Hii mada inajadiliwa kwa mara ya tatu sasa..lakini kama kawa 99% ya posts humu ndani ni ZERO INPUT..Yaani ni kujaza tu bandwidth kwa UPUPU..
Na sielewi mpaka dakika hii thread haijaunganishwa na zile nyingine KWANINI..sijui ni kwa sababu imeanzishwa na Mwanakijiji? JF imeshaanza kuniboa sasa..
Hii mada haina tatizo lolote; tatizo ni wale wanaochangia. Kilichotakiwa kufanywa kisomi ni kusoma hizo nyaraka kuzipinga au kuzikubali. Kuonesha udhaifu wake au kuonesha ni wapi zinafaa. Ndio maana ya kuziweka hapa.
Bahati mbaya mtu mmoja tu ndiye aliyeleta masuala ya udini hapa. Kiasi kwamba BAKWATA wakitoa tamko kuhusu mtazamo wao wa masuala ya nchi tutatakiwa tuangalie dini yao badala ya kupima kile wanachokisema. Ikija taasisi nyingine ya kidini itoe mawazo yake basi tusisikilize na kupima wanachosema bali tuwahukumu mara moja kuwa ni wadini.
Kama Waislamu wanaweza kutoa matamshi yao na miongozi kwa watu wao kwanini iwe vibaya kwa maaskofu kutoa miongozo kwa waumini wao? Hayo yaliyotolewa yametolewa kwa ajili ya Wakatoliki na yanahusu siasa ya nchi yao.
Juzi, Mufti Bin Simba amezungumza na kunukuliwa akiwataka Waislamu kuwa watulivu wakati huu serikali inashughulikia suala la Kadhi. Sasa alifanya makosa kutoa wito huo? Je wakristu waliousikia wakwazike kwanini amewataka waislamu tu kuwa watulivu?
Ni lazima tufike mahali tujadili hoja kwa kupima hoja zenyewe. Tusitafute udini kiasi kwamba tutafika mahali mtu humu akisema kitu kuhusu mhusika Muislamu basi tunajiuliza kama amesema kwa sababu ya udini au la. Mwisho tutafikia mahali wakristu wazungumzie mambo yanayowahusu wanasiasa wakristu na Waislamu wazungumzie mambo yanayowahusu wanasiasa waislamu.
Hoja jamani zijibwe kwa hoja.
a. Je hoja zinazotolewa na nyaraka hizo zina msingi?
b. Ni nini upungufu wa hoja hizo?
c. Je ni kwa kiasi gani zinachangia katika kuleta demokrasia?
Binafsi ningependa jumuiya nyingine za kidini nazo zikatupa mwelekeo wa mitazamo yao kuhusu taifa tunakoelekea uchaguzi mkuu na kutupa mambo ya kutafakari. Kwa kufanya hivyo wanatusaidia kufikia hatimaye maamuzi sahihi kwani ni kwa kupata taarifa za kutosha ndipo tunaweza kufikia kweli uamuzi ambao kwa kadiri tunavyoweza ndio unatufaa.
Na taasisi hizo zikija na matamko yao nitayasooma kwa makini, kuyafanyia kazi na kuyasambaza vile vile ili watu wengine nao waweze kuyapata. Tusiogope kugongana kwa hoja.
Tayari mimi mwenyewe ninaona mapungufu kadhaa kwenye nyaraka zao na inshallah, nitawajibu hivyo hivyo kwa wazi kwani nilishawaandikia mara kadhaa huko nyuma.
HOJA HUJIBIWA KWA HOJA SIYO VIOJA!