Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,261
Kuna mambo makubwa matatu,
Kwanza, matajiri wengi wa Africa wamejipatia utajiri kutokana biashara za uchuuzi tu bila kuhusika katika kufanya mabadiliko ya makubwa ya teknolojia. Hii ni tofauti sana na kwenye nchi za magharibi ambapo matajiri wake wengi wameibuka kutokana na ubunifu mbalimbali.
Pili, kupata utajiri kutumia mgongo wa serikali au viongozi wa serikali. Matajiri wengi wa nchi hizi ambao hugeuka kuwa machawa walijipatia mali za serikali kwa bei chee, wanaongeza utajiri wao kwa kupata tenda za serikali au wanashirikiana na viongozi wa serikali kukwepa kodi.
Tatu, mifumo ya utawala wa kijamaa, Kikomunisti au kidikteta huwa nayo hair hairuhusu watu wengine zaidi wa wanasiasa watawala kuwa na ushawashi mkubwa katika nchi.