Mkuu,
Wanyamwezi huwa tuna kaushamba fulani. Utaona jitu limesoma ila bado halijaelimika. Sidhani kama Mnyamwezi akipewa nchi tutafika mbali.
Nakubaliana na wewe tu kitu kimoja kuwa, Wanyamwezi wa Kaskazini (Wasukuma) na Wale wa Kusini (Wadakama) kama tungeliungana na kutunga WARAKA wetu wa uchaguzi, basi tungelileta mwanga mkubwa sana kwa wananchi. Ingeliwekwa wazi miiko ya viongozi. Tungelikuwa na Wapelelezi wetu na kila kiongozi FISADI, tungelimjadili na kumuumbua hapohapo mbele ya jukwaa na kuwambia apeleke huo uongo wake huko mbali. Na watu kama Chenge na Hosea, basi na wao wangelipewa palepale LIVE. Amini usiamini, makabila mengine yangelituiga na kuanza KUKEMEA ndugu zao (Ila sidhani Wachaga wangelifanya hivyo/Nyantuzu na Wakinga) maana hawa jamaa, mhhhhh.............
Ila la muhimu ni kuwa, mtu gani wachague hilo linaachwa WAZI kwao wenyewe wachague na mtu akijifanya kutumia ukabila kupendekeza fulani achaguliwe, basi tunaMPONDA dawa. Ila option ya kusema "fulani hatumtaki", hiyo inabaki wazi.
Mtu kama Waziri wa Energy, pamoja na kutoka huko, kuna haja gani kuwa naye? Tuko wengi saana na kama tukitumia huo wingi wetu kuirekeisha nchi basi tutafika mbali. Ila la muhimu ni HAKUNA kuoneana aibu. Akija Fisadi mnamtoa BARU.