Wapambanaji watazamaji...

Wakuu maneno yaliyoko hapa ni mazuri sana na nafikiri imefikia wakati wa kujitoa kweli. Thanks Invisible, Mwana kijiji kwa kutuweka nafikiri katika sehemu zote kuna member wa viwango mbali mbali. Katika hili weka viwango na weka GOLD member, silver member, member nk. Hii iwe kulingana na viwango vya member. Kwa mfano dola 5 kwa mwezi ni member, 10 senior, dola 20 Silver, zaidi awe gold. Wakati huo mnaweza kuongeza credit kulingana na mchango wa mawazo kutoka kwa muusika.

Nafikiri itasaidia sana katika kulipia garama zote
 
sasa wale wanaotoa 5, 10, na 20 wote wana hadhi sawa? Maana kama Gold member anapata kile kile anachopata "member" kuna motivation gani ya kuwa gold memba?

Ukiweka level mbalimbali za membership ni muhimu kuweka level mbalimbali za benefits.
 
Nadhani hakuna haja ya motivation ili kutokuweka matabaka. Kuwe na minimum amount, na kila mtu atoe kadri ya uwezo wake. Ila hiyo minimum amount iwe in such a way kiasi kitakachokusanywa kifikie malengo ya kucover at minimum basic costs na contigency...so kisiwe chini ya $15 (kwa mwaka may be????)
 
Mkuu

Ukisha tofautisha unaweka kila kitu huwezi kuwa member ukawa sawa na gold. Gold anaweza kunusa hata taarifa ambayo haijatoka mkuu. lakini vile vile tuwe makini hapa tujue kwamba siyo kila Mtanzania mwenye utaifa anaweza kuwa na kiasi kikubwa sana. Tufikirie kwamba kuna wengine watapenda kuona wako juu kidogo. Unaweza kuongeza kima cha chini hili kupata kufikia malengo yetu.

Lengo liwe katika mission na Vission ya JF, itasaidia sana.
 
Nadhani hakuna haja ya motivation ili kutokuweka matabaka. Kuwe na minimum amount, na kila mtu atoe kadri ya uwezo wake. Ila hiyo minimum amount iwe in such a way kiasi kitakachokusanywa kifikie malengo ya kucover at minimum basic costs na contigency...so kisiwe chini ya $15 (kwa mwaka may be????)

dola 15 kwa mwaka!? mmh... nadhani hiyo itakuwa ni sawa na dika 1.25 kwa mwezi. Ukishaweka minimua amount itakuwaje tena kila mtu atoe kwa uwezo wake?

Kwenye subscription nadhani yanayowezekana ni kama hivi:

a. Jambo Forums inakuwa ni kwa kulipia kila mwezi.
b. Gharama ya uanachama ni dola 12 kwa mwezi na dola 144 kwa mwaka.
c. Hulipi huingii kusoma lolote isipokuwa vichwa vya habari tu. d. Mtu anahuru wa kulipa kila mwezi au mara moja au kwa miezi sita.
e. Gharama ya kujiandikisha ni non-refundable
f Anayelipia kwa mwaka mzima anapata a 10% discount
 
Mzee Mwanakijiji na Invisible,
Kwanza natoa shukran zangu za dhati kwenu kwa sababu mmekuwa Wazi ktk swala hili na bila kujinyonga kwa tai mnajaribu kupokea ama kutoa nafasi kwa wanachama wengine wapate kusaidia.

Hivi ndivyo inavyotakiwa na sio kufa kama Jaluo, isipokuwa tu inaonyesha unajiuliza maswali mengi ambayo hayatakiwei kujiuliza hata kidogo.. Ni sawa na mtu anayetaka kufunga ndoa lakini kinachomtisha ni siku ya kuvunjika ndoa wakati huo huo hataki kuweka sahihi ya makubaliano (Prenuptial agreement) kwa sababu itamfunga kimapenzi.

Mkuu, binafsi naamini kabisa kvijiwe vyote hivi viwili watu wanaingia kwa mapenzi yao na hata siku moja mapenzi haya hayawezi noga ikiwa upande mmoja unaweka shaka la uhusiano kati ya washiriki. Na wala haitakuwa vema ikiwa kuna masharti nje ya penzi lenyewe hasa yanayohusiana na fedha lakini pamoja na yote hayo fedha ndio huendesha maisha kati ya wapendanao...

Hivyo basi sioni tatizo kabisa ikiwa kutakuwepo na mpangilio wa mchango wa wanachama ktk kuviendesha vijiwe hivi kinachotakiwa ni makubaliano wazi kwa kila atakaye kubali kujisajili kama mmoja kati ya wafadhili wa vijiwe hivi.

Na wala msije ogopa nafasi ya mchangiaji ktk vijiwe hivi kwa sababu zitakuwepo sheria tofauti kati ya Uanachama wa JF na mlezi wa vijiwe hivi. Na kumbukeni kwamba hamuwezi ku win kila kitu kama mnavyotarajia nyie, laa ni lazima pia mkubali kutoa nguvu zaidi kwa wachangiaji walezi ikiwa ni pamoja na kuwazawadia kitu ambacho kitaendelea kuwavuta ktk mapenzi ya JF..

Mfano mkuu nimeona hofu yako kubwa ni pale mchangiaji atakapo dai kuwa shareholder, jambo ambalo binafsi naliona kama ni wasiwasi yako tu kwani zipo site kibao watu tume subscribe bila kujali nani mmliki wa site hiyo na kiasi gani cha fedha anaingiza...

Kweli kuna uwezekano mtu akaona kafungwa kifungo cha nje kulipia dollar 5 kwa kila mwezi lakini sio haya mawazo mabaya yenye kupitwa na wakati tunayojaribu kuyafanyia mageuzi?...

Ni hadi lini Watanzania tutakuja fikiria kwamba nguvu ya kuendesha mapinduzi ya kifikra hayawezi kuja bure..Ni lini sisi wadanganyika tutaweza kuelewa adha na vitisho mnavyopitia nyie kwa gharama ya kueneza habari hizi kiasi kwamba sisi tufikie kuthamini dollar 5 kwa mwezi huku tukiwa kifungo cha nje na huru..

Ni lini sisi tutafikia kuelewa muda mnaoutumia kupanga na kuziendesha tovuti hivi kiasi kwamba yawezekana kabisa ndoa zetu zikawa mashakani?.. Ni lini sisi Wadanganyika tutaelewa kwamba mchango wa dollar 5 kwa mwezi hauwezi kulingana na thamani ya kukosa vijiwe hivi kwa week moja tu...

Mkuu nadhani imetosha!.. nakuombeni wekeni hiyo subscribing option na watakao taka kuchangia watajitokeza kwa hiyari yao na kama siku watakuja dai shareholding basi kipengele fulani cha sheria ya tovuti zote hizi kitawafunga midomo yao kuwa donor wa dollar 5 kwa mwezi ni hiyari ya mtu, haikupi mamlaka ya kumiliki, share wala mamlaka zaidi ya uendeshaji wa tovuti hizi isipokuwa kuzawadiwa ktk vitu fulani fulani..

Labda kikubwa hapa ni kujiuliza zawadi gani itatolewa kwa wanachama walezi wa tovuti hizi mbili pengine kupewa hizo T shirt bure kama ikiwezekana.

Ni muhimu nanyi mfikirie kitu kidogo cha ziada kwa hawa walezi tofauti na mwanachama wa kawaida ili kuwatia moyo zaidi pamoja na kwamba somo kubwa hapa ni kuvieweka vijiwe hivi hai..hiki .Chakula cha akili zetu..
Binafsi kutosoma JF ama KLH kwa siku nzima ni sawa na nimepoteza kazi ya siku nzima kwa malipo ya dollar 15 kwa saa... itaniuma zaidi...
 
dola 15 kwa mwaka!? mmh... nadhani hiyo itakuwa ni sawa na dika 1.25 kwa mwezi. Ukishaweka minimua amount itakuwaje tena kila mtu atoe kwa uwezo wake?

Kwenye subscription nadhani yanayowezekana ni kama hivi:

a. Jambo Forums inakuwa ni kwa kulipia kila mwezi.
b. Gharama ya uanachama ni dola 12 kwa mwezi na dola 144 kwa mwaka.
c. Hulipi huingii kusoma lolote isipokuwa vichwa vya habari tu. d. Mtu anahuru wa kulipa kila mwezi au mara moja au kwa miezi sita.
e. Gharama ya kujiandikisha ni non-refundable
f Anayelipia kwa mwaka mzima anapata a 10% discount

Say ada ya mwaka itatakiwa ilipwe kabla ya march kila mwaka.
$1.23 * member 1500 = 1845 kwa mwezi. Umoja ni nguvu.
 
dola 15 kwa mwaka!? mmh... nadhani hiyo itakuwa ni sawa na dika 1.25 kwa mwezi. Ukishaweka minimua amount itakuwaje tena kila mtu atoe kwa uwezo wake?

Kwenye subscription nadhani yanayowezekana ni kama hivi:

a. Jambo Forums inakuwa ni kwa kulipia kila mwezi.
b. Gharama ya uanachama ni dola 12 kwa mwezi na dola 144 kwa mwaka.
c. Hulipi huingii kusoma lolote isipokuwa vichwa vya habari tu. d. Mtu anahuru wa kulipa kila mwezi au mara moja au kwa miezi sita.
e. Gharama ya kujiandikisha ni non-refundable
f Anayelipia kwa mwaka mzima anapata a 10% discount

Kwa hesabu za makisio ya haraka aklizotoa invisible, nadhani $12 kwa mwezi ni nyingi, let us be realist. haya lets say flat rate iwe $15 kwa mwaka. Unless unataka kuniconvince vinginevyo. I hope hapa huongelei suscription ya JF na KLHN.

Terms and conditions ni muhimu na katika ulizoziweka hapo zinapendeza ila hazitoshi na zikae kisheria zaidi ili kuilinda JF, malipo ya mwaka au ya kila baada ya miezi sita nadhani ni bora zaidi kuliko ya kila mwezi.
 
Wazo jingine ni kuwa; Kwasabau JF ni chombo credible ambacho kiko mstari wa mbele kupiga vita corruption na uongozi mbovu then mnaweza pia kuangalia kama kuna mashirika yenye kufinance institution kama hizi!
Ni wazi zipo tuanze pia kufikiria hilo!

Kuna misaada mingi tu serikali inapewa inayotakiwa kuwekezwa kwenye uimarishaji wa demokrasia lakini wao wanazila!

Huu ni wakati wa kusimama kiume wana JF in any means neccessary!
Kashfa zote ambazo hao wafadhili wamezisikia zimetolewa hapa JF! Stinky Buzwagi,EPA etc etc! Na ni credible! Pia zimefanyiwa kazi na serikali! Evidence ipo!

Sasa ebu niambieni kweli kama JF iko hatarini kufa kwenye nyakati hizi za mfumo bazazi wa kibepari ni nani atakayeweza kuikomboa kutoka kwenye mikono ya mafisadi?

Hii issue ni serious!

Sitaki kusema kwamba siamini kuwa JF haiwezi kuendelea kuwepo kwasababu za kifedha!

Lakini kama sababu ni kujaribu kushindana na fisadi kifedha..Then nanyoosha mikono juu!
 
Mission Statement;
"JF NI CHOMBO HURU CHENYE KUHAMASISHA MAENDELEO YA KIDEMOKRASIA IKIWA NI PAMOJA NA KUWA ELIMISHA WANANCHI"
 
Wakuu

Nafikiri tunaitaji jamii ijue tunazungumza nini. Pia tunaitaji wanachama. Kuna organization nyingi sana ambazo zimekuwa zikifanya kazi kama hii.

Hapa kuna mambo mawili mtu kusoma habari na mtu kutoa mawazo yake.

Kutoa mawazo hiyo iwe members, inamaana unahitaji kuwa na kiingilingilia na fee pia ya mwezi.
Kwa kawaida organization nyingi duniani unaweza kuweka US dolla 100 kwa mwaka kuwa member wa kawaida.

lakini kiwango kinaweza kuongezeka kulinga na mahitaji.

Vile vile unaweza kuamua kuwa member wa kawaida watakuwa wasomaji na siyo wachangiaji. lakini pia ina madhara yake.

Vile vile unaweza kuamua kuwa hakuna haja ya kila mtu kusoma kilichopo JF hii pia ina madhara yake.

Mimi ningefikiria kuwa weka kiwango kwa mwaka let say 100USD for members basi. Hawa members wawe na uwezo wa kusoma na kutoa mawazo.

Ambao siyo members wasome tu lakini hawana uwezo wa kutoa mawazo yao. Au ambao siyo members wapewe abstract ya information iliyopo iliwapate kama kishawishi cha kuwawezesha kutoa mawazo/kusoma zaidi.
 
acha utani bwana meku, this case is serious here
Bibi tafadhali usiniite Meku na sina utani!
Nailewa seriousness ya issue!
Ama sasa umeshakuwa expert member so unaleta dharau!
 
Bibi tafadhali usiniite Meku na sina utani!
Nailewa seriousness ya issue!
Ama sasa umeshakuwa expert member so unaleta dharau!

pole kwa hilo la umeku, kumbe wewe ni mkyekue. Nilidhani swala la kutaka kuinunua JF ilikuwa utani, kumbe ulimaanisha.

Haya na hilo la uexpert linatoka wapi, tena ndio umenishtua, hivi inakuwaje kupanda daraja hapa? nilidhani kila mtu ni member haya kwenye huu expert nimeingiaje maana napata dhihaka pengine.
 
Pole pole BIBI!
 
tartibu bidada na utani huo, id yako haina kiashiria jinsia
Utani upi huo na sexism yako?
Unaweza ukawa either a man or a woman! Nuttin in btn I dont believe on he/she's!
Unaweza pia kuwa Mama kwa someone elese na ukawa BIBI kwa someone else!
Ndio maisha!
 
Mawazo yote safi isipokuwa jaribuni kutazam upande wa pili wa shilingi hiyo mkizingatia mazingira na hulka ya Wadanganyika walio wengi...
Je, hayo madhara yaliyozungumziwa yataweza vipi kuathiri uendeshaji wa tovuti hizi maanake kumbukeni Mdanganyika hatabiriki....Nimeyaona ktk vyama vyetu vya jumuiya za Kitanzania.. I mean Kidanganyika hasa fedha inapokuwa sheria...
 
Nafurahi kuwa JF ipo kuelimisha na wengi wanatambua hilo. Kadiri tunavyoishi ndivyo tujifunzavyo.

Kwa wale wenye nia ya kuichangia JF kwa njia yoyote incl KLH News wanaweza kuwasiliana nami via webmaster@jamboforums.com au wawasiliane na Mwanakijiji kwa njia anayoweza kuwapa. Wapo ambao hawajajisajili najua ambao kwao si rahisi kutuma Private Messages (PM) hivyo fursa ya barua pepe bado ipo. Your privacy is highly respected.

Mkuu Expect to hear from me soon!
 
Hofu yangu kwenye mambo haya ya kufanya subscription ni kuwa watu watatimka kwani wametakiwa kulipia. Wengi wamezoea vya bure na inakuwa kama entitlement ya aina fulani na ukiwaambia walipie utaona jinsi wanavyoanza kutoa udhuru na mwisho utajikuta na wale wale ambao wanachangia kwa hiari wakajikuta wanajiandikisha peke yao.

Hao wengine hasa ukiweka uhuru wa kusoma tu bila kuchangia, watafanya hicho hicho cha kusoma bila kuchangia kwani hadi hivi sasa tunawanachama 5000, kati yao ni chini ya 500 ndio wako active (yaani online) sasa hivi na katika hawa wanachama ni 39 na wageni zaidi ya 400!

Wakati ambapo tumewahi kuwa na watumiaji (wanachama na wageni) wengi kwa wakati mmoja ni Feb 12, ambapo tulikuwa karibu 1500.

Sasa kama trend ni hiyo, I bet you logically (if betting has anything to do with logic) watakaojiandikisha kwa kulipia hawatazidi 100, so tunapofikiria kufanya subscription tusiwafikilie 5000 walioko mtini, tuwafikirie hawa 100 walioko tunduni.
 
Back
Top Bottom