzito unaostahili kwa lengo la
kutafuta kushughulikia maendeleo yetu kwa dhati zaidi, uelewa huo utatuwajibisha
tuamue ni nani mwenye uwezo wa kushirikiana nasi ili tujinasue kutoka hapa tulipo
na kupiga hatua za dhati mbele.

"Viongozi wanaochaguliwa na watu wanapewa dhamana,wanao wajibu wa kutambua na kujadili maslahi ya wote kwa kufanya juhudi za dhati na makusudi ili kuvielewa na kuvishughulikia vipaumbele halali na sahihi bila kujiruhusu kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila udini au ubaguzi wa aina
yoyote," alisema.

Alipoulizwa msimamo wa kanisa hilo kuhusu mchakato wa Mahakama ya Kadhi kwa
kuzingatia kuwa tayari baadhi ya wabunge wameonesha nia ya kuwasilisha hoja binafsi
kupinga Bunge kujadili tena suala lolote la kidini, alisema yeye binafsi anaishauri
sana Serikali kuheshimu Katiba ya nchi.

"Mimi Ningependa tu kuishauri Serikali kuheshimu Katiba, nchi hii inaongozwa kwa
Katiba na sijawahi kusikia sheria za nchi hii zimeshindwa kuwapatia watu wake haki
yao, sasa hakuna sababu ya kuingiza chombo kingine kinachoweza kuvuruga umoja,
mshikamano ulipo, kama kuna upungufu katika sheria basi sheria hiyo ndiyo
ingerekebishwa,"alisema.

Alipotakiwa kueleza ni lini utoaji wa elimu hiyo utakoma, alisema elimu
hiyo ni endelevu na kamwe haitakoma kwa kuwa ni haki ya Kanisa kuelimisha wananchi
wake kila inapoona inafaa kufanya hivyo.

Alisema kiongozi yeyote anayetimiza wajibu wake hawezi kuwa na hofu juu ya mtu
mwingine kutoa elimu inayolenga kuwakomboa watu anaowaongoza na kusisitiza kuwa
Kanisa hilo lina nia njema na halina ugomvi wowote na Serikali wala chama chochote
isipokuwa linatimiza wajibu wake wa kuelimisha wananchi kuhusu elimu ya uraia.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya madhehebu kuweka wazi nia ya kutoa waraka kama huo
alisema "Ni haki yao, tena wamechelewa kufanya hivyo, nawashauri watoe na waelimishe waumini wao,"alisema.

Naye Reuben Kagaruki kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Padre wa Kanisa Katoliki, Shirika la Wamisionari wa Afrika, Baptiste Mapunda, amesema watu wanaopinga waraka huo wanachezea amani ya Tanzania na wanataka kuendelea kubaki madarakani mileleni.

Amewataka watu hao kutambua kuwa viongozi wa dini, hawakuchaguliwa kwa vidole, bali ni wateule wa Mungu.

Akizungumza kwenye ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Padre Mapunda alisisitiza; "Waraka unapotoshwa na kuchezewa na watu wanaojihisi mafisadi, wanafanya hivyo kwa kuogopa mabadiliko.

Alisema wao (Wakatoliki) hawatarudi nyuma kwa kuacha kumtii Mungu na kuanza kufuata matakwa ya watu, kwa kuwa waraka huo haulengi kuvuruga amani.

"Hata kama mtu hana Mungu ndani yake, basi aupitie kwa akili za kibinadamu ataelewa kilichoandikwa," alisema Padre Mapunda na kuongeza;

"Wanaoupinga hawataki Watanzania wajue elimu ya uraia, ili waendelee kubaki madarakani."

Aliendelea kusisitiza kuwa; "Kinachonitisha ni kuona baadhi ya viongozi wanag'ang'ania watu waishi kwenye giza, najiuliza hawa ni viongozi wa aina gani? Hii siyo alama ya demokrasia, bali ndani yake kuna chembechembe za udikteta."

Padre Mapunda alisema wakati umefika sasa wa viongozi, kuongozwa na elimu na siyo uzoefu. "Watu wanafanyakazi kwa mazoea ndiyo maana hatuendelei!" alilalamika Padre Mapunda.

Aliongeza kuwa kama waraka huo, ungekuwa na matatizo watu wa kwanza kuulalamikia wangekuwa wakatoliki, kwa kuwa wengi wamesoma na kuuelewa.

Alisema waraka huo ulipitishwa na maaskofu zaidi ya 30, hivyo kama ungekuwa unahatarisha amani ya nchi wasingeupitisha.

Padre Mapunda, alisema Serikali imekuwa ikiziomba taasisi za dini kusaidia kujenga maadili ndani ya jamii, lakini inashangaza kuona inageuka na kuanza kuona viongozi wa dini kama maadui.

Alisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kitatawala milele. "Kama kuna watu wenye mawazo hayo wanajidanganya kwani anayetawala milele ni Mungu," alisema na kuongeza;

"Ni lazima utafika wakati watu watachoka na huo, ndiyo utakuwa mwisho wa mfumo mzima." Alisema wanaopinga waraka huo hawataki mawazo mapya.

Pia Padre huyo alikemea tabia ambayo imeanza kushamiri ambapo watoto wa vigogo wamekuwa wakijiingiza kwenye siasa kwa kufuata nyayo za wazazi wao.

"Mbegu hii ni chafu, hakuna sababu ya kila mtoto wa kiongozi kuwa mwanasiasa," alisema na kushauri uigwe mfano wa watoto wa Baba wa Taifa Marehemu Julius Nyerere, ambao hawakufuata nyayo za baba yao.
Anachoshindwa kuelewa huyo Askofu Juda Ruwa'ichi ni kwamba hata mahubiri ya dini zote yana nia nzuri kwa wananchi na binadamu wote -Tunaelewa hilo, isipokuwa tumetengana na kila mmoja wetu anaamini dini tofauti, na kinacholeta tofauti zetu kinatokana na Mafundisho na MWONGOZO wa kila dini...

Hivyo ktk Siasa mwongozo wetu ni Katiba ya nchi..ndiyo inaweza kusomeshwa kwa kila raia kama vile wanavyofundisha hesabu na masomo mengine kwa waumini au wananchi watakao taka kuelemika ktk somo hilo. Kanisa haliwezi kutunga mwongozo wa somo lolote hata iwe hesabu kwa wizara ya Elimu nchini ila kanisa litachukua mwongozo wa elimu hiyo toka serikalini..jinsi ya kufundisha wanafunzi wake ni jukumu la kanisa ama shule husika.. huko ndiko unaweza tunga mwongozo wa shule au taasisi inayohusika.

Katiba ndio mwongozo wetu sote iwe hata kifungu cha Uchaguzi, watafundisha tu kile kilichokubaliwa na Bunge letu na sio wao kutoa mwongozo kwa serikali hata kama wana nia nzuri... Na hakuna aliyesema hawana nia nzuri ila ni kinyume cha taratibu za kiutawala. Na lini kanisa likajua Siasa jamani kama sii kamba hizi...

Najua fika kanisa lina nia nzuri hata katika mafundisho yake ya dini lakini hukini mimi sii muumini wa dini hiyo wala mwongozo wao..Ikiwa mwongozo huu ni kwa Wakristu tu nahauhusiani na uchaguzi ila elimu ya Uraia hapo poa wafundishe mashuleni wananchi watakuja pata elimu hiyo..
Anavosisitiza kwamba mahakama ya Kadhi ni lazima serikali iheshimu katiba hata kama ni kwa waislaam,iweje anashindwa kuona kama huu mwongozo ni lazima uheshimu katiba tena unahusu watu wote kwa madhehebu tofauti..
 
Ule waraka kwa waliousoma una mambo mengi. Hawa wanaoujadili nilitegemea wawe na huo waraka waseme ni sehemu gani yenye matatizo na inahitaji marekebisho. Kwa vyo vyote waraka mzima hauwezi kuwa na matatizo. Nafikiri tatizo ni ukatoliki na sio waraka kwa kuwa wote wanaoupinga hawajui hata rangi ya jalada lake.
 
WAPENDWA Tuache kuwanyooshea kidole watumishi wa Mungu.

nawashauri tujitahidi sana ktk hili. Ukisoma ktk Biblia, David alimkuta Saul pangoni amelala usingizi. Saul alikuwa amepumzika ktk harakati za kumtafuta David ili amuue.

Askari mmoja wa David akamwomba David amruhusu ampige Saul na kumuua. David alikataa na kusema hawezi kumnyooshea mkono mpakwa wa Bwana licha ya ukweli kuwa anatafuta kumuua.

MUNGU AWABARIKI
 
Kwa upande wa muendesha kipindi mzee makwaia ...nashauri kipindi kijacho awaalike wawakilishi wa kanisa katoliki ..ili nao waweze kujibu mashambulizi ambayo wamekuwa wakitupiwa tangu wiki iliyopita kupitia kipindi chake
e-mail:makwaia@makwaia.com
​
Cell:​
+25575436520 /+25577306674Office Location:
2nd Floor,
Bakwata Building, Junction of Bibi Titi/Morogoro Road,
Dar es Salaam,
Tanzania​
​
​
​

Kwa udini wa Makwaia, Je, Tutafika?
 
Waraka wa Katoliki wamkuna Lipumba
broken-heart.jpg
*UNDP NAYO YAUUNGA MKONO

Na Elias Msuya

MWENYEKITI wa CUF, Ibrahim Lipumba ameunga mkono waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki, unaohusu Uchaguzi Mkuu ujao kwa sababu unaeleza sifa zinazompasa mtu kuongoza taifa, lakini akapinga baadhi ya vipengele kwenye mwongozo huo akidai kuwa vinapingana na utaratibu wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Akitoa maoni yake kuhusu mwongozo huo muda mfupi baada ya kufungua warsha kuhusu mikakati na mbinu za kuongeza uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi serikalini iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Lipumba alisema ameona mambo makuu mawili kwenye mwongozo huo.

Alisema kwanza umejadili vizuri mambo ambayo serikali inapaswa kuyarekebisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Alisema kwamba, ni waraka mzuri ambao umetoa mwongozo kwa serikali kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kwamba hata vyama vya siasa vinaweza kuuingiza kwenye ilani zao.

"Serikali inapaswa kurekebisha mambo kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Ni mambo ambayo hata vyama vya siasa vinaweza kuyaingiza kwenye ilani zao," alisema.

Lakini pia, kiongozi huyo wa CUF alisema waraka huo umejiingiza kujadili mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Alidai kwamba suala la waraka kujadili kwamba taasisi za dini zisihusishwe katika kuendesha serikali ndilo analotofautiana nalo.

"Kama umeusoma waraka huo katika ukurasa wa tisa, wamezungumzia kutofautisha serikali na taasisi za dini na wamezitaja kabisa kuwa ni Mahakama ya Kadhi na OIC. Sasa hapo utaona kwamba kuna hali ya kutoeleweka kwa waraka huo," alisema.

Nao Boniface Meena na Beatus Kagashe wanaripoti kuwa, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), limeunga mkono mwongozo huo wa Kanisa Katoliki likisema kuwa ni mzuri na ni muhimu kusambazwa ili watu wapate elimu iliyomo ndani yake.

Pia UNDP imeeleza kuwa ni hatari elimu hiyo isipotolewa kwa kuwa wananchi wanaihitaji.

Shirika hilo limesema linaandaa mchakato ambao utashirikisha taasisi za kijamii katika kutoa elimu kwa jamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kaimu Mkurugenzi mkazi (Mipango) wa UNDP, Louse Chamberlain alisema kuwa, mjadala unaoendelea hivi sasa nchini ni mzuri kwani unasaidia kujua ni jinsi gani elimu imewafikia wapigakura, viongozi na jamii kwa ujumla.

"Mjadala unaondelea ni mzuri kwa nchi ambayo demokrasia inakua; watu wanatoa maoni jinsi gani ya kuifikia jamii kwa urahisi," alisema.

Alisema kuwa, hivi sasa wanafanya mazungumzo na serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini na taasisi za kijamii kuangalia ni jinsi gani elimu ya uchaguzi inaweza ikatolewa kwa wananchi.

Chamberlain alisema UNDP itahitaji michakato kutoka taasisi za kijamii ambazo zina uwezo wa kutoa elimu hiyo, ili zipitiwe na kupatiwa fedha kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

"Muda utakapofika, tutahitaji michakato hiyo na itakuwa wazi na maelezo yatatolewa ili kuchagua zile taasisi zitakazokuwa na uwezo ziweze kupatiwa fedha," alisema.

Aliongeza kuwa taasisi zitatakiwa kuwa bunifu katika kutafuta mbinu za kufikisha ujumbe kwa watu wengi ili waweze kutumia kura kama silaha zao.

Chamberlain alisema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005 taasisi 34 za kijamii zilipewa kiasi cha dola 1.9 milioni za Kimarekani kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii nchini kote.

Alisema kati ya taasisi hizo, tatu zilikuwa ni za dini ambazo ni Kamati ya Kikristo ya Huduma kwa Jamii ambayo ilipewa Sh 275.4 milioni kutoa elimu kwa kila wilaya hapa nchini, Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) ambalo lilipewa Sh 172.6 milioni kwa ajili ya kutoa elimu kwa wilaya 16. Taasisi nyingine ni World Conference on Religions for Peace (WCRP).

Naye Nora Damian anaripoti kuwa, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, amesema anaunga mkono waraka huo kwa sababu unaeleza sifa zinazompasa mtu kuongoza taifa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mtikila alisema uamuzi wa Kanisa Katoliki kutoa waraka huo ni ushindi mkubwa kwani utasaidia jamii kuelewa kwa mapana kuhusu chaguzi mbalimbali, hasa Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge.

Alisema wanaopinga waraka huo hawana nia njema na kwamba wana lengo la kuendelea kulea mafisadi, huku akimwelezea mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ambaye alitaka kanisa lifute waraka huo, kuwa anazeeka vibaya.

"Kingunge anazeeka vibaya; madhehebu mbalimbali yameuunga mkono waraka ule kwa sababu unaeleza sifa zipi zinazompasa mtu kuongoza. Je, haya ni mambo mabaya?" alihoji Mtikila. "Nangojea makanisa mengine yatoe miongozo yao halafu mimi nitafanya majumuisho na nitatoa elimu kwa watu wote kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao," alisisitiza.
 
duh ....sasa mtu kupanga ofisi kwenye jengo la bakwata imekuwa mdini! ...inaonyesha tanzania sote kama si wadini ni mafisadi.
kuanzia mashule ni ya dini, na majengo karibu ya yote yanamilikiwa na mafisadi ....tutafika hivi kwa tunavyonyoosheana vidole jamani?
 
Waraka wa Katoliki wamkuna Lipumba
broken-heart.jpg
*UNDP NAYO YAUUNGA MKONO

Na Elias Msuya

MWENYEKITI wa CUF, Ibrahim Lipumba ameunga mkono waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki, unaohusu Uchaguzi Mkuu ujao kwa sababu unaeleza sifa zinazompasa mtu kuongoza taifa, lakini akapinga baadhi ya vipengele kwenye mwongozo huo akidai kuwa vinapingana na utaratibu wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Akitoa maoni yake kuhusu mwongozo huo muda mfupi baada ya kufungua warsha kuhusu mikakati na mbinu za kuongeza uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi serikalini iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Lipumba alisema ameona mambo makuu mawili kwenye mwongozo huo.

Alisema kwanza umejadili vizuri mambo ambayo serikali inapaswa kuyarekebisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Alisema kwamba, ni waraka mzuri ambao umetoa mwongozo kwa serikali kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kwamba hata vyama vya siasa vinaweza kuuingiza kwenye ilani zao.

“Serikali inapaswa kurekebisha mambo kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Ni mambo ambayo hata vyama vya siasa vinaweza kuyaingiza kwenye ilani zao," alisema.

Lakini pia, kiongozi huyo wa CUF alisema waraka huo umejiingiza kujadili mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Alidai kwamba suala la waraka kujadili kwamba taasisi za dini zisihusishwe katika kuendesha serikali ndilo analotofautiana nalo.

“Kama umeusoma waraka huo katika ukurasa wa tisa, wamezungumzia kutofautisha serikali na taasisi za dini na wamezitaja kabisa kuwa ni Mahakama ya Kadhi na OIC. Sasa hapo utaona kwamba kuna hali ya kutoeleweka kwa waraka huo,” alisema.

Nao Boniface Meena na Beatus Kagashe wanaripoti kuwa, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), limeunga mkono mwongozo huo wa Kanisa Katoliki likisema kuwa ni mzuri na ni muhimu kusambazwa ili watu wapate elimu iliyomo ndani yake.

Pia UNDP imeeleza kuwa ni hatari elimu hiyo isipotolewa kwa kuwa wananchi wanaihitaji.

Shirika hilo limesema linaandaa mchakato ambao utashirikisha taasisi za kijamii katika kutoa elimu kwa jamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kaimu Mkurugenzi mkazi (Mipango) wa UNDP, Louse Chamberlain alisema kuwa, mjadala unaoendelea hivi sasa nchini ni mzuri kwani unasaidia kujua ni jinsi gani elimu imewafikia wapigakura, viongozi na jamii kwa ujumla.

"Mjadala unaondelea ni mzuri kwa nchi ambayo demokrasia inakua; watu wanatoa maoni jinsi gani ya kuifikia jamii kwa urahisi," alisema.

Alisema kuwa, hivi sasa wanafanya mazungumzo na serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini na taasisi za kijamii kuangalia ni jinsi gani elimu ya uchaguzi inaweza ikatolewa kwa wananchi.

Chamberlain alisema UNDP itahitaji michakato kutoka taasisi za kijamii ambazo zina uwezo wa kutoa elimu hiyo, ili zipitiwe na kupatiwa fedha kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

"Muda utakapofika, tutahitaji michakato hiyo na itakuwa wazi na maelezo yatatolewa ili kuchagua zile taasisi zitakazokuwa na uwezo ziweze kupatiwa fedha," alisema.

Aliongeza kuwa taasisi zitatakiwa kuwa bunifu katika kutafuta mbinu za kufikisha ujumbe kwa watu wengi ili waweze kutumia kura kama silaha zao.

Chamberlain alisema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005 taasisi 34 za kijamii zilipewa kiasi cha dola 1.9 milioni za Kimarekani kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii nchini kote.

Alisema kati ya taasisi hizo, tatu zilikuwa ni za dini ambazo ni Kamati ya Kikristo ya Huduma kwa Jamii ambayo ilipewa Sh 275.4 milioni kutoa elimu kwa kila wilaya hapa nchini, Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) ambalo lilipewa Sh 172.6 milioni kwa ajili ya kutoa elimu kwa wilaya 16. Taasisi nyingine ni World Conference on Religions for Peace (WCRP).

Naye Nora Damian anaripoti kuwa, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, amesema anaunga mkono waraka huo kwa sababu unaeleza sifa zinazompasa mtu kuongoza taifa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mtikila alisema uamuzi wa Kanisa Katoliki kutoa waraka huo ni ushindi mkubwa kwani utasaidia jamii kuelewa kwa mapana kuhusu chaguzi mbalimbali, hasa Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge.

Alisema wanaopinga waraka huo hawana nia njema na kwamba wana lengo la kuendelea kulea mafisadi, huku akimwelezea mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ambaye alitaka kanisa lifute waraka huo, kuwa anazeeka vibaya.

“Kingunge anazeeka vibaya; madhehebu mbalimbali yameuunga mkono waraka ule kwa sababu unaeleza sifa zipi zinazompasa mtu kuongoza. Je, haya ni mambo mabaya?” alihoji Mtikila. “Nangojea makanisa mengine yatoe miongozo yao halafu mimi nitafanya majumuisho na nitatoa elimu kwa watu wote kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao,” alisisitiza.
 
MKUU
umekuwa mdini tangu lini maana umegeuka abruptly na kasi yako sasa si haba tena.
teh teh teh teh teh
Ni kweli Lunyungu hachangii hoja siku hizi zaidi za ya kushambuliwa. angalia thread zake alizoanzisha!
 
achana nae mnyakyu huyo!ANATAFUTA INFLUENCE
Nadhani ukisema....mnyakyu...utakuwa umemaanisha kuwa wewe na Mch.Antony Lusekelo hamko tofauti kimawazo kwa yale aliyochefua ktk kipindi hicho ila wewe umeenda upande mwingine zaidi wa Kibaguzi pasipo kuweka mjadala wa kimawazo kwa kuweka ujumla mawazo ya Mch.Antony Lusekelo kuwa ni mawazo ya ...wanyakyu..hiyo tu inakuweka ktk fikra mfinyu isiyo tabainisha kilichozungumzwa katika kipindi cha Makwaia pale Channel Ten.

Kwa ujumla Mch.Antony Lusekelo hakufunuliwa Kiroho nini kilimaanisha katika kipindi kile na akajipeleka bila maandalizi! na kwa kufanya hivyo akaishia kuongea asichokipenda akimaanisha anakipenda kumbe sivyo.Dini inafundisha watu wawe waadilifu,waaminifu,wenye subira na wenye kutanguliza utu na hicho kiluchoelezwa katika Ilani ya wakatoliki,anaposema inachefua anamaanisha basi hata anachokihubiri basi hakina mantiki ya kuwapeleka watu kumiliki na kula matunda ya nchi.Ndo maana nikasema hakujua nini anatakiwa kufanya kwenye luninga.nadhani atakaporudia kukiangalia kipindi atajua wapi alikosea.

Joune,
Ndikupasya Buno Malafyale anganile kangi Ambokile.
 
Wengi ndani ya forum hii wanaangalia kitu kimoja, waraka ni mzuri hivyo hakuna shida kama wakatoliki ndio wameutoa. Pamoja na hayo wengi hao wanasema hakuna shida kuchanganya dini na siasa, ukiwauliza kwanini kuchanganya dini na siasa ni kitu kizuri, hutapata jibu la moja kwa moja.

Hutapata jibu la moja kwa moja kwa sababu dini ni imani, na imani haihitaji ushahidi ili ikubalike. Ukishakuwa na imani basi hakuna haja ya sababu. Ukishaamini biblia au korani ina majibu yote hata yale ya kisiasa, huna haja ya kuhoji kuhusu hili kwani imani yako inakuambia hili ni neno la Mungu. Nani anabishana na neno la Mungu?

Matatizo ya mitazamo kama hii yanaepukika ikiwa kuna mipaka kati ya dini na siasa. Ukweli kuhusu yale yaliyomo kwenye Biblia au Korani hauwezi kuzungumziwa katika Siasa. Na serikali haiwezi kusema ni vipi Biblia au Korani itafsiriwe kwenye mada mbalimbali. Serikali inaweza kutafsiri "policy" mbali mbali lakini haiwezi kutafsiri maana za Biblia au Korani. Kwanini dini ijiingize kutafsiri "policy" za serikali wakati serikali haiwezi kufanya hivyo hivyo kwa dini?

Serikali inatakiwa kuwa kali katika kutenganisha dini na siasa. Ujinga wa kuzipa asasi za kidini fedha ili zisaidie huduma za jamii ni kuzifanya kuwa mikono mingine ya serikali.

When religious people begin to believe that they are the kingdom, this is the beginning of the end.

Insurgent, mswalie mtume bwana! kuna dhambi gani kwa watu wa dini kujadili siasa ilhali wao pia ni sehemu ya jamii au ndo una mpango wa kuwakosanisha na Mungu wao. Mchungaji mzuri hupeleka kondoo wake kwenye malisho mazuri. Na hili ndilo watumishi wa mungu wanalojaribu kulifanya. Lakini umesahau mjadala wa serikali kuhusu ibada yetu ya mahakama ya kadhi?
 
Nadhani ukisema....mnyakyu...utakuwa umemaanisha kuwa wewe na Mch.Antony Lusekelo hamko tofauti kimawazo kwa yale aliyochefua ktk kipindi hicho ila wewe umeenda upande mwingine zaidi wa Kibaguzi pasipo kuweka mjadala wa kimawazo kwa kuweka ujumla mawazo ya Mch.Antony Lusekelo kuwa ni mawazo ya ...wanyakyu..hiyo tu inakuweka ktk fikra mfinyu isiyo tabainisha kilichozungumzwa katika kipindi cha Makwaia pale Channel Ten.

Kwa ujumla Mch.Antony Lusekelo hakufunuliwa Kiroho nini kilimaanisha katika kipindi kile na akajipeleka bila maandalizi! na kwa kufanya hivyo akaishia kuongea asichokipenda akimaanisha anakipenda kumbe sivyo.Dini inafundisha watu wawe waadilifu,waaminifu,wenye subira na wenye kutanguliza utu na hicho kiluchoelezwa katika Ilani ya wakatoliki,anaposema inachefua anamaanisha basi hata anachokihubiri basi hakina mantiki ya kuwapeleka watu kumiliki na kula matunda ya nchi.Ndo maana nikasema hakujua nini anatakiwa kufanya kwenye luninga.nadhani atakaporudia kukiangalia kipindi atajua wapi alikosea.

Joune,
Ndikupasya Buno Malafyale anganile kangi Ambokile.

Tatizo ni upeo wa kuelewa kwake. Na huyo ndiye mtu afundishae na kuongoza kondoo wa bwana. Sasa kwa nini woote wamsikilizao na kumfuata wasiwe kama yeye? Mwalimu sharti awe na upeo wa juu zaidi ya mwanafunzi, kinyume chake ni kama vipofu wawili wanafundishana kusoma na kuandika
 
Nadhani ukisema....mnyakyu...utakuwa umemaanisha kuwa wewe na Mch.Antony Lusekelo hamko tofauti kimawazo kwa yale aliyochefua ktk kipindi hicho ila wewe umeenda upande mwingine zaidi wa Kibaguzi pasipo kuweka mjadala wa kimawazo kwa kuweka ujumla mawazo ya Mch.Antony Lusekelo kuwa ni mawazo ya ...wanyakyu..hiyo tu inakuweka ktk fikra mfinyu isiyo tabainisha kilichozungumzwa katika kipindi cha Makwaia pale Channel Ten.

Kwa ujumla Mch.Antony Lusekelo hakufunuliwa Kiroho nini kilimaanisha katika kipindi kile na akajipeleka bila maandalizi! na kwa kufanya hivyo akaishia kuongea asichokipenda akimaanisha anakipenda kumbe sivyo.Dini inafundisha watu wawe waadilifu,waaminifu,wenye subira na wenye kutanguliza utu na hicho kiluchoelezwa katika Ilani ya wakatoliki,anaposema inachefua anamaanisha basi hata anachokihubiri basi hakina mantiki ya kuwapeleka watu kumiliki na kula matunda ya nchi.Ndo maana nikasema hakujua nini anatakiwa kufanya kwenye luninga.nadhani atakaporudia kukiangalia kipindi atajua wapi alikosea.

Joune,
Ndikupasya Buno Malafyale anganile kangi Ambokile.

Ndaga

atafunuliwaje mzee wa konyagi na toto's?
 
Makwaia ana mawazo ya kiislam ni Muhahidina wa nguvu hana hata heshima mbele za Umma .Huyo wa Upako ndiyo kanisa lake linachunguza sadaka ? Tunaendelea .
Hakuna muhahidina katika uislam labda sema mujahidina(anayetetea na kusimamia dini yake).HAta hivyo mbona Makwaia tumeshasali nae kanisa la kkkt pale sinza?Au ana dini mbili?
 
Kwani LUSEKELO naye ni mchungaji?Mzee Makwaia kwanza alikosea kumwita na kujadili huo waraka kwa wazifa wa mchungaji ilihali hana hiyo sifa ya uchungaji,jamani wachungaji si wanajulikanaa,sasa ngoja namimi nianzishe kanisa na nitajiita Askofu ala kwani uchungaji ni cheo kidogo halafu nitajipeleka kwa mzee Makwai nikajadili huo waraka
 
Tuesday, 21 July 2009 16:39 *Wasema ni haki ya kanisa kuelimisha wananchi wake
*Viongozi wanaopinga wana uelewa finyu wa siasa
*Wanaotimiza wajibu hawaogopi wenzao kuelimishwa
*Lataka dini zote zitoe waraka na kuelimisha waumini
*Mahakama ya Kadhi:Serikali iheshimu Katiba

Na John Danile, Dodoma

KANISA Katoliki nchini limetoa tamko rasmi kwa viongozi wanaopinga waraka wake uliotolewa hivi karibuni unaolenga kutoa elimu ya uraia na kuwaelezea kwamba wana upeo finyu kuhusu siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Holy Cross mjini hapa jana, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini, Askofu Juda Ruwa’ichi, alisema waraka huo una nia nzuri kwani unalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwatoa wananchi pale walipo.

“Kiongozi yeyote anayepinga au kuwa na wasiwasi na waraka huo na kuujadili huenda
ana uelewa finyu kuhusu siasa, Kanisa halishughuliki na viumbe hewa, Kanisa
linajishughulisha na watu wanaohitaji kila kitu kama sehemu ya haki yao ya msingi
ikiwemo elimu ya uraia,”alisema Askofu Ruwa'ichi.

Alisema amesikitishwa na mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yalitolewa na watu
mbalimbali wakiwemo wanasiasa kuhusu waraka huo na kuonya kuwa tafsiri wanazotoa zinajenga chuki miongoni mwa jamii kwa kuwa ni potofu na zinalenga kukwepa uwajibikaji.

“Mkanganyiko wa mawazo na mawaidha yalitotolewa na wanasiasa unadokeza wazi, wapo wanaojadili ilani hiyo bila kujua kwanza yaliyomo ndani yake, hali hii
inasababisha upotoshaji, kuwakanganya watu na hata kuzusha hisa za chuki katika
Jamii, huu si uwajibikaji, katika hili ninapenda kuwaasa Watanzania kuwa watu wenye kutafuta ukweli na kujenga kauli za hoja juu ya msingi huo wa ukweli na uelewa
sahihi.

“Kanisa Katoliki linatafuta kwa nia njema kabisa kuwasaidia raia wa nchi hii bila
ubaguzi kujizatiti kutambua na kushughulikia maslahi ya wote siyo tu kwa kuzingatia leo, bali pia kwa namna inayoihakikishia nchi hii na raia wake wote amali za amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo mtambuka yaliyo endelevu. Mwelekeo unaokithiri sasa hautuhakikishii hayo,”alisema Askofu Ruwa’ichi.

Alisema anasikitishwa kuona watu wanahusisha waraka huo na uchaguzi wa madiwani na
ule mkuu ujao mwaka kesho wakati si lengo la waraka huo kumwambia mtu achague mtu
fulani bali inalenga kuwatoa watanzania pale walipo kwa kujitambua na kutimiza
wajibu wao.

“Ni Muhimu kuzielewa changamoto na kuzipa kila mmoja uzito unaostahili kwa lengo la
kutafuta kushughulikia maendeleo yetu kwa dhati zaidi, uelewa huo utatuwajibisha
tuamue ni nani mwenye uwezo wa kushirikiana nasi ili tujinasue kutoka hapa tulipo
na kupiga hatua za dhati mbele.

"Viongozi wanaochaguliwa na watu wanapewa dhamana,wanao wajibu wa kutambua na kujadili maslahi ya wote kwa kufanya juhudi za dhati na makusudi ili kuvielewa na kuvishughulikia vipaumbele halali na sahihi bila kujiruhusu kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila udini au ubaguzi wa aina
yoyote," alisema.

Alipoulizwa msimamo wa kanisa hilo kuhusu mchakato wa Mahakama ya Kadhi kwa
kuzingatia kuwa tayari baadhi ya wabunge wameonesha nia ya kuwasilisha hoja binafsi
kupinga Bunge kujadili tena suala lolote la kidini, alisema yeye binafsi anaishauri
sana Serikali kuheshimu Katiba ya nchi.

“Mimi Ningependa tu kuishauri Serikali kuheshimu Katiba, nchi hii inaongozwa kwa
Katiba na sijawahi kusikia sheria za nchi hii zimeshindwa kuwapatia watu wake haki
yao, sasa hakuna sababu ya kuingiza chombo kingine kinachoweza kuvuruga umoja,
mshikamano ulipo, kama kuna upungufu katika sheria basi sheria hiyo ndiyo
ingerekebishwa,”alisema.

Alipotakiwa kueleza ni lini utoaji wa elimu hiyo utakoma, alisema elimu
hiyo ni endelevu na kamwe haitakoma kwa kuwa ni haki ya Kanisa kuelimisha wananchi
wake kila inapoona inafaa kufanya hivyo.

Alisema kiongozi yeyote anayetimiza wajibu wake hawezi kuwa na hofu juu ya mtu
mwingine kutoa elimu inayolenga kuwakomboa watu anaowaongoza na kusisitiza kuwa
Kanisa hilo lina nia njema na halina ugomvi wowote na Serikali wala chama chochote
isipokuwa linatimiza wajibu wake wa kuelimisha wananchi kuhusu elimu ya uraia.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya madhehebu kuweka wazi nia ya kutoa waraka kama huo
alisema “Ni haki yao, tena wamechelewa kufanya hivyo, nawashauri watoe na waelimishe waumini wao,”alisema.

Naye Reuben Kagaruki kutoka Dar es Salaam anaripoti kuwa Padre wa Kanisa Katoliki, Shirika la Wamisionari wa Afrika, Baptiste Mapunda, amesema watu wanaopinga waraka huo wanachezea amani ya Tanzania na wanataka kuendelea kubaki madarakani mileleni.

Amewataka watu hao kutambua kuwa viongozi wa dini, hawakuchaguliwa kwa vidole, bali ni wateule wa Mungu.

Akizungumza kwenye ofisi za gazeti hili, Dar es Salaam jana, Padre Mapunda alisisitiza; "Waraka unapotoshwa na kuchezewa na watu wanaojihisi mafisadi, wanafanya hivyo kwa kuogopa mabadiliko.

Alisema wao (Wakatoliki) hawatarudi nyuma kwa kuacha kumtii Mungu na kuanza kufuata matakwa ya watu, kwa kuwa waraka huo haulengi kuvuruga amani.

"Hata kama mtu hana Mungu ndani yake, basi aupitie kwa akili za kibinadamu ataelewa kilichoandikwa," alisema Padre Mapunda na kuongeza;

"Wanaoupinga hawataki Watanzania wajue elimu ya uraia, ili waendelee kubaki madarakani."

Aliendelea kusisitiza kuwa; "Kinachonitisha ni kuona baadhi ya viongozi wanag'ang'ania watu waishi kwenye giza, najiuliza hawa ni viongozi wa aina gani? Hii siyo alama ya demokrasia, bali ndani yake kuna chembechembe za udikteta."

Padre Mapunda alisema wakati umefika sasa wa viongozi, kuongozwa na elimu na siyo uzoefu. "Watu wanafanyakazi kwa mazoea ndiyo maana hatuendelei!" alilalamika Padre Mapunda.

Aliongeza kuwa kama waraka huo, ungekuwa na matatizo watu wa kwanza kuulalamikia wangekuwa wakatoliki, kwa kuwa wengi wamesoma na kuuelewa.

Alisema waraka huo ulipitishwa na maaskofu zaidi ya 30, hivyo kama ungekuwa unahatarisha amani ya nchi wasingeupitisha.

Padre Mapunda, alisema Serikali imekuwa ikiziomba taasisi za dini kusaidia kujenga maadili ndani ya jamii, lakini inashangaza kuona inageuka na kuanza kuona viongozi wa dini kama maadui.

Alisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kitatawala milele. "Kama kuna watu wenye mawazo hayo wanajidanganya kwani anayetawala milele ni Mungu," alisema na kuongeza;

"Ni lazima utafika wakati watu watachoka na huo, ndiyo utakuwa mwisho wa mfumo mzima." Alisema wanaopinga waraka huo hawataki mawazo mapya.

Pia Padre huyo alikemea tabia ambayo imeanza kushamiri ambapo watoto wa vigogo wamekuwa wakijiingiza kwenye siasa kwa kufuata nyayo za wazazi wao.

"Mbegu hii ni chafu, hakuna sababu ya kila mtoto wa kiongozi kuwa mwanasiasa," alisema na kushauri uigwe mfano wa watoto wa Baba wa Taifa Marehemu Julius Nyerere, ambao hawakufuata nyayo za baba yao.
Nendeni huko German kuna chama cha kidini(Christian Party),hapa Tanzania tuna Chadema,Cuf,CCM,TLP,UDP na vingine ambavyo sio vya kidini.Anayetaka waraka safari ya kwenda German imewadia.Acheni kuchefua nchi na ndio maana JKN alisema kamwe usimpe mbwa kilicho kitakatifu!
 
Date::7/21/2009Waraka wa Katoliki wamkuna Lipumba
broken-heart.jpg
*UNDP NAYO YAUUNGA MKONO

Na Elias Msuya

MWENYEKITI wa CUF, Ibrahim Lipumba ameunga mkono waraka uliotolewa na Kanisa Katoliki, unaohusu Uchaguzi Mkuu ujao kwa sababu unaeleza sifa zinazompasa mtu kuongoza taifa, lakini akapinga baadhi ya vipengele kwenye mwongozo huo akidai kuwa vinapingana na utaratibu wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Akitoa maoni yake kuhusu mwongozo huo muda mfupi baada ya kufungua warsha kuhusu mikakati na mbinu za kuongeza uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi serikalini iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Lipumba alisema ameona mambo makuu mawili kwenye mwongozo huo.

Alisema kwanza umejadili vizuri mambo ambayo serikali inapaswa kuyarekebisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Alisema kwamba, ni waraka mzuri ambao umetoa mwongozo kwa serikali kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kwamba hata vyama vya siasa vinaweza kuuingiza kwenye ilani zao.

“Serikali inapaswa kurekebisha mambo kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010. Ni mambo ambayo hata vyama vya siasa vinaweza kuyaingiza kwenye ilani zao," alisema.

Lakini pia, kiongozi huyo wa CUF alisema waraka huo umejiingiza kujadili mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Alidai kwamba suala la waraka kujadili kwamba taasisi za dini zisihusishwe katika kuendesha serikali ndilo analotofautiana nalo.

“Kama umeusoma waraka huo katika ukurasa wa tisa, wamezungumzia kutofautisha serikali na taasisi za dini na wamezitaja kabisa kuwa ni Mahakama ya Kadhi na OIC. Sasa hapo utaona kwamba kuna hali ya kutoeleweka kwa waraka huo,” alisema.

Nao Boniface Meena na Beatus Kagashe wanaripoti kuwa, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), limeunga mkono mwongozo huo wa Kanisa Katoliki likisema kuwa ni mzuri na ni muhimu kusambazwa ili watu wapate elimu iliyomo ndani yake.

Pia UNDP imeeleza kuwa ni hatari elimu hiyo isipotolewa kwa kuwa wananchi wanaihitaji.

Shirika hilo limesema linaandaa mchakato ambao utashirikisha taasisi za kijamii katika kutoa elimu kwa jamii kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kaimu Mkurugenzi mkazi (Mipango) wa UNDP, Louse Chamberlain alisema kuwa, mjadala unaoendelea hivi sasa nchini ni mzuri kwani unasaidia kujua ni jinsi gani elimu imewafikia wapigakura, viongozi na jamii kwa ujumla.

"Mjadala unaondelea ni mzuri kwa nchi ambayo demokrasia inakua; watu wanatoa maoni jinsi gani ya kuifikia jamii kwa urahisi," alisema.

Alisema kuwa, hivi sasa wanafanya mazungumzo na serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini na taasisi za kijamii kuangalia ni jinsi gani elimu ya uchaguzi inaweza ikatolewa kwa wananchi.

Chamberlain alisema UNDP itahitaji michakato kutoka taasisi za kijamii ambazo zina uwezo wa kutoa elimu hiyo, ili zipitiwe na kupatiwa fedha kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.

"Muda utakapofika, tutahitaji michakato hiyo na itakuwa wazi na maelezo yatatolewa ili kuchagua zile taasisi zitakazokuwa na uwezo ziweze kupatiwa fedha," alisema.

Aliongeza kuwa taasisi zitatakiwa kuwa bunifu katika kutafuta mbinu za kufikisha ujumbe kwa watu wengi ili waweze kutumia kura kama silaha zao.

Chamberlain alisema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005 taasisi 34 za kijamii zilipewa kiasi cha dola 1.9 milioni za Kimarekani kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii nchini kote.

Alisema kati ya taasisi hizo, tatu zilikuwa ni za dini ambazo ni Kamati ya Kikristo ya Huduma kwa Jamii ambayo ilipewa Sh 275.4 milioni kutoa elimu kwa kila wilaya hapa nchini, Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) ambalo lilipewa Sh 172.6 milioni kwa ajili ya kutoa elimu kwa wilaya 16. Taasisi nyingine ni World Conference on Religions for Peace (WCRP).

Naye Nora Damian anaripoti kuwa, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, amesema anaunga mkono waraka huo kwa sababu unaeleza sifa zinazompasa mtu kuongoza taifa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mtikila alisema uamuzi wa Kanisa Katoliki kutoa waraka huo ni ushindi mkubwa kwani utasaidia jamii kuelewa kwa mapana kuhusu chaguzi mbalimbali, hasa Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge.

Alisema wanaopinga waraka huo hawana nia njema na kwamba wana lengo la kuendelea kulea mafisadi, huku akimwelezea mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ambaye alitaka kanisa lifute waraka huo, kuwa anazeeka vibaya.

“Kingunge anazeeka vibaya; madhehebu mbalimbali yameuunga mkono waraka ule kwa sababu unaeleza sifa zipi zinazompasa mtu kuongoza. Je, haya ni mambo mabaya?” alihoji Mtikila.
“Nangojea makanisa mengine yatoe miongozo yao halafu mimi nitafanya majumuisho na nitatoa elimu kwa watu wote kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao,” alisisitiza.
Tuma maoni kwa Mhariri
​
 
Date::7/21/2009Rais wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki azungumza kuhusu waraka
askofurwaichi.jpg
Mhashamu Thaddaeus Ruwa'ichi, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC).
broken-heart.jpg
Na Frederick Katulanda, Dodoma

RAIS wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Mhashamu Thaddaeus Ruwa'ichi amesema wanaoujadili waraka wa kanisa lake bila ya kuusoma, ni maskini wa mawazo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Holly Cross mjini hapa, Mhashamu Ruwai’chi ambaye pia ni askofu wa Dodoma, alisema mgawanyiko na mawaidha yanayotolewa na watu mbalimbali, wakiwemo wanasiasa unadokeza wazi kabisa kwamba, wapo wanaoijadili ilani (waraka) hiyo bila ya kujua yaliyomo ndani yake.

“Hali hii inasababisha upotoshaji, kukanganya watu na hata kuzusha hisia za chuki katika jamii. Huu si uwajibikaji na katika hali hii napenda kuwashauri Watanzania kuwa wawe watu wenye kutafuta ukweli na kujenga kauli za hoja juu ya msingi huo na ukweli na uelewa sahihi,” alieleza.

Alisema ilani hiyo ni sehemu ya harakati zinazotudai sisi sote kuchangia kujenga uzalendo kwa njia ya elimu ya uraia na kwa sababu uelewa na uzalendo ni mhimili ya uwajibikaji.

”Ieleweke kwamba, Ilani hii ni mafundisho yanayohusu jamii, inabainisha changamoto, fursa, vipaumbele na matatizo yanayoihusu jamii na taifa letu katika zama hizi za leo," alisema.

"Kwa kutoa Ilani hii, Kanisa Katoliki linatafuta kwa nia njema kabisa kuwasaidia raia wa nchi hii bila ya ubaguzi; kujizatiti kutambua na kushughulikia masilahi ya wote siyo tu kwa kuzingatia uleo, bali pia kwa namna inayoihakikishia raia wote nchi hii amani, haki, mshikamano, uwajibikaji na maendeleo yaliyo endelevu.”

Askofu huyo alisema kuwa, kutafsiriwa kwa Ilani hiyo ya kanisa lake kuwa ni sehemu ya kigezo cha zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka huu na uchaguzi wa bunge na rais mwakani ni jambo ambalo linahitaji kuwekwa sawa kwa vile ilani hiyo haifundishi wananchi kuchamgua fulani na kumkataa fulani, bali inabainisha vipaumbele na changamoto.

"Ni muhimu kuzielewa changamoto na vipaumbele na kuzipata kila mmoja kwa uzito unaostahili kwa lengo la kushughulikia maendeleo yetu kwa dhati. Uelewa huo utatuwajibisha tuamue ni nani mwenye uwezo wa kushirikiana nasi ili tujue tunapiga hatua mbele," alisema.

"Viongozi waliochaguliwa na watu wanapewa dhamana, hivyo wana wajibu wa kutambua masilahi ya wote badala ya kutumbukia katika mitego ya ubinafsi, ukabila, udini au ubaguzi wa aina yoyote.”

Akizungumzia mjadala wa sasa wa nchi kujiunga na OIC pamoja na suala la serikali kuanzisha Mahakama ya Kadhi, mkuu huyo wa Kanisa Katoliki alisema Tanzania ni nchi ambayo ina katiba na imekua na kujengeka kwa misingi ya katiba hiyo, hivyo viongozi wa serikali wanapaswa kuifuata badala ya kupendelea dini fulani.

"Nchi hii inao raia wenye dini ingawa serikali haina dini, tusipofuata katiba na kuingia katika kusaidia dini fulani tutaingia katika ukabila na udini na katika hili nawaalika watazame kwa undani chimbuko la migogoro ya Rwanda, Burundi na hata Congo,” alisema.

Akizungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar alisema kuwa, viongozi wanapaswa kuuheshimu na kuuthamini Muungano huo kwa vile ni taifa pekee lenye Muungamo ingawa kasoro zilizopo zinapaswa kuangaliwa kama changamoto.

Aidha, Askofu Ruwai’chi aliutambulisha waraka mpya mwingine wa kanisa hilo ambao ni "Hati Fundishi"’ uliotolewa na Baba Mtakatifu Benedicto XVI Julai 7, mwaka huu ujulikanao kwa jina Kilatini la Caritas in Veritate lenye maana ya "Upendo Katika Ukweli".

Alisema waraka huo mpya wa papa utajikita katika kufundisha juu ya masuala yanayohusu jamii na kwamba unatoa mafundisho kuhusu changamoto inayohusu maendeleo ya mwanadamu.
Hati hiyo fundishi imetolewa ikifuta hati nyingine mbili za Baba Mtakatifu Benedicto XIV ambazo ni "Mungu ni Upendo" iliyotolewa Desemba mwaka 2005 na "Wokovu kwa Njia ya Matumaini" iliyotolewa Novemba mwaka 2007.
Tuma maoni kwa Mhariri
​
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom