Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Walimwita chaguo la mungu kwasababu alishawahakikishia "upendeleo" kwenye kodi, position nk. just curious?
Je una uhakika gani kwamba watafanya hivyo kwa yeyote ambaye atatimiza masharti yao au matakwa yao bila kujali jamii zingine, just curious?
Kwani kuna ulazima gani wakristo wafanye kazi ya kutoa elimu ya uraia? Does it mean wakristo are so ignorant hawana elimu? shame on them? just curious?

Hivi udini ni upi kati ya hivi: waraka unaowataka Watanzania kupiga kura 'responsibly' au wale wanaotaka Mahakama ya Kadhi iwe sehemu ya mfumo wa sheria za nchi na pia kujiunga OIC kuwe kwa nchi na siyo taasisi ya dini yenyewe?
 
Last edited:
Kwani nyie mnalalamika kuhusu kanisa katoliki Tz hamjui ndo linaloongoza dunia? Ujue MAFI ndo wanaoongoza dunia so msilaumu tz sana hili ni tatizo la dunia, watanzania tusije kutukanana na kulaumiana, hata wazungu wanajua nn kanisa katoliki sasa ss second user tunatoana nishai bure, Serikali lazima itishike inaposikia viongozi wa kikatoliki wanatishia suala fulani. I beg my tz brothers tuthamini utanzania wetu Kanisa linatimiza maagizo ya Rome wala si kwa manufaa ya Mtanzania, wake up jamaniiiiiiiiiiii

Hayo mawazo yanatoka kwenye 'corrupt mind'. Labda ungesema hujui kitu gani waraka umesema lakini hakuna agizo lolote la Rome. Kama hatuwezi "kujitafiti/kujihoji" kama waraka unavyotusihi, then tumekufa!
 
MagobeT,

..suala la OIC na Kadhi halijadiliki sasa hivi bila watu kukimbilia majoho yao ya udini-udini.

..waraka huu utawatenga Waislamu kwasababu ya hoja hiyo ya Kadhi na OIC.

..hata Wapalestina na Waisraeli wanapofanya mazungumzo hatima ya mji wa Jerusalem huachwa kando kwanza.

Lakini katika kuchangia au kutoa maoni kila Mtanzania ana haki hiyo. Na in fact, Kanisa linasema "tunapendekeza" halijasema hayo mapendekezo ni Amri Kumi za Mungu au 'gospel truth'. Kwa upande mwingine sioni kwa nini Kanisa Katoliki liogope kusema "taasisi za dini zisiwe sehemu ya mfumo wa sheria kama Katiba inavyosema".
 
Mimi nawashangaa wadanganyika.

Kila siku tunalalamika jinsi gani CCM wanavyotuibia kura kwa kuwatumia wananchi wasiojua haki yao. Sasa leo kanisa limejitolea kuwaelimisha watu tunapiga kelele badala ya kuwapongeza. Kweli CCM watatawala TZ milele.

Mungu ibaliki TZ!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwahiyo "elimu" hiyo ni kuitoa CCM madarakani sio?
 
Haya yote yanakuja kutokana na ombwe la uongozi na itikadi katika nchi hii. Maji huenda palipo na nafasi na hatimaye kupajaza na kisha kuendelea na safari. tusubiri
 
Halisi,

..nadhani ulichokosea ni jinsi ya kuwasilisha thread yako.

..ungeweka bayana kwamba heading ya thread yako inawa-quote gazeti la raiamwema.

..nadhani raiamwema wameamua ku-sensationalize tu, lakini mambo yote yaliyopo ndani ya habari yao yamekuwa yakizungumziwa mitaani kwa muda mrefu tu.

..halafu ni siri gani hiyo inayowekwa ktk maandishi na kuandaliwa waraka? binafsi nimeshangazwa na jinsi raiamwema walivyoitoa habari hii.

..kwa maoni yangu waraka wa Kanisa Katoliki ungekuwa mzuri na INCLUSIVE kama ungeepuka suala la mahakama ya Kadhi.

..nadhani kwa kulitumbukiza suala hilo[mahakama ya kadhi] ktk waraka wao Maaskofu, na walioandaa waraka huo, wameshindwa kuisoma hali ya kisiasa na kijamii iliyoko Tanzania sasa hivi.

Samahani kuchelewa kujibu. Ila maneno yako ya utangulizi sikubaliani nayo. Nakubaliana na wewe kwa kila neno baada ya hapo. Kimsingi heading si yangu ni heading ya gazeti kama uliovyosema mwenyewe. Nimebandika (paste) tu. Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye source na kuangalia kama nimeongeza ama kupunguza kitu. Kama ni kukosea waseme wenye gazeti, jambo ambalo umelifanya kwa kusema kwamba wamezidisha chumvi kuuza gazeti. Lakini pia suala la "siri" ama "si siri" ni muono wa mtu, jambo ambalo linajadilika.
 
These are the true colors za wakatoliki, sasa makucha yapo nje nje. Niwakumbushe tu usia wa Baba wa Taifa kwamba chonde chonde waachane kabisa na dhambi hii wanayotaka kuitenda ya ubaguzi kwa misingi ya dini, hawatakaa salama hata wakichukua dola.
 
Hata kama tuna matabaka tofauti ktk kuabudu lakini hicho si kigezo cha kuchochea ubaguzi wa kifikra.
__________________
Hapa umezungumzia utaifa hasa,tunasema ya dunia ipe dunia na akhera ipe akhera,fanya mazuri kama utakufa sasa wakati ukiitumikia dunia kama hautakufa milele.
 
Jamani tuwekeeni huo waraka....nasi tuusome naomba mtu ambae anao ani PM
 
Kwahiyo "elimu" hiyo ni kuitoa CCM madarakani sio?

Elimu hiyo ni kutaka Watanzania wapige kura kwa kuwajibika na wasikubali kudanganywa au kununuliwa na viongozi wa kisiasa au kuchagua viongozi kwa misingi ya dini, chama au kabila. Is it wrong to sensitise people on responsbile voting?
 
These are the true colors za wakatoliki, sasa makucha yapo nje nje. Niwakumbushe tu usia wa Baba wa Taifa kwamba chonde chonde waachane kabisa na dhambi hii wanayotaka kuitenda ya ubaguzi kwa misingi ya dini, hawatakaa salama hata wakichukua dola.

Aisee! Hivi haya uliyoandika umeyafikiri au umeyawaza?
 
Watuambie kama Zanzibar ni nchi au si Nchi au hawakugusia mambu ya Muungano ?

Na wewe toa waraka wako na utwambie whether Zanzibar ni nchi au la? Kwani hili lina uhusiano gani na kupiga kura 'responsibly'?
 
Msisitizo wa Wakristo katika Uchaguzi ni kukataa Viongozi wasiowaadilifu,wazinifu,mafisadi,wabinafsi,wenye upendeleo na ubaguzi.Tatizo hapo ni nini,acheni kupotosha ukweli.
 
Geofrey Nyang`oro, Anna John na Fredy Azzah

ASKOFU msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amesema mafisadi wanauhofia mwongozo uliotolewa na kanisa hilo ambao unaweka vipaumbele vya nchi katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ndiyo maana wanaupinga.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya misa ya upadrisho iliyofanyika jana kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam, Kilaini alisema mwongozo huo ulianza kutumika tangu uchaguzi wa mwaka 1995 na kusisitiza kuwa kwa mwaka huu watu wengi wameshtuka kutokana na masuala ya ufisadi.

Kanisa hilo lilitoa vitabu viwili vya mwongozo na vipaumbele vya nchi kabla ya kuuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, mwongozo ambao umekumbana na vipingamizi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kwa madai kuwa dini inaingilia mambo ya siasa.

“Kwanza napenda watu waelewe kuwa mwongozo hauna lolote kuhusu dini kama watu wanavyodhani, kwa sasa jamii imeshtuka kuhusu vitendo vya rushwa na ndiyo sababu baadhi ya wanasiasa wanapinga mwongozo huo kwa kuwa unalenga kuwafungua watu macho na kukemea vitendo vya ufisadi,” alisema Kilaini.

“Ninachowataka wanasiasa wote washiriki ni kupiga vita ufisadi. Asiyetaka kupigana na ufisadi tusimchague, na ndivyo mwongozo huo unavyosema,” alisema.

Alifafanua kuwa mwongozo huo unazungumzia juu ya serikali na msimamo wake na wala si kumchagua mtu fulani wala chama fulani kwa ajili ya kumpa uongozi.

Alisema kama kutakuwa na kiongozi wa dini au mtu yeyote wa dini atakayezungumzia masuala ya kumchagua mtu ama chama fulani cha siasa, atakuwa amepotoka na kwamba huo ndio msimamo uliomo kwenye mwongozo huo.

“Watu wausome mwongozo huo kwa moyo mweupe na ninaamini wataufurahia, utakuza ufahamu juu ya masuala ya kidemokrasia,” alisema Kilaini.

Kauli ya Kilaini imetolewa wakati ambapo baadhi ya wabunge wamejitokeza kuitahadharisha serikali kuhusu mwongozo huo kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge la Muungano, wakidai kuwa ukiachwa nchi inaweza kuingia kwenye matatizo ya udini.

Mbunge wa Kigoma Kusini, Manju Msambya aliushutumu mwongozo huo aliouita kuwa ni "waraka wa Kiaskofu" wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Sheria na Katiba, akisema unawafundisha waumini wake kuhusu namna ya kuchagua viongozi kwa imani zao na kuonya kuwa nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.

Msambya ambaye hakutaja moja kwa moja dhehebu la dini lililotoa waraka huo, alisema unapingana na kanuni kwamba watu wasichanganye dini na siasa.

Akizungumza kwa jazba, Msambya, ambaye katika mchango wake alitaka tamko la serikali kuhusu sababu za nchi kutojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na kutoundwa kwa Mahakama ya Kadhi, alisema alichukizwa na kitendo cha waziri ambaye hakumtaja jina, kwamba alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na waraka huo, aliusifu akisema ni mzuri kwa sababu ni moja ya elimu ya kupiga kura.

Lakini Askofu Kilaini alisema mwongozo huo haukutungwa na maaskofu wala mapadri wa kanisa hilo na kufafanua kuwa umetungwa na Chama cha Wataalamu wa Kanisa Katoliki (CPT) na kwamba wao waliupa baraka zote baada ya kuusoma na kuona unafaa.

Kabla ya kuongea na waandishi wa habari, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliwapa daraja la upadri, mashemasi watatu.

Mashemasi hao ni pamoja na Joseph Mkonde, Joseph Mapunda ambao watakuwa mapadri wa jimbo, huku Hendrick Mambwe akienda kulitumikia kanisa hilo nchini Ethiopia.

Source:
Mwananchi
 
Nyaraka hizi ndizo ambazo zimezua mazungumzo na gumzo kwa watu mbalimbali. Ni nyaraka ambazo CCM haina budi kuzihofia endapo zitafuatiliwa kwa karibu, kutekelezwa na kuzingatiwa ujapo uchaguzi mkuu ujao.

Habari zaidi:

Na. Geofrey Nyang`oro, Anna John na Fredy Azzah

ASKOFU msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amesema mafisadi wanauhofia mwongozo uliotolewa na kanisa hilo ambao unaweka vipaumbele vya nchi katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ndiyo maana wanaupinga.
​

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya misa ya upadrisho iliyofanyika jana kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam, Kilaini alisema mwongozo huo ulianza kutumika tangu uchaguzi wa mwaka 1995 na kusisitiza kuwa kwa mwaka huu watu wengi wameshtuka kutokana na masuala ya ufisadi.

Kanisa hilo lilitoa vitabu viwili vya mwongozo na vipaumbele vya nchi kabla ya kuuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, mwongozo ambao umekumbana na vipingamizi kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kwa madai kuwa dini inaingilia mambo ya siasa.

“Kwanza napenda watu waelewe kuwa mwongozo hauna lolote kuhusu dini kama watu wanavyodhani, kwa sasa jamii imeshtuka kuhusu vitendo vya rushwa na ndiyo sababu baadhi ya wanasiasa wanapinga mwongozo huo kwa kuwa unalenga kuwafungua watu macho na kukemea vitendo vya ufisadi,” alisema Kilaini.

“Ninachowataka wanasiasa wote washiriki ni kupiga vita ufisadi. Asiyetaka kupigana na ufisadi tusimchague, na ndivyo mwongozo huo unavyosema,” alisema.

Alifafanua kuwa mwongozo huo unazungumzia juu ya serikali na msimamo wake na wala si kumchagua mtu fulani wala chama fulani kwa ajili ya kumpa uongozi.

Alisema kama kutakuwa na kiongozi wa dini au mtu yeyote wa dini atakayezungumzia masuala ya kumchagua mtu ama chama fulani cha siasa, atakuwa amepotoka na kwamba huo ndio msimamo uliomo kwenye mwongozo huo.

“Watu wausome mwongozo huo kwa moyo mweupe na ninaamini wataufurahia, utakuza ufahamu juu ya masuala ya kidemokrasia,” alisema Kilaini.

Kauli ya Kilaini imetolewa wakati ambapo baadhi ya wabunge wamejitokeza kuitahadharisha serikali kuhusu mwongozo huo kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge la Muungano, wakidai kuwa ukiachwa nchi inaweza kuingia kwenye matatizo ya udini.

Mbunge wa Kigoma Kusini, Manju Msambya aliushutumu mwongozo huo aliouita kuwa ni "waraka wa Kiaskofu" wakati akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Wizara ya Sheria na Katiba, akisema unawafundisha waumini wake kuhusu namna ya kuchagua viongozi kwa imani zao na kuonya kuwa nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.

Msambya ambaye hakutaja moja kwa moja dhehebu la dini lililotoa waraka huo, alisema unapingana na kanuni kwamba watu wasichanganye dini na siasa.

Akizungumza kwa jazba, Msambya, ambaye katika mchango wake alitaka tamko la serikali kuhusu sababu za nchi kutojiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na kutoundwa kwa Mahakama ya Kadhi, alisema alichukizwa na kitendo cha waziri ambaye hakumtaja jina, kwamba alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na waraka huo, aliusifu akisema ni mzuri kwa sababu ni moja ya elimu ya kupiga kura.

Lakini Askofu Kilaini alisema mwongozo huo haukutungwa na maaskofu wala mapadri wa kanisa hilo na kufafanua kuwa umetungwa na Chama cha Wataalamu wa Kanisa Katoliki (CPT) na kwamba wao waliupa baraka zote baada ya kuusoma na kuona unafaa.

Kabla ya kuongea na waandishi wa habari, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliwapa daraja la upadri, mashemasi watatu.

Mashemasi hao ni pamoja na Joseph Mkonde, Joseph Mapunda ambao watakuwa mapadri wa jimbo, huku Hendrick Mambwe akienda kulitumikia kanisa hilo nchini Ethiopia.
 
Attachments

Last edited:
Ngoja nisome kwanza na hicho kilichomo ndani yake, na Hongera sana kwa kazi yako nzuri Babu yangu Mwanakijiji
 
Niliposoma hizi document nimegundua kuwa kanisa lingejitanga moja kwa moja kwamba ni chama mbadala na katiba iruhusu vyama vya kidini haraka iwezekanavyo wananchi wachague christian party kama wanaona itafaa kwasababu zifuatazo:-
a) watoa elimu hiyo kama ilivyo ainishwa katika ngazi ya famili, vigango, ktiongoji etc...ni viongozi wa kanisa na wakristo..kwa vyote vile lazima wana conflict of interest hivyo waruhusu vyama vya kidini
b) Report system: wakisha fanya mikutano na kutoa elimu wanareport kwa wakubwa kwenye hierachy ya kanisa ili kupata nini? directive? au nini wakubwa lazima wana conflict of interest na watu ya dini yao???
c) Ni dalili mbaya na ni aibu kwamba imetoka kwa maaskofu wa Tanzania shame on them!!!
NB. Nafikiri waislamu waanzishe the same move na katiba iruhusu kuwepo na vyama vya kidini watanzania waamue chama cha dini gani zipongoze kwa kuangalia sera na dira yao
Otherwise: huu ujinga wa maaskofu wa Tanzani ukomeshwe mara moja...

Jibu hoja zao zilioandikwa humo. Kwa mfano onesha mfano wa mahali ambapo wametoa hoja zenye msingi wa kidini.
 
Mkuu Mwanakijiji asante sana kwa hizi nyaraka, nitazisoma. The big point katika makala ya gazeti (hapo juu) ni aya hii hapa chini

"Ninachowataka wanasiasa wote washiriki ni kupiga vita ufisadi. Asiyetaka kupigana na ufisadi tusimchague, na ndivyo mwongozo huo unavyosema,"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom