Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,296
Duh! Kisa kilianzia pale lamu baada ya kuongea na bwana balozi ndie aliwapa maelezo ya kwenda kuonana na bwana makenzie aishie mwishoni mwa mto tana akawaamibia inabidi muwe na wapagazi wa kuwabebea vitu vyenu nje ya mji kuna wakazi walikuja na bwana wao alie kuwa amekwenda kuupanda mlima kilimanjaro lakini wakati wa kurudi akapata maradhi ya homa na kufariki nendeni mkawaone .Guasa...
Mwaga vitu...
Naisubiri ile ya ''kubonga.''
We mtu hatari sana kaka.
Hizi hazina za kale ndugu yangu.
Asubuhi kuliko pambazuka tukaenda tuliwakuta watatu wamekaa nje nao sura zao zilikuwani zenye kutumainiwa lakini loh !tulipo waeleza shauri letu walikataa kabisa wakasema bado wana uchungu wa kufiwa bwana wao nikawauliza nimeambiwa mpo sita wengine wapo wapi?
Wakajibu wamelala kwani usingizi huondoa uchovu na pia huleta usahaulifu lakini walikubali kuwaamsha.
Wale wawili kati ya wale watatu walikuwa wanafanana na wale watatu niliosema nao mwanzoni ila yule wa tatu nikasema huyu si mkazi ni mzulu halisi alitoka huku ameuweka mkono wake mdomoni labda apige mwayo alipotoa mkono nikaona kinywa cha ucheshi cha kizulu na macho madogo ila makali kama mwewe.
Japo kuwa nilikuwa sijamuona kwa muda wa miaka 12 nilimtambua na kumsalimia kwa sauti ndogo kwa lugha ya kizulu
Hujambo umslopogaaz?
Yule mtu mkubwa nusura shoka lake la vita lianguke
Mkuu !mkuu baba! Makumazahn! Mzee mwindaji! Akeshae! Hodari mwepesi! Rafiki mwaminifu! Muuwaji wa simba mla tembo! Mkuu mkuu baba! Ama kweli ile methali ya kikwetu isemayo milima haikutani ila wanadamu hukutana ni ya kweli kabisa na tena ni yenye busara! Tazama alikuja tarishi kutoka natal akalia na kusema makumazahn amefariki na nchi haitomuona tena! maneno haya yameongewa zamani ila tizama leo baba yangu katika nchi ngeni tena yenye harufu mbaya kama hii namuona tena makumazahn hakika ndie yeye bila shaka! Manyoya ya mzee mbweha yamekwisha ingia mvi! Lakini macho na meno yake bado ni makali vilevile kama zamani! Mkuu baba unakumbuka namna ulivyo pitisha risasi penye jicho la nyati aliekuwa akishambulia?