Wapambanaji watazamaji...

Naomba katika kufuatilia tuweke makundi mawili:

a. Wanaotaka JF&KLHN iendeshwe kwa michango ya hiari:
-
-
-

b. Wanaotaka JF&KLHN iendeshwe kwa ada ya mwezi
- Kitila Mkumbo
-
-
-
c. Wanaotaka JF&KLHN viendeshwe kwa hiari na ada (huna haja ya kujiandika kwenye orodha ya a au b)

-
-
-
-
d. Wanaotaka JF & KLHN viendelee kuwa vya bure na wamiliki na waendeshaje waendelee kujitolea kubeba gharama hizo kwa manufaa ya Taifa.

-
-
-
-

Haya karibuni kujiorodhesha.
 
1.

Mkuu ninaomba nirudie kwenye hili kuwa Mwanakijiji sio John Mashaka, ninaongea nao wote wawili kwa simu kwa wakati mbali mbali, John yuko Wachovia Bank North Carolina ana kazi inayomfanya asafiri all the time between US na Europe, hata muda wa kuingia kwenye internent huwa hana, kwa hiyo tafadhali rekebisha hilo Mwanakijiji sio Mashaka,

2.

Kuna ishu zinazohitaji maneno mengi na kuna ishu ambazo ni black and white, hazihitaji maneno mengi,

kwa mfano fulana za JF ziwe rangi gani yes hapo panahitaji maneno mengi sana, lakini mchango wa kuiweka JF hapa na KLH, kweli kunahitajika maneno mengi? No ni kutoa au kutotoa na ikibidi kunyamaza kimyaaa na kuendelea kupiga keyboards, au!
Kwa hiyo kichwa cha habari kilitakiwa kiseme either changa ama piga kimya?
If thats the case then shukran kwa taarifa coz nildhani michango ya kimawazo pia ni accepted!
Once again thanks for the info na kwa kweli now nitakuwa kimya!
 
MKJJ: This is really movingly inspirational!

Nami pia nawapongeza sana wale wachache kabisa katika kundi la watu zaidi ya 5000 ambao wamekuwa wakijitoa mhanga ili kuhakikisha JF inaendelea kuwepo. Nafikiri kuna haja, kama hao wandugu wataridhia, siku moja uwataje hapa ili tuwape shukrani zetu moja kwa moja ili kuonyesha unyenyekevu na appreciation yetu kwao.

Nina mambo matatu mahsusi ya kuchangia katika mada hii:

i)Niliwahi kusema huko nyuma na ninasema tena kuwa hapa ilipofikiwa JF imekuwa kubwa mno. Kwa ukubwa wake, ni muhimu sana ikajibadilisha namna inavyojiendesha. Ili JF iweze kuendelea kufanya mambo mazuri na ifike mahala ifanye mambo makubwa, na kutimiza hio dira ambayo MKJJ kaieleza vizuri sana katika makala yake, ni lazima sasa ijiweke kitaasisi badala ya kuendelea kutegemea nguvu za watu hao wachache aliowasema. Tatizo moja la nchi yetu ni kushindwa kuimarisha taasisi. Ukiangalia matatizo yote tunayoyaongelea hapa, likwemo la ufisadi, chanzo chake ni kimoja tu nacho tu ni udhaifu wa taasisi zetu. Mafanikio ya nchi yetu siku zote tumeyaacha kwa mtu mmoja moja. Kwa hivyo ilipotokea huyu mtu mmoja akawa dhaifu ilibidi nchi nzima iyumbe. Kwa hiyo, kwa mfano, baada ya mwalimu Nyerere tumejikuta tumeshindwa kusimama kwa sababu mafanikio yetu yote yalijengwa katika yeye mwenyewe na sio katika taasisi zetu. Kama tutaendelea kuiacha JF ijiendesha kama ilivyo sasa, yaani kwa kutegemea nguvu za mtu moja moja, tusitarajie ikue sanaaaa kama tunavyotaka na ikitokea ndugu zetu akina Mac na Mike wakapata kitu kingine ambacho wataona ni cha maana zaidi kuliko hiki huo ndio utakuwa mwisho wa chombo hiki mahsusi. Na ukweli ni kwamba mifano tunayo. Walipokamatwa ilibidi JF ipotee na tukaanza kuhangaika. Kama JF ingekuwa taasisi kipindi hicho, ingeendelea kusimama na kupiga kelele ili viongozi wake waachiwe. Tulikuwa na bahati kwamba kulikuwa na KLH News iliyotupasha, vinginevyo tungekuwa tumeliwa. Sitakuja kusahau pia jinsi BCS ilivyotutenda. Hiki chombo kilifika mahala kikatikisika nchi. Lakini mmiliki wake aliamua kubadilisha biashara akajiunga na CCM na kugombea ubunge ndio ukawa mwisho wa bcs nasi sote tungasambaratika hadi ndugu yetu Mac na mwenzake walipokija kutukutanisha tena. Ndio kusema siku Mac na mwenzake watakapobadilisha upepo, siombei hili lakini inawezekana, ndio utakuwa mwisho wa JF. Ndio maana siku zote ni muhimu sana kuwekeza zaidi katika taasisi kuliko kwa mtu moja moja. Yote hii ni kwa sababu ni rahisi sisi binadamu kuyumba na kuyumbishwa kuliko taasisi.

ii)Moja ya ajenda ya JF imekuwa ni kujaribu kukosoa jinsi uongozi wa nchi unavyopatikana na unavyoendeshwa. Tumejikuta kama nchi tunapata viongozi wetu kwa kubahatisha. Hakuna mkakati wowote wa maana wa kuwaandaa viongozi wa nchi na taasisi mbalimbali. Ni kama vile tumeamua kuamini kwamba viongozi huzaliwa na kuna watu waliojaliwa kuwa viongozi na hakuna haja ya kuwatengeneza. Hili ni kosa. Ajabu ni kwamba tunashangaa mtu ni profesa lakini anashindwa kuendesha taasisi. Hatujiuliza huyu profesa aliwahi kupata wapi msasa wa uongozi. Sasa kama tungeiendesha JF kama taasisi ingekuwa ni furaha muhimu sana ya kubadilisha taswira hii. JF ingeweza kabisa kuwa ni tanuru pia la ku-train viongozi wajao wa nchi yetu na taasisi zetu mbalimbali. So far tunaona, kwa mfano, jinsi Mac na mwenzake walivyoweza kuitoa JF from no where to this level; wameonyesha uongozi wa hali ya juu kabisa. Sasa JF ingekuwa ni taasisi maana yake ni kwamba tungeweza kuibua vipaji vya kutisha hapa vya wahasibu, waweka hazina, wenyekiti wa bodi, wakurugenzi, n.k., ambao hao huko mbele ndio watakuwa magavana wa benki kuu. Kama ni ufisadi, tungeanza kuuona mapema kabisa sio kama sasa ambavyo watu wanatustukiza wakishafika huko juu kwa sababu hatukuwajua huku nyuma.

iii)Wazo la kuendelea kuichangia JF kwa hiari ni zuri sana. Hata hivyo michango ya hiari inamatatizo mawili makubwa ambayo msingi wake yote ni uwajibikaji. Tatizo la kwanza, kwa kuwa ni hiari mtu hawajibiki kutoa huo mchango na unatarajia mtu atoe kwa sababu ana roho nzuri. Sasa tatizo la roho nzuri inategemea sana nafasi ya kuwa na ka-surplus fulani. Sio watu wengi wanatoa kipa umbele kwa matumizi ya roho nzuri. Tatizo la pili ni kwamba kwa kuwa mchango ni wa hiari huwajibiki kuhoji matumizi yake na anayepokea huo mchango hawajibiki kutoa mahesabu ya hayo matumizi.

Ni kwa sababu hizi na zingine, ndio maana mimi nafikiri ni muhimu sana kama kweli tunataka hiki chombo chetu kikue tukiendesha kama taasisi ili wanachama wawajibike kukichangia. Na tunaposema wanachama watoe subscription fee sio lazima wote wanaojiunga na JF basi wawe wanachama kwa subscription fee. Utatengenezwa utaratibu wa kuhakikisha kwamba kutokuwa mwanachama wa kuchangia hakumnyima mtu haki ya uanachama wa kawaida wa kusoma na kuchangia mada.

Kwa hiyo napendekeza hivi:
a)Itengenezwe katiba haraka ambayo itaigeuza JF kuwa taasisi. Hapa tuna options mbili:
a.JF kampuni-ambayo itaendeshwa kwa mtindo wa shares. Hii sio option nzuri sana kwa kitu kama hiki maana kitatupeleka kwenye taswira ya kibiashara zaidi kuliko huduma ya habari
b.JF kama association-hii ni option nzuri zaidi maana wanachama wote watakuwa na haki sawa na kwamba itakuwa ni non-partisan and not for profit membership based organisation/association.

Ni kweli kabisa kila mtu anaweza kufanya mambo mazuri, lakini mambo makubwa hufanywa na ushirikiano wa watu wengi. JF imeshafanya na inaendelea kufanya mambo mazuri, inaweza kufanya mambo makubwa kama tukiamua kushirikiana vizuri tukaiendesha kama taasisi. Ikiwa taasisi, tutaendelea kuwajibisha watu katika serikali yetu na sisi pia tutajifunza zaidi namna ya kuwajibika na kujiajibisha!
 
Safi sana Mkuu!
Halafu naona pia umetupa somo la leadership theories kwenye highlight!
 
Naomba katika kufuatilia tuweke makundi mawili:

a. Wanaotaka JF&KLHN iendeshwe kwa michango ya hiari:
-
-
-

b. Wanaotaka JF&KLHN iendeshwe kwa ada ya mwezi
- Kitila Mkumbo
- Gembe
-
-
c. Wanaotaka JF&KLHN viendeshwe kwa hiari na ada (huna haja ya kujiandika kwenye orodha ya a au b)
-
-
-
-
d. Wanaotaka JF & KLHN viendelee kuwa vya bure na wamiliki na waendeshaje waendelee kujitolea kubeba gharama hizo kwa manufaa ya Taifa.

-
-
-
-

Haya karibuni kujiorodhesha.
ila Mwanakijiji Hoja ya Kitila naiunga mkono...soma uone tutafanya vipi??
 
Hili hapa la highlight kwenye ushauri wa Mh Kitila Mkumbo
2. Trait Theories: Similar in some ways to “Great Man” theories, trait theory assumes that people inherit certain qualities and traits that make them better suited to leadership. Trait theories often identify particular personality or behavioral characteristics shared by leaders. But if particular traits are key features of leadership, how do we explain people who possess those qualities but are not leaders? This question is one of the difficulties in using trait theories to explain leadership
 
Ni hoja nzuri sana na yote yanafikirika na kujadilika.

a. Tatizo la kuandikishwa kama taasisi hasa ukiwa nyumbani unakuwa unafungwa na sheria za nyumbani. Na hilo lina implication yake kuhusu uhuru wa hiyo taasisi. Lakini kimsingi it is the more practical and efficien way. Hii naamini ibakie kuwa ndiyo kilele cha morphosis ya Jambo Forum. Sasa kabla hatujafikia huko ambako lazima tufikie kabla ya election year 2010, tufanye nini kwanza? KM nakubaliana na wewe on principle kuhusu hili la Taasisi.

b. Sasa kabla hatujaweza kufikia huko kwenye taasisi ni lazima tuone kwanza kama tunaweza kujisupport au kutengeneza association or a loose network ya wanachama kama ilivyo sasa. Ieleweke zaidi kuwa model za kufanya mambo ambazo zimekuwa zikitawala sana miaka mamia iliyopita zinaanza kuvunjwa na kubadilishwa kabisa na ujio huo wa teknolojia ya mawasiliano. Hivyo, tukijaribu kufikiri nje kidogo ya njia tulizozizoea tunaweza kuwa na kitu gani? Itabidi nipie sheria za NGO...za Tanzania. Vinginevyo wazo la kuanzisha taasisi itabidi lifanyike kwenye nchi ambayo ni more liberal na ambayo inalinda sana uhuru wa maoni na wa habari.

Haya hadi hivi sasa ni wawili tu wamejiorodhesha kwenye suala la ada.
 
I am going with both this and Kitila's
 
Ni muhimu kuwafahisha wanachama gharama halisi ya uendeshaji wa JF na mchanganuo wa gharama hizo

mfano kama unamwambia mwanachama alipe shilingi 10, kwa nini iwe shilingi kumi na si shilingi tano au shilingi ishirini?

haiwezekani ikawa "where we dare talk openly" katika kutoa hoja na kuchangia mijadala mbali mbali lakini isiwe kwa waendeshaji/wamiliki wa JF kuwa na "where we dare talk openly" kuhusu gharama halisi za undeshaji wa JF.

Tupeni gharama halisi za uendeshaji wa JF, kisha ndo mpendekeze uchangiaji uende vipi.
na pia na sisi tuweze kuamua ni aina gani ya upatikanji wa pesa za kuiendesha JF ni nzuri
 
Hivi ni wangapi wanaoenda kununua huduma au bidhaa wanauliza gharama ya kila kitu ili waweze kukinunua? Bei wakati mwingine hupangwa na vitengo vya ndani na factors nyingi that are taken into account.

Tukiamua kupiga hesabu za gharama halisi (actual cost) ya Jambo Forums watu watakimbia hapa. Ndiyo maana binafsi naamini wanachama waone thamani ya JF na wao wachangie vilivyo.

Hata hivyo, nakubaliana na wewe kuwa tunaweza kuweka gharama ya kuendesha JF (total cost) na tuone inagharimu kiasi gani, na pia ili iwe bora ingegharimu kiasi gani.

So, ni wazo zuri kujua angalau kuwapa watu idea. Lakini siamini kuwa ni msingi wa mtu kuchangia au kulipa ada, kwani mimi ni memba wa Detroit Zoo, na walichoniambia ni kuwa kwa kiasi fulani nitakuwa mwanachama wa aina fulani na nitapata faida hii na hii na hii. Lakini sijawahi kuona au kusikia mtu anawaambia society kama Detroit Zoo wamwekee gharama ya kuendesha zoo nzima na walifikiaje fikiaje kiasi hicho ili aamue kuwa mlipaji au mtazamaji.
 
Naomba katika kufuatilia tuweke makundi mawili:

a. Wanaotaka JF&KLHN iendeshwe kwa michango ya hiari:
-
-
-

b. Wanaotaka JF&KLHN iendeshwe kwa ada ya mwezi
- Kitila Mkumbo
-
-
-
c. Wanaotaka JF&KLHN viendeshwe kwa hiari na ada (huna haja ya kujiandika kwenye orodha ya a au b)

-
-
-
-
d. Wanaotaka JF & KLHN viendelee kuwa vya bure na wamiliki na waendeshaje waendelee kujitolea kubeba gharama hizo kwa manufaa ya Taifa.

-
-
-
-

Haya karibuni kujiorodhesha.

Mimi niweke kwenye kundi (c)

Pawe na Ada- na wanachama wachangiaji wa ada wapewe special recognition kama ilivyo kwa premium members na wapewe special access ya ukumbi maalum. Lakini kila mtanzania awe na haki ya ujumla ya kusoma na kuchangia.

Pawe na michango ya hiyari- kwa wenye kupenda kuchangia zaidi ya ada. Lakini michango ya hiyari toka kwa mtu mmoja ama taasisi isizidi dola 1000 kwa mwaka. Kama ikizidi kiwango hicho toka kwa mtu mmoja au taasisi moja basi iwe declared. Hii ni kuondoa possibility ya undue influence.

Otherwise, wakati umefika sasa wa kuhakikisha wanaosimamia JF tunawa-support kuisimamia. Huu mzigo unaelekea kuwa mzito kadiri siku zinavyozidi kwenda. Ni jambo la kawaida duniani kwa talent kama hizi kuwa supported. Kama tuko kuna watu wako tayari kulipa fedha nyingi kutazama wanamuziki ama wacheza soka kwanini tusichangia hii kazi takatifu?

JJ
 
Tangu februari baada ya sakata la JF wanachama zaidi ya 1300 wamejiandikisha; na kama mwendo utaendelea hivyo sitoshangaa tunaweza kufikia watu elfu kumi muda si mrefu hasa kipindi cha bajeti ambacho tumewaandalia mambo manono na matamu toka DDM.

Hivyo mzigo wa MoDs ni mkubwa sana na mambo mengine nayo yanasumbua.

Hata hivyo kuna hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa sasa hivi ambazo zitainua JF to the next level. Vijana wetu Mac na wenzie wanafanya kazi mchana na usiku (bila kulipwa mind you) kuhakikisha ukiamka asubuhi unaikuta JF!

Mnyika mawazo yako mazuri sana... na umenipa wazo la nyongeza pia..
 
MKJJ: You are right. Wakati tukiendelea kutafakari lazima kazi iendelee. Labda kwa kuanzia kwa nini watu/mtu asijitolee apendekeza kamuundo fulani hivi na ada ya kuanzia ili tuanze.

Halafu, tunaweza na kuanza hata na watu watano halafu tunaendelea. Tuliopanda sana mabasi ya vijijini tunajua kwamba kuna abiria wengine huwa hawawezi kuingia kwenye basi hadi lianze kuondoka!

Gamba: haya mambo ya shilingi ngapi nafikiri ni ya logistics. Kitu cha muhimu sasa hivi tukubaliane kwanza principle. Cha kuzingatia hapa ni kwamba tunajaribu kuona the best way ya kuifanya JF iwe sustainable. Matumizi ya hizo hela yanajulikana na yataendelea kujulikana. Lakini ni wazi kwamba tunahitaji fungu la uhakika la kulipia hiyo domain (nyie wataalamu mnajua zaidi). Huko mbele tunaweza hata tukakubaliana kabisa kuajiri some few staff, some on part time wengine on parmanent basis ili kuhakikisha JF inasimama all the time na haikwami kwa sababu za kawaida ambazo zipo ndani ya uwezo wetu. Kama kweli tunaithamini hii kitu tusingependa kuona itapotea kwa sababu ya kudaiwa fee.

Imani yangu ni kwamba through michango ya wanachama (subscription fees) JF itakuwa more sustainable and accountable kuliko michango ya hiari.
 
KM.. right on.. kwa sababu tukianza kuchangia...

a. Tunaweza kulipia gharama za kawaida

b. Inapopatikana ziada na kutegemea na kiasi cha ziada ndipo hatua zaidi za kujijenga zinavyofanyika.

Tutakachoweza kuomba kwa wakati huu ni kuweza kufungua akaunti specifically kwa ajili ya JF. Na wanachama wale waliolipia ndio watapewa mapato na matumizi ya kila quarter na hivyo kuwa updated na fedha zinazoingia n.k n.k

Lakini tukubaliane kwanza kwa mwezi ni kipi kilichobora kuanzia, binafsi naamini kiwe kati ya dola 10-15 kwa mwezi.. halafu tutaona mwitikio wa watu ulivyo. Tusipopata hata watu 100 hivi waliotayari kujicommitt hivyo.. it WILL NOT work.
 
bandugu tufahamu kwamba JF nguzo yake kuu ni waendeshaji/wamiliki kwa kulipia gharama za uendeshaji na Wanachama kwa kujitolea michango yao ya kimawazo.

utakapotwambia sisi wanachama tuanze kulipia ada, ambayo ukikusanya total ya hiyo ada ni maelfu ya pesa kibao kuliko gharama za uendeshaji, tuambiane hizo pesa zinazobaki tunazipeleka wapi?

Hata kama ni chakula kwa waendeshaji wetu,mbona hicho chakula ni kikubwa sana?.kwa sababu nazungumzia mamilioni ya pesa hapa,si pesa kiduchu.

kumbuka mwanachama anachangia mawazo, kisha achangie ada ya uendeshaji ambayo kumbe kimsingi kuna surplus kubwa ambayo inabaki baada ya kuondoa gharama za undeshaji,hii itakuwa ni sawa na mwanachama anatoa pesa kununua mawazo yake mwenyewe na ya wenzake.huku waliokuwa wakiendesha jf wakiwa hawalipii gharama tena bali kukaa mkao mzuri wa kututunzia mamilioni yetu.

kwa maoni yangu ili tuweze kupata pesa za kuiendesha jf(na si mamilioni ya ziada ambayo hatujaelezwa bayana yatafanya nini),tunaweza kutumia mtindo wa kutoa kwa hiyari au tukasema kwamba members idadi kadhaa kutoa kwa zamu, mathalani tunaweza kusema hivi, tuchague members kadhaa wachangie gharama za uendeshaji kwa miezi mitatu ya awali, then kundi jingine miezi mitatu inayofuata, na kundi jingine hivyo hivyo, then mwaka ukiisha tunacycle tena, by the way members watakuwa wanaongezeka kila kukicha hivyo na gharama za michango ziwe zinapungua kulingana na member wanavyoongezeka. bottom line ni kwamba gharama za kweli za undeshwaji wa JF zikifika basi member waliotakiwa kutoa wanaweza kuendelea kutoa au wasitoe kwa sababu lengo la kukidhi gharama za uendeshaji limefikiwa.

My take:tusiigeuze JF mradi wa watu kujitengenezea mamilioni, kwa mawazo na keyboard za Members wenyewe.iwapo wazo la Kitila la Kuigeuza JF taasisi watu wataona linafaa, basi iwe ni Taasisi huru ya wananchi huru, ambayo mapato yoyote yapatikanayo yawe ni kwa ajili ya kutimiza malengo ya JF(kumwamsha Mtanzania),na wala mapato hayo yasiingie mifukoni mwa mtu yeyote zaidi ya taasisi yenyewe
 
Umesikika vilivyo!
 
MKJJ: I think $10-15 kwa mwezi is fair enough. Basi fungueni account maalumu ya JF ili watu waanze. Ninaamini in a couple of months to come tutapata wanachama wasiopungua 50 angalau. Tunajuana humu, tutahamasishana.

Gamba: Mimi bwana nakuelewa sana concerns zako. Inaeleweka zaidi kwa sababu tumeshaumwa na nyoka. Zaidi ya yote, hatutaki tuwape loop holes maadui zetu (mafisadi) waseme eeeh mbona hata hao nao ni mafisadi tu wamekula michango ya wanachama. So, we must be very very careful. Ni bora watu wasichangie kama hawana imani kuliko kuchangia halafu mioyo yao inawadunda na wanafikiri kuna watu watakula mapesa yao. Mimi binafsi nina imani kubwa sana na waendeshaji wa JF na KLH na sioni hata moja atakayetaka kunyanyuka (kama hajanyanyuka!) kupitia michango ya JF. That said, sisi ni binadamu, ni muhimu sana kuweka taratibu very clear from the very beginning in a very transparent way. Again, I don't see how we can achieve this without JF being an institution with a clear set of rules, regulations and procedures.
 
Nakubaliana sana na wazo la J.J Mnyika...Kisha Kitila kafunga mjadala...
MKJJ tafadhali wewe twambie ktk mahesabu ya haraka haraka ni kiasi gani mnataka toka kwa kila mwanachama anayetaka kuchangia tuanze sasa hivi kisha tutazame tuimefikia wapi, kama tutakwama tutatafuta njia nyingineyo...Pengine hilo pendekezo la 2.
Mkuu kama ulivyosema Wabongo inapofikia swala la LAZIMA basi wapo radhi wakachangie site ya Mkenya kuliko ya Mbongo..watakukimbia wengi nawajua..tuna kikorosho fulani cha kusema aaah nitamtajirisha MKJJ..
Mkuu ni mawili toka kwenu nyie wamiliki wa hizi site, kutegemea michango ya watu ama kuibadilisha na kuwa biashara..
Biashara yoyote inayotanuka haraka na kushinda uwezo wa mmliki huuzwa hisa kupanua mtaji na mnunuzi wa hisa hana sauti ndani ya management inayoendesha biashara hiyo isipokuwa yule mwenye majority share ambaye anaweza kuwa ktk BoD..bila shaka watu hao ni nyie wamiliki wa sasa hivi.
Hivyo KLH na JF wote mna viongozi wenu wa ndani na nihawa hawa wataendelea kuendesha tovuti hizi wakipanga malengo ya juu kufikia chombo kukibwa cha habari nchjini kama sio cha kimataifa..Huwezi jua JF ama KLH ninaweza kuwa Yahoo ikatafutwa kununuliwa na magazeti makubwa nchini... who knows.

Kwa hiyo kama mnataka kuendelea kuwa wamiliki kwa kidogo mnachokipata lakini mnahitaji misaada ni jukumu lenu kuweka masharti kama yapo ama kutoweka kwa sababu ninaamini by now you guys mmeisha fahamu undani wa kuendesha shughuli hii iwe non profit ama tofauti.
Sisi tupo na tumesha extend mikono yetu kupokea uamuzi wenu kwani wengine hapa JF ni chakula cha akili zetu hatuwezi kukosa..
 
Back
Top Bottom