Nimekumbuka mbali sana. INKUBU! Enzi zileee unaenda Maktaba ya Mkoa unapewa kadi(3)za usajili, unampelekea mzazi anakusainia kisha unapeleka shule kwa mkuu anakusainia na kugonga muhuri.
Tayari unakuwa member wa library. Kazi yako hapo ni kuazima vitabu. Kila baada ya wiki mbili unarudisha kitabu library na kuchukua kingine
Ipogolo,
Nami umenisafirisha hadi 1967 St. Joseph's Convent, Dar es Salaam.
Mwalimu wetu wa English
Mrs. Grant.
Mumewe na yeye alikuwa mwalimu vilevile Chang'ombe Teacher's
College.
Hawa walikuja katika mradi maalum wa British Council wa kusomesha
Kiingereza.
Mrs. Grant ndiye aliyetuambia kuwa ili tukijue vyema Kiingereza ni lazima
tuwe tunasoma vitabu hivyo akatuambia tujiunge na Tanganyika Library.
Hii ilikuwa Mtaa wa Makunganya mbele ya Bilicinas.
Siwezi kueleza raha niliyopata katika maktaba ile.
Siku zile serikali ilikuwa na uwezo.
Maktaba ilikuwa na kila aina ya vitabu.
Hapa pakawa ni ''second home.''
Nikiingia saa nane nashtuka saa 12 jioni naangalia nje taa zinawaka.
Mimi nikiishi Libya Street Kisutu.
Kwa hiyo natembea kurudi nyumbani nina vitabu nimechukua.
Haya ndiyo yalikuwa maisha yangu.
Kokote duniani niendapo nahakikisha kuwa nimekwenda bookshop kuangalia
kuna kipi kipya.
Nikiwa Uwanja wa ndege pia nitaangalia bookshop mna kipi.
Msiba wanetu wanakusanya DVD.