Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Asante silencer. Kuna watu wamejisahau sana na kuwa extremist hapa badala ya kuleta hoja. Wanashinda hapa, wanalala hapa, lakini hoja hakuna maana wanarudia zile zile tu. Matusi kama vile wao kwao ni fahari. Wanatamani kujilipua humu jf.
 
several members who have been in this thread have been banned for 3 days beginning today. If people can not monitor themselves it'll be our pleasure to do that for them.

For Admins.
aaah silencer ban zake za kikatoliki......Painkiller angetoa mwezi.....nashukuru kwa tumaini kula ban......
 
Mimi nadhani kanisa katoliki wamefanya kile ambacho kanisa lilijisahau kulifanya kwa miaka mingi.
Leo Matokeo mabaya ya ufisadi na rushwa katika nchi hii ambayo yanatokana na washirika wa kanisa hayakuwahi kufanyiwa kazi ingawa watu hawa wamekuwa miongoni mwa washirika wa dini.
Hapakuwa na kukemewa kwa washirika waovu.
Hawakutengwa, bali kukumbatiwa na kusifiwa na leo nchi iko njia panda kwenye mgawanyiko mkubwa.
Kila uendako. Hadithi na mijadala ni kama unavyoona hapa JF.
Natamani na makanisa mengine ya kikristo yachukue the same trend. Washirika mpaka vijijini huko wajue, adui yao ni nani! wajue kabisa wasichague waleta pesa na vikanga. Wala wasichague waleta kofia na tshirt bali wachague mtu wanayedhani ataleta maendeleo hata kama anatoka kati yao.
Kumekuwa na kasumba siku hizi kwamba huyu ni msomi wa degree 10. Huyu ana pesa wewe acha tu, huyu ni mfanya biashara mkubwa n.k. Hii haitatuondoa kwenye shida maana hawa ndio wabaya zaidi ya wasiokwenda shule. Hawa wenye pesa ndio usiseme maana wao kwao pesa yao ni mtaji wa kupata mara mia mbili zaidi ya zile mnazoziona. Ole wao wanaotoa kura kwa kulambishwa utamu uliowekwa juu ya uchungu mtaishi kwa uchungu ule ule.
Thanx Pengo na kampuni yako. Thanx again.
Let God bless you.
 
Hahahaaaa!!!!!

Huyu Tumaini anajaribu kuongeza posting zake haraka haraka ili atafute jina humu!!!!!

Hahahaaaa!!!!!
Jamaa yupo hapa day and night yuko kwenye paylist ya wajamaa nini?🙂😀
Kula na kula saa ngapi? kufanya kazi nyingine saa ngapi?
I am worried. Ngoja apumzike kidogo. Apate Vakesheni.
Yo yo muelekeze ulikokuwa umekwenda vakesheni wewe ili akainjoi pia😀
 
Mpinge mwezio kwa Hoja Makini...Maswali yako ungemuhoji Mwanakijiji...kufikisha post yake yote....au member mwingine !!!! Unapomwambia mwenzako comments hizo the same na kwako!!!!

Kama kurekebisha matusi nafikiri wote tuwe na jukumu la kuwe Lugha zetu sawa. Isiwe akifanya Fulani ndio achukuliwe hatua...Unapoamsha ARI ya mtu, basi tegemea reaction yake...

Tumekuwa tukilalamika kuhusu Mwanahalisi....kufungiwa na Serikali for what?...
 
Mimi nadhani kanisa katoliki wamefanya kile ambacho kanisa lilijisahau kulifanya kwa miaka mingi.
Leo Matokeo mabaya ya ufisadi na rushwa katika nchi hii ambayo yanatokana na washirika wa kanisa hayakuwahi kufanyiwa kazi ingawa watu hawa wamekuwa miongoni mwa washirika wa dini.
Hapakuwa na kukemewa kwa washirika waovu.
Hawakutengwa, bali kukumbatiwa na kusifiwa na leo nchi iko njia panda kwenye mgawanyiko mkubwa.
Kila uendako. Hadithi na mijadala ni kama unavyoona hapa JF.
Natamani na makanisa mengine ya kikristo yachukue the same trend. Washirika mpaka vijijini huko wajue, adui yao ni nani! wajue kabisa wasichague waleta pesa na vikanga. Wala wasichague waleta kofia na tshirt bali wachague mtu wanayedhani ataleta maendeleo hata kama anatoka kati yao.
Kumekuwa na kasumba siku hizi kwamba huyu ni msomi wa degree 10. Huyu ana pesa wewe acha tu, huyu ni mfanya biashara mkubwa n.k. Hii haitatuondoa kwenye shida maana hawa ndio wabaya zaidi ya wasiokwenda shule. Hawa wenye pesa ndio usiseme maana wao kwao pesa yao ni mtaji wa kupata mara mia mbili zaidi ya zile mnazoziona. Ole wao wanaotoa kura kwa kulambishwa utamu uliowekwa juu ya uchungu mtaishi kwa uchungu ule ule.
Thanx Pengo na kampuni yako. Thanx again.
Let God bless you.

Mwambie Pengo aanzishe Chama cha SIASA...Ule wimbo wa Kutochanganya DINI na SIASA siku hizi haupo tena au...?
 
several members who have been in this thread have been banned for 3 days beginning today. If people can not monitor themselves it'll be our pleasure to do that for them.

For Admins.

Silencer pls show me one or post ya kufanya kumfungia Tumaini?...
 
Mkuu unaonekana kuogopa Ukatoliki na wakatoliki Tanzania .Hujaona hata akina Obama lazima wafike pale Vatican ? Hata JK alifika pale na akapeleka zawadi mwenyewe hakuitwa na sasa wewe unalia lia .Huu ni upepo mkali sana umesha anza na hakuna wa kuusimamisha .Unajua shida moja ndugu wa kofia si wote lakini wengi wenu hata mkisoma bado mna kasumba za kiarabu tu na mnaondoa maana ya shue yenu,mfano wewe mwenyewe umejiita msomi wa ndani na nje .Umesoma kwa kizungu na nje hujasoma Iran wala Saudia ni Ulaya lakini kwa matusi kwenye hii forum na sisi wazee kunyamaza si haki .Usomi wako uko wapi ndugu matumaini ? Jenga hoja tuone tutakufuata na kukuunga mkono kabisa .Sisi hatuogopi upepo wa kadhi wala nini shida ni kwamba management ni poor na hamna pesa ya kuendesha mahakama hizo na hatutaki kodi yetu itumike kuwasaidia .
..Bro Lunyungu.... "Abdulhalim..". uliemnukuu... Hujamuelewa....labda usome vema posts zake....kiufupi anakuunga mkono tu...!!!
 
Soma thread hii yote utapata jibu!
Nimesoma ndio maana nikaomba Silencer atoe post iliyofanya aende ktk conclusion....Labda kazifuta...!!! Nilizopo siioni...Tumain katoa Angalizo tu muhimu...kitendo cha Kumfungia hakikuwa Right at ALL...

Mie nataka atoe comments/mchango anaona mbaya wa Tumaini...then tutanukuu comments za wengine!!!

Please tuweni wakweli...na Tujifunze Kuvumiliana na kuheshimiana
 
Mi nashangaa ni member wengi wakifungiwa hawaishi kulalamika au wanaingia watu kulalamika kwa ajili yao kwamba wameonewa wakati hata mimi ningekuwa mod ningewafungia maisha.
Nilitegemea watu wawe wanawaombea msamaha na au wao wenyewe wakirudi waje wakiomba msamaha, lakini wapi lawama weeeeeeeeee juu ya mods tu bila sababu. Kweli hapa unategemea hawa hawa ndio wanataka tuwape mitaa kata na bunge kweli 2010?
Nakumbuka kukaa kwangu kwote JF nimeona mtu mmoja tu ambaye ali regret kufungiwa kwake na akaja na thread ya kuomba asamehewe kwa sababu jambo hilo lilitokea kwa bahati mbaya alipotoa password yake kwa rafiki ili ainjoi JF.
Otherwise wengine ni kulalamika tu wakati kukosa wamekosa. Sana sana utasikia mtu akilalamika kuwa nilitukanwa. Kwani kutukanwa kuna halarisha matusi toka kwa memba mwingine?

Silencer do your work please. Mi naona umefanya kazi yako kwa halali kabisa. Hata hivyo ulikuwa na uvumilivu vinginevyo ungewafungia wengine siku 3 zilizopita! Tena😀 umetoa kifungo kidogo sawa na kifungo cha nje
 
Mbona hujahoji kuhusu Abdulhalim kufungiwa vile vile?

Kutoka kwa wakatoliki hatuna cha kujifunza ila uwizi, ufisadi na unafiki (kujificha kwenye nyasi hila) so huko hatuwezi kufika sisi waungwana

bado una mawazo kwamba kila mwenye jina la Juma ni muislamu na mwenye jina la John ni mkristo "so ignorant wake up" jina siyo dini....

Mwache ale ban hakuna atakayemiss posts zake.
 
Mbona hujahoji kuhusu Abdulhalim kufungiwa vile vile?

Mwache ale ban hakuna atakayemiss posts zake.

Mdanganywa naye kapigwa stop au nini? Nilisoma post zake kama mbili lakini ghafla bin vuu sizioni!
 
Mpinge mwezio kwa Hoja Makini...Maswali yako ungemuhoji Mwanakijiji...kufikisha post yake yote....au member mwingine !!!! Unapomwambia mwenzako comments hizo the same na kwako!!!!

hukuweza kujizuia eh? it is unhealthy infatuation.
 
Kanyaga Twende However unayetaka kuwaelimisha wananchi juu ya Elimu ya Uraia maana hata hapa JF wengi tunaimiss hii Elimu thats why tumekuwa na majibu yaleyele kwa hoja Tofauti.

Kanyaga Twende kanisa, Kanyaga Twende Misikti, Kanyaga Twende NGOs, Kanyaga twende however
 
NOTE: Waraka anaoushutumu Kingunge unapatikana HAPA

MBUNGE wa kuteuliwa na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ameushambulia waraka wa kichungaji uliotolewa na Kanisa Katoliki nchini, unaoelekeza namna ya kupata kiongozi anayefaa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu ujao adai kuwa utaligawa Taifa.

Kingunge alitoa kauli hiyo alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, ambayo iliwasilishwa na George Mkuchika bungeni mjini Dodoma jana.

Hata hivyo, Kanisa Katoliki kupitia Baraza lake la Maaskofu (TEC), limekuwa na utamaduni wa kutoa mwongozo kama huo wakati Taifa linapoelekea Uchaguzi Mkuu, huku kumbukumbu zikionyesha kuwa pia lilifanya hivyo mwaka 2005.

Katika kikao hicho cha jana kilichokuwa chini ya Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama aliyekuwa mwenyekiti, Kingunge alizungumza kwa msistizo huku akiwataka wabunge wamsikilize kwa makini na kutahadharisha kwamba asinukuliwe vibaya.

``Na sasa nimalize, nina jambo moja kubwa, naomba mnisikilize kwa makini, lakini msininukuu vibaya. Kanisa Katoliki, viongozi wake rafiki zangu, wale wa juu nawafahamu sana, Kanisa hilo limetoa mwongozo kuelekeza anayefaa kuchaguliwa katika uchaguzi ujao.

“Mimi nikautafuta na kuusoma. Sasa hili Kanisa Katoliki linatoa mwongozo wa kuchagua kiongozi wa kisiasa, kwa maana hiyo huu ni mwongozo wa Wakatoliki. Si utakuwa mwongozo wa Wakatoliki pekee?” alisema Kingunge akihoji.

Aliendelea kusema: “Kwa hiyo KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) nao watoe mwongozo kwa sababu wao hawaongozwi na Kanisa Katoliki, ni Wakristo ndiyo, lakini mantiki tu. KKKT wakitoa, Pentekoste watatoa wakwao na Anglikana bado, nao watatoa wakwao, Waislamu bado na wao watoe wa kwao.”

Kingunge ambaye ni mmoja wa wabunge wa muda mrefu ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu enzi za Mwalimu Nyerere Rais wa Kwanza wa Tanzania aliongeza kuwa anazungumza hayo kwa kuzingatia mantiki ya mwongozo huo.

“Ni mantiki tu, nasema kwa heshima zote nawaomba viongozi wa Kanisa Katoliki, nawapenda sana, nawaomba warudishe ule mwongozo wao, sisi tunataka nchi moja na tuishi pamoja kwa kushikamana, hatutaki kugawanyika kama Lebanon,” alisema Kingunge bila kufafanua zaidi kuwa waurudishe wapi na kwa vipi.

Kauli hiyo ya Kingunge imetolewa wakati waraka huo wa Kanisa Katoliki umezua mjadala miongoni mwa watu wa kada mbalimbali, huku baadhi wakilishutumu kanisa hilo wakidai kuwa linaingilia masuala ya kisiasa.

Hata hivyo, juma lililopita Askofu Msaidizi wa Kanisa hilo Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini alisema mafisadi wanauhofia mwongozo huo.

Kwa mujibu wa Kilaini mwongozo huo unaweka vipaumbele vya nchi katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ndiyo maana wanaupinga.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya misa ya upadrisho iliyofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jimboni humo, Kilaini alisema mwongozo huo ulianza kutumika tangu uchaguzi wa mwaka 1995 na kusisitiza kuwa kwa mwaka huu watu wengi wameshtuka kutokana na kugusa masuala ya ufisadi.

Kanisa hilo lilitoa vitabu viwili vya mwongozi na vipaumbele vya nchi kabla ya kuuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010, mwongozo ambao umekumbana na vipingamizi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kwa madai kuwa dini inaingilia mambo ya siasa.

“Kwanza napenda watu waelewe kuwa mwongozo hauna lolote kuhusu dini kama watu wanavyodhani, kwa sasa jamii imeshituka kuhusu vitendo vya rushwa na ndiyo sababu baadhi ya wanasiasa wanapinga muongozo huo kwa kuwa unalenga kuwafungua watu macho na kukemea vitendo vya ufisadi,” alisema Kilaini na kuongeza.

“Ninachowataka wanasiasa wote washiriki kupiga vita ufisadi. Asiyetaka kupigana na ufisadi tusimchague na ndivyo mwongozo huo unavyosema,” alisema.

Alifafanua kuwa mwongozo huo unazungumzia juu ya serikali na msimamo wake na wala si kumchangua mtu fulani wala chama fulani kwa ajili ya kumpa uongozi.

“Watu wausome mwongozo huo kwa moyo mweupe na ninaamini wataufurahia, utakuza ufahamu juu ya masuala ya kidemokrasia,” alisema Kilaini.

Awali Mbunge wa Kigoma Kusini, Manju Msambya alishutumu mwongozo huo aliouita kuwa ni "Waraka wa Kiaskofu" wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Sheria na Katiba, akisema unawafundisha waumini wake kuhusu namna ya kuchagua viongozi kwa imani zao na kuonya kuwa nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.

Msambya ambaye hakutaja moja kwa moja dhehebu la dini lililotoa waraka huo, alisema unapingana na kanuni inayosema watu wasichanganye dini na siasa.

Lakini Askofu Kilaini alisema mwongozo huo haukutungwa na maaskofu wala mapadri wa Kanisa hilo na kufafanua kuwa umetungwa na Chama cha Wataalam wa Kanisa Katoliki (CPT) na kwamba wao waliupa baraka zote baada ya kuusoma na kuona unafaa.

Source: Mwananchi

=====================
​

UPDATES:

Askofu Kilaini: Kingunge anajadili hewa kuhusu mwongozo

*Asema kanisa litazidi kuusambaza nchi nzima

Zaidi soma hapa
 
Last edited by a moderator:
..WAKATOLIKI wako very organised kupitia mashina yao wanaita VIGANGO.

..huu waraka ukisambaa mpaka vijijini, na wananchi wakauelewa, CCM wanaweza kupata matatizo ktk uchaguzi.

..tatizo la waraka huo ni kwamba unaweza kuwa exposed to ANTI-CATHOLIC sentiments na hivyo kukosa nguvu ya ushawishi.
 
Hivi huo waraka kuna mtu anao nasi tuusome kabla hatuja changia? Kama waraka ulisha wekwa hapa naombeni link. Maana kwa ninavyo jua kuna watu humu wataanza kuchangia kwa hisia au kufuata mkumbo bila kujua kwanza nini kilicho semwa dani ya waraka huo. Je waraka unaelezea vigezo vya kiongozi bora? Au unatoa maagizo kuchagua watu wa kundi fulani? Maana isije ikawa inasema msichague mafisadi hapo lazima tutajua "mafisadi" nao wanaona "wanatengwa".
 
Kinguge yeye mawazo yake ni ya kisiasa zaidi.maana anaona huo waraka utavuruga kura za CCM hasa vijijini amabko viongozi wana kanisa wana nguvu.

Mbona hajasema anahofu mahakama ya kadhi? watawala wa kijadi wa kisukuma, kihaya wa kinyamwezi wakitaka mahakama zao je? hajalifikiria hilo? haya zikija na dini nyingine na zenyewe zikitaka mahaka zake.

Nadhani JK anongee na huyu mzee apumzike. sasa badala ya kuanza kuwa mrekebisha mambo ataanza kuwa mvurugaji.
 
Mkuu;

Mafisadi wana kazi kwelikweli. Askofu msaidizi amesema waraka uo hauzungumziii dini yeyote.Jamani wabunge si mnao kwanini mhandikie mate angali wino upo. Vuta waraka huo bungeni chambua ambako kumendikwa kuchagua viongozi wakatoliki na sio dini nyingine waite na kuwafungulia mashitaka walioandika.

Mimi nadhani waliotunga sio wajinga, wameandika na kupitisha kwenye mikono ya serikali na ikawapa baraka zote baada ya kuona hakuna shida sasa kerere za nini.

Tulizeni boli, ila mafisadi mtakipata cha moto.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom