Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Ule waraka kwa waliousoma una mambo mengi. Hawa wanaoujadili nilitegemea wawe na huo waraka waseme ni sehemu gani yenye matatizo na inahitaji marekebisho. Kwa vyo vyote waraka mzima hauwezi kuwa na matatizo. Nafikiri tatizo ni ukatoliki na sio waraka kwa kuwa wote wanaoupinga hawajui hata rangi ya jalada lake.
Angalia ukurasa wa kumi wa waraka huo ndio utajua haswa kilichokusudiwa na kanisa katoliki.Wengi huwa mnaangalia ukurasa wa kwanza tuu chukueni waraka mzima mpate majibu na sio kukurupuka kulaumu watu eti tatizo ni katoliki.Najua wengi wenu mmesoma/mmeenda shule lakini hamkuelimika kwani kuna tofauti kubwa kati ya kusoma na kuelimika na ndio haswa panapokuja swala la kupambanua mambo mnaboronga na kukimbilia eti hamna 'roho mtakatifu'!Jamani elimikeni na sio kumaliza madarasa tuu!
 
Ebwana huyu jamaa makwaia, mimi huwa nashangaa sana pale anapojiita eti yeye ni senior journalist,sasa nashindwa kuelewa hivi ni nani ambaye amempa hicho cheo wakati hata hastaili,kwa sababu embu angalia katika vipindi vyake avyoendesha channel ten yaaani jamaa huwa hawezi kabisa kumsikiliza mtu pale anapokuwa anatoa hoja fulani yeye anataka kila mtu aongee kama yeye anavyofikiri ambapo si sahihi,kawida mwandishi anatakiwa awe objective yaani value free na sio kuwa value laden,kwa hiyo mimi huwa inanishangaza sana pale ninapomuona mwakwai a katika vipindi vyake utakuta mtu anachangia mada fulani lakini kabla hata hajamaliza utashangaa amemkatisha hii kwa kweli inasikitisha sana na inachukiza sana,alishawahi kunialika katika moja ya vipindi vyake nilikataa kuitikia wito wake kutokana na uendeshaji wake mbovu wa kipindi ,kwakweli nina wasiwazsi na taaluma yake huyu jamaa hivi amesomea kweli mambo ya journalism? au anataka apate sifa tu kutoka kwa watu,hivi kwanini asijifunze kwa wenzake kama akina Salum mwalim,David Ramadhan,Jenerali ulimwengu,Hamza kasongo,Rainfred masako,Steven chuwa,Marine Hassan marine,Adam sembeye Nk,yaani unapokuwa unaangalia vipindi vinavyoendeshwa na hawa jamaa unaona kabisa kwamba wanaweza na wanaviendesha kwa umakini kabisa na ufanisi wa hali ya juu sana,ambapo watu ambao wanakuwa wamealikwa wanapewa uhuru wa kusema yale yaliyokuwa muhimu nakuyaeleza kwa ufasaha sana bila ya hata kukatishwa katishwa. Wanjamii forum wenzangu embu tujitahidi huyu jamaa aweze kabadilika maana anaidhalilisha tasnia nzima ya undishi wa habari hapa nchini.
 
Huyu Makwaiya mimi huwa nafuatilia sana vipindi vyake, mara zote anapenda kuwalisha watu alionao katika kipindi chake maneno ya kusema, na inapotokea msemaji akatoa neno analolitaka basi yeye hulidaka na kulipigia mstari. Hapo ndipo watazamaji wengine tunaomwelewa tunapata picha mara moja lengo lake la kuanzisha huo mjadala.

Ila sasa naona anaelekea kubaya kuingia katika kundi la mafisadi wanaopinga wananchi wasielimishwe kuchagua watu wanaomjua Mungu watakaowatumikia badala ya kutumikia kundi dogo la mafisadi kwa ujira mdogo wenye kushibisha matumbo yao.
 
Mimi nilidhani niko peke yangu.Ni kweli Bwana Makwaia wa kuhenga aka Senior journalist kama anavyopenda kujiita ameshindwa kwa kiasi cha kusikitisha kuendesha kipindi chake "Je tutafika".Mara nyingi hampi nafasi mgeni kuchangia hoja hadi mwisho bila kumkatisha hata bila ya sababu za msingi.Kwa mfano utamsikia akimkatisha mchangiaji kwa kumwambia ebu rudia hapo pazuri/patamu,au watazamaji mmesikia fulani maneno mazito sana.

Bwana Makwaia anatatizo lingine kubwa mara nyingi kama si zote anachagua wageni bila kuzingatia uwakilishi [balanced]au kwa kujua msimamo wao kabla.Sikupata bahati ya kukitazama kipindi cha wiki hii lakini Bwana Makwaia alitakiwa kumwalika kiongozi wa kanisa katoliki ili kutoa fursa kwa mtazamaji kuweza kupata maoni tofauti lakini kwa maksudi Bwana Makwaia aliamua kumwalika Mzee wa upako kwa kujua hana elimu ya kutosha hata kuhusu imani yake.Mzee wa Upaka alikuwa mpiga debe mzuri wa uanzishwaji wa mahakama ya kadhi mara zote ukimsikiliza hana hoja ya msingi bali ushabiki tu.
 
Haya mkuu ni mawazo yako wewe.. hakuna mtu aliyepinga tu bila hoja.. hoja tumeziweka wazi labda wewe hufuatilii. tazama majibishano ya hoja baina yangu na Mzee Mwanakijiji.

Hata hivyo kwa kukufahamisha tu, hakuna mtu anayepinga wasomi wa Kikatoliki kukaa wakatunga kitu.. hii ni sifa ya elimu yao ktk uchaguzi na miiko ya Uongozi ikiwa ni pamoja na vita dhidi yaUfisadi. Lakini kosa/tatizo linakuja pale mapendekezo yao yanapitia TEC na kisha ati hao TEC wakutane na viongozi wa serikali kuwapa MWONGOZO wao..Halafu basi, tazama vifungu vya malengo ya hao TEC, dini imetumika zaidi ktk kuelezea vifungu vya haki ya wananchi badala ya kutumia elimu zao za darsa..

Mkuu wangu ukipata shahada yako Nyegezi unakubalika ktk nafasi yoyote ya kazi kulingana na elimu uloipata iwe hata kuandika waraka inayohusiana na kazi au elimu yako, lakini unapoitumia dini kuwa juu ya uwezo wako (elimu) ukawakilisha kazi za shirika (waraka) kanisani ikapate baraka hapo ndipo utata unapokuja..Kisha ati madaraka ya kanisa ndilo li deal na shirika.. huoni kama hapa wanachemsha mkuu.. Wahusika wa shirika itawalazimu waondoe hiyo elimu yako na waanze kufikiria uwezo wa Padri ktk maswala ya shirika hilo jambo ambalo haliwezekani.

Kuwa na sifa mbili sii tatizo hata kidogo, tatizo ni pale unapotaka kucheza NBA kwa kutaka watazamaji waitambue degree yako..U wanna play ball paly utasifiwa lakini sio kuingiza degree wakati mchezo huwezi kucheza hata kama rules unazijua..Kila sifa huenda mahala pake huu waraka umepotosha maana na taaluma ya waandalizi..
Kwa madai yenu mnasema ni hulka ya Kanisa Katoliki kutoa mwongozo kila unapokaribia Uchaguzi.. jamani sisi hatutaki, kama mlizoea mchezo huo basi UFE! huko nje fanyeni huko huko iwe Zimbabwe au Italia, kwetu hatutaki - ufe!

Mhe. Mkandara, mie huwa naheshimu na kuyapenda maandiko yako 'yaliyokwenda shule' lakini wakati mwingine unaji-expose kwamba wewe ni Muislam kwa namna ambayo Makwaia wa Kuhenga naye hufanya hivyo hivyo yanapojitokeza masuala yanayogusa dini.

Waraka wa Wakatoliki sidhani kwamba unakiuka ama unavunja sheria yoyote ya nchi. Wenzetu hawa nadhani wametumia tu uhuru wao wa kueleza hisia, mtazamo ama labda maono yao. Tunaruhusiwa kupinga ama kuunga mkono lakini sidhani kwamba tunapaswa kulaani.

Umekwenda mbali kidogo Mkuu kwa kusema kwamba "UFE na 'sisi' hatutaki" Sisi akina nani?
 
Huyo anajiita mzee wa "upako" ukimchunguza sana utagundua analo tatizo, mimi nina wasiwasi kama hiyo mtu ameenda shule na akaelimika, kanisa la Katoliki kila mwenye akili timamu anajua kwamba lina wasomi wanataaluma katika nyanja zote anazozifahamu bwana Lusekelo na huyo Makwaia ambao ndiyo waliotengeneza huo waraka, sina uhakika kama jina linalowafaa ni kuitwa "kundi la watu wanaowasababishia kichefuchefu watanzania!" Mimi najiuliza huyu Lusekelo kwa lugha hiyo, anafaa kuwa mchunga Kondoo wa Mungu? au ndo anataka kututhibitishia minong'ong'o inayoenea kuwa naye ni mmoja wa mafisadi waliojificha katika dini, maana hukusanya fedha za watu waliokata tamaa ya maisha kwa lugha ya kuwapatia upako kwa viwango tofauti kulingana na pesa wanazotoa.
 
Lipumba yuko sahihi kwa upande wake. nilitegemea hata Waislam wanaoupinga wapinge baadhi ya vipengele kama viko ambavyo hawakubaliani nanvyo ila sio waraka wote.

Kimsingi mimi nilipousoma niliamini hicho kipengele cha kupinga mahakama ya kadhi na OIC kuwamo kwenye serikali ndio tofauti kubwa ambayo Waislam hawawezi kuipenda. Ila kiujumla lazima tukubali waraka ujadiliwe na ni mzuri.
 
Kilichotokea jana ilikuwa niaibu tupu
Ukweli ni kuwa makwaia anatakiwa kubadilika katika uendeshaji wa kipindi chake,na kama hana washauri inabidi atafute lasivyo kama anapewa ushauri hapokei basi anaelekea kubaya.
Najua mzee wa upako umaarufu umeshashuka vya kutosha kabisa iliyopo tumsamehe bure
 
Sidhani kama kuna mapya sana katika ukimwengu wa dini. Yote ni yale yale kila siku. Kuna haja ya kuitazama Afrika katika mtindo wa harakati za kiuchumi na maendeleo.
 
Niliwahi kusema jambo hili katika moja ya posts zangu kuhusu huyu bwana Lusekelo kwamba shida yake ni elimu tu.
We msikilize muda wote anapozungumza. Utagundua shida yake ni elimu.
Angelikuwa na elimu angelikuwa more constructive kwenye mambo anasema. Lakini sasa anajisemea tu kumbe maskini..........
Siwezi kusema mengi kwa ajili yake zaidi ya hili.

Mchukia Fisadi

Pole nadhani hukuelewa vizuri; Lusekelo anayesemwa hapa sio yule unayemdhani kwani anaongelewa Mchungaji wa Upako Lusekelo wa Liver side ubungo sio Adam Lusekelo wa Daily News kwa jinsi nilivyokuelewa. Muombe samahani basi!!!!

Turudi kwenye mada; hiki kipindi sijakiona ila kwenye vipindi kama hivi kwangu mimi mtu ambaye anajua kuviendesha ni Steven Chuwa wa ITV kwani yeye hapindishi na anastahili sifa sana. Ni vizuri kama unaendesha vipindi kama hivi uwe na wadau wote washiriki na wachangie, huyu basi alikuwa na malengo yake si mnajua ----------

Pili ukimchunguza huyo mzee wa Upako sasa hivi waumini wamemuhama na hakupaswa kuongelea yeye bali Wakatoliki ndo wangeshiriki kwani umetokea kwao lakini sio mbaya kila mtu anauhuru wa Kuchangia ila aje na hoja isiwe kama Kingunge yeye anapinga tuu haelezei ni wapi kunahitilafu!
 
Makwaia wa Kuhenga, katika hicho kipindi chake ambacho nikiri sijakiona, kama angeunga mkono huo waraka isingekuwa mada. Suala ukipinga Waraka ndio inakuwa mada. Spika na Lipumba wameunga mkono, hapo wote furaha, Kingunge na walioutolea tahadhari wanaonekana wabaya.

Hili ni suala la muda, kama kuchanganya Dini na Siasa sasa sawa, tusubiri baadae msije piga kelele. Huu Waraka ni muhimu kwa kumbukumbu, na hauko huu tu, ziko Nyarakanyingine. Kuna wengine walipojaribu kuzungumzia Siasa waliambiwa wanachanganya Dini na Siasa. Kwa Waislam kuonekana kuchanganya dini na siasa na Serikali ni jambo la kawaida. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu na huu Waraka Serikali kamam vile imelala. Ndio tunazidi tambua kuna nini Tanzania. Heko Kanisa Katoliki.
 
Tatizo waraka umetolewa na wakatoriki huu waraka ungetolewa na Anglikana watu wote mngekuwa kimyaaa kweli vikanisa vya kilokole vina bifu zoto la chini chini na Katoriki lakini Wakatoriki wana waignore tu ndo maana wanasumbuka sana na dhamira inawasuta.
 
Haya mkuu ni mawazo yako wewe.. hakuna mtu aliyepinga tu bila hoja.. hoja tumeziweka wazi labda wewe hufuatilii. tazama majibishano ya hoja baina yangu na Mzee Mwanakijiji.

Hata hivyo kwa kukufahamisha tu, hakuna mtu anayepinga wasomi wa Kikatoliki kukaa wakatunga kitu.. hii ni sifa ya elimu yao ktk uchaguzi na miiko ya Uongozi ikiwa ni pamoja na vita dhidi yaUfisadi. Lakini kosa/tatizo linakuja pale mapendekezo yao yanapitia TEC na kisha ati hao TEC wakutane na viongozi wa serikali kuwapa MWONGOZO wao..Halafu basi, tazama vifungu vya malengo ya hao TEC, dini imetumika zaidi ktk kuelezea vifungu vya haki ya wananchi badala ya kutumia elimu zao za darsa..

Mkuu wangu ukipata shahada yako Nyegezi unakubalika ktk nafasi yoyote ya kazi kulingana na elimu uloipata iwe hata kuandika waraka inayohusiana na kazi au elimu yako, lakini unapoitumia dini kuwa juu ya uwezo wako (elimu) ukawakilisha kazi za shirika (waraka) kanisani ikapate baraka hapo ndipo utata unapokuja..Kisha ati madaraka ya kanisa ndilo li deal na shirika.. huoni kama hapa wanachemsha mkuu.. Wahusika wa shirika itawalazimu waondoe hiyo elimu yako na waanze kufikiria uwezo wa Padri ktk maswala ya shirika hilo jambo ambalo haliwezekani.

Kuwa na sifa mbili sii tatizo hata kidogo, tatizo ni pale unapotaka kucheza NBA kwa kutaka watazamaji waitambue degree yako..U wanna play ball paly utasifiwa lakini sio kuingiza degree wakati mchezo huwezi kucheza hata kama rules unazijua..Kila sifa huenda mahala pake huu waraka umepotosha maana na taaluma ya waandalizi..
Kwa madai yenu mnasema ni hulka ya Kanisa Katoliki kutoa mwongozo kila unapokaribia Uchaguzi.. jamani sisi hatutaki, kama mlizoea mchezo huo basi UFE! huko nje fanyeni huko huko iwe Zimbabwe au Italia, kwetu hatutaki - ufe!
Mkuu Mkandara kwanza nashukuru kwamba "...hakuna mtu anayepinga wasomi wa Kikatoliki kukaa wakatunga kitu.. hii ni sifa ya elimu yao ktk uchaguzi na miiko ya Uongozi ikiwa ni pamoja na vita dhidi yaUfisadi" (Very good hii ina maana hata wewe hupingi). Umesema tatizo nadhani sio tatizo ila hofu yako ni utaratibu uliotumika kuwasilisha mawazo yao serikalini. Jibu lake ni rahisi tu kwamba ni masuala ya itifaki tu. Nakuomba usitishike na vifungu vya dini kutumika kuelezea haki za wananchi. Naamini hakuna haki isipokuwa kwa hofu ya Mungu, vinginevyo ni usanii mtupu. Msingi wa kutenda haki ni utu, na maadili ya ki-utu ni neema ya Mungu. Hivyo basi, kwa kuwa watumishi wa mungu, mbali na elimu dunia wana elimu ya dini ni haki yao kutumia taaluma zote walizonazo ili mradi nia ya ni kusisitiza somo lao na kulifanya lieleweke vizuri zaidi. Na kwa sababu hii pengine ingekuwa bora zaidi kama na wasomi wa dini zingine wangeunga mkono jitihada hizi. Watumishi wa Mungu ni sehemu ya jamii, wana mahitaji ya msingi sawa na binadamu wengine. Ni haki na wajibu wao kutoa michango yao kwa namna yoyote iwayo ili mradi ni kwa manufaa na ustawi wa nchi yao. Kwa kuwa wao si malaika mawazo yao hayawezi kuwa sahihi kwa asilimia mia moja. Wajibu wetu ni kuangalia ni mapungufu na kusaidia namna ya kuboresha. Kuendelea kubeza ni kutowatendeea haki wahusika. (Kauli yako ya kwanza inaonyesha hubezi japo umemalizia kwa kubeza) . Jamani mimi (nimejitoa kwenye "sisi" yako kama ulinijumuisha) nataka kazi hii nzuri na wala sio mchezo kama unavyotaka kutupotosha iendelee na ikiwezekana na wataalam wa dini nyingine waunge mkono jitihada hizi.
 
Niliwahi kusema jambo hili katika moja ya posts zangu kuhusu huyu bwana Lusekelo kwamba shida yake ni elimu tu.
We msikilize muda wote anapozungumza. Utagundua shida yake ni elimu.
Angelikuwa na elimu angelikuwa more constructive kwenye mambo anasema. Lakini sasa anajisemea tu kumbe maskini..........
Siwezi kusema mengi kwa ajili yake zaidi ya hili.

Mimi naungana na wewe tatizo lake Mzee wa Upako ni elimu ndogo na kwa sababu hiyo upeo wake wa kuchambua mambo ni mdogo pia,asamehewe bure kwa kua hajui asemalo.
 
Mi nadhani MAKWAIA anatakiwa kuaviod biasness,asionekane amejikita sana upande wa islam maana ajue kipindi chake is not for islams only even christians.Na lengo ni kujenga siyo kubomoa ayupo pale kidini bali kijamii na kutransfer knowledge ktk jamii. Lakini pia naona ni wakati wa Viongozi wa madhehebu ya KATORIKI kujitokeza watoe briefly wa walaka wao ili waweze kuu convince UMMA.Halafu viongozi wetu wa serikali wasipende kupinga vitu bila sababu za msingi,watakiwa kumention out reason why they reject.Hapo ndipo tutajenga future yaTANZANIA.
 
Tatizo waraka umetolewa na wakatoriki huu waraka ungetolewa na Anglikana watu wote mngekuwa kimyaaa kweli vikanisa vya kilokole vina bifu zoto la chini chini na Katoriki lakini Wakatoriki wana waignore tu ndo maana wanasumbuka sana na dhamira inawasuta.
jamani acheni hizo, rejea waraka wa Msemaji wa Pentecost jana, David Mwasota, Pentecost kama wakristo tunaamini ktk umoja na si kukosoana.
Pili waraka umelenga kuelimisha jamii kuhusu viongozi wasiofaa na sifa za wanaofaa. Ndo unataka kutwambia walokole tunapendelea mafisadi.
Nilishasema kiongozi kama kiongozi ni binadamu na taswira ya anaowaongoza, Mzee wa upako akisema ni kwa niaba ya huduma yake, na Msemaji wa Makanisa ya Pentecost ni David Mwasota ambaye katoa kauli jana.
Inatupasa kupinga hoja zilizomo na si udini ktk huo waraka, mtoa hoja mwenyewe amepingana na muandaaji kwa kuchagua wahusika wanaopinga tu badala ya pande zote mbili. Ndo kinachojadiliwa hapa.
 
Mama Joe tatizo hapa ni huyo mzee wa Upako umesikia hapo juu yaani ana chuki zake na Wakatoriki nae aandae wa kwake.
 
Nchi inapokosa uongozi thabiti (wa kisiasa) na dira, ombwe hilo huzibwa na imani ya kidini kama dira mpya. Na kwa kuwa tuna dini na madhehebu mengi, matokeo yake ni mkanganyiko na hisia za kutoamini "dira" za wengine.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom