Hayati Magufuli aliona bora awavalie miwani ya mbao afanye kazi, wapinzani wakamuita ni dikteta, Rais Samia piga kazi tusizidi kuchelewa

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Friends and Enemies,

JPM Marehem, alikuwa ana Msemo wake pendwa ''Turichereweshwa Sana'' na hawa wanaojiita wanademokrasia na watetezi wa Haki za binadamu,nakumbuka pia katika suala la mradi wa bwawa la Nyerere alizungumza pia kuwananga wale waliokawa wanampinga katika mradi ule Kwa hoja ya uharibifu wa mazingira.

JPM alikuwa anawajua Kwa undani wapiga madili na wezi ndan ya nchi hii hawawez acha kupiga kelele na kupotosha wananchi hasa pale wanapoona mianya yao ya kuiba inazibwa au pale wanapoona kuwa serikali imeamua kufanya maamuz mazito Kwa maslahi ya nchi.

Siyo vibaya kukosoa na kutoa maoni na Wala siyo dhambi ndani ya Taifa letu,ni Haki kabisa ya kikatiba na kila mwananchi ana uhuru katika Hilo,ila je kwanin baadhi ya watu wapotoshe umma wa wengi Kwa maslahi Yao binafsi??

Ukikaa na kuwasikiliza hao wanaojiita wanasheria wasomi mwabukusi na wenzake unaona kabisa ni watu wenye mihemko inayoondeshwa Kwa Njaa na chuki.

Maelezo ambayo watu kama Hamza Johari wameyatoa kuhusu suala la mkataba wa DP World yamezid kuwaacha uchi waganga Njaa hao kias kwamba inapelekea mtu uwaze kwamba hasira zao zoote zile na kauli zao za kashfa, dhihaka na chuki Kwa serikali kiasi Cha kufikia hatua ya kusema serikali inauza bandari na wameshindwa kuongoza nchi yapo nyuma ya nguvu Gani haswa wanaoitegemea?

Ukiwasikiliza na kuwatazama usoni wakizungumza unaweza dhania kuwa hawa ndiyo haswa wazalendo kweli kweli wa Taifa kumbe ni waganga Njaa na wapotoshaji.

Kwenye masuala ya msingi yanayohusu maslahi ya Taifa kama haya ya uwekezaji wanathubutu vipi kuingiza siasa uchwara na upotoshaji wa kuligawa Taifa?

JPM Marehem, alikuwa anajua fika kuwa waganga Njaa kama hawa ndan ya Taifa hili wapo wengi,na Hususan unapotaka kusonga mbele katika kuleta maendeleo lazima watasabotage Kwa maslahi Yao huku wakijifanya kuvaa vazi la uzalendo,na ndiyo maana alikuwa hawapi nafasi na ikibid alikuwa anawazimisha Kwa maslahi mapana ya Nchi.

Sikuwa muumini wa siasa zake lakini inafikia wakati inabidi ukubali kuwa kumbe alikuwa anafanya vile Kwa sababu ya watu wa sampuli kama hii tunayoiona sasa.

Uhuru wa kujieleza umerudi na watu wako free kuzungumza lakini umepitiliza sana kias kwamba waganga Njaa wanajisahau na kuongea lugha za reja reja Kwa Kiongoz wa nchi na serikali bila wasi wasi wowote huku wakijua fika kuwa hawakuwa na nafasi kama hiyo miaka miwili iliyopita.

Rais Samia Kazi iendelee,wapiga kelele na waganga Njaa wapo,walikuwapo na wataendelea kuwapo katika nchi hii, Wilbroad Slaa anakuja mbele ya kamera Leo na kusema kwamba Rais aache kuteua machawa kama Msigwa kwani wanakula Kodi zetu za bure,Msigwa ni mteule wa Rais tokea zama za JPM kwanini wakati ule alipopewa ubalozi hakuthubutu kumwambia JPM ampige chini huyo Msigwa ambae yeye Leo anamuona chawa pale anaposimama kuisemea serikali?

Mara ooh bandari imeuzwa, bandari imeuzwa, Zanzibar mbona haipo kwenye mkataba kama huku bara,why wasiseme pia kwanini Mtwara pia haipo kwenye mkataba pia?

Wamesema wanataka kuhamasisha watanzania waingie barabrani kuandama,waanze hivyo mara Moja tuone,maana hizo kelele zao za kwenye vyombo vya habari na mitandaoni hazitawapeleka popote.
 
ukiendekeza kuwasikiliza wabongo hutofanya chochote, unachotakiwa ni kanyaga twende.

Hakuna Rais ambaye hajawahi kulaumiwa kwa jambo lolote alilo lifanywa, awamu zote zimewahi kulaumiwa lakini kamwe hawakurudi nyuma.
kazi iendelee kamwe tusirudi nyuma.
sisi wananchi tupo pamoja na Rais na Serikali kwa ujumla.
 
Shujaa Magufuli alikuuwa Mtu mwema sana na alichofanya katika Utawala wake ni Sawasawa na Yesu alivyopindua Meza za Walanguzi na Wahuni pale Hekaluni 😀😀

Mufti Zubeir, Shehe wa DSM alhad Musa Salum na Kardinali Pengo walimkubali Sana

Nawatakia Sabato njema!
 
Ukiwa dereva usisikilize abiria fanya vile unajua.

Magufuli alikuwa mwamba sana hawa waporokaji alikuwa anawabinya kimtindo wanakaa kimya,wanasiasa wengi ni kuleta hofu kwa ajili ya maslahi yao.

Kila kitu ni kik wameachana na katiba mpya wamehamia huku😂😂.
 
Unaanzaje kulinganisha mtu na kivuli?

Sifa moja wapo ya JPM ni kuzitungia sheria maliasili zetu zote ili ziwe chini yetu sote, na sifa ya serikali iliyopo, ni kupeleka mswaada wa kutangua sheria zote zinazolinda maliasili zetu ili ziwe za wachache!

Nauliza hapo nani anastahili sifa ya u Rais?
 
Mama nimemshauri atumie style ya magufuli bila hivyo hawa kenge watampeleka peleka sana naona kaanza kunielewa huko mbeya eti kuna wakina mdude wa chadema eti wameenda kumsindikiza mambuzi polisi ninefurahishwa nao wamekamatwa wapo lupango. Hii nchi ukiruhusu siasa zilizozidi unaharibu.
 
MKuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya kazi gani kwa Tanganyika labda kuuza loliondo. JPM angeweza kusaini IGA kama hii?

Umeme, maji kuwa adimu. Kuchagua viongozi vilaza, watupu kuingia mikataba ya hovyo.
Hizi chuki zako tu sisi mama katuboreshea sana huduma za afya , shule, vyuo vya kati na elimu ya juu. Maji , barabara pamoja na maslahi ya watumishi wa umma
 
Ukiwa dereva usisikilize abiria fanya vile unajua.

Magufuli alikuwa mwamba sana hawa waporokaji alikuwa anawabinya kimtindo wanakaa kimya,wanasiasa wengi ni kuleta hofu kwa ajili ya maslahi yao.

Kila kitu ni kik wameachana na katiba mpya wamehamia huku😂😂.

Inashangaza hata wale Covid 19 wamewasahau kabisa.

Na usikute hata ruzuku wanachukua kimya kimya.
 
MKuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya kazi gani kwa Tanganyika labda kuuza loliondo. JPM angeweza kusaini IGA kama hii?

Umeme, maji kuwa adimu. Kuchagua viongozi vilaza, watupu kuingia mikataba ya hovyo.

Unaonaje basi uteuliwe wewe uwe waziri Mkuu wa Nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom