Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Diversion >>>

Ukiangalia 'series' ya 'Prison Break', utaona ni kiboko ya 'series...'

Nafananisha (si kimaudhui) na Kitabu cha Mashimo ya Mfalme Suleiman (King Solomon Mines)

Lakini ukiangalia 'series' ya 24 ndio utajuwa kuwa kumbe 'prison break' ni kama 'intro' tu...

Nafananisha na Kitabu cha Hadith za Allan Quatermain (si kimaudhui)

Hakika ni utunzi ulio bora kabisa.
 
... Perfumed Garden!!! Hiki kitabu niliwahi kusikia sifa zake but sijawahi kisoma, hebu funguka kiduuchu mkuu..



Duh...nasita kidogo kueleza kwa kina, kwani kwanza sijui umri wako na pili ni kwamba nadhani upo wakati kitabu hiki kama kumbukumbu zangu ni sahihi kiliwahi kupigwa marufuku...yaani Enzi zile za miaka ya 70 na kuendelea kidogo...Lakini kwa ufupi kitabu hiki kimeandikwa nadhani kwa lugha ya Kiaarabu lakini kimetafsiriwa in English na Sir Richard Burton...katika cover yake ya juu kimeandikwa title ya kitabu yaani THE PERFUMED GARDEN na pia maneno yafuatayo: '...The most daring book ever written on the THE ARABIAN ART OF MAKING LOVE'....sasa baada ya maelezo haya sasa kazi kwako...mimi siendelei zaidi, labda nigusie jambo moja pia nalo ni kwamba huyu SIR RICHARD BURTON aliyetafsiri kitabu hiki ndiye mtunzi (but , Iam not so sure) wa kitabu kingine maarufu kwa mambo ya mapenzi cha KAMA SUTRA (ambacho nadhani kinaelelezea mapenzi ya kihindi)...ila kumbuka kuna videos za KAMA SUTRA... Kumbuka pia kuwa vitabu hivi ni vya zamani, lakini kwa hakika bado ni vizuri kweli kweli, na havifai kwa watoto wadogo (kwa maoni yangu) ila kwa kweli ni vizuri...na miaka hiyo ya wakati wetu (yaani miaka ya 70 na miaka ya 80) vitabu hivi vilikuwa 'maarufu' kwa vijana (teenagers na wale wenye miaka ya 20 hadi 30) ....
 
1954! KAMA SUTRA nilikisoma 1980's. Nilikuwa kijana barubaru. Machejo niliyo yapata mule nili apply kwa GF wangu. Alichanganyikiwa. Vitabu vya zamani SHIKAMOO
 
Baba Mkuu Guasa...
Kutwa nzima sina umeme.

Si kama LUKU yangu imakata, la hasha.
TANESCO kazima!

Ndiyo maana nimechelewa kuja barzani.
Ahsante umenileta kwenye, ''kubonga.''
 
Guasa! Kitabu hiki unacho au maneno haya unayatoa kichwani (creaming)? Hii kweli Cambridge kama ya Mohamed
 
Kwanza nikushukuru mkuu for taking your time to respond on this. Pili kuhusu age worry not coz kama ni mmoja wa wapenzi wakubwa wa vitabu vya akina Umsolopagaas basi jua mvua kadhaa zimenipitia. Tatu nashukuru pia nimeshakipata hicho kitabu humu kuna member amekiweka hapa, asante.
 
Guasa! Kitabu hiki unacho au maneno haya unayatoa kichwani (creaming)? Hii kweli Cambridge kama ya Mohamed
Kichwani ndugu yangu miaka imebaki kulikumbuka kava lake lilikuwa rangi ya zambarau na weupe katikati kwa kweli mshana katurudisha katika kumbukumbu tamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…