Huyu Kingunge Ngombale Mwiru asitubababaishe na maneno yake ya kinafiki hapa. Mpagani huyu ndiye kwa unafiki ambaye alijifanya kuwa kaisahau katiba ya nchi ambayo haiongozwi na misingi ya dini bali kila mtu ana uhuru wa kamini na kuabudu dini aitakayo ili mradi asivunje sheria. Sasa iweje maswala ya OIC na mahakama ya kadhi yawe ya kitaifa??? Kama waislam wanataka hayo mambo waingie kama wao through BAKWATA na si kama nchi. Sijui ni kwa nini tunapenda kupindishapindisha mambo Tanzania only for the sake ya ku win kura za watu.
Ni mnafiki huyu huyu ambaye kwa unafiki mkubwa walishiriki katika azimio la Zanzibar la kupindisha Azimio la Arusha ili viongozi wajipatie utajiri kwa ufisadi, na matokeo yake tunayaona kwa kuzaliwa kwa matabaka Tz na tunakoelekea tutazidi yale matabaka yaliyoko India. Kama kuna mkuu hapa ambaye amesoma au ana ufahamu wa tamaduni wa India atakubaliana na mimi jinsi gani kule kuna matabaka. Kwa Tz itakuwa even worse, akina mzee matonya watakuwa na kundi lao, slums zitaongezeka, sijui nielezeje. Naumia kwa kuwa tumekubali kuibadili Tz na kila kitu. Sikatai Mtanzania kuwa na mali au utajiri ila utajiri huo chanzo chake ni nini??? Hebu fikiria matajiri kama Chenge, Idrisa Rashidi, Rostam, Somaias, Patels, Manjis, Mrambas, Yonas, Mkapas, Kingunges (kupitia hasa tender za manispaa za DSM na shares), Chandes, Nonis, Balalis, Lukazas, Njakes, Makubos, .....nth. The list is endless.
Wewe Kingunge ambaye ulistahili kupumzika, unaenda Bungeni na vikao vya Chama kusinzia na kusubiri mgawo wa sitting je umechangia kuipotezea Tanzania mwelekeo kiasi gani??? Hebu niambie tender unazopewa na manispaa zote tatu za DSM kwa kazi zile za kisaniii za Stand ya Ubungo, Uzoaji taka, n.k je unailipa serikali vilivyo au unatoa chochote ili pate tender zile ili hali wanafahamu pia wewe si mtendaji mzuri?? Ulizika Azimio la Arusha ili mkumbatie Rushwa vilivyo halafu leo mnafanaya usanii eti mna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, wakati mliiibariki Rushwa?? You are not serious man. Acha wakristo waamke wawape dosi ya electric shot ili muweze kuamka huo usingizi fofo mliolala. Ndiyo maana umeamua kukurupuka kuanza kupigia magoti Wakatoliki na huku ukihofia pengine other denominations may do the same. Yes, they may as they are fed up with your longolongos, ufisadi, rushwa kwa haki au stahili za wazalendo, uonevu kwa wananchi kuchukua ardhi zao kwa nguvu bila fidia za maana, yaani watanzania wanakuwa homeless and refugees in their own country. You are not serious man.
Mzee wetu Kingunge, tafadhali pumzika, sijaona mchango wowote wa maana kwa nchi hii kwa lengo la kumtetea mzalendo, ulichofanya ni kushiriki kwa asilimia 100 kuleta Azimio la Zanzibar la kuleta matabaka ya kisiasa na matajiri. Ni nyie ambao mtaisababisha Tz imwage damu siku zijazo. Fahamuni kuwa kila ovu lina mwisho wake na kila uonevu ni lazima ufike mwisho, msitake wazalendo waingie msituni, msitake hapa pawe kwa Savimbi, msitake hapa pawe kwa Makaburu, msitake hapa..... sina la kusema zaidi. Wakati huo mtatukimbia na mtaenda uhamishoni kwenye majumba mlionunua nje na vitega uchumi, mtaacha ndugu akimkata mwezake kichwa, mtatujeuza mauaji ya kimbari. Kingunge omba msamaha watanzania kwa niaba ya wote mlioshiriki kutufikisha hapa tulipo na mkiahidi kuwa mtaleta tena Azimio lingine ambalo litotoa ufumbuzi wa matabaka yaliyopo kwa sasa.
Aluta continua JF kwa kutupa nafasi ya kutoa hisia zetu hapa. Wazalendo watasoma bila ubishi. Mafisadi, vibaraka wa mafisadi, watoto wa mafisadi, ndugu wa mafisadi, wala rushwa watataka wanipige mawe au wanijibu kuwa nimeandika utopian, ni sawa una uhuru wa kuona utakavyo ila nimesema.