Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Mimi pia nimeona kwenye muhtasari wake kwenye magazeti, mbona huo waraka hauna neno???...unasisitiza usawa kwa watanzania wote na kutokuchagua viongozi wabovu kama hawa tulionao.

Kingunge lazima aumie kwa sababu alishiriki kutu chagulia kiongozi mkuu mbovu, na pia yeye ni mbovu mwenye ufisadi tele ukiwamo wa mradi wa ubungo bus stand na kumuendekeza mwanae (Kinjekitile) hadi kufikia hatua ya kuua watu ovyo akijua baba yake anamlinda. (Rejea kesi yake ya kuua mtu kwa kumgonga na gari makusudi, then akashinda kesi kimizengwe.)
 
Huo waraka ni mzuri na ukisoma vizuri unasisitiza usawa kwa watanzania wote na kutochagua viongozi wabovu, walafsi, wabinafsi na mafisadi, wawachague viongozi wenye uwezo wa kuwaletea maendeleo na kugawana pato letu kwa usawa kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Lakini nimebahatika kuangalia kipindi cha bunge leo, kwa kweli Kigunge amewaka sana na kusema watanzania hatutaki kugawanywa, ni vizuri, je lakini huu waraka una dhumuni gani hilo la kuwagawa watanzania au ni hofu tu ya watu wachache ambao wanaiona hii nchi kama mali yao na watoto wao, wenye tabia ya kurithishana madaraka kama vile tuko kwenye nchi za kifalme, inabidi tufikie hatua tusemae NO,No No; unajua Nyoka wanaoishi kwenye mdimu wana hila sana, sasa hapo wanaona watu watapata elimu na kujua haki yao ya kuchagua viongozi bora na siyo bora viongozi, Hizo ni hofu ambazo hazina maana, hapa tatizo ni maslahi yao yanataka kuguswa ama yameguswa.

Kigunge amekaa madarakani kwa miaka mingapi mpaka sasa? je hakuwa kushuhudia mali za taifa zikitafunwa kama njugu pengine hata yeye kama siyo familia yake kushiriki? je ameisha wahi kukemea huo ulafi kwa mali za uma? vituo vya mabasi dar nani ambaye hajui nini kinaendelea huko? sasa kwa nini kitu chema, lengo ni kuwaelimisha wananchi ili waweze kuwachagua viongozi wenye uchungu na rasmali za taifa ili wajiletee maendeleo yao, absolutely nonsense kigunge kuushutumu huu waraka wa kanisa katoliki.
 
mzewahoja huitwa mdini. mbona huyu aliopost hpa haitwi mdini.au?? au sio mzeewahoja
 
Tukubali tusikubali tumeingia kwenye matatizo na migogoro ya kidini bila kujijua. Haya yote yamesababishwa na Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2005 ambayo imekumbatia Mahakama ya Kadhi. Watu wameshaanza kuwa na religious line of thinking hata bungeni! Sasa hivi serikali inatakiwa eti ikae na waislamu kujadili mahakama ya kadhi ambayo ni ibada ya dini ya kiislamu. Labda wakimaliza watakuja kukaa na wakristo, wahindu, wasio na dini, nk ili kuunda mahakama zao, who knows. If you can go ten miles, why not fifty?
 
Mmmmmhhhhhh. Hivi ni yule Kingunge mpagani?
Sasa wakatoliki wapi na wapi na yeye?
Wao wametoa waraka kwa followers wao na yeye atoe wa kwake kwa ajili ya pagans kama yeye. asilalame bure.
 
Hivi huo waraka kuna mtu anao nasi tuusome kabla hatuja changia?

Mimi pia nimeona kwenye muhtasari wake kwenye magazeti
Msiandikie mate na wino upo. Mbona waraka huo upo hapa JF siku nyingi tu?

5161d1246544359-kanisa-katoliki-laandaa-waumini-uchaguzi-2010-ilani_kanisa.jpg


Angalia hapa kupata attachments zote
 
Huyu Kingunge kakurupuka kutoka wapi hajui kwamba KKT wanamuangano na madhehebu mengine ya kikristo nchini unaitwa CCT na wapentoksti na waasmblies nao wana muungano wao kama ni kuwaelekeza namna ya kuchagua viongozi bora ruksa tuu ,hata yeye andike tuu kwenye dini zao za kipagani kama wanamuungano
Mbona hakusemea jinsi anavyofisadi vituo vya parking katika jiji na hata Ubungo terminal hana vollume tena nchini kashuka hadhi ndio maana JK alimtema hata kwenye ushauri
 
Nimewahi kusema CCM lazima wakubali kubebeshwa lawama zote kama nchi itaingia kwenye mtafaruku wowote wa kidini, haya yote ni matunda ya utawala mfu, ukosefu wa maadili serikalini na wizi wa demokrasia unaofanywa wazi wazi na viongozi wa serikali ya CCM ikiongozwa na JK.

Ahadi za uongo na ahadi zisizotekelezwa kila mtu kachoka. Ni haki ya viongozi wa taasisi za dini kuwaelimisha waumini wao adui yao ni nani adui yao dhidi ya umasikini, maradhi, ujinga na tapiamlo kuwa ni serikali mbovu ya CCM, ni lazima madhebu ya dini zote yaangalie ni nini wameadhirika kwa uongozi huu dhalimu.

CCM ambao hawajui maneno yao na ahadi zao za uongo ni sumu na uuaji mbele ya jamii, mfano walitoa ahadi ya kuanzisha mahakama ya kazi wakiwa wamelala au hawakulifanyia kazi wakati wanatamka au hulka ya kisiasa wakadanganya waumini wa kiisilamu ili tu kupata kura zao, sasa wanaulizwa mahakama iko wapi wanaambiwa hakuna kitu kama hicho. Huu ndio mwanzo wa fujo.Je ccm hawakujua kwamba watapata pingamizi kikatiba au hawakujua kwamba waumini hawatasahau? haya yote Kingunge anatakiwa kujua ulaghai wao matunda yake ndio haya,kila mmoja anajikomboa kivyake

Kingunge anatakiwa kujilaumu yeye na viongozi wenzeka waandamizi. Vilevile kiongozi kama yeye anatakiwa apumzike kwani hawezi kwenda na treni hili la umeme wakati yeye alitumia la makaa. Kingunge na wenzake walikuwa viongozi wakati Tanzania ikiwa na chuo kimoja chenye wanafunzi chini 1000, hakuna TV, hakuna Computer, ikulu pekee ndio walikuwa wanaona cnn. Sasa hata sisi huku mtoni mtongani kama kawa.

Elimu na uelewa wa wananchi vinakuwa na demokrasia ya kweli itapatikana.Waraka huu hauna kitu kibaya unazungumzia jinsi ya kumkomboa mwananchi kutoka kwenye makucha ya ukoloni fisadi. Sasa mafisadi wanagwaya, na hilo liko wazi kabla ya kuanguka kwa himaya ya kifisadi inayoongozwa na CCM vumbi zito sana litatimka ni wale majasiri tu wataweza fika mwisho ila wengi watanunuliwa na kufa macho yakiwa wazi.
 
Kingunge is idiot and in most cases he spells rubbish!
 
Inaonekana wakristo wanatetea ukristo na waislamu wana komaa na mahama zao za kadhi.Kwa kifupi udini unaivagaa Tanzania, yaani ni vigumu kuamini kwamba sasa tunakaribia kuvuna dhambi ya dini. Nadhani Kingunge ana point kuhusu waraka wa kanisa Katoliki, ili kuziba mianya ya mgawanyiko wa nchi through dini.

Na kwakuwa Kingunge ni mwanasiasa wa kweli, ndo maana hakuzungumzia issue ya Uislam na Msambiana mahama zao za kadhi. Msambia ni kama Mugabe, kaanza kuzama kisiasa, anatafuta hoja mbovumbovu.
 
Nchi inakoelekea kubaya .....kila dini inavutia upande wake.

Tusubiri na tuone kama hatutagawanyika badala ya makabila tukafikia kwenye dini
 
Toka Mzee huyu afungue mdomo wake na kuwatetea mafisadi, na toka alipotukejeli watanzania, lolote analosema naona kama halistahili kutuliwa maanani. Huyu si mtu ambaye ana nia nzuri na Tanzania. Yeye kazi yake ni kupigania maslahi yake na ya baadhi ya wana CCM.

Niko radhi nimsikilize Sheikh Mkuu wa siku nzima, au nimsikilize Muadhama kwa saa 24 lakini sio kumsikiliza Kingunge kwa dakika moja. Alitufanya wajinga sana, sijui sasa anataka nini tena.

In fact background yake haimpi cridet ya ku-comment mambo yanayotoka kwa mtu kama Padri au Sheikh. Alijaribu kujibu aliyosema Dr Slaa ambaye ni Padre, matokeo yake tunayajua. sasa anajaribu kuwajibu waliojuu ya Slaa ataona matokeo yake.

Angeweza kucomment zake kama kiongozi wa wapagani, may be angesikilizwa.
 
mzewahoja huitwa mdini. mbona huyu aliopost hpa haitwi mdini.au?? au sio mzeewahoja
Kumbe huwa hauelewi kwa nini wanakuita mdini, na inaelekea ni tatizo la upeo zaidi. Huyu aliyepost hapa (bnhai) ameleta source (gazeti la mwananchi) ambalo lilinukuu kile ambacho huyo mzee wa propaganda (Kingunge) amekisema. Wewe unapoleta habari, huwa hatuelewi imechunguzwa na nani, huwa inakuwa tu kama tangazo fulani. Huna source, na unapenda kutumia maneno (Inasemekana, Nimesikia, kuna habari kwamba). Ingekuwa heri at least useme "Kwa mujibu wa uchunguzi wangu ....". Nimeangalia post na hasa thread zako unazoanzisha, za dini na zisizo za dini, na hata hii ya leo ya magari ya kifahari, huwa zinakuwa kama ulikaa mahali jamaa wakapiga stori, ukaileta humu bila utafiti. Leo pia umeweka hii:
INASEMEKANA NCHI NYINGI ZILIONDELEA KAMA jAPAN, DENMARK SEREKELI NA RAIA HUTUMIA GARI ZA BEI YA CHINI TOFAUTI NA TZ UTAONA MASHINGI, BMW , LAND CRUSER. KWNINI
 
Kingunge hajasikika siku nyingi kwa hiyo anataka watu wafahamu na yeye yupo.

Cha msingi ni kwamba watu wengi ambao wametendea nchi hii uovu mwingi wana hofu kuwa wananchi wakifahamu uovu wao nafasi zao ziko hatarini. Hivyo Kingunge na wenzake wanakuwa na hofu nyingi wakiona wananchi wanapata elimu ya uraia na kuona siku za sisiemu kuwa madarakani zinakaribia mwisho
 
Lazima Kingunge aogope naweza kusema that man is a big hypocrite aliyewahi kutokea Tanzania.

Enzi za mwalimu aliiishi kinafiki sana na immidiately baada ya mwalimu kuondoka kamekuwa kafisadi kwelikweli na kanabebwa kwenye mbeleko ya mafisadi.
 
Si ndo Kingunge huyu huyu anayehusishwa na kuingiza mahakama ya kadhi na OIC kwenye election manifesto ya CCM? Kuna watu wameshasema kuwa Kingunge na Mangula ndo waliingiza mambo haya kwenye manifesto ya CCM.

Ikiwa hayo ni kweli basi hatupaswi kushangaa yeye kupinga wakatoliki kwani huo msimamo ambao yeye anao, wakatoliki wanaupinga. Lakini inapaswa ajue kuwa kwa kuingiza kadhi na OIC ndani ya manifesto ya CCM aliingiza mambo ya dini ndani ya CCM.

Hapaswi kushangaa vile vile ikiwa dini zinaanza kuamka. Ameshakula nyama ya mtu!!
 
MBUNGE wa kuteuliwa na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru ameushambulia waraka wa kichungaji uliotolewa na Kanisa Katoliki nchini, unaoelekeza namna ya kupata kiongozi anayefaa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu ujao adai kuwa utaligawa Taifa.

Source: Mwananchi

Huyu Kingunge akatafute dini kwanza ndio aongee... he may not be the best to advice
 
Kingunge ana hofu kwani kwa muda mrefu amelelea ufisadi ambao ndo uhai wa chama chake CCM...

Waraka umemtisha kwani umebainisha ukweli kwa kutoa mwongozo sahihi kwa jamii nzima (mwongozo ni zaidi ya wakatoliki) ya watanzania..

kwa wenye kupenda mabadilikoo ya dhati mwongozo huu ni chachu ya hatua kubwa kufikia demokrasia endelevuu..
 
Kingunge ana hofu kwani kwa muda mrefu amelelea ufisadi ambao ndo uhai wa chama chake CCM...

Waraka umemtisha kwani umebainisha ukweli kwa kutoa mwongozo sahihi kwa jamii nzima (mwongozo ni zaidi ya wakatoliki) ya watanzania..

kwa wenye kupenda mabadilikoo ya dhati mwongozo huu ni chachu ya hatua kubwa kufikia demokrasia endelevuu..

Thanks Mkuu, pia sikumbuki kuona sehemu yoyote ya waraka ikisema chagua mkatoliki, nilichoona ni sifa za kiongozi bora!!! sasa kama huyo mtu hupo dini yoyote au hata kama hana kini kama yeye KINGUNGU, basi ndio huyo huyo

afterall sio lazima kutekeleza waraka kwani mwanajumuiya halazimiki!!! inawachoma sana wale wasio safi...

Ningependa kusikia pia waraka wa dini na madhehebu mengine ili viongozi wachafu wawekwe kando
 
Mheshimiwa Kingunge sijamwelewa kinachomfanya atoe shutuma kama hizo muda huu. Je nikwakuwa kanisa au viongozi wa kanisa wanawaambia "kondoo" wao wafumbue macho kwa kinachofanywa na viongozi mafisadi? Awaache waseme kile ambacho yeye kama mzee alipaswa kukisema lakini amenyamaza! Je anaona mambo yako sawa kama siku zote alizokaa kwenye system?Anachoogopa ni nini hadi atoe shutuma hizo na si kwa mengineyo? Sikumsikia awapongeza walioposema JK ni chaguo la Mungu. Je yeye ni mmoja wa hao mafisadi?
Nasubiri na tamko la Walimu leo. Na akumbuke CCM hawazibi ufa basi watajenga ukuta.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom