Uchaguzi 2020 Wapinzani mnatambua kabisa Rais Magufuli ni mtendaji, mchapa kazi na mtekelezaji mzuri. Bado hamuoni aibu kuchukua fomu za urais!

Ndugu zangu watanzania wazee kwa vijana wababa na wamama mimi nawapa siri moja tu uchaguzi wa mwaka huu 2020 twende na Dr Magufuli. Huyu ndie kiongozi wa kweli atakaye tufikisha nchi ya ahadi nchi yenye maziwa na asali.

Kwa miaka mingi watanzania tumekuwa na siasa zakuwekewa masinia ya ubwaubwa siku za uchaguz na mwisho tumekuwa na shida kubwa na kuwa omba omba ndani ya taifa letu wakati wageni wakivuna asali yetu na maziwa yetu nakuwa ma trilionea kipindi hiki imekuwa tofauti sana sasa tumeanza kuambiana ukweli na kutambuwa kumbe tulikuwa tuna nyonywa na wasio julikana.

Ukiniuliza siri yakukatika umeme na kuwa na mgao ndani ya taifa hili kwa tawala zote zimepita nitakujibu jibu moja tu upigaji watu walizima umeme ktk kipindi fulani nakufanya tanzania kuwa mnunuz wa generator fakes namwisho kuwa na maisha magumu ila kupitia idara zetu nyeti na Rais wetu Dr Magufuli miaka mitano inakata hakuna kukatika umeme jiulize why? Hii ndio Tanzania

Taifa hili tulifika mahali pabaya watu walikuwa wazembe hawafanyi kazi na ofisi zilikuwa kijiwe cha mipango kuihujumu serikali mh Rais alipo ingia madarakani hiki kilikuwa kipaumbele cha kwanza kurudisha nidhamu ktk ofisi za serikal na taasisi zake leo nyote mnakubali kuna a big change.

Kuna jambo na penda nisiwafiche vyama vya upinzani kupitia wagombea wao nia yao sio njema kwa taifa hili na kama ni njema basifungueni masikio muwasikilize vizuri hawa nia yao nikutujaza ujinga ili tuwe watumwa ndani ya taifa letu while wengine wanakula maisha.

Ndugu zangu nikweli ajira ni ngumu sana hiki kipindi ila nataka kuwaambia vijana wenzangu tokeni huko mliko jificha njooni muone tanzania huku mikoani jaman nchi hii ni ya maziwa na asali huitaji ajira ya serikali kuwa tajiri na mh Rais ndio anataka wanazuoni tukijuwe mm nilidhani kama taifa kupitia Rais wetu mpendwa tungekuja na hoja yaku anzisha mfuko maalumu kwa mitaji ya vijana walio maliza vyuo tuanzishe ajira zetu jamani waindi na waarabu mnawaona huko Dar wanakula maisha wana biashara kubwa huku mikoani asiwadanganye mtu ukienda kwa muhindi yeyote mkweli atawaambia nani ametuloga?

Mtu kama Lisu anakuja kushindana na Magufuli hivi nani kinamuingia kichwani kiufupi najuwa akifika ktk ardhi ya Tz ana kesi nzito zakujibu. Kama amesahau clips zake watamsikilizisha kwenye safe house. Huyu ni msaliti na akuna asie juwa ametumika na wapiga deals na ndio maana siku zote alikuwa mtetezi wa kampun za madini zilizo kuwa zinatupiga.

Mzee Membe mimi binafsi sijuwi nini kimemkuta mtu alie shika nyadhifa kubwa ktk taifa nakusomeshwa elimu nzito za kiusalama. Nadhan haya ni moja ya top secret siwez kuyaongelea ila pia naye hatufai why hatufai anaonekana ana agenda yake time will tell us.

Ndugu zangu twenden na Dr John Pombe Magufuli. Asie sikia lakuambiwa uvunjika guu chaguwa kusikiliza wasaliti au wazalendo wa kweli.

Kasi ni ileile Magufuli ndio baba lao.

Kidumu Chama cha Mapinduzi
 
Una maslahi binafsi na madaraka ya Magufuli, lazima uje na ngonjera hizi ili watoto wako waende choo.
 
Kupitai Rais Magufuli hatimaye Chama, Serikali na Nchi imetulia na inafuata maadili.

Hongera JPM kwa hili

Una maslahi binafsi na madaraka yake, hivyo hizi ngonjera ni sehemu ya mrejesho wa mlo wako.
 
Una maslahi binafsi na madaraka yake, hivyo hizi ngonjera ni sehemu ya mrejesho wa mlo wako.

Mleta mada ameshikishwa akili. Hivyo Lumumba imempa buku ngapi kujiaibisha hivi kwa manufaa ya tumbo!!
 
Nimetoka kumsikiliza chakubanga akihojiwa Azam - UTV. Anasema wameimarisha sana matumizi ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kampeni.

Naamini hata posho yenu itakuwa si buku saba tena. Nawapa kongole jingalao na wenzako wote kwa kuhamia kwenye uchumi wa kipato cha "lower - middle".
Nilikuwemo JF kabla ya PolePole Kujiunga Rasmi CCM. Rejea kwenye hoja fikirishi.
 
Hivi kuna sheria yoyote inayomlazimisha kila mtu kusifia mtu anapofanya jambo zuri? Me nadhani wananchi wangeachwa waamue kwenye sanduku la kura kwa uhuru kabisa bila mizengwe ndio itafahamika.
LUMUMBA wana mihemko isiuojulikana inatoka wapi, Wanasema mgombea wao anakubalika lakini wanaogopa Asipambanishwe na mtu yeyote.

Chama chote Wamekuwa kama MAZEZETA. Wametengeneza KINYAGO wenyewe kimegeuka kuwa KIJI mungu Chao.
 
Exactly, hata wajinga na wapumbavu pia huzeeka hapa mkubwa umenena vyema hasa kwa sisi walimu
Ongezeko la umri liendane na kukua kwa akili na mwili.Unaweza kuongezeka umri, ukafikisha hata miaka 65 lakini ukawa "bichwa-maji",and that's you literally.
 
Wapo wapi akina kamuzu Banda, Robert mugabe, Elbashiri, chiluba, Bokasa, Gadafi, Sadam Hussein, mabutu, Abacha, idd Amin Dada? hakuna mabaya yasiyo na mwisho na mwisho wa ubaya ni Aibu kubwa.

sidham kama mna justifications zenye mashiko kiasi cha kwamba hizo point znaweza kua critical sana, watu wana chuki binafsi ambapo mwisho wake ni mbaya, mpaka sasa cdm hakuna any justification ya cdm ambayo ina mashiko kweli inahusiana na magu, kama swala ni lissu hakuna any justification pia maana inawezekana cdm wenyewe wanahusika, na pia unavosema wako wapi hao watu kaa ukijua pia hata wewe mwisho wako unaweza kua mbaya na unaedhan sie akawa na mwisho mwema
 
Mimi CCM lakini uchaguzi Ni lazima kikatiba hata wakati was chama kimoja kulikuwa na uchaguzi vipi wewe.labda wewe ndiyo hufikiri au hujui.
 
Kuna tatizo la kufikiri kwa kutumia akili za kawaida ndani ya vyama vya upinzani hapa Tanzania. Sababu kwa akili za kawaida tu unaweza kupata uthubutu upi wa kupambana na rais kama Magufuli?

Chama Cha Mapinduzi kina misingi imara na thabiti ambayo kimekuwa kikiisimamia tokea kuanzishwa kwake. Na moja ya misingi ni usawa na haki kwa wote. Kwa ujumla kwa CCM binadamu wote ni sawa.

Mwaka 2015 alipopewa ridhaa ya kuwa mgombea wa CCM ni dhahiri kuwa CCM ilimpa kazi ya kutekeleza mambo muhimu kwa watanzania.
JPM ametekeleza mambo makubwa kwa muda mfupi na hii ni kwa sababu anaongoza kwa kufuata misingi ya CCM.

Aliahidi atajenga SGR kipande cha kwanza Dar to Moro kitakamilika hivi karibuni. Aliahidi kujenga JNHPP na ametekeleza na mradi huu ukikamilika utakuwa na manufaa kwa watanzania wote. Aliaahidi kuimarisha sekta ya afya na elimu na yote watanzania wameshuhudia nini kimefanyika.

Kwa ujumla Tanzania ina rais mchapa kazi ambae akiahidi kitu kwa manufaa ya watanzania lazima atekeleze.

Sasa vyama vya upinzani kama Chadema ambavyo hata kuongoza majimbo na kata ni tatizo inakuwaje wanathubutu kuchukua fomu na kutaka kuweka mgombea wa kupambana na rais kama Magufuli?

Chama kama Chadema ambacho hakiwezi kusimamia ruzuku ya ya mil 360, kitaweza vipi kuwa na rais ambae atawatekelezea maendekeo watanzania?
Kumbe chai ya baridi inalevya hivi
 
angeruhusu na yeye apate changamoto kidogo ya ndani ya chama nahisi angekua ni moja ya raia wanaopepewa na kupumulia mashine ICU
 
Back
Top Bottom