Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
NADHANI HAPA TUNATAKA KUKOSEA. WATANZANIA WOTE WALIO MASKINI HAWANA WAKUWASEMEA. TUME YA UCHAGUZI IMESHINDWA KUTOA ELIMU KWA WAPIGA KURA, INABARIKI MATUMIZI YA PESA KWENYE UCHAGUZI. KWA UFUPI HAINA MAKUCHA. WABUNGE WA CHAMA DUME WAO KILA SIKU WANAIMBA MASILAHI YA CHAMA. JE MASLAHI YA MTANZANIA WA KAWAIDA YATALINDWA NA NANI? KWA KUWA VIONGOZI WA DINI WANATAGULIZWA KUOMBA WAKATI WA KUAPISHWA RAIS.... NI VYEMA WAKATOA ELIMU KWA WAPIGA KURA..... DINI ZOTE ZIIGE MFANO WA WAKATOLIKI, WAWE WAZI WASEME YALIYO MOYONI MWAO.......NAWAUNGA MKONO

Tanzania will never develop under ccm
 
watu wahalifu mara zote huwa wanatafuta kuungwa mkono hata kwa hoja za hovyohovyo. msambya hana kitu chochote zaidi yakujipendekeza watu waone ana fikiri kumbe mshamba tu.
Ameishaabmbiwa aombe huo waraka ausome vizuri, na kama haelewi aombe ufafanuzi pia
 
Hii mikakati ya kanisa sasa inajitokeza ,ninavyowasoma wakatoliki wanakasumba mbaya sana ,kuwa hapa duniani ni wao tu na wanao uhuru wa kumuua yeyote yule ambae si mkatoliki,ukisoma kitamu cha mauaji ya Mwembe Chai utaona mwandishi ni jinsi gani ameweza kuonyesha msimamo wa wakatoliki na makanisa mingine ,inaonyesha wakifanikiwa kuwaweka pembeni Waislamu watawageukia wenzao.

Kitabu cha Mauaji ya Mwembechai katunga nani, maana na chenyewe kina harufu ya kidini!
 
Mashehe, Maaskofu, Mapadri, Wachungaji, Ma-Rabi, n.k.. wakiungana kuhamasisha waumini/wafuasi wao kuchagua viongozi wanaofaa, itakuwa njia mojawapo madhubuti ya kuwafanya viongozi wetu waanze kuwajibika, kwani pungufu ya hilo ni kuwang'oa wababaishaji nyakati za uchaguzi!

nimekupata mkuu
lakini je hawa viongozi wa kidini wanaweza kukaa pamoja????????

huwa nadhani Maaskofu wa kikatoliki wana confidence wanaweza kukaa na yoyote, pia baadhi ya masheikh hawana shida. sijui wengine hasa wa makanisa ya pentekoste (deci) kama wanakubali? maana wanazidi kutengana kila kukicha na kunyang'anyana wafuasi
 
Wabunge wetu wengi sio wasomaji wazuri. Msambya shida yake kubwa ni kwa nini waraka huu utolewe na MAASKOFU. Hana na wala hakuonyesha nia kuyashambulia yaliyoandikwa mle. Waraka ule ungeandikwa na TAMWA, REDET au NGO yoyote mbali na MAASKOFU, Msambya asingehangaika nao.
Hilo moja, la pili tusisahau wanasiasa wanapokuwa wamefilisika kisiasa na mambo yanaelekea kuwaendea kombo ( hasa hawa wa kuchaguliwa) watatafuna njia yoyote ile kujihalalisha upya kwa wapiga kura wao ikiwemo DINI, KABILA, JINSIA, PESA,...

Ninavyo vijitabu hivyo kwa Kiingereza na Kiswahili. Waraka umeandikwa na Christian Professionals of Tanzania (CPT). CPT ni chama cha Wakristo wenye taaluma mbalimbali - lawyers, judges, teachers, doctors, journalists, economists, nurses, etc. Kwa kifupi, waraka huo ni mchango wa wanataaluma mbalimbali Wakristo (Wakatoliki) kuhusu hali ya maisha ya Watanzania na nini kifanyike ili kuinua maisha yao

Kwenye sehemu ya Madhumuni/Lengo la Ilani ya Kijitabu kilichoandikwa ILANI (Mapendekezo ya Vipaumbele vya Taifa), imeandikwa hivi:

"Kwa Ilani hii, tunatoa mwaliko kwa wote na kuwasihi Watanzania wote kufikiri kwa makini changamoto kuu zinazokabili nchi yetu na wananchi wake wengi ambao ni maskini wa mali, waliotengwa na wasio na uwezo. Kuzishughulikia changamoto hizi kunahitaji kuweka vipaumbele sahihi na njia sahihi za ufumbuzi ambazo zinashughulikia kikamilifu matatizo ya umaskini, utenganisho wa kijamii na hali ya kukosa uwezo kwa watanzania wengi. Ilani hii itakuwa mwongozo kwa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010." (pp 4-5).
 
Kwa namna ambavyo hii thread inajadiliwa, inathibitisha kuwa kile kilema chetu cha baadhi ya Watanzania kutopenda kusoma vitabu, majarida, machapisho, ramani na hata alama, bado kipo, miaka kadhaa baada ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya umma kuimarika zaidi.

Tabia hii ni mbaya ni eneo muhimu kwa ustawi wa ujinga, maradhi na umasikini. Tuipige vita kwa nguvu zetu zote, waungwana, hali ni mbaya. Tusome jamani, porojo hazitaisaidia nchi yetu hii, na hatutakuwa na nafasi kwenye dunia ya utandawazi tena. Tutasukumwa pembeni na kubaki kulalamika tuuuuu!!!

Sijui nani alisema "If you want to hide a diamond piece from a Tanzanian, put it in a book"...was damn right!
 
nimekupata mkuu
lakini je hawa viongozi wa kidini wanaweza kukaa pamoja????????

huwa nadhani Maaskofu wa kikatoliki wana confidence wanaweza kukaa na yoyote, pia baadhi ya masheikh hawana shida. sijui wengine hasa wa makanisa ya pentekoste (deci) kama wanakubali? maana wanazidi kutengana kila kukicha na kunyang'anyana wafuasi

Rafiki,
Hizo kwenye nyekundu ni pumba hasa. Inabidi uchukue ungo uzipepete ukazitupe jalalani.
 
Kwanza Mada hii iliyotolewa na Kanisa Katoliki siyo SIRI! Kila mtu ameweza kuisoma hapa JF, na naambiwa nakala zake zimesambazwa na zinatolewa bure.

Hii ni mada nzuri sana inayotoa civic education. Shule zetu zitumie Mada hiyo ili vijana wetu waelewe majukumu ya kila raia, hasa wakati wa uchaguzi na waeleze wakazi wa vijijini waelewe maudhui yake. Wakati wa uchaguzi kila Raia aamue kwa uhuru na ujasiri kwamba ni nani atampigia kura ili anayechaguliwa aweze kuboresha maisha yake na ya jamii kwa jumla.

It is only a coincidence that the Catholic Church initiated this idea of civic education so that the forthcoming elections can be more beneficial to Tanzanians. In observing its guidence, we shall elect better leaders and hopefully salvage our country from the abyss of poverty and corruption into which our country has fallen.

On reading it several times, I do not see anything which would make a non-catholic like myself or even a Moslem object to the action recommended. I recall that it was Christian leaders in 2005 who proclaimed that Jakaya Kikwete was the choice of God!

In this treatise the Church is not advocating for any person, but putting forward proposals which will result in the choice of a person best qualified to lead Tanzania. He could be Jakaya Kikwete or someone else. We are only being implored to exercise our judgement judiciously.

We should thank these leaders of people for the initiative. We await other proposals which I gather may be put forward by other religious leaders.

I only wish all of these religious leaders could get together and, trusting each other, thrash out a document to guide us, without anyone among us, trying to read between the lines.
 
Last edited:
We Masatu, wewe!!! shame on you!, huo udini udini upi? Nakuaminia mkuu wewe ni mtu mweledi unayeweza kujua katika hiyo thread hakuna hata nukta moja ya neno niliyoweka, sasa hapo unanihukumu kwa lipi? na huo udini upi na dini ipi? Halafu tukirejea kwenye source ya habari husika utaona kwamba hata wao kichwa cha habari kimelenga kuwafahamisha wasomaji wao wengi na hata hapa JF unaona wengi ni wale ambao hawajawahi kusoma hiyo ILANI na waliosoma pengine wapo ambao hawajapata vionjo vyake. Mfano ni Mbunge aliyechangia bungeni huku akiwa hajawahi kuusoma waraka husika. Tafadhali tafakari kwanza.

Mkuu nafikiri uko sahihi,swala la udini lita depend na mtizamo wa mtu binafsi.Mahali ambapo nchi yetu imefikishwa si dhani kama mtu aliyechukua muda wa kutafakari ilani hiyo ataanza kunyoshea kanisa lolote.
Wakati serikali ikitawala wananchi na mali zao kanisa linawaongoza kiroho
wananchi wanapokuwa hoi kanisa halitakuwa na amani kwani ni waumini haohao ambao pia ni raia.
Tumekuwa na Bunge ambalo limeshindwa kuwasaidia wananchi,sasa kanisa au msikiti ukiweza tuwape nafasi waufahamishe umma waelimishe umma ambao kwa muda mrefu umedanganywa sana na wana siasa.
 
kwa wakatoliki inashangaza kwa sababu wao wenyewe hawana mfumo wa kuchaguana.sasa hiyo democrasia wanaijuaje wakati wao wenyewe hawana ndani ya dini yao.Huu ni unafiki Hata hivyo nadhani tatizo ni serikali kwa sababu ilitakiwa kutolewa kauli ya kukemea hilo kwani viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa ni kuhatarisha amani ya nchi wao wahubiri neno la mungu.ya kaisari wamuachie kaisari.

Mkuu kwa wale wanaosoma Biblia watakumbuka kuwa kunakipindi manabii wa Mungu walitumwa kukemea watawala wabovu,nijukumu la viongozi wa dini kukemea tatizo kubwa tulilokuwa nalo viongozi wa dini walikumbatia watawala wetu pasipo kukemea maovu katikati ya jamii.
Huu ni wakati mwafaka viongozi wetu wa dini waingilie,kwa hilo siyo kwamba wanaingilia shughuli za serikali.
hatuwezi kuendelea kuona uozo unaendelea na hasa walevi wa madaraka na wezi wa rasili mali ya taifa na tukae kimya eti tunaingilia serikali
wakati wa kuamka ni sasa.
swala la udini linakuja kama hujiamini,watu wanaoamini kuwa imani yao ina nguvu hawana sababu ya kuipigania kwani inauwezo wa kujitetea bila kupiganiwa.
 
Endapo waraka huu, wangetanguliya kuutoa Waislamu, what would had been Christain respond?
 
nimekupata mkuu
lakini je hawa viongozi wa kidini wanaweza kukaa pamoja????????

huwa nadhani Maaskofu wa kikatoliki wana confidence wanaweza kukaa na yoyote, pia baadhi ya masheikh hawana shida. sijui wengine hasa wa makanisa ya pentekoste (deci) kama wanakubali? maana wanazidi kutengana kila kukicha na kunyang'anyana wafuasi


Nakubaliana na wewe mkuu, kwani hata mimi ni mpentecost!

Ila sijajua kuwa unasema wananyang'anyana wafuasi sijaelewa hwa ni watu au matunda?? kama ni watu na akili zao hujawatendea haki, bado huko nyakati zile za ujima. Kwa nini wameondoka huko? na kwa nini kila siku wanaondoka, kwa nini hawa watu ni dynamic?

1.Kuna wafuata upepo
2.Kuna wafuata kweli ya Mungu
3.Kuna wafuata miujiza na uponyaji, wakisoma biblia zao zina waambia vitu hivyo ni possibe wakija kwenye real life na wachungaji au mapadre wao 'hamna kitu'

4.Kuna critical thinkesrs waliowaza na kufikiri kuwa walipo sipo wanatakiwa wapate kitu fulani mahali fulani.

Then kuna mawili inawezekana wewe usiyehama wala kuwa dynamic ndio mbumbumbu kabisa hujui uanzie wapi huko gizani ila unajiona unaona!, au ndio umeridhika na hali hiyo ili mradi unajua kubaya, au ndio unashindwa kutoka kuogopa ndugu na majirani...yote possible!
 
Endapo waraka huu, wangetanguliya kuutoa Waislamu, what would had been Christain respond?

Hilo ndilo tatizo ndivyo tulivyo kituo kikubwa.


si-support hii hali, ila ina impact yake. sijajua kuamka huku kwa hawa wakatoliki na hawa jamaa wengine kumetokna na uislamu kutaka sana kuingia serikalini? OIC , mahakama ya kadhi imewaamsha sana hawa jamaa. Na kwa taarifa yenu wakatoliki wazuri sana kwa secret agencsies hili ni zaidi ya kanisa. hivyo mjue kuwa mnapotaka ***** ***** wakristo wakikaa kimya ni hatari zaidi.


Pili haya madini yenu ya ukristo na uislam wengi wenu ni mafisadi, hamna lolote mtakalosema ambalo linawatisha serikalini -HAMNA , kwa hiyo wewe Mkamap na Mtwike msijifanye kuwa waislam wangesema wakristo wangesema nini.

Mafisadi wakubwa ni hao hao mashekh , mapadre na wachungaji, kwa kifupi taasisi za dini zingekuwa makini na serious tusingekuwa na hali hii, note this; huo waraka HAUMTISHI MTU YEYOTE,LOWASSA MTU WAO, JK WAO n.k, HATA WANGEANDIKA MASHEKH HAMNA KITU PIA WOTE NYIE NA MAKANISA YENU NA MISIKITI YENU NI MAFISADI WATOAJI WAKUBWA WA SADAKA WENGI MAFISADI NA WACHUNGAJI WAO WANAWAJUA! WAJENGA MISIKITI WENGI MATAJIRI NI MAFISADI MASHEKH MNAWAJUA!

KWA KIFUPI DINI HIZI MBILI NGULI LENU MOJA! HAKUNA VITA YA KIDINI WALA MIFARAKANO YA KIDINI TZ, WOTE WASANII SANA SANA WANACHOSHINDANA NI NANI ANAPIGIWA MAKOFI

KULIKO WENGINE!

Okokeni Yesu anawapenda
 
si-support hii hali, ila ina impact yake. sijajua kuamka huku kwa hawa wakatoliki na hawa jamaa wengine kumetokna na uislamu kutaka sana kuingia serikalini? OIC , mahakama ya kadhi imewaamsha sana hawa jamaa. Na kwa taarifa yenu wakatoliki wazuri sana kwa secret agencsies hili ni zaidi ya kanisa. hivyo mjue kuwa mnapotaka ***** ***** wakristo wakikaa kimya ni hatari zaidi.


Pili haya madini yenu ya ukristo na uislam wengi wenu ni mafisadi, hamna lolote mtakalosema ambalo linawatisha serikalini -HAMNA , kwa hiyo wewe Mkamap na Mtwike msijifanye kuwa waislam wangesema wakristo wangesema nini.

Mafisadi wakubwa ni hao hao mashekh , mapadre na wachungaji, kwa kifupi taasisi za dini zingekuwa makini na serious tusingekuwa na hali hii, note this; huo waraka HAUMTISHI MTU YEYOTE,LOWASSA MTU WAO, JK WAO n.k, HATA WANGEANDIKA MASHEKH HAMNA KITU PIA WOTE NYIE NA MAKANISA YENU NA MISIKITI YENU NI MAFISADI WATOAJI WAKUBWA WA SADAKA WENGI MAFISADI NA WACHUNGAJI WAO WANAWAJUA! WAJENGA MISIKITI WENGI MATAJIRI NI MAFISADI MASHEKH MNAWAJUA!

KWA KIFUPI DINI HIZI MBILI NGULI LENU MOJA! HAKUNA VITA YA KIDINI WALA MIFARAKANO YA KIDINI TZ, WOTE WASANII SANA SANA WANACHOSHINDANA NI NANI ANAPIGIWA MAKOFI

KULIKO WENGINE!

Okokeni Yesu anawapenda

Mkuu vipi tena!!
Fuatilia uone tangu mwanzo nimesema nini,duu taratibu ,mimi nimesema Tanzania na hata Afrika nzima hakuna mtu mwenye udini,kinachogomba kwa kawaida ni ROHO MBAYA TULIOJALIWA.

Watanzania wanapinga ajenda nzuri kwa misingi ya roho mbaya wanayoificha nyuma ya kundi fulani na kuendeleza ule mwendelezo wa sisi ndivyo tulivyo.
 
Hivi tatizo hasa linalosababisha haya yote liko wapi; liko kwenye content ya waraka wenyewew au liko kwenye waraka kutolewa na kanisa (katoliki)?? Nakiri kwamba sijausoma waraka wenyewe, lakini kutokana na maoni yanayotolewa hapa na baadhi ya watu naona hawajadili content badala yake wanona noma waraka kama huo kutolewa na kanisa. Je, waraka ni controversial kiasi unawagawa watu kidini na kuhatarisha umoja wa kitaifa? Sidhani kama hivyo ndivyo. Kama waraka unatoa yu elimu ya kawaida kwa wananchi kutambua wajibu wao katika kufanya maamuzi wakati wa uchaguzi, kuna ubaya gani? Ungekuwa umetolewa na REDET ingekuwaje? Kama controversy inaletwa na suala la mahakama ya kadhi na OIC, mbona haya maswala yamekuwepo toka muda mrefu na yamekuwa yakizungumzwa na kujadiliwa, na makanisa wameshatoa matamko yao?
Mi nadhani kuna watu wanaona tatizo liko kwenye waraka kutolewa na kanisa, hawaoni kama kanisa linafaa kutoa tamko la wazi kuhusu civic education. Watu wanadhani kanisni kanisa (au dini kwa ujumla) hazipaswi kuzungumzia civics kwa ujumla. HIYO NI WRONG PERCEPTION! Mara nyingi utawasikia hata wanasiasa wananukuu kimakosa msemo wa Yesu kwamba "...ya Mungu mpeni Mungu, na ya kaisari mpeni kaisari," kumaanisha kuwa kanisa halipaswi kuzungumzia siasa. Alichomaanisha Bwana Yesu ni kuwa, wakristo wana double responsibility - kwa Mungu na kwa Kaisari. Yale yanayomstahili Mungu wampe Mungu (kumwamini, kumwabudu, kumtukuza, kumtolea sadaka nk), na yale yanayomstahili kaisari wampe kaisari (kumwombea, kumshauri, kumkosoa, na kumpa heshima anayostahili kama anatimiza wajibu wake). Yesu Kristo hakumaanisha kwamba wakristo wanawajibika kwa Mungu peke yake.
Kwa mantiki hiyo, mi nalipongeza kanisa kwa kutimiza wajibu wake wa kutoa elimu itakayowasaidia wananchi kufanya maamuzi ya busara katika uchaguzi. Dini nyingine pia zinapaswa kufanya hiyo. Tanzania ni yetu sote, hatujawabinafsishia wanasiasa pekee. Ni jukumu letu sote kufanya kila linalowezekana kuiendeleza nchi yetu. Kwa pamoja tunaweza.

UMK.
 
Dini ni kioo cha Jamii, sioni udini kwenye waraka huu. Viongozi wetu ambao ni sehemu ya dini hizi wamekufa hawana hamasa ni wezi na hawajali jamii wanaoingoza. Mwizi mkubwa Ben Mkapa kanisa lilifikiri ni mtu safi kageuka kuwa Jambazi mwanae Jk kasahau kuhudumia wananchi kageuza shingo, hawa wote wamewakilisha dini zote, sio mkristo, muislam au mpagani anaweza simama akasema maisha yake ni bora kwa sababu ya raisi mwenye dini sawa na yake au kiongozi yeyote. Viongozi wetu hawaibi kwa misingi ya dini zao bali kukosa maadili na utu wa kibinadamu.

Wezi kama Mkapa,Yona, Mramba, Mkono, Warioba, Pinda nk ni wakristo na Rostam, Jk, Karamag, Msabaha, Idrisa, nk niwaislam na Kingunge ni mpagani sasa hapa tunaona tatizo.

Na wote tunaathirika na utawala wa hawa wezi sio mkristo au muislam au mpagani. Sote tumekalia moto. Kama yupo shekh amabaye kweli akiwa rais atafuata dini inavyosema na kukataza wizi na kuhudumia wahitaji na akafanya hivyo kweli hivi viwaraka havitakuwepo tena. Au akitokea kiongozi mkristo akawahudumia watu kutokana na imani yake bila ubaguzi na akakemea kweli na kushughulikia ubadhirifu bila woga na wananchi wote wakafaidi matunda hivi viwaraka visinge kuwepo.

Hivyo tunapoona maelekezo ya dini yeyote hayafai tukatae ujumbe husika je walichokisema ni pumba au kweli kina manufaa kwetu sote? nani ambaye anafaidika na utawala dhalimu uliopo? je sio sisi wananchi tunatakiwa kuwa mstari wa mbele wa kutetea maslahi yetu.

Dini ndizo zimetumika duniani kote kuleta haki na utawala wa sheria hasa pale serikali iliposhindwa, rejea USA Martin luther na Voice of Islam Lois Farakan . Rejea South Afrika Des Mond tutu. Rejea uhuru wa watanzania Muislim harakati. Kwa hiyo tunaona dini zilivyokuwa mstari wa mbele kudai haki.

Kwa hiyo hatuwezi kuficha nyuso zetu serikali zetu zimeshindwa kufanya kusudio ni lazima viongozi wa dini waislam na wakristo kuamka na kupambana na udhalimu na kuleta mwanga mpya kwa waumini wao na taifa.

Akitokea kiongozi anayejua nini waumini na wananchi hawapendi tunaweza kuendelea, viongozi wa sasa hawamwogopi Mungu hivyo hawawezi kuogopa wananchi, wanaiba mpaka siku yao ya kufa hawa sio watu ni wanyama.

Tujadili yaliyomo sio mwandishi je yanamanufaa kwetu??
 
Hayo mamlaka uliyojipatia ya kunichagulia cha kuandika hapa yaishie hapo kwenye kibodi yako ......... Asante.







Waafrika ndivyo ....... kila mara .... kila mwaka .....bila kubadilika ....

Naweza kuwa mwafrika lakini siko kama ulivyo. Unatishia kivuli? Hunifahamu na mimi sikufahamu na zaidi sihitaji hata kukufahamu. kujaribu kuja na lugha na lugha kali haitakusaidia. Amri kama hizo peleka nyumbani kwako.
 
Kwani nyie mnalalamika kuhusu kanisa katoliki Tz hamjui ndo linaloongoza dunia? Ujue MAFI ndo wanaoongoza dunia so msilaumu tz sana hili ni tatizo la dunia, watanzania tusije kutukanana na kulaumiana, hata wazungu wanajua nn kanisa katoliki sasa ss second user tunatoana nishai bure, Serikali lazima itishike inaposikia viongozi wa kikatoliki wanatishia suala fulani. I beg my tz brothers tuthamini utanzania wetu Kanisa linatimiza maagizo ya Rome wala si kwa manufaa ya Mtanzania, wake up jamaniiiiiiiiiiii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom