Wanyamwezi na wasukuma

Ogah nakubalina na wewe!Wachaga wamezidi Tanzania nzima!Mama Anna Mkapa na Basil Mramba are typical Chagas!!!!
 
Mwanamasala said:
Tangu uhuru makabila haya yamepigwa chini na makabila madogo madogo!Maendeleo ya mikoa yao yako chini sana,ingawa natural resources nyingi zinatoka huko.Kisiasa tangu akina James Mapalala,Kasanga Tumbo,
Chief Fundikira na Chief Makwaia wapigwe chini na Nyerere ,mikoa hiyo haina uwakilishi kabisa katika maamuzi ya serikali.

Ukiangalia mafisadi wengi wanatoka makabila madogo madogo!Wapinzani wa serikali pia ni kutoka makabila madogo.Mpaka haya makabila yaibuke ,yaseme enough is enough,ufisadi na stupidity ya nchi yetu utaendelea milele.Tujadili!!!!!!!!!!!!!!!!

Mwanamasala,

..kweli wazee kama Kasanga Tumbo,Kasela Bantu,na Fundikira, walipata matatizo na Mwalimu Nyerere.

..pamoja na sidhani kama Wasukuma na Wanyamwezi wamekuwa marginalised ktk nchi hii.

..naomba nikukumbushe viongozi kama Paul Bomani, Francis Nyalali,Wilbard Chagula, Charles Kabeho,Abubakar Mgumia, Timoth Shindika, Samuel Sitta,Prof.Shija, Andrew Chenge,Paul Diallo, Rostam Aziz,Dr.George Mlingwa, kama baadhi ya wananchi toka Usukumani, na Unyamwezini, ambao wameshika nafasi nyeti za uongozi ktk nchi hii.

..kama wananchi hawakufaidika na kilimo cha pamba, na vyama vya ushirika vilidorora, basi Paul Bomani na Timoth Shindika walikuwa na nafasi nzuri ya kurebebisha kasoro zozote. hawa wawili walikuwa na uzoefu mkubwa sana na vyama vya ushirika.

..Samuel Sitta aliwahi kuwa waziri wa ujenzi,mawasiliano na uchukuzi. Dr.George Mlingwa alikuwa katibu mkuu ktk wizara hiyo. matatizo ya barabara kuingia na kutoka Tabora,Shinyanga,na Mwanza, hawa wanapaswa kutoa maelezo.

..Dr.Mlingwa alishtakiwa kwa tuhuma za rushwa na ubadhirifu ktk mradi wa barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza. sasa hapa sidhani kama ni halali kusema makabila madogo yamewapiga chini.

..suala la madini waulizwe Prof.Shija aliwahi kuwa Waziri wa Madini na Nishati, na Andrew Chenge ambaye nadhani ni AG aliyedumu kwa muda mrefu kupita wote ktk nafasi hiyo. nadhani Shija alikuwepo pale wakati sheria ya madini inabadilishwa mwaka 97, na pia mikataba mingi ya madini imesainiwa wakati Chenge ni AG.

..lakini ukiangalia kwa undani, Chenge angekuwa makini zaidi ktk masuala ya mikataba ya madini, Watanzania woote bila kujali makabila yetu tungefaidika. kama Mlingwa angekuwa makini ktk mradi wa barabara ya Dom-Mwanza, si Wasukuma na Wanyamwezi peke yao wangesafiri ktk barabara hiyo, bali Watanzania wote.

..kwa upande mwingine Watanzania ktk ujumla wetu tumezingirwa na umaskini wa kutisha. katika suala muhimu kama Elimu sina uhakika kama asilimia zaidi ya 7 ya wanafunzi wanaoanza primary school wanafika chuo kikuu. sasa kuanza kusema eneo fulani limewapiga chini eneo lingine ni kujenga uadui usiokuwa na ulazima wowote.

NB:

..kuna kitendawili kigumu sana umekitoa ktk posting yako.

..ikiwa Usukumani na Unyamwezini mmenyimwa nafasi za uongozi, maendeleo, na hata opportunities za kufanya ufisadi, kwanini basi mnaendelea kuipigia kura CCM?
 
Joka Kuu ya right to some extent.Hawa wote ni sell out!Ni wasukuma wa CCM,sidhani wana nyumba hata huko wanakotoka,ni Dar based bureacrats
 
Mwanamasala,

..majuzi nilisoma kwamba Dr.Cyril Chami na wananchi wa jimbo la Moshi Vijijini wameshirikiana kujenga kituo cha polisi.

..binafsi sijasikia lolote kama wabunge wa mikoa ya Mwanza,Tabora,na Shinyanga, wakijitolea kushughulikia kero za wananchi.

..hapa nawazungumzia wabunge matajiri wakubwa kama Rostam Aziz, Lau Masha, Salum Khamis Salum, Paulo Dialo.

..Nimrod Mkono amefungua shule nzuri tu ya sekondari, je Lau Masha ambaye ni mwanasheria na mwenye mapesa kama Mkono amefanya nini kwa community yake?

..Salum Khamis Salum naye amefungua kiwanda chenye thamani ya mabilioni ya shilingi. tena badala ya kujenga kiwanda hicho Mwanza au Shinyanga ambako pamba inapatikana kaenda kujenga Arusha. sasa sijui Meatu jimboni kwake kuna hali gani. sijui kama amejenga walau Zahanati.
 
Angalia hata Elimu,ukichukua Mwanza ,Shinyanga na Tabora only one University in the region: SAUT!Thanks to Catholic church!Si walaumu wagogo kupata UDOM.
Hizi regions zina resources nyingi,watu wengi but still marginalised.

Blame pia ni kwa wasukuma wenyewe!Hasa wabunge wetu toka independence!Wengi wameloe dar es salaam,bila kujali maendeleo ya watu wao.Good luck wabunge wa Kichaga,Kipare etc tangu Msuya walivyojitahidi kuendeleza kwao
 
...Jamani hivi huyu Ngereja si anatoka kwetu? Masha pia lakini wamefumba midomo kiasi kwamba hawasikiki. Ukiangalia mikoa kama ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro Mbunge akipewa uwaziri atahakikisha kwanza hiyo wizara italeta mpaka kijijini maendeleo halafu baadae wengine.Hiyo ndio inatakiwa unakula huku unapuliza(unaiba huku unaleta maendeleo.
Mfano angalia EL japokuwa anatuhumiwa kwa ufisadi lakini wananchi wake wanaona ni kipi alichokifanya kwa hiyo hata kama mseme wataendelea kumchagua hata kama akiweka mtoto wake bado atapita,

...Mfano mwingine ni Bazir Maramba nasikia japo sijaona kuwa umeme mpaka migombani, maji na barabara ni safi jimboni kwake hata kama mseme ataendelea kuhudumia jimbo kama mbunge sijasikia kama kuna mtu kasema atakwenda kumpinga
...Mrema, Ngawaiya,Mbowe,Sumayi,Msuya na wengine bado wanakubalika majimboni kwao.
Lakini angalia Mwanza mjini hakuna Mbunge aliyekwisha tawala zaidi ya vipindi viwili(Achilia Diallo MWANZA VIJIJINI). Bomani alishakuwa mtu maarufu mpaka kuwa waziri lakini hakuna hata cha kumkumbukia alichokifanya, Masha sijaona lolote, Ngereja mpaka wananchi wake hawamtaki tena kwani ndiko madini yanakotoka na hakuna hata cha maana alichokifanya kwa wachimbaji wadogodogo.
....Kuna huyu marehemu Ernest Kisumu Nyanda alikuwa mbunge wa MAGU na waziri wa mambo ya ndani cha maana alichokifanya ni kupeleka vijana wengi Jeshi la polisi,Maendeleo hola. Dr Festus Limbu alishawahi kuwa Naibu waziri wa Fedha
nenda jimboni kwake hakuna lolote.
 
...Wabunge wengi wa Mwanza na wilaya zake hawajiamini, Kina Mama Mongera, Pius Msekwa, Ngereja,Masha na wengineo wana nafasi nzuri tu za kukaa pamoja na kuuendeleza mkoa wa Mwanza. Mfano ni shilingi ngapi uwanja wa ndege wa Mwanza umeingiza kwenye Sangara, Silaha kwenda nchi jirani, ni uwanja huo huo hawa Barrick na wengine wazee wa madini wanautumia kupitishia mizigo yao. Lakini umeacha utadhani mtoto yatima aliyekataliwa hata na vituo vya kulelea yatima.
 
Wasukuma na Wanyamwezi wenzangu mpo?

Kwenye mchango wangu wa kwanza kabisa kwenye thread hii niliahidi kuwa nitaendelea. Ukweli unabaki palepale kama mtoa maada alivyoanza kuchangia.
Ni dhahiri kabisa kuwa hii mikoa ya Wasukuma na Wanyamwezi imesahauliwa tangu enzi za Mwalimu. Siyo siri maendeleo katika maeneo haya ni duni na yanatia kichefuchefu. Hakuna barabara za lami, hakuna shule wala vyuo vikuu ambavyo aghalabu ni ndiyo vichocheo vya maendeleo.

Labda tujaribu kurudi huko nyuma enzi za Mwalimu baada ya uhuru. Kwa habari ambazo haziwezi kuthibitishwa yasemekana kwamba mara baada ya uhuru Marehemu Baba wa Taifa alikuwa na hofu sana na watu hawa: Wasukuma na Wanyamwezi. Nyerere mwenyewe alitokea kikabila kidogo cha Wazanaki(Wasukuma wanawaita Washashi) pale Musoma-Mara. Kwa hiyo Nyerere alikuwa na hiofu na makabila makubwa kama yetu. Wakti wa vuguvugu la kuelekea kwenye uhuru kulikuwa na chama maarufu sana cha Wana-ushirika au Wakulima(Balimi) kilichokuwa kikiitwa Nyanza Federation. Chama hiki kilikuwa kimejijengea umaarufu kiasi kwamba kilikuwa ni tishio hata kwa vyama vya siasa. Nyerere alilijua hili kwa hiyo yeye akaamua kusambaratisha chama hiki kwa kuwapa vyeo viongozi waliokuwa wakitoka maeneo haya, vyeo ambavyo vingewafanya wasijulikane wala kuwa karibu na Wananchi(Wasukuma na Wanyamwezi).

Watu kama kina marehemu Paulo Bomani(msukuma wa Ng'wanza) waliteuliwa kwenye balozi za kuduma huko USA(Marekani) ili wasiendelee kujijengea umaarufu na hatimaye kutwaa uongozi wa nchi hii. Jaji Mark Bomani naye alipelekwa Zambia na kukaa kwa muda mrefu tu. Kwa mtindo huo wengi waliwasahau na umaarufu wao kupotoea. Njia nyingine ilikuwa viongozi kutoka maeneo haya kupewa nyazifa ambazo hazina umaarufu wa kujulikana kwa haraka. Vyeo kama ukuu wa Wilaya, mkoa au Uwaziri katika Wizara zisizo nyeti. Kwa kipindi chote hicho mpaka leo hakuna Msukuma au Mnyamwezi ambaye amepata kuwa Waziri Mkuu. Anza na watu kama kina Kawawa ambaye ndiye alikuwa PM wa kwanza Tanganyika, mtu ambaye hata shule ilimpita pembeni, mtakubaliana nami kuwa Kawawa alikuwa ni msanii(mwigizaji) wa filamu akijulikana kama Mhogo mchungu kwa jina la usanii. Kwa kisomo asingeweza kuwafikia Wasukuma na Wanyamwezi wa wakti huo ukianzia na kina Paulo Bomani, Jaji Mark Bomani, Chief Abdulla Fundikira, Kasanga Tumbo,Kasela Bantu na wengineo.

Baada ya Kawawa wakaja kina Marehemu Sokoine(Masai),Dk.Salim A. Salim(mpemba),Joseph Sinde Warioba(Muikizu),Fredrick Sumaye(mbulu) Edward Lowasa(Masai) na sasa Mizengo Kayanza Pinda(sumbawanga). Wote hawa ni kutoka kabila ndogo ambazo hazina umaarufu kama walivyo Wasukuma na Wanyamwezi. Nyerere alijua kile alichokuwa akifanya kwa makusudi kabisa huku akisingizia anaondoa ukabila.

Kama hiyo haitoshi Mwalimu aliamua hata kuhamisha utajiri na raslimali za Wasukuma na Wanyamwezi na kuzipeleka maeneo mengine na maeneoa haya kuendelea kuwa hoi bin taabani. Tuchukue mifano hai kabisa ambayo haina ubishi. Pale Mwadui- Shinyanga kuna mgodi wa Almasi ulioanzishwa na Wakoloni tangu mwaka 1940 ulijulikana kama Williamson Diamonds. Mgodi huu haujawasaidia Wasukuma kwa lolote. Nenda pale leo barabara ni vumbi na mashimo mpaka uvunguni. Hakuna lami wala ndugu yake lami. Miaka ya 1970 kukatakiwa kujengwa kiwanda cha kukatia Almasi. Kwa mategemao ya wengi kingejenwa Mwadui au Shinyanga mjini lakini kwasababu za kutowaendeleza Wasukuma wa Shinyanga kikapelekwa Iriiinga kwa Wahehe. Njoo kwenye viwanda vya nguo mambo ni yaleyale. Mwanza Textile pekee ndicho kilichokuwa mahali sahihi. Lakini ukija Viwanda kama Musoma Textile(MUTEX) kilikuwa Musoma, Urafiki Textile kiko Dar, unakuta kwamba Pamba ilikuwa inasafrishwa toka Shinyanga, Mwanza na Tabora kupelekwa Musoma na Dar kwenye Viwanda vya nguo. Yote hii ni katika juhudi za kuididimiza mikoa ya Wasukuma na Wanyamwezi.

Ni kweli kuna vipindi tumekuwa na Mawaziri miaka ya 90 hivi kwenye Wizara kama Mawasiliano na Ujenzi kina Dk. Pius Yasebasi Ng'wandu au Ernest Nyanda, lakini hawakuwa na ubavu au jeuri ya kuchota pesa na kuzihamishia kwenye miradi ya mabarabara ya Usukumani na Unyamwezini kama ambavo Mawaziri wenye jeuri kama kina Basir Pesambili Mramba.walivokuwa wanafanya.

Mojawapo ya sifa za Wasukuma na Wanyamwezi ni Ukarimu wao na Upole wao kwa kila mtu. Pengine vitu kama hivi vina gharama yake. Hawapendi vurugu wala fujo na mambo ya kifisadi, wao wanataka amani, haki na usawa kwa kila mtu. Kweli mafisadi wapo lakini si kwa skeli kubwa kama ilivyo kwa haya makabila madogo madogo. Wengi watasema aah, mbona Chenge yumo! Sawa lakini mi mmoja tu, na hiyo ni kawaida katika jamii kuwa na mtu mmoja mmoja mwenye tabia tofauti na majority. Kwa hiyo yale waliyokuwa wanafanyiwa na Nyerere walikuwa wanaona ni sawa tu hakuna matata.

Lakini this time naona tumeanza kubadilika,Watanzania wameanza kuona tofauti ya Wasukuma/Wanyamwezi kwa kuanza kupambana na mafisadi. Mfano halisi ni vita vinavyoendelea ndani na nje ya Bunge kwa sasa. Mheshimwa Samweli Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mnyamwezi),Lucas Selelii-MB(Mnyamwezi),Mpendazoe-MB(Msukuma) wanaongoza jahazi la kupiga vita ufisadi kwa Viwango na Mwendo(Standard and Speed).Kwa vile CCM ilijengwa kwa mtazamo wa kuyabana makabila makubwa kama haya kwa hofu ileile, sasa hivi CCM wanawasiwasi sana kuhusu haya makabila na ndiyo maana kuna kampeni za chini chini za kutaka kuwang'oa akina Sitta.

Watu wana msemo wa hekima kuwa, ukitaka bubu aseme, mpige mwanae!!! Kama serikali ya CCM inataka kumfanya bubu aseme basi wajaribu kumpiga mtoto. Namaanisha CCM kama watafikia mahali pa kuwatimua kina Sita na kundi lake basi wanaweza kuchochea moto kwa kumwaga peteroli kwenye moto. Mimi naamini kabisa Marais wote wa awamu zote zilizopita na ya sasa ushindi wao walipata mkubwa walipata kutokana na kura za hawahawa Wanyanwezi na Wasukuma wanaowapuuza. Huo ndio ukweli. Sasa kama CCM watawachokoza jamaa hawa basi wana uwezo kabisa wakubadilisha matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2010. Maana ni wengi ati. Kama wakiamua kukipigia chama chochote cha Upinzani basi CCM hawana chao.

Nina hakika Wasukuma na Wanyamwezi tukiungana na kuwa kitu kimoja tunaweza kubadilisha mwelekeo wa nchi hii.Hatuwezi kuendelea kuona DHAHABU YETU,ALMASI YETU, MINOFU YA SANGARA WETU,PAMBA YETU, NG'OMBE WETU vikihamishwa kwenda nje au maeneo mengine ya nchi hii na sisi tukiachiwa mashimo na mapanki. Naamini kabisa tukiamua tunaweza kubadilisha mwelekeo wa nchi hii.

Nitaendelea wakti mwingine mara nyingine.

Ng'wabeja sana banamhala.
 
Wasukuma na Wanyamwezi wenzangu mpo?

Kwenye mchango wangu wa kwanza kabisa kwenye thread hii niliahidi kuwa nitaendelea. Ukweli unabaki palepale kama mtoa maada alivyoanza kuchangia.
Ni dhahiri kabisa kuwa hii mikoa ya Wasukuma na Wanyamwezi imesahauliwa tangu enzi za Mwalimu. Siyo siri maendeleo katika maeneo haya ni duni na yanatia kichefuchefu. Hakuna barabara za lami, hakuna shule wala vyuo vikuu ambavyo aghalabu ni ndiyo vichocheo vya maendeleo.

Labda tujaribu kurudi huko nyuma enzi za Mwalimu baada ya uhuru. Kwa habari ambazo haziwezi kuthibitishwa yasemekana kwamba mara baada ya uhuru Marehemu Baba wa Taifa alikuwa na hofu sana na watu hawa: Wasukuma na Wanyamwezi. Nyerere mwenyewe alitokea kikabila kidogo cha Wazanaki(Wasukuma wanawaita Washashi) pale Musoma-Mara. Kwa hiyo Nyerere alikuwa na hiofu na makabila makubwa kama yetu. Wakti wa vuguvugu la kuelekea kwenye uhuru kulikuwa na chama maarufu sana cha Wana-ushirika au Wakulima(Balimi) kilichokuwa kikiitwa Nyanza Federation. Chama hiki kilikuwa kimejijengea umaarufu kiasi kwamba kilikuwa ni tishio hata kwa vyama vya siasa. Nyerere alilijua hili kwa hiyo yeye akaamua kusambaratisha chama hiki kwa kuwapa vyeo viongozi waliokuwa wakitoka maeneo haya, vyeo ambavyo vingewafanya wasijulikane wala kuwa karibu na Wananchi(Wasukuma na Wanyamwezi).

Watu kama kina marehemu Paulo Bomani(msukuma wa Ng’wanza) waliteuliwa kwenye balozi za kuduma huko USA(Marekani) ili wasiendelee kujijengea umaarufu na hatimaye kutwaa uongozi wa nchi hii. Jaji Mark Bomani naye alipelekwa Zambia na kukaa kwa muda mrefu tu. Kwa mtindo huo wengi waliwasahau na umaarufu wao kupotoea. Njia nyingine ilikuwa viongozi kutoka maeneo haya kupewa nyazifa ambazo hazina umaarufu wa kujulikana kwa haraka. Vyeo kama ukuu wa Wilaya, mkoa au Uwaziri katika Wizara zisizo nyeti. Kwa kipindi chote hicho mpaka leo hakuna Msukuma au Mnyamwezi ambaye amepata kuwa Waziri Mkuu. Anza na watu kama kina Kawawa ambaye ndiye alikuwa PM wa kwanza Tanganyika, mtu ambaye hata shule ilimpita pembeni, mtakubaliana nami kuwa Kawawa alikuwa ni msanii(mwigizaji) wa filamu akijulikana kama Mhogo mchungu kwa jina la usanii. Kwa kisomo asingeweza kuwafikia Wasukuma na Wanyamwezi wa wakti huo ukianzia na kina Paulo Bomani, Jaji Mark Bomani, Chief Abdulla Fundikira, Kasanga Tumbo,Kasela Bantu na wengineo.

Baada ya Kawawa wakaja kina Marehemu Sokoine(Masai),Dk.Salim A. Salim(mpemba),Joseph Sinde Warioba(Muikizu),Fredrick Sumaye(mbulu) Edward Lowasa(Masai) na sasa Mizengo Kayanza Pinda(sumbawanga). Wote hawa ni kutoka kabila ndogo ambazo hazina umaarufu kama walivyo Wasukuma na Wanyamwezi. Nyerere alijua kile alichokuwa akifanya kwa makusudi kabisa huku akisingizia anaondoa ukabila.

Kama hiyo haitoshi Mwalimu aliamua hata kuhamisha utajiri na raslimali za Wasukuma na Wanyamwezi na kuzipeleka maeneo mengine na maeneoa haya kuendelea kuwa hoi bin taabani. Tuchukue mifano hai kabisa ambayo haina ubishi. Pale Mwadui- Shinyanga kuna mgodi wa Almasi ulioanzishwa na Wakoloni tangu mwaka 1940 ulijulikana kama Williamson Diamonds. Mgodi huu haujawasaidia Wasukuma kwa lolote. Nenda pale leo barabara ni vumbi na mashimo mpaka uvunguni. Hakuna lami wala ndugu yake lami. Miaka ya 1970 kukatakiwa kujengwa kiwanda cha kukatia Almasi. Kwa mategemao ya wengi kingejenwa Mwadui au Shinyanga mjini lakini kwasababu za kutowaendeleza Wasukuma wa Shinyanga kikapelekwa Iriiinga kwa Wahehe. Njoo kwenye viwanda vya nguo mambo ni yaleyale. Mwanza Textile pekee ndicho kilichokuwa mahali sahihi. Lakini ukija Viwanda kama Musoma Textile(MUTEX) kilikuwa Musoma, Urafiki Textile kiko Dar, unakuta kwamba Pamba ilikuwa inasafrishwa toka Shinyanga, Mwanza na Tabora kupelekwa Musoma na Dar kwenye Viwanda vya nguo. Yote hii ni katika juhudi za kuididimiza mikoa ya Wasukuma na Wanyamwezi.

Ni kweli kuna vipindi tumekuwa na Mawaziri miaka ya 90 hivi kwenye Wizara kama Mawasiliano na Ujenzi kina Dk. Pius Yasebasi Ng’wandu au Ernest Nyanda, lakini hawakuwa na ubavu au jeuri ya kuchota pesa na kuzihamishia kwenye miradi ya mabarabara ya Usukumani na Unyamwezini kama ambavo Mawaziri wenye jeuri kama kina Basir Pesambili Mramba.walivokuwa wanafanya.

Mojawapo ya sifa za Wasukuma na Wanyamwezi ni Ukarimu wao na Upole wao kwa kila mtu. Pengine vitu kama hivi vina gharama yake. Hawapendi vurugu wala fujo na mambo ya kifisadi, wao wanataka amani, haki na usawa kwa kila mtu. Kweli mafisadi wapo lakini si kwa skeli kubwa kama ilivyo kwa haya makabila madogo madogo. Wengi watasema aah, mbona Chenge yumo! Sawa lakini mi mmoja tu, na hiyo ni kawaida katika jamii kuwa na mtu mmoja mmoja mwenye tabia tofauti na majority. Kwa hiyo yale waliyokuwa wanafanyiwa na Nyerere walikuwa wanaona ni sawa tu hakuna matata.

Lakini this time naona tumeanza kubadilika,Watanzania wameanza kuona tofauti ya Wasukuma/Wanyamwezi kwa kuanza kupambana na mafisadi. Mfano halisi ni vita vinavyoendelea ndani na nje ya Bunge kwa sasa. Mheshimwa Samweli Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mnyamwezi),Lucas Selelii-MB(Mnyamwezi),Mpendazoe-MB(Msukuma) wanaongoza jahazi la kupiga vita ufisadi kwa Viwango na Mwendo(Standard and Speed).Kwa vile CCM ilijengwa kwa mtazamo wa kuyabana makabila makubwa kama haya kwa hofu ileile, sasa hivi CCM wanawasiwasi sana kuhusu haya makabila na ndiyo maana kuna kampeni za chini chini za kutaka kuwang’oa akina Sitta.

Ng’wabeja sana banamhala.

Hizi sentiments ziko overly parochial, zinaona ukabila hata pale usipo, basically whining. Kila mtu akija na imaginary grievances kuhusu kabila lake mbona hata huko Kenya kutakuwa na afadhali?

Tulikuwa hatuulizani makabila, na kama tunaulizana ni kwa sababu ya utani, kulikoni?

Kama issue ni kukosa maendeleo, nchi yetu karibu yote iko nyuma kimaendeleo, sasa huu usukuma una relevance gani nkoi? Au kwa sababu kabila kubwa basi tunataka privileges? Lekaga gete mamihayo genago!

Mimi nafikiri tunatakiwa kuyaangalia matatizo yetu kitaifa, au hata kimataifa zaidi kuliko kikabila, tukiangalia matatizo haya kikabila tunajipunguzia wigo wetu na tunaongeza matatizo, maana kila kabila litakuja kivyake mwishowe itakuwa civil war.
 
Wasukuma na Wanyamwezi wenzangu mpo?

Kwenye mchango wangu wa kwanza kabisa kwenye thread hii niliahidi kuwa nitaendelea. Ukweli unabaki palepale kama mtoa maada alivyoanza kuchangia.
Ni dhahiri kabisa kuwa hii mikoa ya Wasukuma na Wanyamwezi imesahauliwa tangu enzi za Mwalimu. Siyo siri maendeleo katika maeneo haya ni duni na yanatia kichefuchefu. Hakuna barabara za lami, hakuna shule wala vyuo vikuu ambavyo aghalabu ni ndiyo vichocheo vya maendeleo.

Labda tujaribu kurudi huko nyuma enzi za Mwalimu baada ya uhuru. Kwa habari ambazo haziwezi kuthibitishwa yasemekana kwamba mara baada ya uhuru Marehemu Baba wa Taifa alikuwa na hofu sana na watu hawa: Wasukuma na Wanyamwezi. Nyerere mwenyewe alitokea kikabila kidogo cha Wazanaki(Wasukuma wanawaita Washashi) pale Musoma-Mara. Kwa hiyo Nyerere alikuwa na hiofu na makabila makubwa kama yetu. Wakti wa vuguvugu la kuelekea kwenye uhuru kulikuwa na chama maarufu sana cha Wana-ushirika au Wakulima(Balimi) kilichokuwa kikiitwa Nyanza Federation. Chama hiki kilikuwa kimejijengea umaarufu kiasi kwamba kilikuwa ni tishio hata kwa vyama vya siasa. Nyerere alilijua hili kwa hiyo yeye akaamua kusambaratisha chama hiki kwa kuwapa vyeo viongozi waliokuwa wakitoka maeneo haya, vyeo ambavyo vingewafanya wasijulikane wala kuwa karibu na Wananchi(Wasukuma na Wanyamwezi).

Watu kama kina marehemu Paulo Bomani(msukuma wa Ng’wanza) waliteuliwa kwenye balozi za kuduma huko USA(Marekani) ili wasiendelee kujijengea umaarufu na hatimaye kutwaa uongozi wa nchi hii. Jaji Mark Bomani naye alipelekwa Zambia na kukaa kwa muda mrefu tu. Kwa mtindo huo wengi waliwasahau na umaarufu wao kupotoea. Njia nyingine ilikuwa viongozi kutoka maeneo haya kupewa nyazifa ambazo hazina umaarufu wa kujulikana kwa haraka. Vyeo kama ukuu wa Wilaya, mkoa au Uwaziri katika Wizara zisizo nyeti. Kwa kipindi chote hicho mpaka leo hakuna Msukuma au Mnyamwezi ambaye amepata kuwa Waziri Mkuu. Anza na watu kama kina Kawawa ambaye ndiye alikuwa PM wa kwanza Tanganyika, mtu ambaye hata shule ilimpita pembeni, mtakubaliana nami kuwa Kawawa alikuwa ni msanii(mwigizaji) wa filamu akijulikana kama Mhogo mchungu kwa jina la usanii. Kwa kisomo asingeweza kuwafikia Wasukuma na Wanyamwezi wa wakti huo ukianzia na kina Paulo Bomani, Jaji Mark Bomani, Chief Abdulla Fundikira, Kasanga Tumbo,Kasela Bantu na wengineo.

Baada ya Kawawa wakaja kina Marehemu Sokoine(Masai),Dk.Salim A. Salim(mpemba),Joseph Sinde Warioba(Muikizu),Fredrick Sumaye(mbulu) Edward Lowasa(Masai) na sasa Mizengo Kayanza Pinda(sumbawanga). Wote hawa ni kutoka kabila ndogo ambazo hazina umaarufu kama walivyo Wasukuma na Wanyamwezi. Nyerere alijua kile alichokuwa akifanya kwa makusudi kabisa huku akisingizia anaondoa ukabila.

Kama hiyo haitoshi Mwalimu aliamua hata kuhamisha utajiri na raslimali za Wasukuma na Wanyamwezi na kuzipeleka maeneo mengine na maeneoa haya kuendelea kuwa hoi bin taabani. Tuchukue mifano hai kabisa ambayo haina ubishi. Pale Mwadui- Shinyanga kuna mgodi wa Almasi ulioanzishwa na Wakoloni tangu mwaka 1940 ulijulikana kama Williamson Diamonds. Mgodi huu haujawasaidia Wasukuma kwa lolote. Nenda pale leo barabara ni vumbi na mashimo mpaka uvunguni. Hakuna lami wala ndugu yake lami. Miaka ya 1970 kukatakiwa kujengwa kiwanda cha kukatia Almasi. Kwa mategemao ya wengi kingejenwa Mwadui au Shinyanga mjini lakini kwasababu za kutowaendeleza Wasukuma wa Shinyanga kikapelekwa Iriiinga kwa Wahehe. Njoo kwenye viwanda vya nguo mambo ni yaleyale. Mwanza Textile pekee ndicho kilichokuwa mahali sahihi. Lakini ukija Viwanda kama Musoma Textile(MUTEX) kilikuwa Musoma, Urafiki Textile kiko Dar, unakuta kwamba Pamba ilikuwa inasafrishwa toka Shinyanga, Mwanza na Tabora kupelekwa Musoma na Dar kwenye Viwanda vya nguo. Yote hii ni katika juhudi za kuididimiza mikoa ya Wasukuma na Wanyamwezi.

Ni kweli kuna vipindi tumekuwa na Mawaziri miaka ya 90 hivi kwenye Wizara kama Mawasiliano na Ujenzi kina Dk. Pius Yasebasi Ng’wandu au Ernest Nyanda, lakini hawakuwa na ubavu au jeuri ya kuchota pesa na kuzihamishia kwenye miradi ya mabarabara ya Usukumani na Unyamwezini kama ambavo Mawaziri wenye jeuri kama kina Basir Pesambili Mramba.walivokuwa wanafanya.

Mojawapo ya sifa za Wasukuma na Wanyamwezi ni Ukarimu wao na Upole wao kwa kila mtu. Pengine vitu kama hivi vina gharama yake. Hawapendi vurugu wala fujo na mambo ya kifisadi, wao wanataka amani, haki na usawa kwa kila mtu. Kweli mafisadi wapo lakini si kwa skeli kubwa kama ilivyo kwa haya makabila madogo madogo. Wengi watasema aah, mbona Chenge yumo! Sawa lakini mi mmoja tu, na hiyo ni kawaida katika jamii kuwa na mtu mmoja mmoja mwenye tabia tofauti na majority. Kwa hiyo yale waliyokuwa wanafanyiwa na Nyerere walikuwa wanaona ni sawa tu hakuna matata.

Lakini this time naona tumeanza kubadilika,Watanzania wameanza kuona tofauti ya Wasukuma/Wanyamwezi kwa kuanza kupambana na mafisadi. Mfano halisi ni vita vinavyoendelea ndani na nje ya Bunge kwa sasa. Mheshimwa Samweli Sitta, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mnyamwezi),Lucas Selelii-MB(Mnyamwezi),Mpendazoe-MB(Msukuma) wanaongoza jahazi la kupiga vita ufisadi kwa Viwango na Mwendo(Standard and Speed).Kwa vile CCM ilijengwa kwa mtazamo wa kuyabana makabila makubwa kama haya kwa hofu ileile, sasa hivi CCM wanawasiwasi sana kuhusu haya makabila na ndiyo maana kuna kampeni za chini chini za kutaka kuwang’oa akina Sitta.

Watu wana msemo wa hekima kuwa, ukitaka bubu aseme, mpige mwanae!!! Kama serikali ya CCM inataka kumfanya bubu aseme basi wajaribu kumpiga mtoto. Namaanisha CCM kama watafikia mahali pa kuwatimua kina Sita na kundi lake basi wanaweza kuchochea moto kwa kumwaga peteroli kwenye moto. Mimi naamini kabisa Marais wote wa awamu zote zilizopita na ya sasa ushindi wao walipata mkubwa walipata kutokana na kura za hawahawa Wanyanwezi na Wasukuma wanaowapuuza. Huo ndio ukweli. Sasa kama CCM watawachokoza jamaa hawa basi wana uwezo kabisa wakubadilisha matokeo ya Uchaguzi wa mwaka 2010. Maana ni wengi ati. Kama wakiamua kukipigia chama chochote cha Upinzani basi CCM hawana chao.

Nina hakika Wasukuma na Wanyamwezi tukiungana na kuwa kitu kimoja tunaweza kubadilisha mwelekeo wa nchi hii.Hatuwezi kuendelea kuona DHAHABU YETU,ALMASI YETU, MINOFU YA SANGARA WETU,PAMBA YETU, NG'OMBE WETU vikihamishwa kwenda nje au maeneo mengine ya nchi hii na sisi tukiachiwa mashimo na mapanki. Naamini kabisa tukiamua tunaweza kubadilisha mwelekeo wa nchi hii.

Nitaendelea wakti mwingine mara nyingine.

Ng’wabeja sana banamhala.

Makoye hongera kwa mchango wako. Big up!!!!!!
 
all in all nimegundua sisi wanyamwezi na wasukuma tupo na mioyo safi sana.
 
Tangu uhuru makabila haya yamepigwa chini na makabila madogo madogo!Maendeleo ya mikoa yao yako chini sana,ingawa natural resources nyingi zinatoka huko.Kisiasa tangu akina James Mapalala,Kasanga Tumbo,
Chief Fundikira na Chief Makwaia wapigwe chini na Nyerere ,mikoa hiyo haina uwakilishi kabisa katika maamuzi ya serikali.

Ukiangalia mafisadi wengi wanatoka makabila madogo madogo!Wapinzani wa serikali pia ni kutoka makabila madogo.Mpaka haya makabila yaibuke ,yaseme enough is enough,ufisadi na stupidity ya nchi yetu utaendelea milele.Tujadili!!!!!!!!!!!!!!!!

Mwanamasala,
Hoja yako iliyoleta ni nzuri na kwa kiasi kikubwa ni fact umeongea. Wananyamwezi na wasukuma wanatumiwa na wanasiasa kujiapatia kura na kuiba maliasili zao zilizo kwenye maeneo yao ya asili na hakuna kitu cha maana wachofanyiwa kupata maendeleo in return na maliasili za maeneo yao. Angalia miji kama Geita na Kahama dhahabu inachimbwa lakini hakuna hata miundombinu ni vumbi tupu, hospital zimefurika wagonjwa hata ward haziongezeki, reli ya kati means kuu ya usafiri kwa bei nafuu usukumani na unyawezini wamegawa kwa mhindi n.k.
 
Back
Top Bottom