Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Katika hatua ya utekelezaji wa programu hii tunapendekeza:

1) Kufanyika mikutano ya makleri na viongozi wa halmashuri walei. Ni lazima katika mkutano huu ijadiliwe programu hii katika ngazi ya Jimbo na kupewa umuhimu unaostahili.
2) Wajumbe wa Mkutano huu: Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani watakuwa wakufunzi – kueleza na kufafanua mada za programu yetu.
3) Katika kazi ya kuongoza mkutano (no. 1), wajumbe wa CPT na wawakilishi wa Serikali waalikwe kutoa maelezo juu ya hali halisi pale watu wanamoishi.
4) Inapendekezwa paundwe timu ya Jimbo kwa ajili ya ufuatiliaji wa programu hii.
5) Katika ngazi ya Parokia programu ilenge kufundisha wanavijiji/watu mitaani na katika Jumuiya Ndogo Ndogo ili waweze kujadili masuala yaliyomo katika programu.
6) Ripoti za majadiliano hayo zitumwe Parokiani (Paroko na Halmashauri) kila baada ya miezi mitatu. Ripoti hizo zionyeshe mambo yaliyojadiliwa na maamuzi yaliyofikiwa.
Elimu inatolewa na viongozi wa kikristo kwa wakristo kumchagua kiongozi wa taifa wapi na wapi? "huku ni kujificha kwenye nyasi fupi"

Katika mikutano hiyo watu wenye nia njema kama wewe na ma sheikh wanakribishwa maana mjadala uko wazi hadi vitabuni sasa una hofia nini ?
 
Laiti ningelipata URAIS,

Kwanza ningelipiga vita na marufuku DINI zote ili watu kama Tumain anayeshinda humu ndani na baadaye apewe hela za sadaka za walalahoi kama mshahara. Hawa wala vya bure ni hatari sana. Ningelihakikisha kila mtu anafanya kazi haswahaswa, hamna Jumamosi wala jumapili ila tu siku ya mapumziko.

Tunajadili siku hizi maswala ya dini na tumesahau UFISADI. Mtu kama huyu Tumain unaweza kukuta wala dini hana, ila siku nzima kuchanganya watu akili ili wajadili dini na kuonyesha siku nzima jinsi Waislaam wanavyonyanyaswa na Rais wao juu.

Shame on you Tumain na hao maboss wako wanaokulipa hivyo visenti huku wao wakiondoka na Mamilioni. You know them, Fisadi weee!!!!
Shame on all WALA VYA BURE kwa kusema "Kikwete ni Chaguo la Mungu.."
Haya sasa kiko wapi? Mkapa hadi leo hamtaki kumpa ukweli wake, wanafiki nyie.

Tumain kama wapenda mambo ya dini, si nenda mtafute MaxShimba?
 
Hawa wanataka kuwapanda watu vichwani ,we waacha wataumbuka tu ,wanataka kutumia mgongo wa kanisa kula feza za walala hoi ,yaani namna wanavyojiingiza kwenye siasa ,hawaoni hata aibu ,achieni dini muingie majukwaani ili mpigiwe kura ,sio kupenyeza nyaraka kinyemela ,yaani maporoko,makadinali mapadre wote wamekuwa na harakati zisizo za kawaida katika siasa za Tanzania ,jamani taratibuni mtaitibua nchi ,au uongo ?
 
Jamani wanakijiji inabidi tuwe makini kwenye swala hili. Hapa hakuna udini kwenye walaka uliotolewa na kanisa hila nikutaka kuelimisha waumini jinsi ya kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya taifa letu sote.
Kunawatu wanatumia dini kama mtaji wa maisha yao na wengi tunawaona mitaani, hivyo basi hatuna budi kuwaelimisha wananchi ambao wanabuluzwa tu kwenye madhehebu kama mtaji wa viongozi hao. Nilicheka sana niliposikia kauli kwamba heti "Kikwete ni Chaguo la Mungu" SIKONGE na kuunga goti ndugu yangu kwani hakuna chochote kilicho tendeka mpaka sasa jamani tuache ushabiki wa vyama tutazame taifa kwa ujumla wake.
MAFISADI hakuna wakuwagusa, nchi inakwenda tu kiolela, safari nyingi ulaya, hivi mabalozi wetu/mawaziri wanakazi gani? bado sina jibu.
LAITI NINGEKUWA RAISI HATA KWA DAKIKA CHACHE SIJUI NAKWAMBIENI INGEKUWA HISTORIA.

HAKUNA KUKATA TAMAA HIPO SIKU NCHI YETU TUTAWAONDOSHA MAFISADI MADARAKANI.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, IBARIKI TANZANIA.
nawakilisha.
 
Huo ni "MPANGOMZIMA" ni wa kichama wala si dini kwa vyovyote dini haiwezi kufanya kazi
Wakitaka kufanya kazi waanzishe "CHRISTIAN....PARTY" wananchi tutawachagua kwa maelezo yao yote waliyotoa
a) Elimu anato walei (sijui ni nani?) anaripoti kwa padre anawaelimisha wanaparoko ..common sense inakupa kwamba lazima awe na conlict of interest anatoa directive indirectly kwamba mchague mkiristo the whole issue ni nonsense..ni ubaguzi wa kijinga kwelikweli...lakini yakija kama ploitcal party (WAACHE UNAFIKI) tutawachambua kama tunavyofanya kwa DP ya mtikila..without any problem
b) Haya mambo ya kujificha kwenye "NYASI FUPI" huku unaonekani ni UNAFIKI.

Tumain wacha ukali
 
Kwa kweli waliyoyazungumza ni sahihi na yanavutia but they dont have power to make it possible. Ama kunamawili, kunadili wameliona wanataka kunadi ili wapate tender, pili kweli wanauchungu wa nchi yao tanzania, lakini sasa waache tabia ya uchochezi. Kwa hili ikiwa wanania safi wamefanya kazi, but kuhusu kuishinikiza serikali kua isikubali Mahakama ya kadhi walichemsha na imewaharibia mnooooo. Wakijirekebisha tutawaunga mkono
 
Nina wasiwasi na malengo ya hawa jamaa, pamoja na kwamba mawazo ni mazuri. Maaskofu huku niliko na kote nilikowahi kuishi (kwenye secular states) wakati wa uchaguzi huwa wanasimamia agenda zao za kiroho - e.g. kupinga utoaji mimba, stem cell research, etc. Sijawahi kuona Maaskofu wanajiingiza kujumlajumla kwenye kila kitu cha kisiasa kwa kiwango hiki. Ni hatari jamani .. Serikali ionyeshe leadership na kukemea kwa ukali.
 
Cynic sijui unazungumzia wapi lakini Mabaraza ya Maaskofu Katoliki kote duniani wamekuwa wakifanya hivyo. Hawa wa Tanzania walishatoa kabla ya uchaguzi wa 1995 waraka wao tena mkubwa zaidi kwani ulikuwa ni "waraka wa kichungaji" uitwao "Dhamira Safi Dira ya Taifa letu".

Siyo maaskofu wa Tanzania tu bali wale wa Zimbabwe wamewahi kutoa waraka mkali wa kupinga utawala wa Mugabe tena kwa maneno na wale wa Afrika ya Kusini wamewahi kufanya hivyo hivyo.

Hivyo hilo siyo jambo geni ni sehemu ya majukumu yao ya kichungaji na kitume. Wakikaa kimya ndiyo yanatokea kama yale ya Pius 12 ambaye anadaiwa alikaa kimya wakati Wayahudi wanaokwa na utawala wa Hitler. Siku Maaskofu wakiweza kunyamazishwa kukemea utawala wa kifisadi basi siku hiyo tutakuwa tumeingia rasmi katika utawala wa kiimla.
 
Mzee Mwnakijiji,

Mkuu nilikubaliana sana na mpango wa kanisa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na Upigaji kura.. na nadhani nilieleza makosa madogo yaliyofanyika kwa kutosema mpango huo unahusu wananchi wote bali Waumini wa dhehebu hilo..
Sasa napokuja soma na haya najenga hisia kwamba sasa hivi kanisa Katoliki linataka kujiingiza ktk Siasa... Hii ni hatari kubwa!..
Unapoodai kuwa hili ni jukumu lao walilopewa, wamepewa na nani?.. wapi ktk Biblia inasema hivyo!...Mkuu Hata Yesu alipokuwa hapa duniani alikuwa ktk utawala mbaya sana, tena labda niweke hivi kwamba Israel ilikuwa ikitawaliwa na warumi..Lakini hakuna hata sehemu moja ya mafundisho yake Yesu ama waliofuatia baada yake walifundisha siasa na jinsi ya kuung'oa utawalka dhalkimu wa Mrumi..hakuna sura wala Aya moja inayotuonyesha Yesa kajiingiza ktk siasa pamoja na kwamba wale wate aliowafundisha dini walikuwa watumwa wa utawala huo dhalimu..
Leo tunapoona dhehebu la dini linapotaka kutumia Jina la yesu kufanya mambo ambayo kimsdsingi hayajengi nadhani hatuna budi kusimama wima na kuwaambia kwamba hoja yao tu inatosha lakini kujiingiza kwao ktk maswala haya kama wao ni wasuluhishi ambao wametumwa na Yesu, bila shaka hii ni kuanzisha mjadala mzito sana..

Kibaya zaidi ktk walaka wa Kanisa nimesoma kipengele kinachotaka reportza majadiliano zitumwe Parokiani..tena wakisisitiza kila baada ya miezi mitatu kama vile hili ni swala la Kanisa.. Wao ndio wafanye kitu gani ikiwa wao sii wanasiasa wala Wachumi wakati katiba na dira ya Kitaifa hazikufuata mwongozo wao..
Kifupi inaonyesha wazi hawa watu wanataka kuweka m,wongozo wa Kitaifa jambo ambalo dini imetumika ktk kila majibu au niseme maamuzi ya mwisho.. Mfano..Wanasema

Kwa kupata uelewa zaidi mada zilizojadiliwa katika mkutano wa Wakurugenzi wa Kichungaji na Wajumbe wa Tume ya Haki na Amani (TEC) ni:
1)Vipaumbele kwa mujibu wa Mafundisho ya Kanisa kuhusu Jamii.
2) Umuhimu wa uongozi wenye maadili katika kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kidini katika Tanzania.
3) Mfumo wa Sheria Tanzania: Nguvu na Changamoto.
4) Haki za Binadamu katika sera za biashara na fedha.
5) Mtazamo wa kimaadili katika mfumo wa kisiasa na kiuchumi.
6) Hifadhi ya jamii.

Bila shaka kutokana na maelezo hayo hapo juu inaonyesha wazi maamuzi mengi yatatokana na mafundisho ya kanisa ktk jamii, hivyo uwakilisha wahoja na maamuzi utatoka dhehebu moja..

Mkuu nionavyo mimi maswala ya kanisa yabakie na kanisa, uhuru waliopewa ni kutangaza uovu na dhlma inayotendeka laa sivyo waunde chama cha kisiasa ambacho kitawakilisha mawazo yao..Yawezekana wanalozungumza ni kwa faida ya wananchi wote na tungependa sana kuwaunga mkono lakini maadam huu ni MWONGOZO amabo siku zote hutokana na imani ya mrengo wa waumini wake, inanipa shida sana kukubaliana kwa sababu imani yangu na mrengo wangu ni tofauti na ule wanaofundisha..
 
Binafsi sioni kama kanisa linajiingiza kwenye siasa!Kinachozungumzwa na wao kimsingi sio SIASA.kwakweli mimi naona kama ni hali-halisi!

Na kanisa LINAWAJIBU wa kukemea maovu/dhambi.Kuwa chombo cha imani isije ikawa kikwazo kwa wao kutoinusuru jamii wanayoihudumia!

Otherwise,HONGERA KANISA-KATOLIKI
 
WE mgonjwa wa akili sijaleta thread hii mimi??
Nashinda humu kama unavyshinda humo wewe??? nani anakulipa???

Shame on you, kama una chuki zako jinyonge ndugu niko huru kifedha, kiakili, na hata kidini (my best choice is Islam)

Huna issue lala mbele unaboa


I thought kwamba tunajadili kwa nia njema tu!kumbe..............
 
I thought kwamba tunajadili kwa nia njema tu!kumbe..............



Ni kwa njia njema lakini haujamfanyia vizuri tumaini, kwani ww ukipewa nchi utashindwa hata kabla, hapa tu hujapewa ushaanza mtukana tumaini wa watu wakati hii ndo sehemu sensitive hata ikulu, ww ni dikteta na unataka kuwafanya watu wasichangie wanayohisi ni mazuri. Wacha mambo yako bwana. ww kama unafanya kazi kweli ulipata wapi statistics zakuonyeshesha tumaini anashinda humu? Be care mkuu
 
Binafsi sioni kama kanisa linajiingiza kwenye siasa!Kinachozungumzwa na wao kimsingi sio SIASA.kwakweli mimi naona kama ni hali-halisi!

Na kanisa LINAWAJIBU wa kukemea maovu/dhambi.Kuwa chombo cha imani isije ikawa kikwazo kwa wao kutoinusuru jamii wanayoihudumia!

Otherwise,HONGERA KANISA-KATOLIKI
Mkuu nakubaliana na wewe kama ingekwua hivyo lakini hapa tunaona kanisa likijenga MWONGOZO wa Kitaifa ambao sii wote tunakubaliana nao..Ikiwa leo tunapinga CCM kujenga mwongozo wa kitaifa iweje kanisa litujengee mwongozo wakati halihusianani kabisa na Utawala!..Kisha basi hata maamuzi ya mwisho yatolewe na Parokia..Who are they?

Ushauri wao ni mzuri na unaweza kupokelewa tu ikiwa kanisa litaunda chama chake na likaweka mwongozo wake ili wananchi wachague kukubaliana ama kutokubaliana.
Hata kama wanazungumzia maswala ya Ufisadi hizi ni hoja kama tunavyofanya hapa JF lakini sisi hatuwezi kuunda mwongozo kwa ajili ya taifa zima pamoja na kwamba tunafikiria njia bora za kulinda maslahi ya Taifa..Njia bora kwetu ni kuunda chama ambacho kitawakisha mawazo yetu kwa wananchi kama chama na sii mkusanyiko wa maamuzi ambayo wapo Watanzania wengi sana hawakubaliani..
 
Tumain,
Mkuu nimekusoma ila mimi nionavyo haitakuwa jambo zuri kujiingiza ktk siasa hasa hili wazo la kufungua Chama - kulingana na Watu na Mazingira..Ni mwanzo wa kuharibikiwa kwani watu wenyewe unatuona tulivyo! tumeshagawanyika kwa sura zetu..Isipokuwa ni ruksa kwa Kanisa kutoa hoja zao kama Kanisa na zikasikilizwa.. Na mara zote ni vizuri sana kama hoja hizo zitawajenga watu wote pale zinapowahusu wananchi wote laa sivyo tutajenga matabaka.. Makosa yanayotumika ni ujenzi wa mawazo kwa waumini ktk swala la Kitaifa, wanaweza kuwa na nia njema kabisa lakini likatafsirika vibaya kutokana na direction waliyochukua.
 
Sasa hivi utawasikia washika utamu wanaanza old arguments zao kuwa tusichanganya dini na siasa. wakati wao wanachanganya wizi, ufisadi, biashara na siasa
 
Mhh Katoliki ni BABA wa CCM ee mnataka kuwapangia kila kitu Sasa Chaguo la Mungu limekuwa CHUNGU e hahaha... Sasa ni bega kwa bega

(Lakini Askofu Kilaini alisema mwongozo huo haukutungwa na maaskofu wala mapadri wa kanisa hilo na kufafanua kuwa umetungwa na Chama cha Wataalamu wa Kanisa Katoliki (CPT) na kwamba wao waliupa baraka zote baada ya kuusoma na kuona unafaa.)

sasa huu Muongozo umetungwa na katoliki kalafu mnakataa katoliki ni dini sio wanasaisa inashangaza
mHHHHHShaMe...........

MpAka kIeLeWEkE

 
Hili suala la dini kujiingiza kwenye siasa na hasa kuonesha inaegemea upande gani sidhani kama ni uamuzi wa busara..
 
Kama kweli maaskofu wana nia njema (of 100% I dought) wafanye yafuatayo
a) Waanzishe chama cha siasa chenye Malengo, Dira na Methodologia ya utekelezaji kama walivyosema watapambana majukwaani na CCM, CUF na Chadema halfu tutwapa mandate through vote ---siyo kujificha kwenye nyasi???
b) Watangaze chama ambacho kimekubaliana na sera, na dira yao---ili tukiunge mkono au tukikatae??? siyo kufanya undeground movement oh tutaka hiki, tunataka hiki blablah.... huku wakijidai kuelimisha wakristo kanisani kwa kutumia mapdre, walei etc..(whoever their leaders are??) kuchagua viongozi wa kikristo shame on them???
c) In every Action there will equal opposite reaction (I can't wait muslims start the same ni their masjid (educate muslim)

Waislam walifanya sana hayo wakati Mkapa akiwa raisi.

Cha kufanyika sasa hivi ni CCM kujigawa na kujiandikisha kama

1. chama cha kiislam - kwa wanaccm walioko mikoa ya Pwani
2. Chama cha kikristo - kwa wanaccm walioko mikoani
 
Hii mada inajadiliwa kwa mara ya tatu sasa..lakini kama kawa 99% ya posts humu ndani ni ZERO INPUT..Yaani ni kujaza tu bandwidth kwa UPUPU..

Na sielewi mpaka dakika hii thread haijaunganishwa na zile nyingine KWANINI..sijui ni kwa sababu imeanzishwa na Mwanakijiji? JF imeshaanza kuniboa sasa..
 
Hii mada inajadiliwa kwa mara ya tatu sasa..lakini kama kawa 99% ya posts humu ndani ni ZERO INPUT..Yaani ni kujaza tu bandwidth kwa UPUPU..

Na sielewi mpaka dakika hii thread haijaunganishwa na zile nyingine KWANINI..sijui ni kwa sababu imeanzishwa na Mwanakijiji? JF imeshaanza kuniboa sasa..

Mkuu umesema kweli kabisa, tena inasikitisha kuona watu wazito hapa JF wamejaa udini tu. siku zote wanadai wapo kwa ajili ya maslahi ya taifa, uongo tupu, wapo kwa ajili ya maslahi yao, dini zao na mambo yao. Kweli kazi tunayo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom